Ni nani Dr. William Mgimwa?

Kwa sasa hatujali CV tunataka utekelezaji.Mtu wakuondoa au kupunguza matatizo ya mifumo ya kifedha na ukuaji wa uchumi na atimaye maisha ya kila Mtanzania yasonge mbele bila shida

CV muhimu ijulikane huko alikopita labda kafisadi
 
Njaa ina matatizo makubwa sana hivi mimi nashindwa kuelewa ni kitu gani hasa mpaka Kikwete achukiwe hivi? Mmetaka avunje Baraza La Mawaziri kavunja ametulia na kulipanga upya kila mtu analaumu tu hivi nyie watu wa Chadema mnao watu wanaofaa kuwa Mawaziri? Sugu ama Vincent Nyerere ama Mchungaji Msigwa ama aliekuwa Mbunge wa Arusha Mjini wanafaa kwa Wizara gani? Mbona hao ndo CV zao hazieleweki kabisa? Tuache mambo ya ushabiki ambao hauna msingi Mawaziri wameteuliwa tuwaache wafanye kazi karibu Mawaziri wote waliokuwa wanalalamikiwa wametoswa na wengine waliobaki wamebadirishiwa Wizara Raisi kwa kiwango kikubwa amejitahidi ila nyie watu wa Chadema sifa yenu kubwa ni kulaumu tu hata kama kilichofanyika kiko sahihi!

Acha kutapika usivyokula wewe,mawaziri wa CDM hawatokani na wabunge kwataarifa yako CDM ina hazina ya vichwa zaidi ya umri wako times ten
 
karibia 90% ya mawaziri ni either dr or professor sasa naomba niulize huu udoctor wa mawaziri ni udoctor wa kutibu wagonjwa/wanyama, udoctor wa phd, udoctor wa kupewa(kama kikwete, mengi) au udoctor wa kuchakachua:thinking:

Muulize Emmanuel Nchimbi aliupataje udoctor Mzumbe University na alitumia shlng ngapi au Prof. Kuzirwa VC wa Mzumbe anaweza kuwa na majibu mazuri. Nchimbi alishindwa kupresent mpaka panel ikakosa cha kuandika cha ajabu wakashanga siku ya graduation anatinga na press.
 
I was gonna ask that! Kumbe kila karipoti ukiandika unaita publication? Ngoja ni-update kwangu mweh!
Afu atakuwa dr of MBA, kwani JK ni dr of what vilee?

dr. Of travelling and ombaomba. Anatuombea mpaka na ucameroon
 
Babu mwenzangu Dark City naona unazeeka vibaya. Kwani rais JK wako siyo Dokta? Stuka!

Mkuu- jeykey sio Dokta tena bali kapanda hadhi - zile Phd zake ni nyingi saaanaaa so siku hizi anaitwa Professor Kikwete,maana ana degree nyingi na karibia zinafikia idaddi ya tai zake za kuvalia suti!!!
 
Last edited by a moderator:
I know him.Ni mtu muadilifu na mchapa kazi.alikuwa NBC Iringa kama accountant,then akawa lecturer pale chuo cha NBC cha Amon Nsekela Iringa after that alihamishiwa hapa DAR na kisha kushika nyadhifa mbalimbali mpaka kuwa Director.na baada ya hapo alienda BOT na baadae kujiunga na shughuli za siasa ambapo kwa sasa ni mbunge wa kalenga.nimesoma na watt wake pale IR na mkewe (mama Flora) ni mwanamke mwenye roho nzuri sana na kwa ujumla ni familia yenye maadili,wachapa kazi na ni mfano wa kuigwa.ni majiran pia so nawafahamu vizuri.ameandika publications nyingi tu kiumjumla anatufaa na tutegemee mabadiliko mengi ikiwa ni pamoja na kudhibiti mfumuko wa bei.Kila la heri Dk.william Mgimwa
Lets hope for the best , wengi huwa wanaingia wakiwa na sifa kama hizi ila mfumo wanaoukuta ndo huwa unawabadilisha
 
nimewahi kusoma sekondari na dada mmoja akiitwa Thecla Mgimwa pale Lugalo ya Iringa, huyo ni familia yake pia? just want to knw.

yaani JF imekuwa ya kudiscuss mtu binafsi badala ya kudiscuss nini matarajio yetu kutoka kwake na hata yeye kama ni member wa JF anaweza kupata maoni yetu.
ila cha kushangaza badala ya kudiscuss mustakabali wa nchi tunashindana tunavyomjua ambacho hakina mchango wowote kwa taifa.
awe dr au prof haina maana kama hata kidhi matakwa yetu kwani wapo wengi akina prof. Kapuya ambao licha ya kisomo chao kusaidia nchi waliishia kuanzisha bendi za muziki.
nadahani tufike mahala tuchange ili JF irudi katika hadhi yake wakati wa jambo forums.
 
Wewe Mwanamasala ndio Big Joke... Tatizo mkishapata vidigrii vyenu mnajifanya mnajua kila kitu. Hebu angalia publications alizofanya hapo then niambie kama hazitoshi kumpatia PhD kama alikuwa anatafuta!? PhD is all about publications we ****, sio kutudharau watanzania kuwa vile tu kuna wapuuzi wachache
Labda kwenye vyuo vyenu vya kata ndio publications zinakupatia PhD. After all, hizo publications amepublish kwenye journal zipi? Hizo ni repoti tu.
 
Jaman ukitaka kukech Cv za Mp na kuweka humu au mtandao wowote unafanyaje
 
Huyu ni fisadi wa elimu
1. Sidhani kma mwa 1991 IDM mzumbe walikua wanatoa MBA (I stand to be corrected)

2. Sijaona sehem aliyosomea hiyo PhD na kama kapewa ilibidi ataje alipewa PhD ya nini na chuo gani na mwaka gani ili tujue ni vyuo accredited au ni kma SUZA tu

3. Hizi publication zake ni upuuzi mtupu. Kwa mtaji huo na mie mpaka saiv nna publication zaid ya 10. Anajiita Dr wakati hana international publication hata moja?

Hawa ni wachakachuaji wa elimu tu,kwann ujipe sifa ambazo huna? Kujifanya msomi ili iweje?Me naamini utendaji ni mtu mwenyewe na usomi unachangia asilimia chache tu kwenye utendaji wa mtu
 
Hujui kwamba enzi hizo kuandikishwa darasa la kwanza ilikuwa inabidi upimwe kwa kujishika masikio, kukimbia, kubeba kidumu cha maji nk, naona hakuweza kutosheleza viwango hivyo mpaka alopotimiza miaka 11 ndipo akakubalika. Hata Mwalimu Nyerere alianza darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka 14 baada ya ku graduate masuala ya kuchunga mbuzi wa nyumbani. Hayo ndiyo mambo kale!!!

Ukweli Mama Mdogo nakumbuka mie 1967 mkono haukugusa sikio upande wa pili ilikuwa kasheshe kuanza la kwanza !
 
acheni maneno mengi tumpime kwa kazi aliyopewa tusitafute sana udhaifu wa mtu tuombe mungu awe naye asije kukengeuka
 
cv sawa lakini tunachohitaji utendaji wake huenda anaujuzi wakututia nafuu ktk mifumuko ya bei na kupolomoka kwa shilingi. Hawa maprofesa maranyingi wamekuwa si watendaji wazuri pombe kali zina wapelekea kuwawazembe. Nakukaa nje ya nchi muda mrefu kunawafanya moyo wakizalendo kupotea .hivyo huyu jamaa mgimwa anatufaa sana hawa watu wakati ni wazuri uzoefu wake ni msaada kwetu
 
Wewe , acha utani. Kuna daktari hata wa wadudu mwenye qualifications kama hizi??

ninaomba watu msichanganye fani. Huyo Bw. si mchumi kwa CV yake inavyoenyesha. Uchumi ni zaidi ya Finance. Watu wengi huwa wanachanganya hizi professions lkn kiukweli ni taaluma tofauti.

Lkn hiyo Dr. yake ina walakini kidogo.
 
Dark City, huyu Waziri mteule hili ndilo eneo lake Professionally, tatizo wakishaingia huko wanaenda kufanya wanayoyajua wao ambayo hata darasani hayapo

Tatizo linaweza lisiwe mtu anayeteuliwa kushika wadhifa ambaye ni mchapakazi. Anapobadilika pia huwa kunakuwa na kitu nyuma yake (tukiacha ufisadi) ambacho kinamfanya apunguze kasi au ubora wa utendaji wake. Na ninaamini kabisa kitu hicho huwa ni maamuzi ya rais mwenyewe ambayo yako kisiasa zaidi kuliko kiutendaji kama inavotakiwa. Na ndio tatizo linalotuumiza kwani maamuzi mengi yamekuwa ni ya kisiasa badala ya kuwa ya kitaalamu and that is wrong!
 
Katika CV yake kuna miaka mitano inamiss 1990-1995. Hii ni gap kubwa mno kwenye CV. Je, muda huu alikuwa wapi, anafanya nini? Na je, kwanini hicho alichokifanya hakijaingizwa kwenye CV?
 
CV sio kitu issue is CANN HE DELIVER?
Lets wait and see,personally ninamuamini based on the CV simjui na sijawai fanya nae kazi
 
Back
Top Bottom