Ni nani atakuwa Waziri Mkuu Mpya!

you are right mkuu, hayo ni maigizo. kelele nyingi tumeshazisikia hakuna mabadiliko yeyote! watu wanataka kujitafutia umaarufu na watanzania wanadanganyika kirahisiii. Tunataka matendo,tuone mtu kang'oka, au wamepiga kura kutokua na imani na pm hapo tutajua watu wako serious!
Tupunguze hisia wakuu, mbona tunakuwa kama hatuijui nchi yetu!?
Kinachoendelea dodoma ni igizo la wabunge wa ccm kutaka kuwahadaa wananchi wajinga ili waone bado ccm ni chama chao na kwamba wabunge wa ccm pia wanajua kubwata!
Hamna wa kuangusha serikali pale, tunachokitaka toka kwa wabunge wa ccm ni kikubwa kuliko uwezo wao wa kutenda kwa mazoea!
Sisi tulioelevuka japo kidogo tukianza kulewa hisia utafikiri kinachotokea bungeni ni kipya sana ndo tutawayumbisha masikini wengine kuona uh kumbe hata wabunge wa ccm wanafanya kazi wakati hamna chochote walichofanya mpaka sasa.
Tuwaangalie mwisho wao kwanza
 
Mwanri anafaa manake anavyoongea nahisi ukikaa karibu nae utalowa

Haahaaa:) Wewe unaleta masihara! Ina maana mtu akikaa jirani naye lazima awe na RAIN COAT au mwavuli? Basi huyu hafai; tunataka kiongozi na siyo MTENGENEZA MVUA aka mthailand:)
 
Hizo hasira za Wabunge wa CCM ni kutoka moyoni au ni lile panga la nyongeza ya posho?
 
Tupunguze hisia wakuu, mbona tunakuwa kama hatuijui nchi yetu!?
Kinachoendelea dodoma ni igizo la wabunge wa ccm kutaka kuwahadaa wananchi wajinga ili waone bado ccm ni chama chao na kwamba wabunge wa ccm pia wanajua kubwata!
Hamna wa kuangusha serikali pale, tunachokitaka toka kwa wabunge wa ccm ni kikubwa kuliko uwezo wao wa kutenda kwa mazoea!
Sisi tulioelevuka japo kidogo tukianza kulewa hisia utafikiri kinachotokea bungeni ni kipya sana ndo tutawayumbisha masikini wengine kuona uh kumbe hata wabunge wa ccm wanafanya kazi wakati hamna chochote walichofanya mpaka sasa.
Tuwaangalie mwisho wao kwanza

JG bora umesema
Huu usanii huu sinaona mfano wake
hakuna kitu maana tungetemea pamoja na kutoa mapovu ya jana tungeona hata mkurugenzi wa TBS amejiondoa nafasi yake kwa ubadhirifu
Ila hakuna hata anayetikisika wala kuogopa na wala hatuoni kama serikali ya huyu waziri mkuu aliyepo inatishiwa nyau na hawa wabunge wapiga kelele
hakuna kti hapa na hii inatokea baada ya kuona upepo hauko salama kwao sasa wanaogopa kuona kuwa watakosa kura wasipotoa mapovu yao kupiga kelele ambazo ni kama unampigia mbuzi gitaa
Hadi muda huu tungekuwa tumeona hata tamko la waziri mkuu kuhusu tuhuma hizi ila yeye nae anaendeleza ule utaratibu wa kusema tunashughulikia au tunafikiri au nadhani au tutaona mambo ya kitoto kabisa
 
Ni kweli tunataka Rais mpya lakini kwa mujibu wa Katiba tuliyonayo kinachowezekana ni kumwondoa Waziri Mkuu kwa kumpigia kura za kutokuwa na imani naye!
Kwani kura ya kutokuwa na imani na serikali manake ni waziri mkuu na si rais? Basi haina maana, maana hapa tatizo si waziri mkuu bali ni Rais! Tuna rais ambaye ni bonge la zuzu, huyu ndiye anayeiweka nchi katika hali ngumu. Pinda hana hata ubavu wa kufanya maamuzi maana kuna maamuzi mengine anayoyatoa lakini Rais anayakataa. Mifano, la Jairo, kwamba afukuzwe Rais akamrudisha kazini, la madaktari na mengine mengi. Kimeo hapa ni rais na si vinginevyo.
 
Sioni km serikali yaweza kupigiwa kura ya kutokuwa na imani na wabunge, hizo kelele wanazopiga ni km kelele za chura zisizo mzuia tembo kunywa maji, na km wameitana kwa kikao leo mchana basi utaona watakavyo anza kusifu serikali kijnga jinga, sisi tu ndo twaweza kutumia nguvu ya umma kuwatoa hawa wezi wa rasilimali zetu.
 
Wakuu nimetazama bunge la asubuhi ya leo, kama ni kweli wale wabunge wa magamba wanayo yaongea yanatoka moyoni basi serikali ya ****** inaweza kuangushwa fasta.
Filikunjombe ameichana live bungeni, mawaziri wanaonekana wanamuangusha sana ****** wetu.
tusubirie kikao chao
 
Hii serikali badala ya kuwa ya chama tawala imekuwa serikali ya wezi na wadokozi wa mali ya umma. Haina hata huruma na watanzania wahangaikaji.
 
Tupunguze hisia wakuu, mbona tunakuwa kama hatuijui nchi yetu!?
Kinachoendelea dodoma ni igizo la wabunge wa ccm kutaka kuwahadaa wananchi wajinga ili waone bado ccm ni chama chao na kwamba wabunge wa ccm pia wanajua kubwata!
Hamna wa kuangusha serikali pale, tunachokitaka toka kwa wabunge wa ccm ni kikubwa kuliko uwezo wao wa kutenda kwa mazoea!
Sisi tulioelevuka japo kidogo tukianza kulewa hisia utafikiri kinachotokea bungeni ni kipya sana ndo tutawayumbisha masikini wengine kuona uh kumbe hata wabunge wa ccm wanafanya kazi wakati hamna chochote walichofanya mpaka sasa.
Tuwaangalie mwisho wao kwanza

ulichosema ni kweli ni sawa na tamthilia kwani si mara moja wanafanya kitu kama hiki wakishakutana wanarudi tofauti na matarajio ya wengi
 
Wakuu nimetazama bunge la asubuhi ya leo, kama ni kweli wale wabunge wa magamba wanayo yaongea yanatoka moyoni basi serikali ya ****** inaweza kuangushwa fasta.
Filikunjombe ameichana live bungeni, mawaziri wanaonekana wanamuangusha sana ****** wetu.
tusubirie kikao chao

Anaangusha na nani kwani yeye ni taahira????? hujaongea kitu
 
Masikini CCM! Huwa nawahurumia sana wanasiasa vijana waliopo ktk chama hii! Sijui baada ya anguko watafanya kazi gani huku mtaani!!! Wameisha zoea dezo na kuhongwa! Wengi wao watapata msongo wa mawazo na kufa!

Wacha wafe tu, huwezi ukawa na akili timamu ukajiunga na mzimu wa CCM, sana sana ni vijana wasiojiamini na huenda wengi wao hawana hata sifa na uwezo wa kufanya kazi nyingine. Wacha wafe tu. CCM kwa upuuzi wao wanakufa watanzania wangapi kwa ajili ya ukali wa maisha huku wachache wakipeta kwa hela za wavuja jasho?
 
Anaangusha na nani kwani yeye ni taahira????? hujaongea kitu

Hayo maneno ya kusema rais anaangushwa na watendaji hayana mashiko. wanamwangusha kwa sababu anataka kuangushwa. yeye ndo mteuzi na kwa kiasi kikubwa amechangia kuendelea kulea wezi kwa sababu anazozijua yeye, nani kawajibika downs, epa richmond, na madudu yote tunayoyashuhudia leo? Halafu leo bila hata aibu serikali inalialia kuwa haina hela.Wacha wamwangushe ni kwa sababu anataka mwenyewe, ana uwezo wa kuchukua hatua km hataki unategemea nini?
 
Wabunge wa CCM hawawezi kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais kwakuwa wanajua hawawezi kushinda chaguzi katika majimbo yao kupitia CCM kulingana na hali ya siasa kwa sasa. Wengi wao wameingiwa na hofu juu ya suala hili na ndio maana wameanza kuamka na wala hawaigizi.

Maoni yangu ni bora wabunge hawa waipiganie nchi hii kwa sasa ili waweze kujijengea heshima na historia kuliko kumaliza awamu yao hii ya mwisho kwa aibu na hata bila kukumbukwa miaka ijayo. Kama inawezekana wangekuwa waungwana kukubali kuivunja serikali hii. Bora kutumia kiasi cha pesa wakati huu kufanya uchaguzi mwingine ili kuokoa upotevu na ukosefu wa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu kwa miaka michache iliyobaki. Tutawashukuru kwa hili.

Nina hakika ikipatikana serikali makini mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali utapungua, sekta nyingi zitaimarishwa zikiwemo kilimo, maji, nishati, afya, usafiri hata mahakama kutenda haki pamoja na kuwahukumu mafisadi na kuwafilisi ili kufanya uchumi wa nchi na wananchi kuimarika.

Wabunge amueni sasa kutupeleka kwenye maendeleo ya kweli kwa manufaa ya wananchi.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom