Ni nani atakayevumilia usaliti huu wa serikali?

oba

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
310
65
[h=6]Blandina Nyoni na Dr Deo Mtasiwa bado wapo Wizarani
Wakati tukiendelea kupokea na kung'amua vitendo mbalimbali vya ufisadi vilivyofanywa na Mapacha wawili wa Wizara ya Afya (Blandina Nyoni na Dr Deo Mtasiwa), habari nilizozinyaka leo kutoka kwa watumishi watatu na baadae nikadhibitishiwa na Mkuu wa Idara mmoja ambae yupo Wizara ya Afya, zinasema Katibu Mkuu na Mganga Mkuu wa Serikali waliosimamishwa kazi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda bado wapo kazini na hata leo wamekuwepo Ofisini.

Habari zinasema kuwa wamekuwa katika heka heka za kuweka sawa nyaraka zao vizuri hasa zile zinahusu Manunuzi. Concern yetu hapa ni kwamba imekuwaje Pinda ameweza kuwadanganya Madaktari kuwa mahasimu wao wakuu Bi Blandina Nyoni na Dr Deo Mtasiwa amewasimamisha kazi tangu mchana wa Alhamisi ya tarehe 09/02/2010 wakati bado wameendelea kwenda ofisini hadi leo?

Hofu inayoibuka hapa ni kwamba kama wataendelea kwenda ofisini wakati tayari wamesimamishwa kazi na Waziri Mkuu katangaza kuwa wanachunguzwa na vyombo vya dola, Je hawawezi kutumia mwanya huu kupika au/na kupoteza nyaraka za serikali ambazo zingesaidia katika ushahidi? Na je Waziri Mkuu Mizengo Pinda, anamdanganya nani kwamba Blandana Nyoni na Deo Mtasiwa wamesimamshwa wakati bado wanaenda ofisini tena kwa kutumia V8 za serikali?
[/h]
 
Wasifunge hata mizigo yao? wasi-handover hata majukumu yao. Ushahidi wa madudu kama upo haufutiki wala haupotei.
 
Kwanza kama mimi ningelikuwa Mizengo Pinda, Ningeshajihachia madaraka siku nyingi tangu inshu ya Jairo, kisa na mkasa kudharaurika katika jamii.
 
Napata hasira sana ninapopata habari kama hizi,hivi Tanzania tuna serikali au tuna genge la wahuni?maana viongozi wetu wote hakuna anayejari,NYIE WAKUU WA NCHI MNAFANYA NINI? Jamani achieni madaraka wajaribu na wengine,nyie mmeshindwa kabisa NG'ATUKENI.
 
Nyoni Kasimamishwa!!! what about Jairo's Story? wote wale kwa uelewa wangu ni makatibu wakuu!! kwa nini ashindwe kumsimamisha Jairo halafu aweze kumsimamisha Nyoni?
Hakika madaktari waliingizwa mjini!! walionyeshwa bulb wakaambiwa ndio mwezi nao wakakubali!! huenda ndio sababu madaktari hawa huweza kufanya operation ya Kichwa badala ya ile ya mguu!!!
WHAT A SAD STORY!!
 
Back
Top Bottom