Ni nani asiyemtambua Dr. Slaa?

ASKOFU MSAIDIZI

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
209
23
Jaman naomba kuuliza ni nani asiyemtambua Dr. Slaa. Mzee huyu namkubali kwa msimamo wake na kwa kutotafuna maneno, Kuanzia kwenye kampeni mpaka hivi leo bado msimamo wake uko pale pale. Kama huwezi amini basi amini hili mfano mzuri Alitangaza kutokumtambua JK kama rais wa JMT na sasa hakwenda Ikulu kwa makubaliano kama walivyofanya viongozi wengine.

Nakukubali sana mzee ndo maana umeenda shule.

Kwa haraka haraka naomba upitie C.V ya Raisi wa Tanzania Ijayo.
 
Dr wa ukweli,

naona kama vile Rais Kikwete kauza vile kale ka-opochuniti tuliompa juu ya Muswada wa Makinda vile. Sasa nadhani njia ni nyeupe kufikisha mashtaka yetu kwa wenye nchi kila kona ya Tanzania Bara naa Visiwani.

Kazi iendelee!!!
 
Rais wake ni nani tanzania au ni mungu tu ndio rais wake? Jamaa anautaka urais kwa nguvu zote.
 
...........Alitangaza kutokumtambua JK kama rais wa JMT na sasa hakwenda Ikulu kwa makubaliano ........

ASKOFU MSAIDIZI,

Nina mashaka makubwa na Madhabahu yako. Itakuwa inawaongoza kondoo wa Bwana kwenda kusiko Mbinguni.

Dr. Slaa na Chadema kwa ujumla hawajawahi kutangaza kutomtambua JK au Rais wa JMT bali walitangaza na daima wanasisitiza kutotambua mchakato uliopelekea Rais kurudi madarakani. Na ili kuleta suluhu ya kudumu katika mchakato na si Tassisi (Rais) au Mtu (JK) ndo maana mara tu baada ya Uchaguzi wakaanza moja kwa moja na moto wa kudai katika mpya. Katiba itakayowezesha mchakato wa kuwa na uchaguzi huru na wa haki. Yaani kupatikana kwa Tume Huru ya Uchaguzi
 
Back
Top Bottom