Ni nani aliyemtuma mkenya kumteka Dr. Ulimboka?

Yani uyo mrundi sujui mulundi sio ishue! Wao walidhani chama flani kiko nyuma mgogoro wa madaktari. Bila kujijua wenyewe ccm walituthibitishia tuhuma hizi dhidi ya cdm Pale bungeni kupitia vilaza wao kadhaa akiwemo yule nyanya. Na hata Dr. Ulimboka wakati anateswa alikuwa akishinikizwa aseme ni nani yuko nyuma ya mgomo huo. Na kama huyo mulundi nae amesema walipewa kazi na mtu ambae wanahisi yuko serikali! so inaweza ikawa kweli uyu jamaa alihusika na hao wenzie 12. Wanasheria kenya wanaotaka arudishwe wana point ! Ni kwa usalama wake maana ushahidi wake ni muhimu sana . Bila hivyo tusubiri kusikia katoroka sababu tumeshaambiwa ni jambazi sugu,kajinyonga au kauawa akijaribu kutoroka! Si alikuwa miongoni mwa waliopewa kazi! Unfortunately kazi imefeli na nahisi waliowatuma wamekataa kuwalipa ndio maana nao wanataka kuwaumbua!
 
Yani uyo mrundi sujui mulundi sio ishue! Wao walidhani chama flani kiko nyuma mgogoro wa madaktari. Bila kujijua wenyewe ccm walituthibitishia tuhuma hizi dhidi ya cdm Pale bungeni kupitia vilaza wao kadhaa akiwemo yule nyanya. Na hata Dr. Ulimboka wakati anateswa alikuwa akishinikizwa aseme ni nani yuko nyuma ya mgomo huo. Na kama huyo mulundi nae amesema walipewa kazi na mtu ambae wanahisi yuko serikali! so inaweza ikawa kweli uyu jamaa alihusika na hao wenzie 12. Wanasheria kenya wanaotaka arudishwe wana point ! Ni kwa usalama wake maana ushahidi wake ni muhimu sana . Bila hivyo tusubiri kusikia katoroka sababu tumeshaambiwa ni jambazi sugu,kajinyonga au kauawa akijaribu kutoroka! Si alikuwa miongoni mwa waliopewa kazi! Unfortunately kazi imefeli na nahisi waliowatuma wamekataa kuwalipa ndio maana nao wanataka kuwaumbua!
 
Ile ni longolongo na pia nia aibu kubwa
Magaidi waingie kutoka nchi jirani wafanye utekaji na wasijulikane
Polisi wasifanyie kazi taarifa zote wasubiri mhalifu ajipeleke kanisani
kabla ya kumfikisha mahakamani baada ya kumhoji na kukiri alitumwa na kiongozi wa Serikali,kwa nini kama ilivyo kawaida askamatwe huyo master planner na kuunganishwa na Case?
Kova,hizi ni sinema za kihindi za enzi ya drive inn hazina mashiko..we are no longer on that age!!
 
Jambazi alipora nini??? Je Uli anaweza kuwa shahidi kwenye hii kesi. Mbona mjambazi ya EPA uchunguzi unaendelea imekuwaje huyu siku moja tu mahakamani.

Wamemkimbaza mahakamani ili kuwafumba midomo watu kila atakaye hoji ataambiaissue ipo mahakamani
 
Kweli kuchamba kwingi huondoka na mavi. Hii Movie aliyotengeneza KOVA asifikiri kwamba itaiacha salama serikali ya Tanzania.

Kwamba Kenya kuna kikundi cha kigaidi, ambacho kazi yake ni kuteka na kutesa watu.

Mimi sitoshangaa kesho Batlida Burian (balozi wetu nchini Kenya) kama hataitwa IKULU ya Kenya atoe maelezo vizuri kuhusu tuhuma hizo zilizotolewa na Kova dhidi ya Kenya.

Kova story uliyotupatia don't pass THE JIGGLE TEST. Try again. BTW mbona hujamuhoji huyo MTU wa SERIKLI aliyemukodi huyo Mkenya.

Mimi ninapendekeza watu wa human rights akina Kija Bisimba mjitolee kumtetea huyo Joshua aliyembambikiziwa kesi hiyo ya Dr. Ulimboka ili serikali ikaumbuke mahakamani.

Kweli sasa nimeamini maneno ya Dr. Ulimboka yule Yuda Isikarioti (Abeid) aliyemsaliti kwa kumletea watekaji yuko IKULU. Na kwa maana hiyo watekaji wa Uli walitumwa kutoka IKULU. Prove me wrong, you know I can put 2 and 2 together!
 
Duh,hyo ya kutawaza kabla ya kunya nimeipenda.kwa mujibu wa kova huyo jamaa ni mzoefu katika matukio hayo.haingii akilini ajutie hicho kitendo.kova kweli govi
Ni lugha ya karaha, lakini jazba ilinituma nitumie huu msemo.

Kwa ufasaha nilikusudia anajisafisha/anawasafisha watuhumiwa kabla ya uchafu haujatoka, sasafikiria unakuja kutoka wakati wanaendelea kujisafisha. Sipati picha!
 
msitu wa mabwe utaumbua wengi bora uchomwe moto uishe kabisa kuliko kutufanya mbolea kwa kunyunyizia damu.
 
Kesi iliyokuwepo ni sensitive na imeligusa Taifa zima na zaidi pale wengine wanaposema ni serikali na wengine wanaposema ni Chadema ,wananchi wanataka kujua ni nani alienyuma ya jambazi hili au tuseme kesi hii .Na kama unavyojua Chadema ni watu wa makanisa kanisa na jamaa ameenda huko ili wamsaidie ila wakanisa wamevunja amri ya mtu anaeungama.

Kushabikia ccm ni upuuzi mtupu na leo nimeamini.
Kwa taarifa hii ulioiandika hapa bila ya shaka kuiamini ni ngumu hata kichaa wa aina gani hawezi kukubali uyasemayo ila kwa kichaa aliyeandika haya maneno mwenyewe ni rahisi kuyaamini.
inabidi serikali ya ccm ijitahidi sana kuchomoka kwenye hili tukio tena wajipange na sio kuja na technic za kipuuzi ambazo watu wa CCM pekee ndo wanaweza kuziamini.
 
Kuna maswali mengi nyuma ya kiinimacho kilichotangazwa na kamanda Kova juu ya utekaji wa dr Ulimboka. kati ya mengi, Maswali yafuatayo yana wafanya Tanzania wasiamini taarifa ya jeshi la polisi juu ya utekaji na utesaji aliofanyiwa dr Ulimboka.
  • Kwamba mtekaji alienda kufanya toba kanisani haiingii akilini hata kidogo.Si rahisi kiasi hicho kwanza kanisa lipo kila mahali. Toba hiyo ingeweza kufanyika Kenya, Uganda na nchi nyingine bila hatari ya mtuhumiwa kukamatwa.
  • Kwamba mtekaji alitumwa na mtu asiyemfahamu tena anafanya kazi serikalini,serikali ipi ya Kenya au hii ya JK? Kwa hiyo Watanzania walikuwa sahihi kuituhumu serikali? Mbona waziri mkuu na Rais walikanusha kwa sauti kali tena ya kuapa? Haya mwajiri wa mtekaji anafanya idara ipi? Kama mwajiri na mwajiriwa hawafahamiani mshahara baada ya kazi ulilipwa vipi? Nani alishawahi kuajiriwa bila kufahamiana kwanza na mwajiri? Kujaza mkataba wa kazi?
  • Mbona katika hili taarifa ya polisi haikuonyesha picha ya mtuhumiwa? Mbona watuhumiwa wengine huonyeshwa picha zao pindi wanapokamatwa?
  • Kwa madhehebu mengi ya Kikristo, toba haifanywi kwa kwenda kuisema dhambi kwa mchungaji isipokuwa kanisa Katoliki,Je kanisa aliloenda mtekaji lina utaratibu huo wa toba?
  • Kwamba polisi imemnasa mtuhumiwa,kwa taarifa hiyo ndo mwisho wa uchunguzi wa chaini ya kiharifu iliyo nyuma ya tukio hili?
Kama ni toba, mbona kakana mashitaka. Hivi ni viini macho. Pia wanataka kutumia delay tactics--eti august ndio itasomwa tena!
 
Hapa Kova Kalikoroga! Hivi kwa tukio lile lilivyokuwa INAWEZEKANA mtekaji akawa MTU MMOJA tu? Tungemwelewa angesema MMOJA kati ya WATESAJI wa Dk Uli. Hivi hata kama mteswaji ni mnyonge (hana nguvu), anaweza kung'olewa kucha, meno na kupigwa nusu ya kufa na MTU MMOJA?
Pili, Mtu huyo huyo aongee na Ulimboka, amweke kwenye gari, amfunike uso na kisha aendeshe gari kuelekea kwenye jumba na kumtesa Uli, na yeye "Asijitetee?" No, hapa Kova kalikoroga, Dkt Uliimboka aliteswa na KIKUNDI cha WATU.
Ushauri, Kova aje kwa staili nyingine. Hii tumeishtukia!
Nnapenda pia kuonesha wasiwasi wangu kwa wanahabari. Wao wanapokea taarifa na kuzitangaza HATA KAMA HAZINA MASHIKO! Je, hapa tukubaliane na zile shutuma walizorushia na Ben Mkapa kwamba THEY ARE NOT CRITICAL? Hivi kweli baaada yankujua mwelekeo wa tukio zima, kwanini walikubali kirahisi kutanga habari TENGE za Kova?
 
Kabla ya kuendelea kujiuliza kuhusu huyo ''Mkenya''. Naomba mkumbuke maneno ya Kamanda Zombe enzi zake kuhusu wafanyabiashara walio huwawa Msitu wa Pande; then tukagundua ilikuwa deal lake mwenyewe. Ntakuwa wa Mwisho kushangaa nikisikia its Cova himself who tried to Kill Dr Ulimboka!
 
kamajambazi ni raia wa kenya je? wametoa taarifa gani khs huyu jambazi wao lazima kuna picha za wanted za hawa watu maana ni jambazi sugu ,hii filamu hainogi ni gear rivers
 
mbona mnajaribu kupotoshwa na ninyi mnajipotosha wenyewe?(U r losing track really).Dr ulimboka ndo anayejua waliomteka na kumfanyia unyama and everybody knows this.Mnadanganywadanganywa na huyu mkenya na nyinyi mnaanza kupoteza mwelekeo.Inawezekana vipi from nowhere mkenya eti aje kumteka Dr Uli,silaa alitoa wapi?gari halina namba,ana utaalamu wa hali ya juu wa kijeshi, and bla bla bla......................., It doesn click in my head.
 
Embu waonyeshe picha zake kwenye vyombo vya habari, si ajabu si Mkenya, wawezakuta ni Mmbongo wa hapahapa, watu wanamjua na ndugu zake!

mnadanganywa na kiini macho hapo. Ni mbinu ya kiintelijensia ya kuwafumba macho msiwafuatilie tena. Huyo mkenya ni wa Kuunda na hana uhusiano na kweli wa tukio lenyewe.
 
Back
Top Bottom