Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
katika siku za hivi karibuni upepo wa kampeni za uchaguzi mkuu zimeanza kuchukua mweleko wa udini. Mweleko huu ni njama zinzoratibiwa na mafisadi kwa kushirikiana na timu ya kampeni ya ccm ili mgombea urais wa cc mhe jakaya kikwete aweze kupata huruma ya watu wa dini fulani na hatiamaye kupigiwa kura eti kwa madai kuwa anasakamwa na watu wa dini tofauti na ya kwake.

Kumbukumbu zinaonyesha japo mgombea wa ccm sasa hivi anaonekana kutumia udini kujinusuru, hana rekodi ya kuwa msaada wowote wa maana kwa dini yake k.m alikubali masuala fulani ya udini kuingizwa katika ilani ya uchaguzi ya ccm ya mwaka 2005, na akanadi ilani hiyo mwaka 2005 ikiwa na ahadi hizo. Lakini alipopata madaraka akshindwa kutimiza hyo ahadi.

Tatizo kubwa lililopo hapa nchini ni ufisadi. Mgombea urais wa ccm katika kipindi cha uongozi wake 2005-2010 amepta fursa mabali mbali za kuweza kufanya maamuzi ya kijasiri kukomesha na kufiutilia mbali ufisadi hapa nchini, lakini mara zote amekuwa akitoa bla blah tu biula ya kuchukua hatua zozote za kufaa dhidi ya wahusika.

Kibaya zaidi katika kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010 mgombea urais wa ccm amefanya lile amablo halikutarajiwa na wengi; nalo ni kuwasafisha watuhumiwa wore wa ufisadi mkubwa hapa nchini ili wacahaguliwe tena kuwa wabunge na viongozi wa taifa hili. Kitendo hiki ndio kimewakera sana wananchi kiasi cha kufikia kudai mabadiliko.

Hivyo watanzania wenzangu, miaka yote waislamu na wakristo tumekuwa tukiishi kwa amani na utulivu bila ya kubaguana. Tusikubali njama za mafisadi kutaka kutugawa ili kudhoofisha nguvu ya mapamabano dhidi ya ufisadi hapa nchini. Ni mategemeo yangu katika mijadala yetu tutazingatia kuwa watu wa dini tofauti hawana matatizo dhidi ya wao wenyewe. Ila watanzania tuna tatizo nz ufisadi unaoshamiri kwa kasi hapa nchini kwa kulelewa na viongozi waandamizi wa ccm
 
hapa tatizo ni lake yeye anakumbatia sana mafisadi anategemea watu wafurahi tuu!! HV NI KILAZA GANI ANAYEMSHAURI MKULU WETU!!
 
Inanishangaza sana kuwa JK na CCM yake wamekuwa mstari wa mbele kulalama kuhusu kushamiri kwa nyufa katika utaifa wetu kwa misingi ya kipato, udini na ukabila sababu wao ndiyo chama tawala na yatokeapo matatizo wao ndiyo wakulaumiwa hivyo hawapaswi kabisa wao nao sasa kuwa walalamikaji. Sasa wakitulalamikia tuwaeleweje?

CCM na JK wake wanapotulalamikia sisi wanataka tufanye nini wakati kazi ya kuongoza nchi tuliwapa kama imewashinda si waseme tu tuweke wengine nao wajaribu?

Mtu unapompa kazi au majukumu yakamshinda na akaanza kulalama akithibitisha si lolote wala si chochote na hana mikakati yoyote ile ya kuhimili changamoto zilizopo mbele yake kazi uliyonayo uliyemtwika hilo zigo ni kumfuta hiyo kazi na kuweka mwingine. Hakuna masihala hapo............

Kwa mfano ni nani aliwatuma CCM kwenye mgawanyo wa ajira, zabuni na miradi serikalini kuzingatia vigezo vya kimapato, udini na ukabila?

Hayo CCM wamejitakia sasa matunda yake ndiyo yameanza kuchipua na kazi imedhihirika ya kuwa imewashinda kabisa.......Jukumu la wapigakura ni kuwafuta kazi tu na kuteua timu mpya ya Chadema itakayoongozwa na Dr. Slaa.........

Hapo kaka yangu JK hakuna "bla-bla" hapo..............Ni tunakufuta kazi tu na CCM yako na huu utakuwa ni mfano kwa wote watakaokufuata... wakivurunda tunawatimua kwa kura zetu...and that is final Bwana...
 
Viongozi wengi wa CCM na wa baadhi ya madhehebu ya dini wameweka mbele kuwa chaguzi hii itapigwa kwa misingi ya kidini huku wakisahahu ya kuwa miaka mitano iliyopita madhehebu zisizo za kiislamu zilimchagua Jk kwa zaidi ya asilimia sabini na tano ya idadi yao. Kwa hiyo kama Jk ataanguka chaguzi hii siyo kwa sababu ya udini ila wapigakura hawakuridhika na utendaji wake na hili JK analijua vizuri na ndiyo maana hata midahalo hataki kwa sababu hana jipya la kutuambia.

Hata majemedari wa CCM safari hii wameufyata mkia kwa sababu wanaona hali ilivyo kiuchumi ni mbaya sana na kama JK akidondoka ni kwa sababu hiyo na wala siyo nyingine.

Kama uchumi ungelikuwa unaenda vizuri hata hizo hoja za ufisadi zisingeshika moto kama ilivyo sasa lakini ugumu wa maisha unafanya jamii ijiulize kulikoni? Inafikia mahali tunajiuliza hivi kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya ugumu wa maisha yetu na hao wachache wanaofaidi?

Jingine ni teuzi za watendaji serikalini, JK amegeuza ni shamba la kuwazawadia jamaa zake na wala siyo kuboresha tija. Mfano mdogo tu, hivi Ephraim Mrema anaendelea kufanya nini hapo TANROADS. Huyu njemba mkataba wake ulikwisha lakini JK haheshimu sheria za uendeshaji wa nchi na huyu Bwana anaendelea kujibana hapo TANROADS kinyume na sheria na isivyo halali. Na hii ndiyo tabia ya JK kutoheshimu sheria alizozitunga yeye mwenyewe na kuzisaini...Katika kipindi cha Mrema hapo TANROADS malipo hewa yamekithiri na barabara nyingi kulipuliwa na kesi kibao mahakamani za kuwanufaisha wajanja wachache kumeshamiri na ungelifikiria JK kama mkereketwa wa kwanza angelisema huyu jamaa sasa tosha aishie mara moja lakini yeye ndiye wa kwanza kusema subiri uchaguzi upite na nitakuongezea mkataba!!!!!!!

Kwa hiyo wapigakura wanajiuliza hivi utawala bora uko wapi? Mbona katika kampeni zake zote JK hajawahi hata kuzungumzia ni vipi atapambana na ufisadi zaidi ya kuwakumbatia watuhumiwa wa dhambi hizo.

Kwa wapigakura wanaona kuwa JK akiendelea muhula wa pili ataendeleza huo ubabe wa mafisadi kuendelea kutesa huku sisi tukiambulia mabaki tu.....

Kuusingizia udini ni kutukosea adabu kama raia wa nchi wakati ambapo ni dhambi ambayo huko nyuma hatujawahi kuifanya na hatuna mpango wa kuifanya sasa. Hivi hao wa dini ya Jk ambao hawatampigia kura nao CCM watasemaje?

Badala ya CCM kumtafuta mchawi wangelijiuliza maswali ya kimsingi kwa mfano mbona hawapo tayari kuzungumzia ni nini walichokifanya kwa miaka mitano iliyopita? Mbona ikifika hapo CCM na hususani JK hubakia kupata kigugumizi kikali mno.......Na kubakia kusema kuna mengi tumefanya na yanaonekana..mengi yapi hayo ambayo unaona hata aibu kuyataja?

Jk mkakati wake wa ahadi lukuki, wapigakura wengi wanashindwa kununua janja hiyo kwa sababu wanaona ni kama JK anawaahidi hongo ili wasahau yaliyopita jambo haliwezekani.

Ili tuweze kusonga mbele kama nchi kama kuna makosa yaliyofanyika wahusika wakiri na watupe nafasi ya kuchangia ni namna gani ya kuyarekebisha lakini wanapogoma hata kutokea kwenye midahalo ambako tungeliulizana ilikuwaje basi ni ushahidi kuwa hawako tayari kujirekebisha hata kidogo........

Hivi kwa nini CCM na hasa JK unaitafuta kura yangu bila ya wagombea wenu kunipa nafasi ya kuwauuliza maswali kwa nini hata mnagombea? Hata hilo swali la kimsingi kabisa CCM hawapo tayari kulijibu sasa kura wanazitafutia nini?
 
Thanks a lot Rutashubanyuma:thumb:
Mimi binafsi nimepata tabu sana hasa kuhusu hili swala la UDINI kuingia kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Kwa muda sasa, nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana kampeni za uchaguzi kupitia vyombo tofauti vya habari, sijaweza kuona/kusikia mgombea mwingine yeyote zaidi ya Dk JK ambaye imekuwa ni kawaida yake sasa kulalama na kutoa miongozo kwa watanzania kutopiga kura kwa misingi ya UDINI.

Hivi ni nani hasa anayehubiri watu wapige kura kwa misingi ya Udini? sote tunafahamu kuwa hii itakuwa dhambi kubwa kabisa kumrusu mpotoshaji yeyoye kutumia dini kama kigezo cha kumpata mtawala hata katika ngazi ya Udiwani. Ni imani yangu kwamba Dk JK angekuwa ameitendea haki nafasi yake kama mgombea uraisi na raisi anayemaliza muda wake kwa kupeleka malalamiko yake kwenye tume ya maadali ya uchaguzi ambayo imepewa mamlaka ya kufuatilia mienendo ya kampeni za vyama vya siasa.

Ni ukweli usiopindika kuwa Tanzania ni ya watanzania (KWANZA) ambao wametokea kuwa itakadi tofauti tofauti za kiimani, na tunapoongela masuala yenye maslahi ya nchi ni vyema basi tuheshimu Utanzania wetu KWANZA.

1. Uchaguzi huu si wa Raisi bali niwaviongozi wangazi tofauti hivyo mtazamo wa UDINI ni wa kibinafisi, wa kifisadi, wa kiwoga, wa kishamba, wa kijinga na unadhirisha kulenga maslahi wa kikundi flani tuu cha watu wanaoitizama Ikulu kama dili.

2. Kwenye nchi tajiri na watu masikini kama tanzania itakuwa ni aibu leo nipige kura kisa eti yule ni dini yangu!!, kama dini yako ni nzuri sana mbona bado maisha yako hayabadiliki (siizungumzii kiimani), mbona huwezi kumsomesha mwanao kwenye ile shule bora, mbona kipato chako si endelevu, mbona hauna hata mradi utakao kusitiri baada ya ile kazi yako kwisha etc. Watanzania hatujafika hapo bado ila tunapelekwa tu.

3. Ombi langu kwa watanzania wenzangu na wanamageuzi kwa ujumla, huu ndio wakati wetu na hii ndio nafasi yetu kuwapeleka watanzania wote (Arusha mpaka Zanzibar) kwenye maendeleo ya kweli mbali na siasa za maji safi na zahanati buu haswa kwenye karne hii ambayo dunia inatafiti kama mwanadamu anaweza kuishi kwenye sayari ya Mars.
 
Sishangai leo hii yaarifiwa kuwa katika misikiti mingi ya hapa jijini ukiwemo wa Manyema kwa Sheikh Jongo wamemmpigia debe mh, Jakaya Kikwete katika misingi ya udini waziwazi ingawa inaeleweka wazi kuwa Sheikh Jongo ni CCM damu nanadhani kati ya watu wanotumika sana na CCM.

Hhii inatokana na kuona kuwa hata kama watashinda basi ni kwaasilimia ndogo hivyo CCM wameamua kutumia misikiti kumpigia debe mh, JK lakini wakumbuke kuwa siasa hizi ndizo chafu tume itanasemaje juu ya hilo? yaani afadhali ya kakobe alichokizungumza katika hotuba yake kwa wauumini hawa jamaa wanasema wazi wazi lakini wanasahau kuwa hata Lipumba ni mwislamu je wanamtenga au hastahili mbona hawamsemei au kumwombea kura? Hapa ndipo utakapogundua kuwa shekhe jongo na wenzake ni watu wanaotumiaka na CCM.

Lazima jamani wa tanzania tutambue kuwa huu si uchaguzi wa kiongozi wa kanisa wala msikiti hii ni ghiliba ya CCM wanaona wamebanwa ishu si udini mbona ni uchaguzi wa kumapata kiongozi bora anayekubalika.

Wanachokifanya CCM ni kuwagawa watanzania kupitia dini zao ili wapate ushindi hawa jamaa hatari!!! Wakati CUF ina nguvu walisema ni chama cha udini leo Slaa wanasemaanapigiwa debe na kanisa wana hila, safari hii watanzani hawatakubali ghiliba zaotutachagua mgombea anayefaa kwa maana ya kukubaliwa na watanzania kimewatisha cha juzi Slaa kupata mapokezi makubwa huko Kanda ya Ziwa kwani inasadikia umatiule haujawahi tokea? Mchezo wa kujaza wabunge wengi wa CCM bungeni wakabebane katika maovu ni hatari kwa afya ya Tanzania.

Ttuwaaaibishe katika hili na viongozi wa dini eendeleeni kuwaelimisha wauumini wenu wachague viongozi safi na si chama au kwa stahili hii ya leo kina Jongo, waumini msifanywe bendera fuata upepo hawa wakina Jongo na wengine katika makanisa kama mzee wetu Kulola wamekula dili tayari wanahesabu yao kulola hakukurupuka bali katengenezwa hali mbaya mwanza kule ni ngome kubwa ya CCM imetobolewa, hii ni baada ya Dr Slaa kupita hivi majuzi CCM wanatetemeka wanahisi serekali ya mseto yaja na bara ni kweli itakuja labada waibe kura watu wanataka mabadiliko wamechoka bunge raba stempu za wanachama wa ccm wanata kupitia kwenye udini unaotengenezwa na ccm ndiostahili zao hawa jamaa kuweni macho.

Yaani Sheikh Jongo anaseama kuwa "viongozi waliowahi kuwa masheikh au mapadri wasipewe nafasi kwani wataleta udini" unaona janja yake hii ni mmoja yanukulu, unaona janja yake unajua jama kapita vijidarasa kidogo

:A S 39:
 
Kura hazitaibiwa kwa sababu tutazilinda kw nguvu zetu zote. Udini unataganzwa na KIKWETE na historia inamhukumu kwa sababu yeye alipewa ubunge wa kuteuliwa kwa sababu Hayati Kigoma Malima alimwomba Mwinyi asaidie kuinua vijana wa kiislaamu kuingia serikalini, baada ya hapo ofisi za serikali zikawekwa misikiti, wakati serikali haina dini.

Kwa uroho wa KIKWETE kubakia kwenye madaraka haoni jambo lolote baya kuwatumia watu wala rusha kama askofu Kulola toka mimi nikiwa mdogo wa shule ya msingi namkumbuka Kulola kuwa mchungaji mwenye upako na uponyaji hiyo karama iliondoka baadayeye kujiingiza katika utapeli mkubwa wa kuwaibia wanachi haswa wasukuma akiwahidi kuwapeleka marekani kusomea uchangaji watu walimwamni wengi wakauza ngombe zao ili watoto wao wakasome marekani walipomdai fedha zao aliwatishia angewaombea kwa mungu walaanike wakaogopa wakamuacha na fedha zao.

Alisababisha mtafaruku mkubwa mpaka umoaja wa makanisa wa TAG ukavunnjika na yeye kwa uroho wake akabaki na EATG kwa hiyo hana moral authority wa kumnyoshea mtu kidole ndio maana amepuuzwa hata na umoja wa makanisa ya kikristo hapa nchini kwa sababu ni kibaraka cha watawala.

Hata afanye nini wanachi wameamua wa dini zote waislamu kwa wakristo kwamba mwaka wa mabadiliko ni huu hakuna wakati mwingine tena tukikosa nafasi hii tutakuwa tumeweka rehani nchi yetu kwa mafisadi
 
Ndiyo maana wenzake wenye akili Mkapa na Mwinyi wamemsusa with his religious campaigns. Lakini Mkapa na mwinyi wanatakiwa wamkane na kumwonya Kikwete hadharani because he is taking the country in the direction of civil wars. Wakifanya hili sisi wananchi tutamsamehe Mkapa na madudu yake kwa vile watakuwa wameokoa nchi yetu. Tutamwambia President Dr Slaa amsamehe kama watamkanya Kikwete siku mbili hizi hadharani kabla ya uchaguzi aache mara moja kampeni za udini.
 
Kura hazitaibiwa kwa sababu tutazilinda kw nguvu zetu wote
Udini unataganzwa na KIKWETE na historia inamhukumu kwa sababu yeye alipewa ubunge wa kuteuliwa kwa sababu Hayati Kigoma Malima alimwomba Mwinyi asaidie kuinua vijana wa kiislaamu kuingia serikalini ,baada ya hapo ofisi za serikali zikawekwa misikiti,wakati serikali haina dini
Kwa uroho wa KIKWETE kubakia kwenye madaraka haoni jambo lolote baya kuwatumia watu wala rusha kama askofu Kulola toka mimi nikiwa mdogo wa shule ya msingi namkumbuka Kulola kuwa mchungaji mwenye upako na uponyaji hiyo karama iliondoka baadayeye kujiingiza katika utapeli mkubwa wa kuwaibia wanachi haswa wasukuma akiwahidi kuwapeleka marekani kusomea uchangaji watu walimwamni wengi wakauza ngombe zao ili watoto wao wakasome marekani walipomdai fedha zao aliwatishia angewaombea kwa mungu walaanike wakaogopa wakamuacha na fedha zao
Alisababisha mtafaruku mkubwa mpaka umoaja wa makanisa wa TAG ukavunnjika na yeye kwa uroho wake akabaki na EATG kwa hiyo hana moral authority wa kumnyoshea mtu kidole ndio maana amepuuzwa hata na umoja wa makanisa ya kikristo hapa nchini kwa sababu ni kibaraka cha watawala
Hata afanye nini wanachi wameamua wa dini zote waislamu kwa wakristo kwamba mwaka wa mabadiliko ni huu hakuna wakati mwingine tena tukikosa nafasi hii tutakuwa tumeweka rehani nchi yetu kwa mafisadi
 
Itakuwa poa sana kama katika ibada ya Jumapili hii katika makanisa mbali mbali nchini Dr Slaa atapigiwa debe la nguvu sana kwamba ndiye anastahili kupewa ridhaa na Watanzania ya kutuongoza.
 
Itakuwa poa sana kama katika ibada ya Jumapili hii katika makanisa mbali mbali nchini Dr Slaa atapigiwa debe la nguvu sana kwamba ndiye anastahili kupewa ridhaa na Watanzania ya kutuongoza.
Hivi mnaona sifa sana kutangaza Udini? Hivi kweli mnafurahia hali hii ya kisiasa kwa sababu ya hao Mashekh ambao pia wanadai wameifkia maamuzi hayo kwa sababu Dr.Slaa anapigiwa debe makanisani.

Jamani eeeh mkienda misikitrini na makanisani na mkamsikia mchunguji au sheikh akileta habari za uchaguzi huu tafadhali mpigeni kofi la kerbu!.. Hatuwezi kuwa na akili za kushikiwa kwa sababu tu CCM wanaendesha siasa hizi hali wanajua fika kwamba hawana silaha nyingine isipokuwa kutumia Udini wakijua fika kwamba hesabu zao zinakubalika kuliko Chadema. Nitazidi kuwatahadhalisheni kwamba CCM mbali na kuwa na rais Muislaam, wamesimamisha zaidi ya asilimia 75 wabunge Wakristu, wana mawaziri wengi wakristu na hata wakuu wa mikoa hivyo kwa mwenye kufikiria akianza kuitazama Chadema kwa jicho hilo atachukulia kwamba Chadema ni wadini kweli wakiongozwa na Dr.Slaa. CCM wanachotaka ni wananchi kutazama watu ndani ya Chadema na sio tena sera zao au uwezo wa Dr.Slaa kwa sababu hawana turufu huko..

Kumbukeni tu kwamba sii Wakristu wote wanapenda Udini na hakika mkianza kuendesha kampeni makanisani kumchagua Dr.Slaa basi CCM watatumia kampeni hizo zaidi kuonyesha Udini wa Chadema na mtakuwa mmehakiki dhana yao. CCM ni Chama kubwa kama Taifa kubwa la Marekani ambao huwachokoza waarabu na kuwaita Waislaam mashetani, hivi na vile wakijua fika Waislaam watakuja react..Na waarabu wasivyokuwa na akili hu react kweli hapo hapo ndipo Marekani huwaonyesha dunia kwamba - mnaona jinsi waarabu na waislaam walivyokuwa ma terrorist?

Hii ndio mbinu ya CCM hivi sasa, wanakulisheni wakisubiri mtakuja ingia wenyewe pasipo kujua wao wanalenga kitu gani..
 
Itakuwa poa sana kama katika ibada ya Jumapili hii katika makanisa mbali mbali nchini Dr Slaa atapigiwa debe la nguvu sana kwamba ndiye anastahili kupewa ridhaa na Watanzania ya kutuongoza.

Tatizo viongozi wengi wa dini ni waoga ambao wakitishwa kidogo tu wanakaa kimya,mbona 2005 tulimchagua jk bila kujali udini wake?leo hii wameona slaa ananguvu ndo wana washauri viongozi wa dini hadi kuchukua rushwa ili wawasifie kuwa wanastahili?

Atakae chukua rushwa kwa ajili ya kumpigia jk kampeni na bado ni kiongozi wa dini ajue amejiweka kaatika nafasi ya yuda eskarioti!
Nieleweke kua me sio mtu wa kutenga watu kwa dini zao ila huu udini wanao uleta ccm unanifanya nisikitike sana
 
Tumepotoshwa na kupumbazwa: Shina na mgawanyiko unaoinyemelea Tanzania si kama inavyoonekana. Haiwezekani tukagawanywa kwa Ukabila, Dini zetu na rangi zetu. Hiyo si kweli kwani hali hizo tumekuwa nazo tangu kuasisiwa kwa Taifa hili. Tumetengenezwa na kupotoshwa kuona na kuamini hivyo. Inabidi tuamke.

Tufunguke macho na tusonge mbele kwa kujiuliza. Ule umoja wetu wa Kupambana na ufisadi tuliouonyesha hivi karibuni kama taifa utasongambele vipi kama tutakuwa sasa tunapambana kwa itikadi za vyama, udini, ukabila na rangizn etu? Nasema tunapumbazwa waziwazi lakini hatutaki kuona. lakini itabidi tuamke na kuona kama tuanataka umoja wa Kitaifa.

Nani ajitokeze aniambie Mafisadi, wataathika kiasi gania pale Mkiristu akinyukana na muislamu au kabila moja na lingine linapopambana kwa mawe na kaila aina ya silaha?

Nani ajitokeze sasa hivi, aonyeshe wale mafisadi papa wakijitokeza kuzima chuki za kidini, za kikabila, za kichama, za kubaguana kwa rangi nk?
 
Kwa hiyo tatizo ni nini maana umetuacha tunaelea tu? Mimi nafikiri tatizo ni CCM kuogopa kupoteza madaraka. Natumaini Mkristu na Muislam tutaendelea kuheshimiana na kuishi kama zamani...Kikwete has to go first
 
Unaelea nini? Tatizo sio chama chotechote, wala dini yeyote ... kuona hivyo kunamnufaisha fisadi yeyote aliyekubuhu ... maana alitakauone hivyo... ni swala la kuelewa kidogo tu!
 
Kwa hiyo tatizo ni nini maana umetuacha tunaelea tu? Mimi nafikiri tatizo ni CCM kuogopa kupoteza madaraka. Natumaini Mkristu na Muislam tutaendelea kuheshimiana na kuishi kama zamani...Kikwete has to go first

SAFI nakubaliana nawe kwa hilo ulilo lisema kuwa tatizo ni CCM kuogopa kupoteza madaraka, kwanini Ukijiuluza sekeseke hili lote ni la nini watukuhamia upinzani ni kuwa Uongozi wa CCM umekumbwa na mapungufu mengi sana mwanzoni wananchi walikuwa na imani sana na Rais JK na mawaziri wake wakawa ndio wamepoteza imani kabisa na wananchi na sasa kibao kimegeuka kabisa kuwa watu wengi wamepoteza imani na serikali iliypo ikiongozwa na viongozi wa CCM huko Juuu.

Kuto ilinda katiba na kuitetea katiba uliyo apishwa nayo ni makosa makubwa hata kama inamapungufu yake, Pili zile sheria zilizowekwa na kufuatwa nazo ukazikiuka hapo ndipo kabisaaa wananchi unao watawala lazima wapoteze imani nawe na ndilo linalo tokea kama Rais unatakiwa uwe mkali kama sitta alivyokuwa akimwambia JK kuwa mkali kidogo maana yake fuata japosheri za nchi uone kama watu hawato rudi kwa mstari yeye JK akapuuzi sasa matokeo yake ndio hayo hata wanachama wengi wa CCM wameisha choshwa na bla bla hili liko wazi kwani tathimni wanazo na wanajua nanndio maaana huu uchaguzi ulitakiwa uwe mwepesi kwani rais aliyeko madarakani anafahamika na anaomba lidhaaa ya wananchi kwa mara ya pili kwanini inamgharimu pesa nyingi kurudi IKULU?? liko wazi hilo utendaji kazi wako hapo IKULU wananchi hawajaridhika nao esp kwa viongozi wako wa chini kuanzia mawaziri ndi wameku let down kabisaaaaa hamkuja na strategy za kulikwamua Taifa kutoka kwenye umaskini.

Kwamini navyoelewa ndio IKULU ni Mzigo ila unapoingi twajua utakuta majukumu ya mwenzio aliye kutangulia kayaacha bali mwatakiwa kuwa na Strategic Plans A,B,C even D kwa maendeleo ya nchi hata Dr. Slaaa nae akiingia pale asitegemee atapakuta sawa kuna mambo mengi sana na madudu mengi sana ya viongozi walio pita jamani. ni jinsi utakavyojipanga na serikali yako.

Kwahiyo matatizo yako mengi tuuu na jingine kubwa ni Miiko ya uongozi kutofuatwa Azimio la Arusha kupuuzwa ndipo hapo mambo yalipo haribikia unajua kuna mambo ni yakurekebisha tuu sasa kama viongozi walioko madarakani hawalioni hilo na kupotezea Alama za nyakati kwa manufaaa yao jamani nchi bila future strategic plan haitokwenda hata kidogo, ifike sehemu tukubakubali democrasia ya kweli kwa taifa letu kwanza

 
Jethro,

Nimeheshimu na kuelewa vema maeelzo yako! lakini sijaona wapi umeainisha, kama ni kweli tatizo la watanzania leo likubalike na kushughulikiwa kama ni Dini na ukabila?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom