Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Akiwahutubia akinamama huko Kigoma, Mama Kikwete kwa nyakati mbili tofauti amezungumzia juu ya wafanyao kampeni za uchaguzi kwa kutumia udini na ukabila kuwa ni hatari kwa amani ya nchi.

Bila kukitaja chama, NGO au watu binafsi alionekana kuguswa sana na hilo swala na alijua kuwa akina mama ndio karata yake ya mwisho katika kulipuuzia hilo na kudumisha amani.

Swali kubwa la kujiuliza hapa, HIVI MAMA KIKWETA ALIDHAMIRIA KUWANYOOSHEA KIDOLE AKINA NANI? CUF, CHADEMA, NCCR, CCM au TLP?

Hiki ni kitendawili ninachowaomba wenzengu hapa JF tutatue bila upendeleo. Natanguliza shukrani zangu za dhati.

Je, Urais ni suala la kifamilia aliwaambia?
 
Hivi wewe una mtindio wa ubongo au kitu gani? Kwa taarifa yako, huyu mama Kikwete hapendwi (aka siyo popular kabisa) humu ndani na almost hakuna anayetilia maanani kauli zake za kisiasa. Huu ni siyo nini wala chochote bali ni uchokozi wa wazi! Heshimu hilo ewe mdada na wewe na Mujahidina wenzako mtupishe na upuuzi wenu!!


Mbona umekuwa mkali sana mshkaj kwa dada wa watu, kwani yeye hana uhuru wa kuweka maoni yake?, sasa hapo mwenye mtindio wa ubongo ni yeye au wewe usojua kuchuja cha kujibu watu? shame on u!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Udini hauna nafasi kwa chama chochote. Kama mama Kikwete amezungumzia hilo ni ujumbe tosha kwa mtu yeyote anayehusika regardless.

Ahsante Mkandara,
Tunatakiwa kujiepusha kwa nguvu zote udini, ukabila na hata ushabiki kama wa Simba na Yanga kwenye mambo yote yanayohusu uchaguzi.
Lazima tujenge misingi imara ya umoja na mshikamano tukijua kwamba maadui wa uma watajaribu kutugawa ili waendelee kutunyonya kwa ufisadi, wizi kwa kushirikiana na wageni, mikataba ya kiMangungo n.k.
Yeyote yule anayepinga mgawanyiko analitakia mema taifa letu, hata hivyo ni muhimu kuhamasisha watu waungane kupinga mambo yanayowarudisha nyuma kimaendeleo kwa kuchagua viongozi watakaoyaondoa.
Ni aibu na laana kubwa kwa watanzania kuchagua viongozi kwa ushabiki kama wa Simba na Yanga!
 
Hivi Mama Salma na kampeni zake zinaunini ndani yake? Na watoto wake wanalilia nini na hizo sms zilizozagaa nchi nzima kumshutumu Dr. Slaa?

Mama Salma akemee hizo sms na amkemee mumewe kwa kuzungumzia umwagaji wa damu na kuugeuza ndiyo ni mtaji wa kisiasa
 
Hivi wewe una mtindio wa ubongo au kitu gani? Kwa taarifa yako, huyu mama Kikwete hapendwi (aka siyo popular kabisa) humu ndani na almost hakuna anayetilia maanani kauli zake za kisiasa. Huu ni siyo nini wala chochote bali ni uchokozi wa wazi! Heshimu hilo ewe mdada na wewe na Mujahidina wenzako mtupishe na upuuzi wenu!!

Suala hapa si kuwa popular, kupendwa au kutopendwa. Suala ni point iliyozungumziwa- kama kuna chama kinatumia udini kama mbinu ya kuingia ikulu ni wakati muafaka wa kuwaamsha masikini.

Napenda kukufahamisha kitu kimoja; hata Hitler anayechukiwa ulaya nzima lakini kuna moja wana uchumi wote wa ulaya wanakubaliana, KUWA ALIKUZA UCHUMI WA UJERUMANI KWANI WAKATI ULE UJERUMANI ILIKUWA KTK HALI MBAYA YA KIUCHUMI. Hata hili gari unalolisifia leo 'VW-Volks Wagen' lilianzishwa kwa mawazo yake kuwa ni gari la wanyonge (la bei ya chini). Volks Wagen ni kijerumani maana yake ni 'Peoples car'.

Kwa maana hiyo naomba uangalie point iliyozungumzwa na sio sura, urefu, rangi, kabila, dini na jinsia ya mzungumzaji. Asante kwa kunielewa!
 
pia ingekua vizuri kama angewaweka wazi kinamama wa kigoma kuhusu swala la familia kuitawala nchi
 
Mwacheni mama wa watu ale maisha, alianza siku nyingi kuitafuta ikulu. Uzuri wa akina mama wa kibantu hawapendani , wanaomkubalia anachosema ni wale wa UWT tu wengine wote wanamyeyusha. First lady kula maisha OCTOBER 31 siyo mbali Slaa anaweza kuja kuwapokea usukani
 

Jenerali Ulimwengu naye hakuwa nyuma kukemea mnukio wa udini pale UCHAGUZI UNAPOKARIBIA. Hebu tumnukuu huyu Jenerali:

"Religion has never been based on rationality - ask Copernicus or Galileo - and that is why it is always accompanied by cocksure intolerance wherein whoever does not agree with your particular brand of opiate is, of course, destined to be consumed by Giga-centigrade hellfire. It is a matter best left to the believer.

When religious bigotry worms its way into the bosom of the body politic, it develops an unbelievable capacity to engender emotions that will destroy whole communities and sunder whole societies, as we have witnessed in Nigeria only recently.

So why are elements in Tanzanian politics bent on sneaking this thing into the centre of political discourse every time there is an election?

Time was when it was about Ibrahim Lipumba and CUF being a Muslim plot.

Well, seeing as CUF originates from Zanzibar, it surely can have no shortage of Muslim supporters.

Now it is about Willbrod Slaa and Chadema being a Catholic conspiracy."


Sasa
wanyonge tunajiuliza hivi Mama Kikwete na Jenerali ulimwengu wanatoa jumbe nzito kama hizo wamehisi nini au wameshuhudia nini. Na nini wanachotabiri kitatokea kama tahadhari hizo hazitachukuliwa hatua.

Well, Jenerali kazungumzia yaliyopita yalimkumba Prof Ibrahim Lipumba, na sasa hivi anamgusa Wilbroad Slaa Hivi yeye ndio mlengwa safari hii katika tuhuma hizo?
 
Hapa mama Salma alikuwa anamlenga mumewe, JK, kwa kuazimia kuanzisha mahakama za Kadhi na kuiuza nchi kwa magaidi ya kiarabu/kiislamu kupitia OIC!
 
Jamani Mods msilale hali ni mbaya JF, fungeni utitiri wa threadi zote za udini. Tunataka threadi zinazojenga utaifa.
 
Unaogopa kujadili ukweli................kwa nini ukweli usijadiliwe?....kitu gani unataka kuficha kupitia udini?..........kwa nini kiongozi wa nchi awe tayari kutetea dini yake kwa vitendo na kwa nini km iko hivyo tusijadili basi wkt anataka kuleta machafuko nchini?.....utajadili lini? Baada ya machafuko?..............tujadili ukweli tuache woga
 
unaogopa kujadili ukweli................kwa nini ukweli usijadiliwe?....kitu gani unataka kuficha kupitia udini?..........kwa nini kiongozi wa nchi awe tayari kutetea dini yake kwa vitendo na kwa nini km iko hivyo tusijadili basi wkt anataka kuleta machafuko nchini?.....utajadili lini? Baada ya machafuko?..............tujadili ukweli tuache woga

dini zimefanya waafrika kuwa mazezeta.
 
ndio, kwani tukijadili mara waislam watafungiwa na kuitwa wadini huku waumini wa dini nyengine wakipeana thanks.
Kwani huu udini wanauanza wao halafu hao hao ndio wanalalamika.
Hasa jel 72

ms,
hivi ninyi na akili zenu bado mnapoteza muda na mambo ya dini katika maslahi ya nchi? Hivi ninyi wakristo na waislamu mnawashwa na nini? Mnadhani tz ni yenu tu? Mnaendekeza ujinga.
 
Religion is what keeps the poor from murdering the rich.
 
ndio weye weye mwenye dini inayotakiwa humu jf

Suala si dini inayotakiwa humu. Suala ni kuwa na makamasi kichwani. Ukiwa Mkristo au Muislamu halafu unaenendekeza haya mambo kichwani unkuwa na makamasi badala ya ubongo.

Waafrika tunatoka katika kundi la wajinga tunaingia katika kundi la wapumbavu.
 
mi sioni haja ya hizo thread kufutwa maana zimejadiliwa na wanajf
 
mi sioni haja ya hizo thread kufutwa maana zimejadiliwa na wanajf

Lakini nini faida yake katika maendeleo ya taifa? Huoni ni upuuzi kuendeleza dhana kuwa Tanzania ni ya Wakristo na Waislamu? Afrika imejaa watu wasioweza kufikiri kwa akili zao, ndo hawa wanaopoteza muda kujadili mambo ya kijinga kabisa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom