Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

Mkuu Ruta unatuchanganya kwa misimamo yako.kwenye thed yako ya nyuma ulijaribu kutuaminisha kwamba ccm inajukumu la kutuletea raisi bora 2015 maana vyama vya upinzani havijajipanga kushika dola. Leo unakuja na uchambuzi wa bajeti kwa kuponda chama ambacho awali ulidai kimekomaa kuongoza nchi..kwa hiyo bado unamsimamo kuwa ccm inaweza kuwa na mbinu mbadala kumwokoa mtanzania kutoka kwenye tope la ufukara.?
 
Rutashubanyuma Nimependa ulivyoona mzigo wa huyu mwenyekiti wa CCM ambaye ndie Raisi wa nchi hii , si ulisema huyu mtu ambaye hana uwezo wa kusafisha nyumba yake anawezeje kutuachia au kutuchagulia Raisi atakaye faa,Ruta nakuuliza kwenye thread yako huko nyuma uliona huyu mtu anatufaa,Raisi Kikwete kazi imemshina na tusitegemee muujiza kwamba kutakuwa na mapinduzi ya kiuchumi nchi hii,wageni watatajirishwa mara elfu kumi wazawa watadhulumiwa hata ile senti ya mwisho.ahsante sana kwa kutunyambulishia mapungufu mengi ambayo yamekuwa somo zuri kwetu
[MENTION]
Froida[/MENTION] JK naye ni mradi na nikwishauponda sana humu ndani jamvini....................mimi siyi shabiki wa JK naamini hukunielewa..............................nilchokuwa napigania tujitambue kuwa mfumo wa utawala tulionao ndiyo chanzo cha umasikini wetu na wala tusikubali kuwa watumwa wa vyama vya siasa ambavyo mifumo yao ya kiutawala na kiuendeshaji ni ileile...........................
 
Mkuu Ruta unatuchanganya kwa misimamo yako.kwenye thed yako ya nyuma ulijaribu kutuaminisha kwamba ccm inajukumu la kutuletea raisi bora 2015 maana vyama vya upinzani havijajipanga kushika dola. Leo unakuja na uchambuzi wa bajeti kwa kuponda chama ambacho awali ulidai kimekomaa kuongoza nchi..kwa hiyo bado unamsimamo kuwa ccm inaweza kuwa na mbinu mbadala kumwokoa mtanzania kutoka kwenye tope la ufukara.?

idawa mimi siyo muumini sana wa vyama vya siasa bali ni ninaamini kwenye kuboresha mifumo ya kutawala ili iwajibike zaidi kwa wananchi.......ccm nilichosema kama itarekebisha utaratibu wake wa kumpata raisi inaweza kutoa Raisi bora lakini nilisema hata upinzani wa kufanya hivyo kupitia presidential primaries wanaweza kutupa Raisi bora.................Sijawahi kutoa a ringing endorsement kwa ccm kama ulifikiria hivyo ni kuwa labda sikueleweka...........
 
Last edited by a moderator:
Wakuu Mimi huwa sioni umuhimu wa Tz kusoma bajeti na Kikao cha bunge la bajeti kwa Sababu zifuatazo...
1. Vikao vyote havichambui bajeti iliyopita Kuona mapungufu na wapi wajipange zaidi...

2. Maeneo yenye kodi za kutosha Kama Madini, viwanda na telecom industries hayaguswi na Mkazo siku zote huko kwenye bbidhaa za walalahoi Kama sigara, bia na soda.
3. Bunge linakuwa ni rubber stamp na Hakuna mabadiliko yoyote zaidi ya watu kupiga kelele kisha wanaunga mkono hoja 100%
ki ujumla bunge la bajeti ni kupoteza hela za mlalahoi....

muonamambo....nimeafiki una kiona mbali
 
Last edited by a moderator:
Nilichoki-note jana kwenye hotuba ya Mgimwa ni kuwa, alikuwa akisoma kitu ambacho amepewa tu asome. Hakujiandaa ipasavyo ku-present budget effectly, there was alot of noisy (hapa naamina noisy in communication siyo kupiga kelele kwa wabunge, bali ni kushindwa kufikisha ujumbe effectively). Nilishangaa pale anaoposema 'utekelezaji huu unaanza mara moja'- baada ya miguno ya wabunge then akarudia kutafuta sehemu kujiridhisha na kujisahihisha kuwa unaanza trh 1/7/2012.

Kwanza ningependa kufahamu udaktari wake ni nini hasa?, wanyama?, binadamu? au philosophy?, kama ni philosophy basi atakuwa amewashusha madaktari wengi sana kwa poor presentation. Hapa naongelea presentation siongelei substance.

Hofstede umenikumbusha jambo jingine ambalo nilikuwa nimelisahau presentation.....it was awful
 
Last edited by a moderator:
Kwa Bajeti hii Wa-Tz wanaofurahia ni wale wanaopokea posho na wanaowategemea tu.
Kyaiyembe hakuna ubishi kwenye hilo.....ni kunenepesha na kuvikarabati vitambi vyao tu.............visiyeyuke
 
Last edited by a moderator:
Jamani huyu jamaa mimi kwa kumuangalia tu simpendi!!, sidhani kama ana jipya huyu!!, walewale tu!!. anachekelea kwamba ni zamu yake kuiba.

BIG Banned tungelikuwa tuna sauti na huu uteuzi wa hawa waheshimiwa wengi tayari tungelikuwa tumewalima red card..............na wangelikuwa wamefungasha virago vyao...........
 
Last edited by a moderator:
Inasikitisha kuona kwamba bakeries imetenga asilmia 30 kwa shughuli za maendeleo wakati matummizi ni 70 %
 
Froida JK naye ni mradi na nikwishauponda sana humu ndani jamvini....................mimi siyi shabiki wa JK naamini hukunielewa..............................nilchokuwa napigania tujitambue kuwa mfumo wa utawala tulionao ndiyo chanzo cha umasikini wetu na wala tusikubali kuwa watumwa wa vyama vya siasa ambavyo mifumo yao ya kiutawala na kiuendeshaji ni ileile...........................
Kwa sasa hivi tukitaka kuvuka 2015 lazima tuhakikishe watu wengi tunaikataa CCm kwa sababu ndio mfumo uliopo wa kuendesha serikali kupitia vyama vilivyoshinda lakini tukitanguliza utaifa mbele kwa kuamini tutakao wasimika tutaweza kutengeneza nyenzo za kuwadhibiti ili wajue kwamba waajiri wao ni wananchi sio kama ilivyo sasa CCM imeoza mwanzo mwisho imepoteza dira haina tena fikra za kuiongoza serikali yake kuweza kujenga uchumi imara ukweli CCM na serikali yake wanadhalilirisha nchi
 
kwa sasa hivi ualimu grade 3A anapoanza kazi anaanza basic 215000/= sasa wanaopata kati 150 mpk 170 ni akina nani?
 
Ukitaka kuchambua sana mambo ya nchi hii, unaweza kujikuta unapata vidonda vya tumbo bure. Tatizo waliopo madarakani wenyewe ni kama visiki, wewe kapuku utaongea lugha gani ili waone sasa umetoa wazo la maana la kuwafanya wawajibike? Na humu JF kila siku zinatolewa hoja mhimu na makini na hawa viongozi wanazisoma, and they real dont care. Kwa ajili ya amani ya nchi, tupunguze tu ukali wa hoja angalau, hili jinamizi Kikwete lipite.
 
Kodi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yeyote duniani ILA matumizi ya ANASA kwa serekali yetu inapaswa kudhibitiwa

Dhana iliopo kwa sasa ni kukusanya kodi na kuongeza maisha ya anasa kwa viongozi wa serekali yetu na washirika wao kibiashara.
 
Nimechoka kabisa mimi Mtanzania!! Ni kwanini serikali imeamua kuwamaliza walalahoi? Hakuna nafuu ya maisha kabisa. Mungu atusaidie, kinachoniumiza, pesa zinazokopwa zinakwenda wapi???
 
Ama kweli bajeti itazama na kama haitapewa angalizo itakula kwetu wanyonge.

FREEDOM IS COME TOMOROW:bange::bange::bange::bange::bange::bange::bange:
 
Only 30% are Development Expenditures and 70% Recurrent Expenditures, Hapa waweza ona ni kwa jinsi gani gharama za kuendesha Serikali ni makubwa sana. Hapa hata ukeshe hutapata maendeleo Tanzania wangu hebu badili upepo toa makapi weka wenye kulipa fadhila jamii sio mahawala zao kuwapa Ubunge, Ukuu wa wilaya na Kuwasomesha Uingereza.
 
Naomba kukuuliza mheshimiwa yafuatayo:
i. Kwani Mh. Waziri kaandaa hiyo bajeti peke yake?
ii. Wataalamu wa wizara ya Fedha, BOT, Mashirika ya Fedha nk hawakuhusika?
iii. Je ana muda gani hapo HAZINA hata tumtoe makosa kupitia bajeti aliyokuta imeandaliwa?.
iv. Mwisho usisahau ni mara ya kwanza yeye kusimama Bungeni na kupewa jukumu kubwa kama hili. It is obvious anaweza kuwa ametetereka ktk kuongea na kuwasilisha mada. Hilo lisitufanye tuendelee kumuona hafai.
v. Watanzania wenzangu safari ya ukombozi wa Mtanzania bado ni ndefu hivyo nasisitiza tumpe muda anaweza kuwa Daudi aliyemuua Goliati. Tupunguze negativity kubwa tuliyonayo inayosababisha upofu hata yaliyo mazuri hatuyaoni wala hatutayaona tukiendelea hivi. Tumuombee yeye na viongozi wengine watuongoze vizuri na kwa uadilifu, pia na tuiombee Tanzania yetu, nani ajuae Daudi amepatikana?
Queen Esther

Ignorance of the Law is not an excuse, hakuna kumtetea eti kwa kua ni mara ya kwanza
 
Rutashubanyuma, There is nothing we can do in between. This is it trust me. Maana mageuzi gani yatakayofanyika yenye uwezo wa kubadili mwelekeo? Wakati si lazima suluhisho liwe limetoka chadema, changamoto yetu ni kupata presidential material wa ukweli....Awe ametokea wapi si hoja kubwa kama uwezo wake wa kuongoza
Bila mfumo kubadilika hata ubadili madereva kiasi gani gari ni mbovu hatufiki, wanatawala kwa mazoea si kwa ubunifu tunataka wabunifu tusonge mbele waoga wa mabadiliko watafuata mkondo
 
FJM ninaafiki nawe ya kuwa kumpigia mtu debe hakuna shida kama content yake ni kuboresha lakini hapa ina shida kwa sababu waziri wa fedha ni mbumbumbu kabisa wa matatizo yetu na huyu kama wale waliomtangulia atakachoweza ni kutuongezea dhiki na maumivu tu huku akilinda kitumbua chake kwa kuelekeza miradi ya maendeleo kwa Pinda na Makinda, Anne.................

Ruta, tusibiri bajeti za wizara, ule mkoa mpya wa PM wenye wilaya 2! na Njombe kwa Makinda.
 
Back
Top Bottom