Ni Mwanamke gani mwengine anaeweza kumfikia huyu ?

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Ndugu zangu wanabodi,
katika mazingira yasiokua yamezoeleka sana, mama mmoja mwenye kumiliki mtoto mmoja na mume.
Siku hiyo ilikua mwanae wa mwaka mmoja alikua anaumwa, mida ya kama saa 3 hivi za usiku alimpa mwanae dawa na akamlaza.
Ilipofika saa 5 usiku akatoka kitandani kwake na kwenda pembeni kilipo kitanda cha mtoto kumuangalia kama body temperature imeshuka.
Mungu aachwe aitwe Mungu , kwani alikua ameshachukua amana yake ! Amana ya uhai wa mtoto.
Mtoto amefariki !
Mama alimfunika marehemu vizuri , hakukubaika wala kutetereka japokua alikua na machungu makubwa moyoni. Na dakika 5 badae mumewe akawa anabisha mlango.
Alimfungulia mumewe huku akimuona Mr akiwa na dalili zote za kwamba usiku huo anahitaji game.
Mwanamke yule kwa kua alikua ameshiba na kupevuka kiimani akajiongeza kua akithubutu tu kumueleza mumewe kifo cha mtoto, basi taharuki litakalozuka hapatatosha na hapatakua na game wala nini .
Kwani mwanamke yule alikwishajilisha neno la kimsimamo kwamba Kifo ni haki toka kwa Mungu , na kumpa unyumba mumewe ni haki pia iliyotolewa na Mungu .
Hivyo alimudu kutokumpa mumewe habari ya msiba wa mtoto, na akampa huduma ya unyumba mumewe.
Baada ya kumpa mumewe haki ya nyumba, akampa wasaa mumewe kupumzika kama saa 1 hivi, na ndiyo akampa mumewe habari ya tanzia .
Katika dunia ya wakati tulionao tunao wanawake wengine wanaoweza kua na misimamo na uthabiti wakaweza kua kama mwanamke huyu ?
Hapa Jf pia wapo ?
 
Hapana, hapana, hapana! Mie hapana asee nna hakika sina huo ujasiri... Sina..
 
wanawake wa siku hizi wanathubutu kuwapangia wanaume ratiba eti jmosi tuu kwa kuwa j2 hakuna kazi!kwa mwezi mara 4 au 3
 
Back
Top Bottom