Ni muda wa kumuomba msamaha AFANDE SELE

binafsi sioni mwanga wowote kwenye bifu la kudumu....

matarajio yangu ni watu kufurahia kumalizika kwa mtafaruku huu... !Kwa sababu tu hapa cloud's media kuna kitu wamejifunza tena kikubwa sana...na as from now watachange policy yao....

fidia ya maralia no more ni haki yake!..ni mradi wake jamani...!mnyonge mnyongeni...
 
[h=6]Mgosi Mkoloni
drP8vlvSl_8.gif
Joseph Mbilinyi
[/h][h=6]TAMKO LA VINEGA JUU YA MAKUBALIANO YA SUGU NA RUGE
Leo hii tarehe 23 ya mwezi February, 2012 mida ya saa 1 usiku mpaka saa 5 na nusu usiku katika eneo la Mwenge Vinega wa anti virus tulikutana katika kufanya tathmini na kujadli maridhiano ya kumaliza ugomvi wa kimaslahi kati ya Kundi la Vinega na Redio Clouds pamoja na Bwana Rugemalila Mutahaba,katika kikao hicho tuliridhiana kutoa tamko hili kwa umma wote wa watanzania na wapenda maendeleo wote wa sanaa yetu.
"Ni kweli hakunaga Vita isiyo na mwisho lakini pia katika kila vita malengo ya msingi yanapaswa kuwa mbele na daima mbele...Harakati hizi za Anti virus zilipoanza wengi tulionekana kama wasaliti na wapuuzi,wahuni na kuonekana kama tuna wivu tu na mafanikio ya baadhi wa wadau ila daima tulisimama katika kweli na hatimae Umma/jamii ya watanzania ukasikia sauti na hoja zetu na kuona kweli tuna mambo ya msingi,Hoja zetu mbele ya umma ndio ilikuwa silaha ya vita hii ya Anti virus na wala si nguvu ya Propaganda na uzushi...Tumepiga makelele na hatimaeTaifa zima wakaona kweli hapa kuna hoja na zinapaswa kuzingatiwa na wala si ugomvi wa mtu mmoja bali ni harakati za kweli za kukomboa sanaa yetu na kuvunja ile mifumo ambayo siyo sahihi inayoendelea kunyonya jasho la wasanii wa Tanzania na kuwafanya kuwa mafukara na wasio na mategemeo na kupelekea kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya na hatimae kufanya mambo ya kihalifu.Sanaa hii kwa muda imekuwa ikihodhiwa na watu wachache na kujitajirisha na kuacha lundo la wasanii kuishi maisha mabovu.Dhamira yetu ni kumaliza kabisa mifumo hii mibovu ambayo tunaamini ikimalizwa msanii wa kitanzania ataweza kupata kipato na kujiajiri na kuendesha maisha yake sawasawa.
Sisi kama kundi la Vinega kwa niaba ya umma wa watanzania wanaotuamini na kutusikiliza tumeridhia mapatano ya kumaliza ugomvi kati ya Mh Joseph Mbilinyi (SUGU) na Bwana Rugemalila Mutahaba(ugomvi uliodumu kwa zaidi ya miaka 10 kabla hata ya anti-virus ikiwemo kutopiga nyimbo zake na kuporwa wazo la mradi wa malaria) ili kuweza kupiga hatua mpya katika kusaidia sanaa na pia kuonyesha dhamira yetu ya msingi kuwa, kwetu sisi ugomvi sio kati ya Sugu na Ruge bali ni mifumo mibovu ambayo imekuwa ikikumbatiwa na Bwana Ruge ili kuvuruga sanaa hii ya muziki na usambazaji,katika hili tutaweza kuwakomboa maelfu ya vijana wanaofanya muziki huu,Sisi ni wawakilishi wa maelfu ya wafuasi wa mlengo huu ambao malengo husika yanafahamika,Si rahisi sana kukaa meza moja na adui yako lakini kwa kuzingatia matakwa na maslahi ya wote na kufanikisha kile tulichokipigania(kwa hatua ya kwanza) mbele ya kamati ya Bunge na katika matoleo ya Anti virus yaliyopita tumejiridhisha kuwa malengo tuliyoyapigania na kuyaeleza kuwa hayapo sawa yamekubaliwa(kwa maana ya hoja zetu kushinda) na utekelezaji wake kufanyika mapema,kama ifuatavyo:-
• Studio iliyotolewa na Mh Rais kurudishwa na kukabidhiwa Chama halali cha kutetea wasanii(TUMA) kinachotambuliwa na BASATA .
• Chama feki cha wasanii TFU kuvunjwa na wasanii kuambiwa kujisajili na chama cha TUMA kwa utaratibu uliopo.(hakuna ubaguzi)
• Maboresho ya malipo kwa wasanii katika maonyesho.
• Kuachwa mara moja kwa mizengwe iliyokuwa inafanywa na redio yao ya kutopiga nyimbo za wasanii mbalimbali kwa kigezo cha chuki na rushwa.
Hayo ni baadhi ya mambo yaliyokubaliwa kutekelezwa na hatuoni kwanini tuendelee kukataa wito wa kumaliza suala hili na iwapo kama hawatatekeleza kama walivyosema hapo jamii itatuelewa kuwa sie sio wakorofi na tulikuwa na dhamira ya dhati katika kupata suluhisho la suala hili.

Tunathamini juhudi zote za upatanishi wa suala hili uliofanywa na waheshimiwa wote katika hili ilikuleta tija na maelewano ya kweli tunataka haya yazingatiwe ili kutekeleza muafaka huu na kutimiza dhana ya dhati ya kusaidia sanaa yetu na wasanii wetu kwa ujumla wake.

Tunaomba haya yafuatayo yazingatiwe na kuwekewa mkazo:-
- Pande hizi mbili zikutanishwe tena kwa nia ya kuweka mambo sawa kwa vyombo vya habari ili kuondoa ile hali ya sintofahamu ilijitokeza na kuchanganya wanajamii nchini kuwa, makubaliano hayo yaliyofanyika ni ya watu binafsi kati ya Sugu na Ruge (waliokuwa na ugomvi kwa zaidi ya miaka 10 sasa) na kamwe hayahusishi kundi la Vinega wa anti virus na redio nzima ya Clouds fm.

- Bwana Rugemalila kutekeleza yale yote yalizungumziwa kuwa chanzo cha magomvi haya pamoja na kutoa suluhisho la tatizo la tuhuma za rushwa na upendeleo katika redio yao.Suala la mfanyakazi wao Othman Suka wa kitengo cha muziki kuwa kinara wa rushwa na upendeleo katika muziki pale redioni kwao pia lizingatiwe ili kupata muafaka wa kweli vinginevyo tatizo baso litaendelea kuwepo.

- Watangazaji wa Clouds Fm na menejimenti yao kuzingatia muafaka huu na kujiepusha na kauli zozote zitakazouweka muafaka huu katika hali ya mashaka,kauli za kejeli za Adam Mchomvu,DJ Fetty,B 12,Ncha kali na wenzake hakika zitauvunja muafaka huu na kurudisha suala hili lilipotoka.

- Utekelezaji ya yaliokubaliwa uende na wakati na katika hili dhamira ya kweli ya kutimiza haya ionekane.

- Kila upande ukaamini kuwa haya yote yamefikiwa kwa ajili ya manufaa ya wasanii wote na si kwa maslahi ya wachache ili makubaliano ya kuivunja TFU na wasanii wote kujiungana TUMA chama cha wasanii kilichosajiliwa BASATA nail kufanyika mapema ili kupata mwanzo mpya katika sanaa yetu.

- Tunaomba watanzania wenzetu waliotuunga mkono waone haya mapatanisho ni ushindi kwa vinega wote kwani tuliopigania yamekubaliwa utekelezaji pamoja na upungufu katika kutoa taarifa kwa mpangilio. Tunaomba watuunge tunavyoendelea na safari ngumu iliopo Mbele yetu.

- Miongoni mwa malengo yetu ni kuhakikisha tunaondoa mfumo wote mbovu unounganisha watu wengi wakiwemo wakurugenzi/mameneja masoko wa makampuni kung'ang'ania kufanya kazi na radio moja na makampuni yake tu ili kuficha rushwa iliokithiri baina yao na kuwahimiza wapanue fursa kwa watanzania wote wenye uwezo wa kuandaa shughuli; kuhimiza redio na watumiaji wengine wa kazi za wasanii kulipa mirabaha watakayokubaliana kwa pamoja na TUMA kwa kutambua wasanii ndio chanzo cha mapato ya tasnia hii na wafanyabiashara wote katika sanaa waone ushirikiano na wasanii ndio njia ya kupata kipato kikubwa na kisicho na tafran, kuondoa woga wa wasanii kujiunga pamoja katika chombo chao ili kupata haki zao kama Vinega tulivothibitsha inawezekana na kuwasaidia wasanii watambue mchango mzuri wa redio na wafanyabiashara watakaofanya biashara nao kwa utaratibu utakaowekwa; Na kuendelea kuithibitishia Serikali na vyombo vyake vyote kama Bunge, TRA, Jeshi la Polisi, Mahakama nk ni manufaa kwao waamke na kufanya kazi ya dhati na TUMA na wadau wengine kuipanga hii "industry" ya SANAA ili kuboresha pato na maisha ya watanzania.

Pongezi zetu kwa Mh Jenista Mhagama(MB) ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Maendeleo ya jamii,Mh Nchimbi Waziri wa Habari na Utamaduni,Mh Tundu Lissu(MB) na wote waliosaidia kumaliza suala hili,Tunaamini kuwa kwa dhamira ya dhati tunaweza kuwakomboa vijana hawa wanaotuamini sisi na kuweka mifumo bora itakayowafanya wasanii wa nchi hii kufaidika na sanaa zao kama wenzetu wa Kenya,Uganda na kwingineko.

Tunapenda kuwapa pole wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine walighafilika na kuwa katika wakati mgumu kutokana na jambo hili,na wito wetu sisi Vinega kwa mashabiki na wanaharakati wote ni kuwa…..bado tunayo kazi kubwa ya kuendeleza haya mapambano kwa faida ya vizazi vijavyo na tusibweteke kwa ushindi huu na pia tusiupuuze ushindi huu kwani ndio njia zinafunguka kuelekea kwenye mafanikio.

HARAKATI DAIMA[/h]
 
binafsi sioni mwanga wowote kwenye bifu la kudumu....

matarajio yangu ni watu kufurahia kumalizika kwa mtafaruku huu... !Kwa sababu tu hapa cloud's media kuna kitu wamejifunza tena kikubwa sana...na as from now watachange policy yao....

fidia ya maralia no more ni haki yake!..ni mradi wake jamani...!mnyonge mnyongeni...

It was all about mradi wa malaria ... Vinega walikuwa wanacheza ngoma wasio ijuwa
 
Sina budi kumuomba msamaha mkali wa rhymes Afande sele kwa kitendo changu cha kumuona snitch alipokubali kuimba kwenye show ya straight music kumbe kweli alifata masirahi, na ndio ambacho hata wenzake walichokua wanataka, so hata wana jf wengine mlio mshtumu mfalme wa rhymes ombeni samahan kama mm SAMAHANI AFANDE SELE
Kaka kweli afande anastahili kuombwa masamaha,ila mm naona suala la sugu na ruge kupatana ni la kupongezwa pia ingawa kama limekaa kisiasa sana ila ngoja tuone
 
maana yangu hapa ni kua afande sele aliposhiriki kwenye tamasha la cloudz wadau wengi tulimponda nikiwemo mm lakin kumbe alikua anatafuta rizik kama alivyofanya sugu juz kati

Tunaomba uthibitisho SUGU alifuata pesa juz kati.au unaongeza post.
 
Mgosi Mkoloni
drP8vlvSl_8.gif
Joseph Mbilinyi

TAMKO LA VINEGA JUU YA MAKUBALIANO YA SUGU NA RUGE
Leo hii tarehe 23 ya mwezi February, 2012 mida ya saa 1 usiku mpaka saa 5 na nusu usiku katika eneo la Mwenge Vinega wa anti virus tulikutana katika kufanya tathmini na kujadli maridhiano ya kumaliza ugomvi wa kimaslahi kati ya Kundi la Vinega na Redio Clouds pamoja na Bwana Rugemalila Mutahaba,katika kikao hicho tuliridhiana kutoa tamko hili kwa umma wote wa watanzania na wapenda maendeleo wote wa sanaa yetu.
"Ni kweli hakunaga Vita isiyo na mwisho lakini pia katika kila vita malengo ya msingi yanapaswa kuwa mbele na daima mbele...Harakati hizi za Anti virus zilipoanza wengi tulionekana kama wasaliti na wapuuzi,wahuni na kuonekana kama tuna wivu tu na mafanikio ya baadhi wa wadau ila daima tulisimama katika kweli na hatimae Umma/jamii ya watanzania ukasikia sauti na hoja zetu na kuona kweli tuna mambo ya msingi,Hoja zetu mbele ya umma ndio ilikuwa silaha ya vita hii ya Anti virus na wala si nguvu ya Propaganda na uzushi...Tumepiga makelele na hatimaeTaifa zima wakaona kweli hapa kuna hoja na zinapaswa kuzingatiwa na wala si ugomvi wa mtu mmoja bali ni harakati za kweli za kukomboa sanaa yetu na kuvunja ile mifumo ambayo siyo sahihi inayoendelea kunyonya jasho la wasanii wa Tanzania na kuwafanya kuwa mafukara na wasio na mategemeo na kupelekea kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya na hatimae kufanya mambo ya kihalifu.Sanaa hii kwa muda imekuwa ikihodhiwa na watu wachache na kujitajirisha na kuacha lundo la wasanii kuishi maisha mabovu.Dhamira yetu ni kumaliza kabisa mifumo hii mibovu ambayo tunaamini ikimalizwa msanii wa kitanzania ataweza kupata kipato na kujiajiri na kuendesha maisha yake sawasawa.
Sisi kama kundi la Vinega kwa niaba ya umma wa watanzania wanaotuamini na kutusikiliza tumeridhia mapatano ya kumaliza ugomvi kati ya Mh Joseph Mbilinyi (SUGU) na Bwana Rugemalila Mutahaba(ugomvi uliodumu kwa zaidi ya miaka 10 kabla hata ya anti-virus ikiwemo kutopiga nyimbo zake na kuporwa wazo la mradi wa malaria) ili kuweza kupiga hatua mpya katika kusaidia sanaa na pia kuonyesha dhamira yetu ya msingi kuwa, kwetu sisi ugomvi sio kati ya Sugu na Ruge bali ni mifumo mibovu ambayo imekuwa ikikumbatiwa na Bwana Ruge ili kuvuruga sanaa hii ya muziki na usambazaji,katika hili tutaweza kuwakomboa maelfu ya vijana wanaofanya muziki huu,Sisi ni wawakilishi wa maelfu ya wafuasi wa mlengo huu ambao malengo husika yanafahamika,Si rahisi sana kukaa meza moja na adui yako lakini kwa kuzingatia matakwa na maslahi ya wote na kufanikisha kile tulichokipigania(kwa hatua ya kwanza) mbele ya kamati ya Bunge na katika matoleo ya Anti virus yaliyopita tumejiridhisha kuwa malengo tuliyoyapigania na kuyaeleza kuwa hayapo sawa yamekubaliwa(kwa maana ya hoja zetu kushinda) na utekelezaji wake kufanyika mapema,kama ifuatavyo:-
• Studio iliyotolewa na Mh Rais kurudishwa na kukabidhiwa Chama halali cha kutetea wasanii(TUMA) kinachotambuliwa na BASATA .
• Chama feki cha wasanii TFU kuvunjwa na wasanii kuambiwa kujisajili na chama cha TUMA kwa utaratibu uliopo.(hakuna ubaguzi)
• Maboresho ya malipo kwa wasanii katika maonyesho.
• Kuachwa mara moja kwa mizengwe iliyokuwa inafanywa na redio yao ya kutopiga nyimbo za wasanii mbalimbali kwa kigezo cha chuki na rushwa.
Hayo ni baadhi ya mambo yaliyokubaliwa kutekelezwa na hatuoni kwanini tuendelee kukataa wito wa kumaliza suala hili na iwapo kama hawatatekeleza kama walivyosema hapo jamii itatuelewa kuwa sie sio wakorofi na tulikuwa na dhamira ya dhati katika kupata suluhisho la suala hili.

Tunathamini juhudi zote za upatanishi wa suala hili uliofanywa na waheshimiwa wote katika hili ilikuleta tija na maelewano ya kweli tunataka haya yazingatiwe ili kutekeleza muafaka huu na kutimiza dhana ya dhati ya kusaidia sanaa yetu na wasanii wetu kwa ujumla wake.

Tunaomba haya yafuatayo yazingatiwe na kuwekewa mkazo:-
- Pande hizi mbili zikutanishwe tena kwa nia ya kuweka mambo sawa kwa vyombo vya habari ili kuondoa ile hali ya sintofahamu ilijitokeza na kuchanganya wanajamii nchini kuwa, makubaliano hayo yaliyofanyika ni ya watu binafsi kati ya Sugu na Ruge (waliokuwa na ugomvi kwa zaidi ya miaka 10 sasa) na kamwe hayahusishi kundi la Vinega wa anti virus na redio nzima ya Clouds fm.

- Bwana Rugemalila kutekeleza yale yote yalizungumziwa kuwa chanzo cha magomvi haya pamoja na kutoa suluhisho la tatizo la tuhuma za rushwa na upendeleo katika redio yao.Suala la mfanyakazi wao Othman Suka wa kitengo cha muziki kuwa kinara wa rushwa na upendeleo katika muziki pale redioni kwao pia lizingatiwe ili kupata muafaka wa kweli vinginevyo tatizo baso litaendelea kuwepo.

- Watangazaji wa Clouds Fm na menejimenti yao kuzingatia muafaka huu na kujiepusha na kauli zozote zitakazouweka muafaka huu katika hali ya mashaka,kauli za kejeli za Adam Mchomvu,DJ Fetty,B 12,Ncha kali na wenzake hakika zitauvunja muafaka huu na kurudisha suala hili lilipotoka.

- Utekelezaji ya yaliokubaliwa uende na wakati na katika hili dhamira ya kweli ya kutimiza haya ionekane.

- Kila upande ukaamini kuwa haya yote yamefikiwa kwa ajili ya manufaa ya wasanii wote na si kwa maslahi ya wachache ili makubaliano ya kuivunja TFU na wasanii wote kujiungana TUMA chama cha wasanii kilichosajiliwa BASATA nail kufanyika mapema ili kupata mwanzo mpya katika sanaa yetu.

- Tunaomba watanzania wenzetu waliotuunga mkono waone haya mapatanisho ni ushindi kwa vinega wote kwani tuliopigania yamekubaliwa utekelezaji pamoja na upungufu katika kutoa taarifa kwa mpangilio. Tunaomba watuunge tunavyoendelea na safari ngumu iliopo Mbele yetu.

- Miongoni mwa malengo yetu ni kuhakikisha tunaondoa mfumo wote mbovu unounganisha watu wengi wakiwemo wakurugenzi/mameneja masoko wa makampuni kung'ang'ania kufanya kazi na radio moja na makampuni yake tu ili kuficha rushwa iliokithiri baina yao na kuwahimiza wapanue fursa kwa watanzania wote wenye uwezo wa kuandaa shughuli; kuhimiza redio na watumiaji wengine wa kazi za wasanii kulipa mirabaha watakayokubaliana kwa pamoja na TUMA kwa kutambua wasanii ndio chanzo cha mapato ya tasnia hii na wafanyabiashara wote katika sanaa waone ushirikiano na wasanii ndio njia ya kupata kipato kikubwa na kisicho na tafran, kuondoa woga wa wasanii kujiunga pamoja katika chombo chao ili kupata haki zao kama Vinega tulivothibitsha inawezekana na kuwasaidia wasanii watambue mchango mzuri wa redio na wafanyabiashara watakaofanya biashara nao kwa utaratibu utakaowekwa; Na kuendelea kuithibitishia Serikali na vyombo vyake vyote kama Bunge, TRA, Jeshi la Polisi, Mahakama nk ni manufaa kwao waamke na kufanya kazi ya dhati na TUMA na wadau wengine kuipanga hii "industry" ya SANAA ili kuboresha pato na maisha ya watanzania.

Pongezi zetu kwa Mh Jenista Mhagama(MB) ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Maendeleo ya jamii,Mh Nchimbi Waziri wa Habari na Utamaduni,Mh Tundu Lissu(MB) na wote waliosaidia kumaliza suala hili,Tunaamini kuwa kwa dhamira ya dhati tunaweza kuwakomboa vijana hawa wanaotuamini sisi na kuweka mifumo bora itakayowafanya wasanii wa nchi hii kufaidika na sanaa zao kama wenzetu wa Kenya,Uganda na kwingineko.

Tunapenda kuwapa pole wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine walighafilika na kuwa katika wakati mgumu kutokana na jambo hili,na wito wetu sisi Vinega kwa mashabiki na wanaharakati wote ni kuwa…..bado tunayo kazi kubwa ya kuendeleza haya mapambano kwa faida ya vizazi vijavyo na tusibweteke kwa ushindi huu na pia tusiupuuze ushindi huu kwani ndio njia zinafunguka kuelekea kwenye mafanikio.

HARAKATI DAIMA

Hapa ninawapongeza kwa statement yenu,dhuluma ndio ilikuwa mwanzo wa mapambano na kweli vinega huu ni ushindi mkubwa juu ya unyonyaji,wasanii wote mnatakiwa kuwa kitu kimoja katika tasnia yenu,msikubali kati yenu kuonewa na kdhulumiwa jasho lenu.

Hakikisheni kila mmoja wenu anavuna stahili yenu,na makubaliano yanatekelezwa ipasavyo.
ilikuwa haiingii akilini kuuwa vipaji vya vijana wetu kwa kuwanyonya na kuishia patupu wakati wao ndio wametoa jasho.
Mpambano uliobakia sasa ni kuhakikisha mnakaa katika mstari kazi zetu haziibiwi tena.

Nawatakia kila la kheri katika mwanzo mpya wenye nuru mbeleni.

Pia nawapongeza MB Lissu na Waziri Nchimbi kwa kusimamia hilo jambo ambalo mwisho wake ulikuwa unaelekea kubaya sana maana mmoja wa mahasimu hao Ruge na Sugu alikuwa na kundi kubwa ambalo liliona linakandamizwa na kikundi cha wachache.
Wadosi wanaowadhulumu vijana waliojiajili katika sekta hii acheni mara moja kudurufu kazi zao bila kibali chao.
Na nyinyi sasa muongeze bidii kwa kujifunza kutumia ala za muziki ili tuwaite wanamziki sio sasa mtanavyojitambulisha wakati hamjui kitu chochote katika kutumia ala.

Mwisho nawapongeza wote waliofanikiwa kujua kutumia ala angalau moja katika muziki,hawa mimi ninathubutu kuwaita wanamziki.
 
AFANDE ATABAKI KUWA SNITCH MPAKA AOMBE MSAMAHA COZ ALISALITI WANAHARAKATI VINEGA,
NLIMSIKIA AKIZUNGUMZA KUWA KALIPWA MIL 1.5 KWENYE ILE SHOO,IZO NI HARAKATI ZA SUGU NA VINEGA,
AFANDE WEWE NI KAMANDA,JEMBE,SOJA,KING,MKALI.
Ila ulibugi.ITABIDI UOMBE MSAMAHA NA UJIUNGE NA WALE WANAOMSHUKURU SUGU NA VINEGA.

Sina budi kumuomba msamaha mkali wa rhymes Afande sele kwa kitendo changu cha kumuona snitch alipokubali kuimba kwenye show ya straight music kumbe kweli alifata masirahi, na ndio ambacho hata wenzake walichokua wanataka, so hata wana jf wengine mlio mshtumu mfalme wa rhymes ombeni samahan kama mm SAMAHANI AFANDE SELE
 
siwezi kumwomba msamaha mtu mwoga rahisirahisi tu mwanaume kupambana sio biti tu unalegea. Afande hastahili kuombwa msamaha yeye hukuona mbali wala nini mdebwedo tu.ila mistari yake naiheshimu kwa sana tu.
 
bora afande alienda zamani,mbona hata wenzie wamefata njia hyo hyo?
 
afadhali wenzie wametuonyesha kuwa kuna kitu walikuwa wanakipigania.hata kama wamefika mwafaka lakini ni baada ya watu kujua kuwa kumbe kuna udhulamaji kwenye mziki.heko vinega hata kama vita vyenu vimengiliwa na wanasiasa.!!
 
hamna mzima pale sugu+afande 1 alitangulia mwingine amefata
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom