Ni mke wa mtu, ni mzuri, ANANITAKA nifanyeje?

Imagine kama kuna mwanaume anamuwazia hivyo mchumba wako utajisikiaje?

Muhimu ni kujiweka mbali na huyo mke wa mtu..Hiyo ni tamaa hivyo basi kabla hujajutia jiwekeee tahadhari. Ridhika na mchumba wako, muone ni more cute than huyo mke wa mtu..
 
Nilimpa lift jumatano asubuhi wiki iliyopita. Anasoma chuo cha usimamizi wa hotel. Aliomba namba yangu ili ikiwezekana niwe nampa lifti siku moja moja hasa nyakati za asubuhi na jioni. Siku hiyo Jioni alinipigia simu kuniuliza kama nimetoka kazini ili nimsaidie lift. Bahati nzuri nilikuwa karibu kutoka ofcn, akaopt kunisubiri. On ourway home Aliniuliza ninaishi na nani, nikamjibu na wadogo zangu na nina mchumba yupo hapahapa Bongo ila hatuishi nae. Akasema yeye anaishi na mumewe na wana mototo mmoja wa miaka minne, mumewe ni mtu wa kusafiri sana safari za mikoani. Lakini Kuanzia hiyo j’tano she keep on trying to be close to me, also she asked my weekend plans. I managed to avoid meeting with her this weekend but I’m not sure if my strength to avoid her forever will persist longer coz she is so cute. Sina uhakika kama anataka mahusiano lakini ni ngumu kumkatalia akitaka. The way she talk, the way she look, the way she ask, her figure Uhhhhh! dud Nifanyeje na huyu mtu? Leo nilipanga sinta mpa-lift sikupokea hata simu yake asubuhi lakini nilipofika kituoni ikawa kama mbwa mbele ya chatu.

Una tamaa sana wewe na itakutokea pabaya!!!!!!!!!!!!!!watchout!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mkuu..kosa moja kubwa umeshafanya ..kugawa namba ya simu.. Kosa la pili.. tayali umeshamweka kwenye akili yako kuwa ni mzuri n.k.. yaani unataka JF watu wakufagilie..hiyo "guilty consciousness" yako.

Umeshaambiwa na wengi.. kimbia... Jinsi ya kukimbia utajua wewe mwenyewe bila ya kumdhalilisha au kum- offend huyo mama/Bint? Ningekuwa mimi.. ningebadili namba.. Gharama ya marafiki zangu kunitafuta kwa namba mpya ni ndogo kuliko mtego huo.. Kwanza huwezi jua anamatatizo gani na familia yake..unaweza kujikuta kwenye ukurasa wa mbele wa magazeti ya uwazi..

Mkuu..hilo bomu..usilishike labda kama unataka kujitoa muhanga..
hasipokuelewa huyo bas tena
 
Nashukuru mkuu nadhani itabidi nibadili muda wa kwenda kazini asubuhi na muda wa kutoka jioni, ikiwezekana evining time niongeze muda hapa jf. sijui ilikuwaje nikatoa namba yangu tena official one siwezi kuibadili kwaajili yake tu nitaharibu vingi
 
Yes nina mchumba ndio maana nataka nisiingie ndani zaidi kuharibu. but she keep on texting and calling me
Nimekuuliza maswali hujajibu kwahiyo nachukulia ni NO..NO and NO!Unavutiwa zaidi na mke wa mwenzio kuliko mchumba wako..na hii inasikitisha kweli maana unaonekana ni mwepesi sana kutamanikwa vigezo vya umbo..sura na sauti...mwenzio sijui akiwa mke utamsaliti mara ngapi kwa kutamani wazuri zaidi yake.
 
No nO No Lizzy! Nampenda mchumba wangu it's just the tread ya huyu dada inanitisha and mimi ni binadamu kama wengine najaribu kutafuta njia ya kujinasua na mitego ningekuwa nimenasa sidhani kama angekatiza weekend hii, kwani awas avoiding her wikiend nzima.
 
Well then weka akili yako kwa mpenzi wako...hiyo mitego unayoongelea hata sijaiona...we unachotaka ni huruma ili ukiamua kufanya kweli urudi hapa kupokea huruma zaidi.Naamini kila mtu anaweza kua na msimamo akitaka....na wewe kua na msimamo.Kam kumpa lift ni tatizo sana mjulishe kwamba hutoweza tena na unaomba msitishe mawasiliano pia.Sidhani kama kuna anachokudai kinachokufanya usiwe na maamuzi juu ya kutaka au kukataa mawasiliano/ukaribu nae.
 
Angalia mwanawani jamaa wameambukizwa ngoma kirahiiiisiiiii!! Sikushauri uache kumpa lifti kwakuwa si lazima kutoka out nk. Hakikisha mahuisianao hayaendi zaidi ya lifti. Mfanye aelewe hivyo na usi entertain mazungumzo mengine.
 
Nashukuru mkuu nadhani itabidi nibadili muda wa kwenda kazini asubuhi na muda wa kutoka jioni, ikiwezekana evining time niongeze muda hapa jf. sijui ilikuwaje nikatoa namba yangu tena official one siwezi kuibadili kwaajili yake tu nitaharibu vingi
Huna haja ya kubadili nambari ya simu wala kubadilisha taratibu na mipango yako. If you have guts, leo jioni toka au kesho asubuhi nenda kazini kama saa zako za kawaida. Bila ya shaka atakuwepo. Simamisha gari, atasogea, usimfungulie mlango bal teremsha kioo na mwambie wazi wazi: "Samahani na tafadhali sana, wachana na mimi". Ondosha gari kiulaini wala usiangalie nyuma.
 
Duh Elia Pole sana; sina ushauri maana hata mimi sijui kama hata ningeomba ushauri hapa labda ningeshamezwa zamani! Ila kama angekuwa siyo mke wa mtu labda ingekuwa njema kwa maana ya kuwa unabadili mchumba, ila ujuwe hapo unataka kuchapa tu kama uzinzi mwingine; kama wewe ni mzinzi tafuta hasiye mke wa mtu maana hutakuwa humtendei haki huyo mwenye mke mbele ya mola wako.

Pia nadhani kila jambo uja kama elimu mbadala, unaweza kujuwa na kuona challenge uliyo nayo kwa Mke baada ya kuowa, wewe kama mwanaume unatakiwa kujiangalia sana kwenye mitego ya kila aina.

Kingine Elia umefanya jambo baya sana kuweka details zake zote hapa, maana hizo details mmewe anaweza kuwa mtu wa JF akamjuwa na kizungumkuti kikaanza home, mara nyingine husiweke all feasible details za kum-describle kwa issue kama hii, maana pamoja na ujinga wake bado unawajibu wakujilinda na kumlinda hata kama ni mpumbavu.
 
Ingekuwa married man anaulizia mambo ya nyumba ndogo mgeona michango ya kumpongeza. Hoo mkewe labda hajitumi, ooh mkewe ana ghubu. Haya sasa na huyu mke wa mtu labda mmewe hajitumi. Huyu kijana (kidumu to be) anaulizia kama ale mke wa mtu watu wote mmekuja juu. Naomba tusiwe biased kwa kung'ang'ania mke wa mtu ni sumu. Hata mume wa mtu ni sumu pia. Ndio mjue nyie wenye vimada ubaya mnaowafanyia wake zenu na utamu mtaosikia wake zenu nao wakiliwa.
 
Tatizo kubwa ni huyo 'mke wa mtu'. Kama yeye kaolewa kwa nini ajilengeshe kwa jamaa? Hata kama hawajafanya chochote kibaya kwangu mimi huko kujilengesha tu kwa mwanaume mwingine ni dealbreaker.

Hasara tupu hapo.
 
ushauri gan unataka?achana nae mke wa mwenzako.mumewe kasafir alitumwa aolewe..huyo msichana mpumbav sana..dat y i hate mariage..
 
My brother Elia , kwanza potezea kabisa huo msaada kaka, badilisha ratiba yako ya kutoka ofisini na hata nyumbani kukwepa hii hali jitahidi kadri uwezavyo kuikimbia hii hali, nasema hivyo kwa sababu future yako yaweza badilika kwa siku moja tu. mke wa mtu epuka si wanadamu wote watakuwa na kikao na wewe kusuluhisha huo ugomvi, bali wengine njia rahisi ni kukupoteza kwenye sura ya dunia.
 
Elia,

Kwani wewe haujawahi kuwa na mahusiano zaidi ya moja? Nenda naye out halafu matokeo utayapata huko huko! Mimi binafsi "mke wa mtu" akijilengesha, sifikirii mara mbili - HIT & RUN!
 
Acha kuzunguka sana, ameshakuambia yeye ni mke wa mtu, halafu mume wake ni mtu wa safari, then anakupigia na kutaka kudumisha mawasiliano, anakuuliza wkend plans, kwani wewe ni mgeni katika gemu mpaka usijue kuwa anakutaka? Mbaya zaidi unamsifu kuwa ni mzuri, yaani unatuambia mpaka ongea yake jinsi inavyokuvutia. Moyoni mwako umeshaanza kuwaza ufuska, na hata tukikushauri tayari unajua nini chakufanya.

Kabla hujafanya huo ufuska, jiweke katika nafasi ya yule mume wake halafu imagine how would you feel? Imagine mchumba wako akijua itakuwa hasara kwa nani? Mume wake akijua na labda ndoa ikavunjika,mtoto wao ataishi katika mazingira gani? Mbaya zaidi unaweza kuondoka dunia hii siku si zako.

Kama hiyo ni tabia ya huyo mwanamke unaweza kuwa msaada kwake, muoneshe kuwa wapo wanaume wanaojali wake za wenzao. Mwekee mazingira ya kuelewa kuwa sisi wanaume hatupendi kuwa mbali na familia zetu, tunafanya hivyo kwa sababu wakati mwingine hatuna jinsi, na tunajua wazi kuwa sisi sote ni dhaifu, lakini tunawaamini kuwaacha nyumbani tukaenda kutafuta riziki, na kwamba tunawapenda sana. Kwa wivu tulionao tungeamua kukaa tu nyumbani kuwalinda, lakini upendo tulionao umezaa imani kwao kuwa watalinda na kuheshimu ndoa zetu kama tunavyo linda na kuheshimu tunapokuwa mbali nao.
 
NDOA IHESHIMIWE NA WATU WOTE. Bro mtoa mada "hata kama huyo mke wa mtu anaonyesha kukutaka, wewe wachana nae na umwambie ukweli kabisa kuwa unaheshimu ndoa za wenzako kama ambavyo ungetaka yako ije kuheshimiwa"
 
Back
Top Bottom