Ni miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika au ya marais wa Tanzania?

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,543
134
Salaam:
Pamoja na kwamba huwezi kutenganisha moja kwa moja ''role" ya marais walioongoza nchi hii kwa vipindi mbalimbali na historia ya Tanzania, mwelekeo unaoonekana hasa katika vyombo vingi vya habari vinavyotoa taarifa kuhusu miaka 50 ya uhuru wetu havitendei haki Watanzania. Kila kukicha baadhi ya Magazeti na TV yanayoonyesha matukio mbalimbali ya miaka iliyopita yanaelezea kwa sehemu kubwa zaidi Nyerere, Nyerere and Nyerere again. Hebu fikiria eneo moja la mfano moja kama usafiri wa aina mbali mbali tangu uhuru hadi leo - watu walivyokuwa wakienda kwa treni toka Kigoma hadi Dar, au wakati kukiwa na Mabasi ya East African Railways na mabadiliko yaliyoendelea kutokea hadi sasa. Ingepedeza zaidi tukapewa experiences za mambo yalivyokuwa katika sekta / shughuli mbalimbali ambazo kwa namna moja ama nyingine watu huzizungumzia kwa hisia zenye furaha na fahari kwa ujasiri na ukakamvu walioonyesha katika mazingira hayo yaliyopita - (JKT,MICHEZO NA BURUDANI,MAISHA YA SHULENI,UGALI WA NJANO, FOLENI ZA SUKARI, nk,) .Frankly inapofika mahali baadhi ya watu wanapotaka kutufanya wengine tusiwaze wala kuona mengine zaidi ya Nyerere .........INABOA!
 
Back
Top Bottom