Ni mda gani nitumie gia namba 2 kwenye gari automatic(nina maana ile 2 iliyoandikwa pale)

sikiolakufa

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
411
54

wakuu mimi nilinunua toyota cresta juzi nilisafiri nayo kwenda moshi, ina kimbia sana sana....ila chakushangaza mbona kila nikitaka kuipita land cruiser iliyokuwa mbele yangu nilikuwa nashindwa? Je nilipaswa kuweka gia namba 2..? Mbona gia hiyo nilivyoiweka gari ilibadilisha mlio na ikalia mlio wa hatari halafu ikawa nzito sana...je ile landcruiser ina speed kubwa kuliko gari yangu cresta gx 100 kwa kweli naomba ufafanuzi maana roho inauma sana mwenye landcruiser aliniacha nikaja kutana nae mombo tayari amemaliza kula nyama choma
 
Mkuu, GIA namba mbili sio kwa ajili ya kuongeza speed. Hutumika hasa wakati unapanda mlima kwa maana kuwa Gari linakuwa na uwezo wa kuhimili mwinuko. Kihandisi tunaita Resistance to gravitational force. Pia gia hiyo hufanya Gari liwe na driving Torque kubwa. Kama ulikanyaga accelerator pedal mpaka mwisho bila mafanikio optional iliyobaki ilikuwa ni ku shift kwenye over drive. Pia usipende kuendesha Gari kwa speed kubwa mpaka unaona kero unaposhindwa ku overtake ni hatari kwa maisha yako. Driving at 80km/hr is advisable!
 
watch out, hapo unalinganisha kobe na chitah. Utakufa kabla ya wakati wako wa kufa.
 
Ili ni tatizo la kutofahamu sheria, leseni za kununua, kutojifunza gari vizuri. Kwanza ufahamu kuwa magari yanatofautiana power - ujazo wa injini, pia yana tofautiana huduma na ubora wa parts - kama gari yako haipati service, tune up tarajia kupitwa tu njiani na kutokupita. Land Cruiser V8 usijaribu kabisa; Mercedez Benzi hasa saloon usijaribu kabisa, Suzuki new model usijaribu kabisa na hako kwa Cresta kako. Pia ujue kuwa kama unalipita Mercedez Banz au Cruiser V8 au machine yoyote V6 au V8 basi ujue dereva wake ameamua kukimbia mwendo wa plan yake.

Siku nyingine bonyeza button ya power kama gari yako inayo.

Pia kwa kuepuka ajali lazima uendeshe gari lako kama ndege yaani kama unaenda Morogoro na umepanga kuondoka Dar saa moja kamili asubuhi na kufika Moro saa mbili na nusu kwa speed ya 100km/ h au 120/ h au 140km/h basi zingatia plan yako ukimkuta mbele yako mwenye 80km/h ni dhairi utampita, ukipitwa na mwenye 160km/h mwache aende kwani nae ana-plan yake.

Hiyo gia namba 2 ni kwa ajili ya kupita kwenye mchanga, tope au kupandia mlima na emergency braking.
 
Mie sijaelewa muuliza swali ana maana gari ni gari na gari zote zinatakiwa ziwe na speed sawa sawa? Mkuu punda hawezi kuwa na mbio kama farasi............
 
Huyo amekasirika atalikuta cruiser linarudi kutoka kwa baba wakati yuko kwenye folen
angalia kwenye kitabu cha gari yako waulize waliotengeneeza watakusaidia zaidi
else mmmhh gerezani
 
safety first, kwa jinsi muuliza swali anavyoongea naweza kujudge kuwa ni mtu asiyezingatioa usalama kabisa
Tips
kabla haujaanza safari yako hasa ya mbali basi fanya kwanza Pre start Check, Check level ya oil, Hydraulic na Blake fluids, maji, any leaks (Fuel, water), belt zote zilizopo kwenye engine yako ziko sawa, fuel level, check kama Tail zimefungwa barabara na zina upepo unaostahiki kwa safari ndefu, hakikisha kuwa una spare tairi hata mbili na ziko kwenye hali nzuri, una jeki na wheel spaner, reflectors-Triangle, Fire extinguishers, insurance na road lisence ziko valid

Unapokwenda safari za mbali jaribu sana kwenda speed amabyo haiitaji concentration kubwa sana ili kukuzuia kuchosha akili, kadri unavyoendesha speed kubwa unakuwa haupo relaxed na unatumia uwezo mkubwa sana wa akili kuzingatia njia na mwisho wake unachoka akili na ni rahisi sana kufanya ajali
angalia umbali unaoenda na panga speed yako mapema na mantain your planned speed wakati wote wa safari, epuka ulevi wa aina yoyote na mara nyingi jaribu kuwa una rekebisha kiti chako ili upate confortability pale mwili wako unapohitaji hivyo na inapokubidi basi ni bora ukawa na vituo vya kuwea kupaki na kuunyosha mwili

kumbuka Ajali zote zinaepukika
 
Mkuu, GIA namba mbili sio kwa ajili ya kuongeza speed. Hutumika hasa wakati unapanda mlima kwa maana kuwa Gari linakuwa na uwezo wa kuhimili mwinuko. Kihandisi tunaita Resistance to gravitational force. Pia gia hiyo hufanya Gari liwe na driving Torque kubwa. Kama ulikanyaga accelerator pedal mpaka mwisho bila mafanikio optional iliyobaki ilikuwa ni ku shift kwenye over drive. Pia usipende kuendesha Gari kwa speed kubwa mpaka unaona kero unaposhindwa ku overtake ni hatari kwa maisha yako. Driving at 80km/hr is advisable!

Ushauri mzuri sana uliomalizia nao.....
 
he he he...unataka kufananisha cruiser na cresta....kwa nini usinunue cruiser, au ulitunze hilo mpaka likue limfikie cruiser....hi hi hi hi

Kweli Preta hujatulia, ama umenichekesha....
 
Duh ulitaka kushindana na LC kwa namba 2! Hiyo 'midude' (LCs) achana nayo kabisa (ina nguvu balaa)! Ukitembea kwa speed ya 150km/h ndani ya LC unaona gari imetulia (stable) tu kama kawaida wakati kwa mwendo huo gari ndogo utaona inakuwa very unstable barabarani (na kusema kweli kwa barabara zetu ni hatari sana kuendesha katika mwendo huo).

Kwa kujibu swali lako, gia namba 2 inafanya gari linakuwa zito na kwenda taratibu na kwa magari ya petroli inatumika kwa ajili ya engine braking (badala ya breki ya kawaida) wakati unataka kupunguza mwendo kwa dharura au hata kwa mfano kama unashuka mteremko mkali kwa muda merefu (kama mlima kitonga kwa mfano) ni vema ukatumia engine braking (namba 2) badala ya kukanyaga breki. Kama gari ipo kwenye overdrive mode inatakiwa ui-switch off kwanza kabla ya kupeleka gear lever yako kwenye namba 2.
 
kutaka kuipita cruser inawezekana kama gari lako Grester lipo kwenye hali nzuri na lisiwe na shida yoyote,pia inategemea kama crester ya engine yake ina ukubwa six (6). Gari ndogo inauwezo wa kukimbia zaid kuliko kubwa kwa sababu ipo chini zaid haiyumbishwi na upepo ili lazima engine iwe kubwa isiwe na piston 4 iwe 6.
 
Mkuu, GIA namba mbili sio kwa ajili ya kuongeza speed. Hutumika hasa wakati unapanda mlima kwa maana kuwa Gari linakuwa na uwezo wa kuhimili mwinuko. Kihandisi tunaita Resistance to gravitational force. Pia gia hiyo hufanya Gari liwe na driving Torque kubwa. Kama ulikanyaga accelerator pedal mpaka mwisho bila mafanikio optional iliyobaki ilikuwa ni ku shift kwenye over drive. Pia usipende kuendesha Gari kwa speed kubwa mpaka unaona kero unaposhindwa ku overtake ni hatari kwa maisha yako. Driving at 80km/hr is advisable!

Inaonekana ni mtaalamu wewe, je na ile "L" ni kazi gani? Mimi huwa ni mwendo wa D tu tangu nzaliwe.
 
hujasema ulienda moshi kulitambikia kwa kuchinja mbuzi na kilimwagia damu
badala ya kulimwagia maji ya baraka au mchungaji kuliombea.
na lasima kule kule nyumbani wajue nimenunua gari ati tena cresiiiita lenye spiiiiddddd mingi hadi linaipita lendkrusaa mangie hee kiruuuuuuuuuu.lasima wajue mshaka anajua kushakua gari linalokimbia sanaaaaaa.
 
Inaonekana ni mtaalamu wewe, je na ile "L" ni kazi gani? Mimi huwa ni mwendo wa D tu tangu nzaliwe.

Kwenye form za leseni mpya kuna section inaonesha restrictions, moja wapo ni automatic transmission, nadhani sasa vizazi vya siku hizi itakuwa ni kawaida kutiki sehemu hii..khaaa!!
 
aisee.. labda utuambie speed meter ilikua inasoma ngapi mkuu, isije kua ulikua 100km/hr halafu unataka ulipite cruser

hizo gx 100 ni noma sana linaweza kukuua hilo manake unaweza kutembea na speed 180km/hr na usijue mpaka utizame speed meter!

usiendeshe kimashindano mkuu..
 
Hongera sana kwa kununua gari, ila, uwapo barabarani usifanye mashindano. Dreva unayeshindana naye anaweza kukufanyia kusudi umpite pale anapoona kuna gari mbele likija. Binadamu tu tofauti. Kuhusu hizo gari za kike "automatic" gia no.2 hutumika kwenye mashimo na sehemu ngumu kupita. Ukitaka kwenda kwa spidi kali bonyeza O/D yaani Over Drive ukiwa kwenye D.
 
Inaonekana ni mtaalamu wewe, je na ile "L" ni kazi gani? Mimi huwa ni mwendo wa D tu tangu nzaliwe.

Kwa baadhi ya gari zinakuwa na L D H au 2 D 1, lkn matumizi ni yale yale. Kwa uendeshaji wa kawaida tunahitaji D tu na si ajabu usitumie hiyo L na H au 1 na 2 milele.
 
usithubutu ku -switch off gari yako ya automatic ndipo uweke O/D. Kama uko kwenye mwendo wewe bonyeza O/D button tu. Kwa L , hii hutumika kupita kwenye mchanga mwingi au matope. Kumbuka gari hizi wateja wakuu ni Arabs. Hivyo lazima ziwe na uwezo wa kupita mchangani (Jangwani).Kwa L/C hutumia four wheel drive. Ambavyo lazima ushuke chini na kui-set kabla ya kuikwamua gari yako au kupita nayo ktk matope/mchangani. Kwa automatic ukiweka L hakikisha moto usiwe mkali, la sivyo itazima. So weka moto wa kawaida tu. Pia ukiwa ktk mwendo kwa Automatic USIFANYE kosa la kukanyaga break ili kubadili D to 2 or L. just badili tu kwa kuweka unapo hitaji.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom