Ni "mbwa" au "mmbwa"?

Kiraka Kikuu

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
5,904
1,976
Wana jamvi,haya maneno yananitatiza!
Je mnyama wa kulinda nyumba ni "mbwa" au "mmbwa"?
yule mdudu anaeneza Malaria ni "mbu" au mmbu?
Unapotoka ndani unaenda "nje"au "nnje"?
Msaada tafadhali!
 
Ni mmbwa, mmbu,nnje, mmbuni(kwa maana ya mti wa kahawa ). Mashine zetu za kuchapia zinatakiwa ziwe na m na n zinazoonesha tofauti hiyo. Maandishi ya hayo maneno yanakuwa na m au n yenye muundo tofauti kidogo.
 
Ni mmbwa, mmbu,nnje, mmbuni(kwa maana ya mti wa kahawa ). Mashine zetu za kuchapia zinatakiwa ziwe na m na n zinazoonesha tofauti hiyo. Maandishi ya hayo maneno yanakuwa na m au n yenye muundo tofauti kidogo.

Ahsante kwa ufafanuzi
 
Tunaandika lugha yetu kwa kutumia maandishi ya watu, huwezi kuandika Kiswahili, Kibarbaig, Ki Hottentont, Kichina au Ki-Bushman kwa kutumia alphabet ya Kirumi.

Tunahitaji herufi zetu.

The closest approximation is a reverse silence letter, Kiswahili hakina doubling letters, kwa hiyo, kwa kuibia hii alphabet ya Kirumi, maandishi yanaandikwa "mbu" "nje" "mbwa"

Compromise ilitakiwa iwe "m'bu" "n'je" "m'bwa" lakini kamwe si "mmbwa".
 
I have a long way to go na hii lugha yetu.Ahsante kwa michango yenu makini.
 
Nilipata shida sana kutoka kwa mwalimu wangu wa shule ya msingi kuhusu namna ya kuyatamka maneno 'mto'(kiingereza river) na 'mti'(tree). Mimi nilikuwa na yatamka bila kuvuta hiyo herufi ya kwanza, kipindi hicho viboko vilikuwa vina ruhusiwa mashuleni.
 
Wana jamvi,haya maneno yananitatiza!
Je mnyama wa kulinda nyumba ni "mbwa" au "mmbwa"?
yule mdudu anaeneza Malaria ni "mbu" au mmbu?
Unapotoka ndani unaenda "nje"au "nnje"?
Msaada tafadhali!

Mkuu hali hiyo isikutishe kwani ni kitu cha kawaida kwenye lugha.Hilo ni tatizo la kiotografia.otografia ni utaratibu wa kutumia maandishi kuwakilisha sauti zisikikazo katika lugha.katika otografia ya kiswahili sanifu kuna sauti ambazo huwakilishwa na herufi zaidi ya moja mf:th,sh,mb,mw,nj,ng, n.k.Ieleweke kwamba baadhi ya maneno ya kiswahili huwakilishwa kimaandishi pungufu na ilivyo kwenye matamshi.Hali hii inapojitokeza ndiyo tunasema hayo ni matatizo ya kiotografia kama yanavyojitokeza kwenye maneno mbwa,nge mbu,nje,ngwe n.k.kwani matamshi yatolewayo huhitaji sauti zaidi kuliko zile zilizowakilishwa katika maandishi.

NAWASILISHA
 
Back
Top Bottom