Ni mashaka matupu kwa utawala huu wa awamu ya nne na bunge lake

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Nijuavyo mimi kwa akili yangu binafsi kazi kubwa ya bunge ni kuisimamia serikali,lakini kwa nchi yetu bunge limekuwa ni kijiwe kama vilivyo vijiwe vingine vya kupiga soga na kuziacha palepale bila kupata ufumbuzi wa tatizo lenyewe.Ni mara ngapi serikali yetu inakaidi mapendekezo halali yanayotambuliwa na katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania,ilihali wabunge wetu wakihongwa mapesa kwa visingizio vya posho za vikao(sitting allowance).Ni upuzi mtupu ikiwa wawakilishi wa wananchi wanapuuzwa kwa ajili ya udhaifu wao kwa kuongezewa posho.Sipendi kuamini kama kelele zote zile zilikuwa ni funika kombe mwanaharamu apite.

Kitendo cha serikali kupuuza mapendekezo ya bunge ni kuonyesha dhahiri bunge letu halina meno,na ni sehemu ya kupiga story huku wakitumia kodi za walalahoi bila faida kwa uwakilishi wao.Tulipowachagua na kula viapo vyenu ambavyo viliahidi kuitii na kuiheshimu katiba ya Jamhuri ya mmuungano wa Tanzania ni unafiki mtupu.Mara mangapi bunge linaonyesha udhaifu wake ikiwa ni pamoja na kuvunja vipengele vya katiba kwa kushindwa kuiwajibisha serikali mara inaposhindwa kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na bunge kwa niaba ya wananchi?Usaliti huu mwisho wake nini kwa mustakabali wa nchi yetu.


Sisi sote ni mashahidi kwa jinsi tukio la Luhanjo lilivyochukua kasi,tena wabunge wakiongea kwa jaziba bila kumung’unya maneno, lakini leo hii nini hatima ya Luhanjo.anastaafu kwa heshima kubwa kwa kulivua bunge nguo na kuliacha uchi mbele ya kadamnasi.Uko wapi uzalendo na uaminifu tuliowatunukia kwa kuwapa nafasi ya kuwakilisha mawazo yetu bila kuchumia matumbo yenu.Sitaki kuamini ni ndoto au ni kweli lakini ninanchokisubiri kwa hamu kubwa ni wabunge na bunge lenyewe kama mhimili wa pili wa dola kutoa maamuzi magumu na kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais. Matukio ya kudhalilishwa kwa bunge letu tukufu huku wananchi tukiamini ndiyo chombo pekee cha kututetea maslahi ya wanyonge mimi ninasema ni uzandiki na unduminakuwili uliopita kiwango.Matukio haya hayakuanza leo,sisi bado ni waathirika wa hali ngumu ya uchumi uliotokana na mapendekezo ya bunge yaliyoshindwa kuteekelezwa kwa kuwakumbatia waliotufikisha hapa kutokana na umeme wa magumashi usio natija uliopelekea nchi kuingia gizani na uchumi wa nchi kushuka kwa kasi kubwa.Tumeona Mwanyika anastaafu tena kwa staili ya waacheni wazee wapumzike,leo hii mwacheni mzee Luhanjo apumzike!hii ni fedheha kwa chombo kilichoaminika kama bunge.Ni bora kama chombo hiki kimeshindwa,wabunge wake wote bila kujali itikadi zao wajiuzulu,huu ni ushauri wa bure tena mtajijengea heshima na kuonyesha nini maana ya utawala bora.


Mwisho,Napata sana mashaka kwa serikali iliyoko madarakani kama kweli inajua nini inafanya madarakani.Mgawanyo wa madaraka mbona unakiukwa na sisi wananchi tunaangalia bila kusema lolote!Serikali legelege siku zote huipeleka nchi kizani.Hujichukulia madaraka yote na kujifanya yenyewe ndiyo refari,mchezaji,kamisaa na mtazamaji.Kitendo cha serikali kutia pamba masikioni na kupuuza mapendekezo ya bunge ni udhallishaji mkubwa si kwa bunge tu bali na watu waliolisimika bunge hilo(wananchi).Umangimeza huu wa serikali una kikomo chake,ipo siku isiyo na jina wenye nchi tutafanya maamuzi magumu yanayoshindwa kufikiwa na bunge hili legelege na hakika hatutarudi nyuma mpaka kieleweke.
 
SEREKALI HII MIMI SINA HAMU NAYO...MIMI NAPENDEKEZA NCHI HII BUNGE LIFUTILIWE MBALI TUWE TUNACHAGUA RAISI TU.NDUGU YANGU S:juggle:
 
• VITA BARIDI YA USPIKA YAWAKERA WENGI

na Mwandishi wetu
UENDESHAJI wa shughuli za vikao vya Bunge kwa mwaka 2011, uliongozwa zaidi na msukumo wa kisiasa na uliolenga kulinda na kutetea masilahi ya upande mmoja badala ya kuzingatia mambo muhimu ya kitaifa.

Wakielezea maoni yao katika utendaji wa Bunge, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Mkuu, Jude Thadaeus Ruwa'ichi, pamoja na Askofu Mkuu wa Anglikana Tanzania, Dk. Valentino Mokiwa, walisema Bunge lilishindwa kufanya vizuri zaidi kutokana na kukosa uongozi wenye uelewa mpana wa kutambua mahitaji ya taifa.

Ruwa'ichi ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Kuu la Mwanza, alisema Bunge la Jamhuri ya Muungano lingeweza kufanya vizuri zaidi kutokana na kuwa na mchanganyiko wa wabunge kutoka vyama tofauti wenye uwezo mkubwa lakini uongozi wake umekuwa ukishughulikia mambo mbalimbali kwa mtazamo wa siasa za chama kimoja.

"Bunge kama lingeongozwa na uelewa mpana wenye kutambua historia ya nchi yetu ilikopitia na wapi tulipo, ni wazi lingeweza kufanya vizuri zaidi kwa kuwa lina watu wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja lakini uongozi uliyashughulikia mambo ya msingi visivyo," alisema Ruwa'ichi.

Alisema bado kuna kigugumizi cha watawala kukubali kwamba nchi iko kwenye mfumo wa vyama vingi, ikiwa ni kukabiliana na changamoto ya hoja zinazoibuliwa kama mbadala wa maendeleo, badala yake kilichofanyika ni kujaribu kuwaziba midomo wapinzani.

Naye Dk. Mokiwa alionesha kushangazwa kwake na namna Bunge lilivyoacha kujadili mambo ya msingi, na kuanza kuwajadili wabunge wa upande mwingine, jambao alilosema halikuwa kipaumbele kwa wananchi.

"Bunge lilikuwa na changamoto kubwa katika baadhi ya matatizo yakiwamo kujadili hoja nzito kwa kufuata masilahi ya chama na kufumbia macho mambo muhimu ya kitaifa," alisema Dk. Mokiwa.

Akizungumzia juu ya mhimili huo wa nchi, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema Bunge lilionesha udhaifu mkubwa pale Spika Anne Makinda na Katibu wake, Dk. Thomas Kashilillah walipopingana waziwazi kuhusu suala la ongezeko la posho.

Alidai kuwa kusigana huko kulitoa kielelezo cha wazi jinsi wakuu hao wa Bunge wanavyoendesha chombo hicho kwa namna ya utengano na pasipo masikilizano.

Pamoja na hayo, alisema idadi kubwa ya wabunge ni mzigo kwa serikali kutokana na kutumia rasilimali nyingi kuwahudumia wao, badala ya kutatua kero za wananchi.

"Hali hii inasabaishwa na mfumo wa muungano wa kuwa na serikali mbili, lakini tungeweza kuwa na Bunge dogo la Muungano lenye wabunge wachache ambalo lingekuwa bora zaidi," alisema.

Hata hivyo, Mwenyekiti Mwenza wa Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) na Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, alisifu uendeshaji wa Bunge akidai lilionesha ukomavu wa kisiasa.

"Tulishuhudia mbwembwe na vitimbi na vilikuwa vizuri vikiashiria kukomaa kwa demokrasia.
"Tulishuhudia wabunge wakitoka nje wakiashiria kwamba kila chama kina wajibu wa kudai haki yake kwa stahili yake," alisema Dk. Bana.

Jambo jingine ambalo alilipongeza ni hatua ya wabunge kuikataa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, hatua iliyosababisha wizara hiyo kuifanyia marekebisho ya hali ya juu kabla ya kupelekwa tena bungeni.

Alisifu pia hatua ya Bunge kulilipua sakata la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, hali iliyosababisha Bunge kuunda kamati ya kuyachunguza.

"Kwa ujumla mambo hayo na mengine yaliibua changamoto kubwa bungeni hivyo kulifanya kutimiza wajibu wake wa kuidhibiti serikali kikamilifu," amesema.

Mbali na viongozi hao, wananchi wengi waliohojiwa na Tanzania Daima, walisema hawakuridhishwa na namna Bunge lilivyojadili mambo mengi ya msingi ya kitaifa.

Suleiman Nassoro, mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam, alisema kuwa wingi wa wabunge wa Chama cha Mapinduzi, ulitumika vibaya kukidhi mahitaji na malengo ya chama hicho na kusahau kuwa walitakiwa kuwakilisha masilahi ya Watanzania wote.

"Hata kama mimi ni mwanachama wa CCM, napenda niseme wazi kuwa wabunge wangu hawakutenda vema kwa mwaka huu. Kwanza kulikuwa kama kuna namna ya kukomoana baina yao, hasa baada ya kuteuliwa kwa spika mpya na kuachwa yule wa zamani, lakini baadaye ikawa vita kati ya wabunge wa upinzani na wa CCM," alisema.

h.sep3.gif

 
Back
Top Bottom