Ni makosa makubwa kushinikiza Serikali - Dk Benson Bana

msomi kutoka chuo kikuu cha dsm dk benson bana amesema ni makosa makubwa serikali kuongozwa kwa mashinikizo.dk bana alikuwa akirejea shinikizo la kuwawajibisha mawaziri mafisadi na wazembe lililotolewa na bunge katika kikao kilichoisha jumatatu wiki hii.dk bana ameonyesha kukerwa na kitendo hicho kwani ni kutaka kuyumbisha serikali.

source:uhuru jumatano

hiyo source inatia kinyaa!!
 
Msomi kutoka chuo kikuu cha DSM Dk Benson Bana amesema ni makosa makubwa serikali kuongozwa kwa mashinikizo.Dk Bana alikuwa akirejea shinikizo la kuwawajibisha mawaziri mafisadi na wazembe lililotolewa na bunge katika kikao kilichoisha jumatatu wiki hii.Dk Bana ameonyesha kukerwa na kitendo hicho kwani ni kutaka kuyumbisha serikali.

Source:Uhuru Jumatano

Kwa kawaida huwa sitoi maoni yangu kwa kila anachokisema huyu "msomi dr" Bana kwa kuwa sijawahi kumsikia akitoa maoni yeyote yanayo-justify hata kidogo kuwa nae ni msomi. Lakini hii ya leo imenikumbusha thread ya mjumbe mmoja hapa ukumbini aliehoji elimu yetu na jinsi watu wanavyopanda vyeo nchini kwetu.

Kusema ukweli lazima kuna uwalakini na mfumo mzima wa maisha yetu kwa ujumla (elimu, namna ya kupata viongozi, kupandisha watu vyeo and all that), otherwise iweje Bana akawa na PhD halafu akawa anatoa utumbo kila siku? Sitarajii mtu awe anatoa maoni yanayokubalika na wote siku zote, lakini kutoa utumbo tu kila siku???

Ilikuwaje kikwete akawa Kanali wa Jeshi? Mwanajeshi gani -tena afisa mkubwa-asieweza kufanya maamuzi? Hivi huyu alipataje degree? Inakuwaje mganga wa kienyeji - na ni semi-illiterate akawa mbunge? Kuna kipindi Hadija Kopa (yule mwimbaji wa taarabu) alikuwa mjumbe wa NEC, kweli unategemea mtu wa aina hii aelewe - achilia mbali kufanya maamuzi- kwa jambo lolote la maana linalohusiana na kuendesha nchi? What is wrong with us????

I can't even begin to understand this situation of ours!!!!!!
 
Pamoja na kwamba mi sio msomi kama yeye lakini nafikiri mojawapo ya majukumu ya bunge ni kuisimamia serikali ikiwa ni pamoja na kumshauri Rais pale inapofaa.... Kuishinikiza serikali sio kosa na ndo mana katiba inaruhusu KURA YA KUTOKUA NA IMANI YA RAIS au WAZIRI MKUU
 
Msomi kutoka chuo kikuu cha DSM Dk Benson Bana amesema ni makosa makubwa serikali kuongozwa kwa mashinikizo.Dk Bana alikuwa akirejea shinikizo la kuwawajibisha mawaziri mafisadi na wazembe lililotolewa na bunge katika kikao kilichoisha jumatatu wiki hii.Dk Bana ameonyesha kukerwa na kitendo hicho kwani ni kutaka kuyumbisha serikali.Source:Uhuru Jumatano
Ukiona msomi wa level ya udaktari(haijalishi kaipata vipi) anakosa aibu na kuzungumza mambo ya namna hiyo ujue anakaribia kufa.Shehe Yahya naye siku za mwisho za Uhai wake alikuwa anatoa matamko tata namna hiyo kilichofuata baada ya muda mfupi wote twakijua. Huyu Bana muda si mrefu tutamwimbia nyimbo na kumuombea
 
Eh!, wasomi wa Tanzania hao....Mwl Nyerere aliwahi kusema mwaka 1966 kuwa tatizo la Africa sasa ni wasomi, baada ya wakoloni kuiba mali za africa, sasa wasomi ndio zamu yao, wanataka mishahara mikubwa, watachukua mashamba yote yawe ya kwao....hela ambazo zingetumika kutoa huduma za afya ndio hizo wanazifuja hovyo.... na akina Bana wanasema serikali isishinikizwe... kazi ipo. Hivi Huyu Bana asingekuwa amepata nafasi ya kusoma angekuwa wapi?bado anadhani ajira yake ni zawadi, si haki yake, anajua kujenga barabara serikali inawasaidia tu wananchi sio haki yetu, bana anadhani serikali kuwasomesha wananchi kama yeye alivyo soma ni upendo tu wa serikali kwake.......hapa mzee , Serikali inakusanya kodi toka katika shughuri zetu wote, ili ijenge barabara, itowe huduma za afya, elimu n.k...... na lazina iwe accountable kwa hele za wananchi
 
Maneno aliosema Dr. Bana yamenifanya nitilie shaka elimu yake na anachowafundisha vijana wetu, Serikali ni yetu na mamlaka yote yapp mikononi ya wananchi, kama serikali tulioipa dhamana imeshindwa kulinda na kutumia rasilimali kwa manufaa ya nchi tuna mamlaka ya kuwatimua achilia mbali kuwashinikiza.
 
Napendekeza iundwe tume ichunguze ni nani alimpa huyu BANA vyeti wakati dalili za awali zote zinaonyesha huyu ni msukuma mkokoteni?

Huyu mzee shule yake ni ya kweli maana PHD yake ni ya Manchester UK.Nimejaribu kusoma gazeti lenyewe la Uhuru alichoeleza ni tofauti na kichwa cha habari .Huu ni uhuni tu umetumiwa na Mhariri wa gazeti la magamba
 
Jamaa anajitahidi kutetea REDET yao. Bilashaka anataka kuvunja rekodi ya Muhammad Saeed al-Sahhaf or Ali Hassan al-Majid (comical Ali), ila Nape bado anaongoza.
 
Hapo sikubaliani na Dr. Bana kabisa, Mawaziri wanafanya ufisadi na ushahidi upo halafu watu wasiwajibike, hiyo hapana, kama kuna shinikizo kwa mtu msafi hapo unasema sawa lakini kwa mtu ambae anaihujumu nchi na wabunge wamehakikisha hilo sasa kwa nini shinikizo lisitoke, TZ ni tofauti na nchi nyingine, kujiuzuru inaonekana ni kitu kigumu saana, ila kwa wenzetu ni kiti cha kawaida

Dr unadhalilisha taaluma hata kama wewe ni mtaaluma wa siasa na mdau mkubwa wa ccm
 
Msomi kutoka chuo kikuu cha DSM Dk Benson Bana amesema ni makosa makubwa serikali kuongozwa kwa mashinikizo.Dk Bana alikuwa akirejea shinikizo la kuwawajibisha mawaziri mafisadi na wazembe lililotolewa na bunge katika kikao kilichoisha jumatatu wiki hii.Dk Bana ameonyesha kukerwa na kitendo hicho kwani ni kutaka kuyumbisha serikali.

Source:Uhuru Jumatano

Amefilisika kisiasa, pia anafungu serikalin, mwambie akaseme Misri, Tunisia vile wananchi wamezipindua serikal zao.
 
Msomi kutoka chuo kikuu cha DSM Dk Benson Bana amesema ni makosa makubwa serikali kuongozwa kwa mashinikizo.Dk Bana alikuwa akirejea shinikizo la kuwawajibisha mawaziri mafisadi na wazembe lililotolewa na bunge katika kikao kilichoisha jumatatu wiki hii.Dk Bana ameonyesha kukerwa na kitendo hicho kwani ni kutaka kuyumbisha serikali.

Source:Uhuru Jumatano

Kwani shinikizo ni nini? Na lina tatizo gani kwa serikali? Je shinikizo linaweza kutokana na makosa ya liutendaji ya serikali? mboa sielewi huu uzi?
 
Katika kauli 20 atakazotoa huyu mzee 2 tu ndio huwa zina mantiki, nyingine zote ni kukoboa tu. Wajibu wa bunge ni kuisimamia serikali. Sasa usimamizi bila maelekezo ni upotofu.
 
Nikwamba huyo dk inawezekana ni mgojwa hajijui ama ni mmoja wa wenye vitaro walio gawiwa bila kuomba tunaomba tume imchunguze ama aende Hospitary
 
Msomi kutoka chuo kikuu cha DSM Dk Benson Bana amesema ni makosa makubwa serikali kuongozwa kwa mashinikizo.Dk Bana alikuwa akirejea shinikizo la kuwawajibisha mawaziri mafisadi na wazembe lililotolewa na bunge katika kikao kilichoisha jumatatu wiki hii.Dk Bana ameonyesha kukerwa na kitendo hicho kwani ni kutaka kuyumbisha serikali.

Source:Uhuru Jumatano

Ndowasomi wa bongo balafu
 
ndiyo mbunifu wa vimisemo vyote unavyovisikia kwa m_kwere, including hiki cha "Ni upepo wa kisiasa tu...utapita"
 
Msomi kutoka chuo kikuu cha DSM Dk Benson Bana amesema ni makosa makubwa serikali kuongozwa kwa mashinikizo.Dk Bana alikuwa akirejea shinikizo la kuwawajibisha mawaziri mafisadi na wazembe lililotolewa na bunge katika kikao kilichoisha jumatatu wiki hii.Dk Bana ameonyesha kukerwa na kitendo hicho kwani ni kutaka kuyumbisha serikali.

Source:Uhuru Jumatano

Duu nilitaka kushangaa nilidhani hii habari imetolewa kwenye vyombo vya habari:ranger:
 
Nawashangaa kutoa maoni yenu muhimu kwa rejea ya gazeti la UHURU.Heri Toilet Paper kuliko Gazeti la Uhuru.Gazeti la Uhuru ni rubbish tu wala usitoe rejea yako kwenye gazeti ilo.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom