ni makosa kuandika ''TUNAUZA MAFUTA YA TAA''...

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,301
4,681
sehemu mbali mbali hapa Tanzania nimekuta tangazo ''TUNAUZA MAFUTA YA TAA''.

Unapoandika unauza mafuta ya Taa inamaana Taa ndio imetoa ama kuzalisha mafuta yale.
Ni kama vile unapokuta mahali pameandikwa ''TUNAUZA MAZIWA YA NG'OMBE'', hapo wanamaanisha kuwa maziwa hayo yametoka kwa Ng'ombe.

Neno sahihi hapo ni ''TUNAUZA MAFUTA TAA''.

So ukikuta mahali pameandikwa hivyo basi mtafute muhusika kisha mnase vibao.
Akikupeleka polisi nitafute.
 
Mkuu ukitaka kulianzisha shurti ulichanganue kwa makini na hata hyo alternative yako umekosea hilo neno limetokana na matumizi mengi yalikuwa kwa ajili ya TAA,swali vp nikinunua kerosene nikaweka kwenye jiko la mchina? Je niite mafuta mchina? Je nikinunua kerosene nikaenda kuweka kwenye jenereta? Je niite mafuta jenereta? Jipange hakuna MAFUTA TAA wala MAFUTA ya Taa,mbona petrol au diseal hawajaita mafuta gari? Coz yana matumizi mengine zaidi ya gari,kwhyo hayo mafuta yanaitwa kerosene kwa kiswahili sijui labda mtafute makii hassan(BAKITA)
 
Mkuu ni wazi kuwa ulifeli darasa la 7 kihalali kabisa.
Nimezungumzia mafuta Taa na wala sijataja mafuta ya alizeti wala mafuta ya karanga.
Ninachojaribu kuelezea ni kitendo cha wazalendo wengi kutumia neno ''MAFUTA YA TAA''...kana kwamba Taa ndio imetoa yale mafuta.
Najaribu kueleza kuwa kwa kiswahili fasaha ni ''MAFUTA TAA''.
 
ok tuambie ww ulitakaje mana umelalamika tu hujatoa matumizi sahihi ili tusiendelee kukosea
 
Mkuu ni wazi kuwa ulifeli darasa la 7 kihalali kabisa.
Nimezungumzia mafuta Taa na wala sijataja mafuta ya alizeti wala mafuta ya karanga.
Ninachojaribu kuelezea ni kitendo cha wazalendo wengi kutumia neno ''MAFUTA YA TAA''...kana kwamba Taa ndio imetoa yale mafuta.
Najaribu kueleza kuwa kwa kiswahili fasaha ni ''MAFUTA TAA''.

Wewe uliyefaulu ndo unachemka kabisa,HAKUNA MAFUTA TAA,hilo neno umelitoa wapi? Google Kerosene uongeze ujuzi kidogo acha kuwapumbaza wananchi waongopee vilaza aka makameruni wenzakoM
 
Katika kuangalia utata huu, nimeona kuwa Tz bara wanasema "gari la abiria" wakati Tz visiwani wanasema "gari ya abiria." Ukiweza kuona utofauti hapo, hapana shaka unaweza kuondoa utata wako wa "mafuta taa."
 
ni kweli kabisa ni mafuta taa. zamani tulikuwa tunayaita mafuta taa na sijui hili neno mafuta ya taa lilitoka wapi. au treni inavyoitwa gari moshi na si gari la moshi.
 
Aaah hayo ni mafuta ya kibatari au kandili,hiyo taa ni yenu nyie wenyewe,neno taa lina wigo mpana sana sina haja ya kulielezea nadhani wote mnajua.
 
Kichomi hata ingekuwa ni kalabai basi yangeitwa ''Mafuta Kalabai''

Kwa sababu unaposema Mafuta ya Kalabai it means Ile ni product itokanayo na Kalabai.

Kwa hiyo hapa Tatizo sio Taa, Chemli, Koroboi wala Kandili
 
Enzi zetu Ilikuwa tunatamka Mafuta Taa kama neno moja. Ila ukilisikilza hilo neno toka kwa mtu mwingine utasikia akitamka MAFUTA YA TAA. Nahisi ndio chanzo cha hiyo YA.
 
sehemu mbali mbali hapa Tanzania nimekuta tangazo ''TUNAUZA MAFUTA YA TAA''.

Unapoandika unauza mafuta ya Taa inamaana Taa ndio imetoa ama kuzalisha mafuta yale.
Ni kama vile unapokuta mahali pameandikwa ''TUNAUZA MAZIWA YA NG'OMBE'', hapo wanamaanisha kuwa maziwa hayo yametoka kwa Ng'ombe.

Neno sahihi hapo ni ''TUNAUZA MAFUTA TAA''.

Bwana mdogo, lugha haiendi hivyo siyo mambo yote yanayofuata sheria. Tatizo lenu munatafsiri neno kwa neno na hasa kutoka kiingereza kwenda kiswahili. Lugha hizi mbili ni tofauti.

Jitahidi ujifunze mbinu mbali mbali za lugha
 
ni kweli kabisa ni mafuta taa. zamani tulikuwa tunayaita mafuta taa na sijui hili neno mafuta ya taa lilitoka wapi. au treni inavyoitwa gari moshi na si gari la moshi.

Labda kama wewe ni muhindi au muarabu, lakini mswahili orijino hasemi mafuta taa.

Jee mafuta taa iko babuji????????
 
Yaani kama hivi:

Mafuta ya taa [Mafuta taa?]
Mafuta ya kupikia [Mafuta kupikia?]
Mafuta ya kula [Mafuta kula?]
Mafuta ya kujipaka [Mafuta kujipaka?]
Mafuta ya ndege [Mafuta ndege?]

Bado sijashawishika!. Lugha, hasa majina, sio lazima iwe na mantiki! Lugha ni mazoea (ya muda mrefu?) tu baina ya wanajamii katika kuwasiliana.

Hata jina la mafuta ambayo tumezoea kwa kiingereza kuyaita 'diesel' (dizeli kwa kiswahili), kimsingi linatoka na matumizi kama ilivyo 'mafuta ya taa'. Kilichoanza ni Diesel Engine (Diesel likiwa jina la mvumbuzi wa aina hiyo ya injini ya gari)....hivyo mafuta ambayo yanatumika kwenye aina ya injini ya gari iliyovumbuliwa na Diesel, wakaanza kuyaita diesel! ('dizeli' ukipenda 'mafuta ya dizeli'). Hata hivyo aina zote hizo za mafuta bado zina majina yake ya kitaalamu.
 
Hayo mnaita makosa yaliyozoeleka...poleni
 
We ulikaa ukafikiria alafu unatuletea hapa na kusisitiza kua ni kiswahili. neno "ya" ni adverb inatumika kama "for" na pia inatumika kama "from". sasa unataka kutulazimisha ni "from" tu na ikitumika kama "for" ni makosa? kuna weza kua exception ila ukweli ndio huo.
 
  • Thanks
Reactions: SMU

Similar Discussions

Back
Top Bottom