Ni lini JK ataacha safari za nje?

bemg

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
2,799
642
Pamoja na Kuwa na utetezi wa safari zake za nje za mara kwa mara kwamba zinafaida kwa taifa .Je lini ataacha hizo safari?Na lini ataanza kufanya ziara kwa wananchi wa tanzania na kujionea mwenyewe kwa macho wanavyoteseka na mfumo mbaya wa serikali yake?Je anajua watanzania wengi wanaishi kwa matumaini ya kuona siku imepita na hajui kesho atakula wapi, atasomeshaje watoto wake na atatibiwaje?

Sidhani kama yuko makini na majukumu tuliyompa watanzania na amini hata moyo wake unamsuta kwamba serikali na chama chake hakiko makini na ameshindwa kukitendea haki kiti cha urais.

Nadhani hadi 2015 atakuwa ameweka record ya Rais aliyedhurura nchi nyingi za nje kuliko rais mwingine hapa Africa.

Rais wetu JK lini utatembelea kila pembe ya tanzania?
 
Unataka record gani? Mbona mpaka sasa kisha weka? Sema ataingia kwenye gns book! Kama hajaingizwa bado mpaka muda huu
 
ataacha pale tukimn'gatua magogoni au tukishindwa basi 2015 mwisho,. au ataomba kurudia waziri wa mambo ya nje tena???
 
Pamoja na Kuwa na utetezi wa safari zake za nje za mara kwa mara kwamba zinafaida kwa taifa .Je lini ataacha hizo safari?Na lini ataanza kufanya ziara kwa wananchi wa tanzania na kujionea mwenyewe kwa macho wanavyoteseka na mfumo mbaya wa serikali yake?Je anajua watanzania wengi wanaishi kwa matumaini ya kuona siku imepita na hajui kesho atakula wapi, atasomeshaje watoto wake na atatibiwaje?

Sidhani kama yuko makini na majukumu tuliyompa watanzania na amini hata moyo wake unamsuta kwamba serikali na chama chake hakiko makini na ameshindwa kukitendea haki kiti cha urais.

Nadhani hadi 2015 atakuwa ameweka record ya Rais aliyedhurura nchi nyingi za nje kuliko rais mwingine hapa Africa.

Rais wetu JK lini utatembelea kila pembe ya tanzania?

Siamini kama watanzania tulimpa jukumu lolote, alijipa yeye mwenyewe na familia yake na ndo maana anaogopa kutembelea wananchi aliowaibia kura.

Jibu la swali lako ni kwamba, JK ataacha ziara za nje siku wasanii wenzake wakifa mfululizo kwa sababu atapanga kuhani misiba mfululizo.
 
Back
Top Bottom