Ni lini inabidi tuseme ndoa hii sasa basi? Sehemu ya mwisho.

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,379
Jambo lingine ambalo linapojitokeza kwenye ndoa, mtu anashauriwa kuvunja ndoa hiyo ni ufujaji. Mara nyingi wanaofuja ni wanaume, ingawa wanawake wapo pia kwa kiasi kidogo.

Kufuja namaanisha kumuumiza mpenzi kwa makusudi kwa kauli au vitendo.
Inaweza kuwa ni kwa kashfa, kusimanga, kubeza, kutukana kuhusu mtu au familia alimotoka ama kuhusu uwezo na pia mwonekano wake. ‘Wewe mwanamke gani, wakiitwa wanawake nawe utakwenda kweli.' Ni baadhi tu ya kashfa.

Kuna kupiga, kusukuma, kusukasuka, kulazimisha tendo la ndoa na matumizi mengine ya nguvu.
Vitendo hivi vinaporudiwa mara kadhaa kwa lengo la kumfanya mwingine ahisi vibaya na kumfanya anayetenda ajihisi mshindi, huku ndiko kufuja. Mara nyingi ushauri wa ndoa za namna hii ni mwanamke kuondoka.

Ushauri huu hutolewa haraka kwa sababu, ni vigumu kwa mfujaji kukubali kwamba anafuja na kusaidiwa kutoka humo. Pale ambapo mfuaji anakubali kwamba hiyo ni kasoro na yuko tayari kusaidiwa, hakuna haja kwa mwanamke kuamua kuvunja ndoa. Lakini pale ambapo mfujaji hakubali kwamba ana matatizo, ndoa hii ni kifo cha moja kwa moja.

Jambo lingine ambalo linachukuliwa kama kigezo halali cha ndoa kuvunjwa ni mume au mke kufanya mapenzi na mtoto wake. Kuendelea kuishi kwenye ndoa baada ya jambo kama hili kutokea ni kujidanganya. Baada ya tukio kama hili, hisia za wahusika hufungwa na uhusiano kwa njia zote hukwama. Wanaweza kukaa kama mke na mume lakini kweli ni kwamba, mmoja atakuwa anaumia kwa saa 24 za siku.

Jambo lingine ni jaribio lolote la mume au mke kutaka kumdhuru mwingine kimwili. Kuna wakati mume a mke anaweza kufanya jaribio la kutoa maisha ya mwenzake iwe ni kwa kumpiga au kumwekea sumu au chochote.

Jambo la mwisho kwa leo ni ni kauli halisi kutoka kwa mpenzi. Mke au mume anaweza kumwambia mwenzake kwamba, hamtaki au hampendi tena. Inapofikia hali kama hii, inabidi aliyejulishwa aulize vizuri kama mwenzake anasema hayo kwa dhati. Aliyesema anaposema ni kwa dhati, inabidi mhusika asubiri tena kauli hiyo kwa mara ya pili.

Anapotamka kauli hiyo kwa mara ya pili, inabidi aliyeambiwa aulize tena, na aliyeitamka akisema ni kwa dhati , mhusika inabidi asubiri kwa mara ya mwisho. Kauli ya ‘sikutaki tena' au ‘nimeshasema sikuhitaji' inaporudiwa kwa mara ya tatu, hapo ni lazma uamuzi ufanywe.

Mpenzi anapokwambia kwamba hakutaki mara tatu, huna sababu ya kujipendekeza, kwa sababu wewe ni binadamu kamili kama yeye. kujipendekeza kuna maana ya wewe kuwa dhaifu kwake na hivyo kujiumiza na kujishusha bure.

Kumbuka kama mume au mke amethubutu kututamkia mara tatu kwamba hakutaki uking'ang'ania kuishi naye, ni lazima atakudhuru. Kumbuka hakutaki na tusichokitaka huwa tunakiondoa kwa njia yoyote tunayomudu kutumia.
 
1.Ndoa ikishafungwa imefungwa,haitakiwi ivunjwe....labda mmoja amefariki au mmoja kashikwa redhanded akifanya zinaa, HAPO NDOA ITAVUNJWA.
2.Zaidi ya hapo ...itabidi KUVUMILIANA NA KUTOHESABU MAOVU YA MWENZAKO.
3.USICHOTAKA KUTENDEWA KWA NINI UNAMTENDA MWENZIO???.........Hapo matatizo tunayaanza wenyewe.
4.Kukashifu,kutukana,kudharau,kumsema au kumpiga mwenzio haisaidii kumbadili mtu tabia.......huyo mpenzi wako miaka yooooote kalelewa na wazazi wake hawakumbadili tabia leo wewe unataka umbadili.......UTAKUWA UNACHEZA MAKIDA......na kwanini uliamua kuoana na mtu kama huyo???
5.Baki na ulie nae UTAMALIZA MABUCHA NYAMA NI ILEILE.
6.Mara nyingi madereva wa hili gari liitwalo T....MAPENZI ni sisi wanaume na ni siri iliyowazi kuwa mara nyingi tunaliingiza gari kwenye mtaro halafu tunamlaumu KONDA/KONDAKTA.
7.TUNAOANA NA BINADAMU WENZETU SI MALAIKA, HIVYO MWENZIO ANA MATATIZO KIBAO NA WEWE UNAYO PIA....DAWA NI UVUMILIVU.
 
Tall hebu rudia kusoma mada kisha utoe ushauri nadhani haujaelewa kilichoandikwa!
 
usipomuenzi mwenzio ni kuwa unajichukia nafsi yako mwenyewe.........na kamwe huwezi ukawa na amani kwenye nafsi yako......................kamwe hailipi kutesa wenzio...................
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom