the truth is that the CCM government has acted arbitrarily and is not alive to the grave situation into which it has plunged the country. By being biased and allowing itself to be duped by the Catholic clergy that Muslim preaching was insulting to Christianity, the CCM government has embarked on a course of action which violates the constitutional rights of Muslims to propagate religion, is arbitrary and without any regard to the due process of law - [URL="http://www.igs.net/%7Ekassim/mwembechai/index.html"](Barua ya Abu Aziz kwa Mwanasheria Mkuu; Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania)
[/URL]
Nipo katika kuandika makala fupi yenye kuhusiana na kichwa hicho cha habari. Swali hili limekuja baada ya kusoma hoja alizotoa Mufti Shehe Shaaban Bin Simba akiitetea serikali ya CCM na uongozi wake.
Nilichukua muda kidogo na kurudi kusoma vitabu viwili ambavyo ni maarufu miongoni mwa Waislamu wa Tanzania ambavyo vinaelezea kwa kirefu jinsi CCM na serikali yake ilivyowakandamiza Waislamu. Kitabu cha Prof. Hamza. M. Njozi - ambaye kwa wanaokumbuka nilifanya naye mahojiano ya kina mwaka 2006 - cha "Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania" na kupitia maandishi ya Bw. Mohammed Said kuhusu historia ya Waislamu katika harakati za uhuru - ikiwemo kile kitabu kinachomhusu Abdulwahid Sykes.
Vitabu hivyo viwili na maelezo mengi ya ziada kabla ya 2010 yalijaribu kutuaminisha kuwa CCM ndio ilikuwa kikwazo cha maendeleo ya maslahi ya Waislamu:
a. Kuanzia kufutwa kwa EAMWS hadi mauaji ya Mwembechai na mambo mengine yote kati yake.
b. Kwamba pamoja na jitihada mbalimbali CCM iligeuka na kuwa sehemu ya Kanisa au kutumiwa na Kanisa - Dr. Njozi na barua ya Abu Aziz vinathibitisha mashtaka hayo makubwa.
Sasa, bila ya kwenda mbali sana kuna kitu kimebadilika hivi karibuni ambacho kinawafanya Waislamu kuiunga mkono CCM na uongozi wake. Utetezi mkubwa uliofanywa na vyombo mbalimbali vya habari vya Kiislamu na watu mbalimbali wakati wa kampeni kuitetea CCM kwa wapiga kura vinanifanya niamini kabisa kuwa kuna kitu cha msingi sana ambacho kimebadilika kiasi cha kuifanya CCM - chama ambacho kilikuwa kinaonekana na kiini cha tatizo ya Waislamu kuanza kupendwa, kukumbatiwa na hata kufikia serikali yake kutetewa kwa kiasi ambacho hatujawahi kuona.
Ndio swali liko mbele yetu; CCM imebadilika kitu gani hadi kuwa rafiki wa Waislamu leo hii? Ni sera na mfumo gani wa CCM ambao unawafanya baadhi ya Waislamu kuona kuwa maisha na maslahi yao yatalindwa vizuri na CCM kuanzia sasa? Je, endapo uongozi ujao wa CCM utakuwa ni wa tofauti na huu uliopo bado CCM itapata support hii kubwa? Je, makosa yote ya CCM na serikali yake ya huko nyuma yamesamehewa na sasa "tugange yajayo" au yamewekwa kiporo tu ili ukija uongozi tofauti na huu wa sasa yakumbushiwe tena?
Je, Waislamu wote wanatakiwa kuanzia sasa kuiunga mkono CCM, kutoikosoa, kutoilalamikia, kutoonesha makosa yake wala kutokubaliana hata kidogo na wale wenye kuikosoa? Kwa maneno mengine, Muislamu anaweza kuwa Muumini mzuri huku bado anaendelea kuipinga CCM kinyume na maelekezo ya viongozi wake wa kidini? Au bado wapo baadhi ya Waislamu ambao msimamo wao haujatetereka dhidi ya CCM na serikali yake?
Ni maswali ya uchokozi wa kifikra tu. Natumaini mawazo yenu juu ya somo husika yatanisaidia kuandika makala ambayo itajaribu kushughulikia suala hili kwa kiasi cha kutosha.
Mimi nina maoni haya:
1. Kama CCM ya zamani, ambayo kwa mtazamo wangu ilikuwa better, inashutumiwa kuwakandamiza Waislamu, CCM ya sasa, ambayo inakumbatia ufisadi na viongozi wasiowajibika, haiwezi kuwa imebadilika kuwanufaisha Waislamu unless kama na wao wanashabikia huo uozo. Ni kitu gani ambacho serikali ya CCM imekifanya kuboresha maisha ya Watanzania wakiwemo Waislamu has huduma muhimu za jamii kama vile elimu na afya wakati matokeo ya shule zetu yanaendelea kuwa mabaya na huduma ya afya ndiyo hiyo tena?
2. Mimi naona provided CCM itakuwa na viongozi wa kuu wa nchi Waislamu kama ilivyo sasa itaendelea kupendwa na Waislamu na ikitokea wakawepo wa dini nyingine mapenzi yataisha.
3. CCM haijabailika kiasi cha kutoka 'bad kwenda good' ila ilipoona inalaunmiwa kutotekeleza ahadi yake ya kutafuta ufumbuzi kwa suala la Mahakama ya Kadhi, ikaahidi kuanzisha Mahakama ya Kadhi na Tanzania kujiunga na OIC. Tangu hapo Waislamu wakaona CCM ni chama kinachosikiliza kilio chao. Wakati wa kampeni walikuwa wanampiga vita Dr Slaa na magazeti yao yalichangia sana na sasa wameanza kukipiga vita waziwazi Chadema na sababu yake si kitu kingine ni udni kwa vile wanaamini chama hicho kina waumini walio wengi Wakristo.