Ni lini CCM ilibadilika na kuanza kuwa rafiki wa Waislamu Tanzania?

Status
Not open for further replies.
My taking of this matter is this: CCM understands that tribal/religious roots go much deeper than the shallow flowers of democracy. The problem is for Waislamu to understand is that in competitive politics enfeebled parties like CCM look for the easiest way to establish their superiority in voters' eyes; providing services like health, schools and roads/ fighting impunity is one way of winning electorates approval, but such things are hard to party which suffers from parochialism to deliver! CCM has played ethnic/ religious identity cards before but it failed in the previous attempts, but this time around it has proved incredibly easily. Hawa viongozi wa kiislamu wajue kwamba we have had no ethno elitism or religious elitsm, what we face today in our country is grossly family/mafisadi elitism. Waiache ccm ijioshe yenyewe kinyesi chake kwani kila utetezi watakaoutoa kwa ccm will not be spared from scrutiny.
 
We ni kadogoo au katotoo ila me nakuita kafisadii.
Kafisadii unasema CDM haina sera yoyote ya kuwaondolea kero waislamu kero zipi hizo? hebu fafanua then CDM sio FBO ni CSO hivyo vision na mission yake hailengi kutatua matatizo au kero za upande mmoja wa dini. CDM ipo kwa ajili ya wananchi wa TZ bila ya kujali dini, rangi, kabila.
 
MZEE MWANAKIJIJI ME HUWA NAKUBALI SANA MAWAZO YAKO NATAMANI KICHWA CHAKO KINGEKUWA KWANGU. GIV ME SOME TECHNIQUES TO BE LIKE U. WE CAN CHAT THROUGH FACEBOOK VISIT TO mchaga mjanja profile.

The best person u can be, is being YOURSELF. Angalia strength zako na uzitumie. Waweza kuwa msikilizaji mzuri kuliko muongeaji, ni talent pia. Jitambue, jipende na jijenge!
 
Historia ya uislam na maendeleo imekuwapo tokea enzi na enzi. Ukiangalia kwa undani utaona kuwa historia hii inaenda nyuma tokea kabla ya uhuru. Mzee wangu alikuwa akinisimulia kuwa wakati wa Ukoloni shule nyingi zilikuwa zikimiliwa na christian missionaries, sharti moja wapo la kusoma shule hizi lilikuwa ni kushiriki katika misa za kikristo jambo amabalo liliwafanya wazazi wengi waliopo katika madhehbu ya kiislam kuogopa kuwapeleka watoto wao shule za kimisionari, japo evidence leo hii inaonesha kuwa wale waliopelekwa majority walibakia na dini yao ya uislam.

Kutokana na sababu hiyo Taifa baada ya kupata uhuru wasomi wengi waliokuwepo wakati huo ni wale waliohudhuria shule za kimisionari ambazo leo hii baadhi yake ambazo zimebadilishwa majina ni kama vile Tanga School, Mirambo, Tabora School, Minaki, Forodhani etc.

Baada ya uhuru serikali ya TANU ilitakiwa kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha inabadili mitazamo ya wazazi wa kiislam kupeleka watoto wao shule kwani hofu ile ya kubadilishwa dini haikuwepo tena ila TANU haikufanya hivyo(Kosa la kwanza la CCM dhidi ya waislam)

Kwa kutambua kabisa kuwa jamii ya waislam ilikuwa nyuma katika elimu kutokana na historia na kutochukua hatua yoyote ya kuiamsha, ilikuwa ni wazi kabisa kuwa serikali ya TANU/CCM ambayo ilikuwa ikiongozwa na wazomi wengi walio katika madhehbu ya kikristo, ilikuwa ni wazi kuwa CCM kwa makusudi haikutaka kuwainua waislam kwa kuhofia kuwa wanaweza kuja kuwazidi wakristo serikalini na kuigeuza nchi kuwa Taifa la kiislam, na hapo ndiyo dhana ya CCM na kanisa kuwa kitu kimoja ikazidi.(Kosa la pili la CCM dhidi ya waislam)

Katika mfumo wa elimu ilitokea kuwa katika wanafunzi mia wanaofaulu kuendelea kidato cha kwanza basi waislamu hawakuzidi 15, japo shule ya msingi walikuwa ni 50%-50%. Hii inawezekana kabisa ilisababishwa na wazazi wengi wa kiislam kutowasimamia vema vijana wao katika kusoma nyumbani na kuwasisitizia elimu ya madrasa kwa kuwa wao hakupata elimu na kujua umuhimu wake, lakini uvumi ulikuwa ni mkakati uliofanywa na serikali ya CCM wakishirikiana na kanisa kuhakikisha waislam hawavuki kwa wingi kwenda elimu ya juu. CCM ilitakiwa kufanya makusudi kuwahamasisha wazazi ambao wengi wao hawakuhudhuria shule umuhimu wa elimu dunia ila kwa makusudi hakawakufanya hivyo. Moja ya matunda haya tunayaona katika safu kuu ya uongozi wa BAKWATA ambapo sheikh mkuu ni mmoja kati ya wazamiaji wakuu wa elimu ya dini ila wana zero understanding of the world as it should be ndiyo maana wanakuja na matamko ya ahera zaidi ya kidunia katika mambo ya dunia.

Kwa ujumla ukiangalia adui mkuu wa maendeleo ya waislam ni CCM na serikali yake ambazo ama kwa makusudi au kwa kutokujua ili wa-ignore waislam mara tu baada ya kupata uhuru na mpaka leo inaendelea kuwa ignore na hata kuwatungia sheria ya ugaidi mara baada ya mashambulizi ya WTC kwa shinikizo la wakubwa. Waislam hawana budi kukaa na kujiuliza maswali yafuatazo

CCM na serikali yake inaendelea kuwadhalilisha waislam mbele ya watanzania wengine kwa kutumia wale ambao hawakupata elimu ya kupambanua mbichi na mbivu, kutumia udhaifu wao wa kiuchumi ambao ulisababishwa na CCM yenyewe kwa kuwalubuni kwa hela ili watoe matamko yanayopingana na hali halisi ya maisha yao ili kuiwezesha CCM iendelee kupata ridhaa ya kuendelea kuwakandamiza wao, watoto na wajukuu zao bila wao kujijua?, Ni nani asiyekuwa na kumbukumbu kuwa waislam hawahawa walisakamwa kwa kutumia uhuru wao wa kikatiba kuchagua chama cha kisiasa na wengi wakafurahishwa na sera za CUF, ambapo CCM iliwazushia kila aina ya majina mabaya yakiwemo chama cha kigaidi kwa kuwa wao walikuwa wengi kwenye chama hicho?, ni nani asiyejua kuwa visu(majamvia) ni silaha zenye uhusiano na watu wenye utamaduni wa masharikiri ya kati ambao majority ni waislam, CCM ikawasingizia kuwa CUF chama cha kigaidi (Kwa kuwa walikuwa wanakisupport wengi walikuwa ni waislam) kuwa wameingiza kwa lengo la kufanyia ugaidi?

1. Je ni serikali ya Chama gani iliyoua waislam wasiokuwa na hatia pale mwembechai mwaka tarehe 13/2/1998?

2. Je ni serikali ya Chama gani iliyoua waislam kule Zanzibar January 26 na 27 mwaka 2001?

3. Je tokea tupate uhuru ni chama gani kimekuwa madarakani?

Kama majibu ya maswali hayo ni CCM, basi waislam hawana haja ya kukilaumu chama chochote kwa maendeleo yao na uonevu dhidi yao zaidi ya CCM. Na leo hii Muislam kusimama na kuitetea CCM kifua mbele ni kukubali kuwa wale waliouwawa mwenyechai, Unguja na Pemba ambao ni waislam wenzao kuwa ni kweli walikuwa magaidi na walistahili hukumu ile, huu ni unafiki na adhabu ya mnafiki ni fi-nari jehanam

Kweli kazi ipo...sasa wewe ulisomaje kama kulikuwa na vikwazo hivyo?....je dini ipi iliikuta ingine Tanganyika?...iliyokuwepo awali kwanini haikujenga shule zake?...unajua shule ngapi za makanisa zilitaifishwa ili watanzania wote wasome(si wakristu na waislam tu hata wapagani,baniani n.k.)?..je unajua kuwa Dr Kighoma Malima mwaka 1982 alimshauri Mwalimu kuwa wanafunzi wote toka seminari wasiruhusiwe kujiunga kidato cha tano hata wafaulu vipi ili waislamu nao 'wasome' na Mwalimu akakubali?...Unajua kuwa Mwinyi mwka 1992 aliataka kuzirudisha shule zilizotaifishwa kwa wenyewe na alipotishwa na BALUKTA ya Sheikh Yahaya akabadili msimamo? Bado utasema waislamu wanaonewa?
 
The best person u can be, is being YOURSELF. Angalia strength zako na uzitumie. Waweza kuwa msikilizaji mzuri kuliko muongeaji, ni talent pia. Jitambue, jipende na jijenge!

Hakuna anayejijenga mwenyewe kwa uwezo wake mwenyewe.
 
mzee mwanakijiji., hii ni mada muafaka kabisa. Jana kulikuwa na kongamano kubwa kabisa pale kwenye msikiti wa bondeni jiji arusha. Kulikuwa na mada mbalimbali na wasemaji tofauti. Wote waliwaaminisha wasikilizaji wengi wakiwa wamevaa baglashia na hijabu kuwa kila anapokuwa rais muislamu basi wakristu huanza chokochoko zao.Pia walidai wakristo hawapendi kuongozwa na muislamu na jeykey kafanya mengi mazuri kuliko chinga ila watu hawataki kuyasema mambo hayo. Pia waliwajibu maaskofu kuwa wao hawakurupuki na wanafanya utafiti kabla ya kusema.
 
Hili ni swali zuri sana kwa brain storming, lakini ni delicate mno pia, kwasababu hatupo wakweli na tu wanafiki zaidi au tuanataka kuwana siasa kali bila misingi ya ukweli.
Nilazima tuonyeshe ukweli kwa matatizo yetu na kutofautisha na uchochezi. Hoja nyingi ni uchochezi zaidi.
Mara nyingi malalamiko ya wale wanaodai waislamu wameonewa wana hidden motives, ambayo nionavyo mimi ni propagation of islamic faith and ideologies, na wao wenyewe au marafiki zao kupata nafasi za juu, pia ni mbinu chafu ya kuwapumbaza wakristu wakati waislamu wana jipatia upendeleo mkubwa. Hivi kweli Nyerere aliwaonea waislamu au wakristu? Tuangalie historia.
Uongozi wa juu wa kiislamu hutumika dunia zima kwa manufaa ya watawala. Sisi tunatakiwa kukomesha tabia hii isiendelee wala kushamiri kwa kutumia katiba na sheria.
Ieleweke tunaishi jamii msete kiimani, kati yetu nani anatatizo na jirani zake? Hawa wenyeuchu wa madaraka kiserikali na kiimani wasitupeleke huko kubaya.
Kuhitimisha MMKJ naona uislamu unatumiwa sijui ni semeje watawala/viongozi/mafisadi wetu kwa manufaa yao. Leo wataonyesha urafiki na CCM kesho uadui kulingana na maslahi ya hao wanaowatumia. Elimu ya uraia ni muhimu sana, kwa mfano Amerika ni muungano wa nchi zaidi ya 53, nani amewahi kusikia siasa za ujimbo jimbo? Hakuna kwa sababu ya katiba naelimu yao ya uraia.
Walaaniwe wale wote wanaotugawa kwa misingi ya imani, kabila ukada au political ideology
 
Kweli kazi ipo...sasa wewe ulisomaje kama kulikuwa na vikwazo hivyo?....je dini ipi iliikuta ingine Tanganyika?...iliyokuwepo awali kwanini haikujenga shule zake?...unajua shule ngapi za makanisa zilitaifishwa ili watanzania wote wasome(si wakristu na waislam tu hata wapagani,baniani n.k.)?..je unajua kuwa Dr Kighoma Malima mwaka 1982 alimshauri Mwalimu kuwa wanafunzi wote toka seminari wasiruhusiwe kujiunga kidato cha tano hata wafaulu vipi ili waislamu nao 'wasome' na Mwalimu akakubali?...Unajua kuwa Mwinyi mwka 1992 aliataka kuzirudisha shule zilizotaifishwa kwa wenyewe na alipotishwa na BALUKTA ya Sheikh Yahaya akabadili msimamo? Bado utasema waislamu wanaonewa?

Wewe unanijua mimi au kujua dini yangu?, au unajua elimu yangu?, au unajua mimi nimebobea kwenye nini?, Je nikikwambia mimi ni Padre au Sheikh utakubali au utakataa. Jibu hoja si ku quote na kuanza kutoa mawazo yako kwa general criticism. CCM ni adui namba moja wa waislam. Pinga kwa fact. Nikikwambia leo hii kuwa JK ni adui wa waislam kwa kuwa alimshughulikia Prof. Kighoma Malima kwa ku-freeze account zake za offshore ili asigombee urais kupitia NRA mwaka 1995 utakataa?.
 
Waislam wanaamini kuwa CUF ndo chama kitakachotetea maslahi yao.wala hawana urafiki na CCM,ila wana urafiki na JK,haya yatadhihiqika 2015.
 
Hili ni swali zuri sana kwa brain storming, lakini ni delicate mno pia, kwasababu hatupo wakweli na tu wanafiki zaidi au tuanataka kuwana siasa kali bila misingi ya ukweli.
Nilazima tuonyeshe ukweli kwa matatizo yetu na kutofautisha na uchochezi. Hoja nyingi ni uchochezi zaidi.
Mara nyingi malalamiko ya wale wanaodai waislamu wameonewa wana hidden motives, ambayo nionavyo mimi ni propagation of islamic faith and ideologies, na wao wenyewe au marafiki zao kupata nafasi za juu, pia ni mbinu chafu ya kuwapumbaza wakristu wakati waislamu wana jipatia upendeleo mkubwa. Hivi kweli Nyerere aliwaonea waislamu au wakristu? Tuangalie historia.
Uongozi wa juu wa kiislamu hutumika dunia zima kwa manufaa ya watawala. Sisi tunatakiwa kukomesha tabia hii isiendelee wala kushamiri kwa kutumia katiba na sheria.
Ieleweke tunaishi jamii msete kiimani, kati yetu nani anatatizo na jirani zake? Hawa wenyeuchu wa madaraka kiserikali na kiimani wasitupeleke huko kubaya.
Kuhitimisha MMKJ naona uislamu unatumiwa sijui ni semeje watawala/viongozi/mafisadi wetu kwa manufaa yao. Leo wataonyesha urafiki na CCM kesho uadui kulingana na maslahi ya hao wanaowatumia. Elimu ya uraia ni muhimu sana, kwa mfano Amerika ni muungano wa nchi zaidi ya 53, nani amewahi kusikia siasa za ujimbo jimbo? Hakuna kwa sababu ya katiba naelimu yao ya uraia.
Walaaniwe wale wote wanaotugawa kwa misingi ya imani, kabila ukada au political ideology

Deo; you are absolutely right. Pamoja na mbinu nyingine nyuma ya pazia, hakuna mbinu yenye nguvu kama ya KUTUNGA UONGO na KUURUDIA RUDIA kila mara na kila nafasi inapopatikana iwe kwenye mihadhara, vyombo vya habari, n.k. Mwishowe uongo huo mbele ya macho ya jamii huonekana kuwa ukweli.

Baadhi ya wachangiaji wamejaribu kuwaita baadhi ya hawa masheikh kuwa ni wajinga na "masheikh uchwara"; hapana! They are so clever, they know what they are doing na wamefundishwa hivyo toka vyuo vyao vikuu vya Uarabuni na kwingineko - KUTUMIA SILAHA YA UONGO dhidi ya taasisi nyingine ili ku-promote kile wanachotaka wao.

Chochote kitakachoongelewa na mwingine hata kama kina ukweli kwa asilimia 100% alimradi kiko kinyume na interest zao au wafadhili wao basi kitatungiwa kila aina ya uwongo na kuenezwa kwa nguvu lengo likiwa kuipumbaza jamii and at the end, through this weapon to win the battle.

LAKINI, kwa kuwa daima UONGO NI WA KITAMBO ndio maana mara kadhaa baadhi yao wanakosa misimamo; leo hii watasimama kutetea CCM bila kujali ufisadi na uchafu wa ajabu ndani ya chama hicho lakini kesho akisimama rais kupitia CCM ambaye hawana interest naye hawakawii kubadilika.

LAKINI kwa wenye busara, bila kujali itikadi au dini ni bora kuukemea uongo bila kujali unafaidika vipi na uongo huo. Kwa mfano hivi hao wa "dini nyingine" ndani ya CCM wanadhani watabaki salama kama CCM itageuka na kuwa chama chenye mlengo wa kiislamu au kufungamana na uslamu hata kwa taathira tu?

TAFAKARI NA CHUKUA HATUA - SIMAMA KATIKA UKWELI DAIMA HATA KAMA ITAGHARIMU MAISHA YAKO.
 
Mzee Mwanakijiji ... kwanza heshima mbele

hapa umemaliza kabisa ..... uadui iliyonayo CCM kwa wananchi wakiwemo waislamu muda wote wa utawala wake kwa kuwanyima maendeleo na maisha bora ndicho kitu tunachotakiwa kujiuliza .... na sasa uadui huu CCM inataka kuupeleka/kuhamishia kwenye chama fulani ambacho imeona ndicho tishio ili basi waendelee kuvimbiwa na rasilimali za nchi yetu nzuri tanzania ..... sasa basi sisiem itujuze je ni lini waliwahi kuwasifia waislam au hata kuwapatia ushauri kwa ajili ya maendeleo ya taifa kwa ujumla na si kuwatumia kwa maslahi tu ya kujikita madarakani .... hivyo basi kuhamishia ugomvi wa watanzaniA wakiwemo waislamu na sisiem kwa CHADEMA ...... hakika sisiem inatenda dhambi ambazo hakuna dini inayoweza kusamehe

Kinachonishangaza kwanini waislamu wasione kuwa ni maharamia fulani ndani ya CCM na wala si CCM wamewateka na sasa wanawatumia kama ngao kupata kile wanachokitaka? Vipi mtekaji akawa rafiki ya yule aliyemteka? Wasipojishugulisha kufikiri wataendelea kulalamika milele huku kila kundi likiwatumia kama daraja kuvuka ng'ambo na wakivuka basi kuling'oa na kulitupa kisha kutengeneza daraja bora zaidi ambalo kamwehalitatumia miti au vifaa vya zamani kwa kisingizio cha kupitwa na wakati; hiari ya shinda utumwa ndugu zangu waislam.
 
Historia ya uislam na maendeleo imekuwapo tokea enzi na enzi. Ukiangalia kwa undani utaona kuwa historia hii inaenda nyuma tokea kabla ya uhuru. Mzee wangu alikuwa akinisimulia kuwa wakati wa Ukoloni shule nyingi zilikuwa zikimiliwa na christian missionaries, sharti moja wapo la kusoma shule hizi lilikuwa ni kushiriki katika misa za kikristo jambo amabalo liliwafanya wazazi wengi waliopo katika madhehbu ya kiislam kuogopa kuwapeleka watoto wao shule za kimisionari, japo evidence leo hii inaonesha kuwa wale waliopelekwa majority walibakia na dini yao ya uislam.

Kutokana na sababu hiyo Taifa baada ya kupata uhuru wasomi wengi waliokuwepo wakati huo ni wale waliohudhuria shule za kimisionari ambazo leo hii baadhi yake ambazo zimebadilishwa majina ni kama vile Tanga School, Mirambo, Tabora School, Minaki, Forodhani etc.

Baada ya uhuru serikali ya TANU ilitakiwa kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha inabadili mitazamo ya wazazi wa kiislam kupeleka watoto wao shule kwani hofu ile ya kubadilishwa dini haikuwepo tena ila TANU haikufanya hivyo(Kosa la kwanza la CCM dhidi ya waislam)

Kwa kutambua kabisa kuwa jamii ya waislam ilikuwa nyuma katika elimu kutokana na historia na kutochukua hatua yoyote ya kuiamsha, ilikuwa ni wazi kabisa kuwa serikali ya TANU/CCM ambayo ilikuwa ikiongozwa na wazomi wengi walio katika madhehbu ya kikristo, ilikuwa ni wazi kuwa CCM kwa makusudi haikutaka kuwainua waislam kwa kuhofia kuwa wanaweza kuja kuwazidi wakristo serikalini na kuigeuza nchi kuwa Taifa la kiislam, na hapo ndiyo dhana ya CCM na kanisa kuwa kitu kimoja ikazidi.(Kosa la pili la CCM dhidi ya waislam)

Katika mfumo wa elimu ilitokea kuwa katika wanafunzi mia wanaofaulu kuendelea kidato cha kwanza basi waislamu hawakuzidi 15, japo shule ya msingi walikuwa ni 50%-50%. Hii inawezekana kabisa ilisababishwa na wazazi wengi wa kiislam kutowasimamia vema vijana wao katika kusoma nyumbani na kuwasisitizia elimu ya madrasa kwa kuwa wao hakupata elimu na kujua umuhimu wake, lakini uvumi ulikuwa ni mkakati uliofanywa na serikali ya CCM wakishirikiana na kanisa kuhakikisha waislam hawavuki kwa wingi kwenda elimu ya juu. CCM ilitakiwa kufanya makusudi kuwahamasisha wazazi ambao wengi wao hawakuhudhuria shule umuhimu wa elimu dunia ila kwa makusudi hakawakufanya hivyo. Moja ya matunda haya tunayaona katika safu kuu ya uongozi wa BAKWATA ambapo sheikh mkuu ni mmoja kati ya wazamiaji wakuu wa elimu ya dini ila wana zero understanding of the world as it should be ndiyo maana wanakuja na matamko ya ahera zaidi ya kidunia katika mambo ya dunia.

CCM na serikali yake inaendelea kuwadhalilisha waislam mbele ya watanzania wengine kwa kutumia wale ambao hawakupata elimu ya kupambanua mbichi na mbivu, kutumia udhaifu wao wa kiuchumi ambao ulisababishwa na CCM yenyewe kwa kuwalubuni kwa hela ili watoe matamko yanayopingana na hali halisi ya maisha yao ili kuiwezesha CCM iendelee kupata ridhaa ya kuendelea kuwakandamiza wao, watoto na wajukuu zao bila wao kujijua?, Ni nani asiyekuwa na kumbukumbu kuwa waislam hawahawa walisakamwa kwa kutumia uhuru wao wa kikatiba kuchagua chama cha kisiasa na wengi wakafurahishwa na sera za CUF, ambapo CCM iliwazushia kila aina ya majina mabaya yakiwemo chama cha kigaidi kwa kuwa wao walikuwa wengi kwenye chama hicho?, ni nani asiyejua kuwa visu(majamvia) ni silaha zenye uhusiano na watu wenye utamaduni wa masharikiri ya kati ambao majority ni waislam, CCM ikawasingizia kuwa CUF chama cha kigaidi (Kwa kuwa walikuwa wanakisupport wengi walikuwa ni waislam) kuwa wameingiza kwa lengo la kufanyia ugaidi?

Kwa ujumla ukiangalia adui mkuu wa maendeleo ya waislam ni CCM na serikali yake ambazo ama kwa makusudi au kwa kutokujua ili wa-ignore waislam mara tu baada ya kupata uhuru na mpaka leo inaendelea kuwa ignore na hata kuwatungia sheria ya ugaidi mara baada ya mashambulizi ya WTC kwa shinikizo la wakubwa. Waislam hawana budi kukaa na kujiuliza maswali yafuatazo

1. Je ni serikali ya Chama gani iliyoua waislam wasiokuwa na hatia pale mwembechai mwaka tarehe 13/2/1998?

2. Je ni serikali ya Chama gani iliyoua waislam kule Zanzibar January 26 na 27 mwaka 2001?

3. Je tokea tupate uhuru ni chama gani kimekuwa madarakani?

Kama majibu ya maswali hayo ni CCM, basi waislam hawana haja ya kukilaumu chama chochote kwa maendeleo yao na uonevu dhidi yao zaidi ya CCM. Na leo hii Muislam kusimama na kuitetea CCM kifua mbele ni kukubali kuwa wale waliouwawa mwenyechai, Unguja na Pemba ambao ni waislam wenzao kuwa ni kweli walikuwa magaidi na walistahili hukumu ile, huu ni unafiki na adhabu ya mnafiki ni fi-nari jehanam

Mbona wanachama wa CUF waliuliwa na CCM huko Pemba lakini CUF wamekubali kuunda Serikali na CCM? yaani ulitaka CUF waendelee kulalamika tu kuwa wanaibiwa Kura zao huku Wa TZ wengine wakiwaita magaidi na Mijahidina! au ulitaka waingie msituni halafu Serikali yenu ikishirikiana na Wazungu wawaite Al-Kaida sio?

Nimepata matumaini kidogo baada ya nyie Wakereketwa wa CDM kuanza kutamka kwa ulimi wenu na kukiri kuwa Tanzania kuna ubaguzi wa Dini tena Wanaobaguliwa ni Waislamu! sasa huku kukiri kwenu sasa ni hatua moja muhimu na kinachotakiwa sasa kufuatia ni Kuwashawashi Waislamu kwa hoja nzito na ikibidi kuingia mkataba nao ili Wakiunge mkono chama chenu kuingia Madarakani!

Nimefarijika sana kuwa mmetambua hilo ingawaje huko nyuma mlikuwa mkiwasakama Waislamu kuwa hawakusoma na kazi yao ni kulalamika, kula kashata, kukaa mabarazani na kupiga soga tu!

Kwa hakika hakuna nchi yoyote inayoweza kupata maendeleo ikiwa nusu ya raia wake hawana elimu! na hili hapa kwetu lipo ndio maana leo ni miaka 50 tangu uhuru lakini zaidi ya nusu ya Wa TZ ni wanaishi chini ya kipato cha dola moja!! wagonjwa zaidi(rejea kikombe cha BABU), na njaa ndio usiseme!!!

Sasa CCM imeshawaahidi Waislamu kuwa itaondoa kero zao, jee CHADEMA na vyama vingine viko tayari kusubutu kutamka kuwa wako tayari kuondoa kero za WAISLAMU? tusidanganyane hapa kuwa ati CDM inaangalia tu maslahi ya WATZ nooo! TZ kila mtu anadini yake na kauli ya TZ haina dini imepitwa na wakati!!!
 
Ndio maana nimesema huwa tunafeli mitihani kirahisi kweli; sijauliza kuhusu kuchaguliwa au kutochaguliwa, sikulinganisha CCM, CUF na Chadema; nimeuliza ni lini CCM ilibadilika na kuwa rafiki ya waislamu? Jibu lako inaonekana ni kuwa ni Kikwete ndiye aliyebadilika na siyo CCM na kuwa akiondoka waislamu wanaweza kurudi na kuwa kinyume na CCM tena? Maana hadi hivi sijaona mahali popote ambapo sera za CCM zimebadilika. Labda kama nakosa kitu.

Kama Kikwete amebadilika basi CCM nayo inaweza kubadilika sababu yeye ndie M/kiti na Rais mwenye madaraka makubwa kwa mujibu wa Katiba! hivyo hakuna ubaya kwa Waislamu kutumia chance ktk kipindi cha Mpito mpaka hapo Katiba yetu itakapobadilika na kuruhusu vyama hata vya kidini( hata Ujerumani, Norwey, Sweden nk. vipo!!!)!!

Dai lako kuwa Waislamu wanaweza kubadilika ikiwa Kikwete ataondoka halina msingi kabisa sababu Waislamu hawamfuati Kikwete kama Kikwete bali Sera, Uadilifu na ahadi kwa vitendo kama alivyofanya kule Zanzibar kukubali Serikali ya Mseto, Mahakama ya Kadhi, OIC nk. kama Rais ajae atakuwa Mbowe, Mbatia, Cheo au Lowassa, Waislamu watamkubali na kumfuata kwa sharti la kulinda Maslahi yao! atakaekiuka mkataba na Waislamu ajue hatapata sapoti yao hata kama ni CCM, CUF , CDM au NCCR!

Watu wengine kama Mzee Mwanakijiji akili yao inawaonyesha kuwa Waislamu wanaangalia ni nani aliye madarakani yaani kama ni Muislamu mwenzao basi watamuunga mkono! huu ni uono finyu kwa sababu kama ni hivyo Waislamu wasingemchagua Nyerere kuwa Rais wa TANU mwaka 1954 kwani 99% ya waliopiga kura walikuwa Waislamu na wangeweza kumpa kura Abdulwahid Syke aliyekuwa mtoto wa Jiji na Muislamu tajiri mpigania uhuru!

Na hakika leo CDM wakikaa meza moja na Waislamu na kuandikiana mkataba wa kumaliza kero za Waislamu, ikulu 2015 itakuwa yao! ila hawathubutu kufanya hivyo kwa kuhofia kukimbiwa na Wakristo!
CDM mmpo?
 
ni lini Nyerere alikaa na waislamu na kuahidi kutatua matatizo yao kama unavyotaka cdm wakaae????????
mwislamu upende usipende utake usitake LOWASA for presidential 2015.............
 
Nipo katika kuandika makala fupi yenye kuhusiana na kichwa hicho cha habari. Swali hili limekuja baada ya kusoma hoja alizotoa Mufti Shehe Shaaban Bin Simba akiitetea serikali ya CCM na uongozi wake.

Nilichukua muda kidogo na kurudi kusoma vitabu viwili ambavyo ni maarufu miongoni mwa Waislamu wa Tanzania ambavyo vinaelezea kwa kirefu jinsi CCM na serikali yake ilivyowakandamiza Waislamu. Kitabu cha Prof. Hamza. M. Njozi - ambaye kwa wanaokumbuka nilifanya naye mahojiano ya kina mwaka 2006 - cha "Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania" na kupitia maandishi ya Bw. Mohammed Said kuhusu historia ya Waislamu katika harakati za uhuru - ikiwemo kile kitabu kinachomhusu Abdulwahid Sykes.

Vitabu hivyo viwili na maelezo mengi ya ziada kabla ya 2010 yalijaribu kutuaminisha kuwa CCM ndio ilikuwa kikwazo cha maendeleo ya maslahi ya Waislamu:

a. Kuanzia kufutwa kwa EAMWS hadi mauaji ya Mwembechai na mambo mengine yote kati yake.

b. Kwamba pamoja na jitihada mbalimbali CCM iligeuka na kuwa sehemu ya Kanisa au kutumiwa na Kanisa - Dr. Njozi na barua ya Abu Aziz vinathibitisha mashtaka hayo makubwa.

Sasa, bila ya kwenda mbali sana kuna kitu kimebadilika hivi karibuni ambacho kinawafanya Waislamu kuiunga mkono CCM na uongozi wake. Utetezi mkubwa uliofanywa na vyombo mbalimbali vya habari vya Kiislamu na watu mbalimbali wakati wa kampeni kuitetea CCM kwa wapiga kura vinanifanya niamini kabisa kuwa kuna kitu cha msingi sana ambacho kimebadilika kiasi cha kuifanya CCM - chama ambacho kilikuwa kinaonekana na kiini cha tatizo ya Waislamu kuanza kupendwa, kukumbatiwa na hata kufikia serikali yake kutetewa kwa kiasi ambacho hatujawahi kuona.

Ndio swali liko mbele yetu; CCM imebadilika kitu gani hadi kuwa rafiki wa Waislamu leo hii? Ni sera na mfumo gani wa CCM ambao unawafanya baadhi ya Waislamu kuona kuwa maisha na maslahi yao yatalindwa vizuri na CCM kuanzia sasa? Je, endapo uongozi ujao wa CCM utakuwa ni wa tofauti na huu uliopo bado CCM itapata support hii kubwa? Je, makosa yote ya CCM na serikali yake ya huko nyuma yamesamehewa na sasa "tugange yajayo" au yamewekwa kiporo tu ili ukija uongozi tofauti na huu wa sasa yakumbushiwe tena?

Je, Waislamu wote wanatakiwa kuanzia sasa kuiunga mkono CCM, kutoikosoa, kutoilalamikia, kutoonesha makosa yake wala kutokubaliana hata kidogo na wale wenye kuikosoa? Kwa maneno mengine, Muislamu anaweza kuwa Muumini mzuri huku bado anaendelea kuipinga CCM kinyume na maelekezo ya viongozi wake wa kidini? Au bado wapo baadhi ya Waislamu ambao msimamo wao haujatetereka dhidi ya CCM na serikali yake?

Ni maswali ya uchokozi wa kifikra tu. Natumaini mawazo yenu juu ya somo husika yatanisaidia kuandika makala ambayo itajaribu kushughulikia suala hili kwa kiasi cha kutosha.

Mwanakijiji unaweza ukawa na pointi za maana juu ya maandiko yako lakini namna ulivyoanza unatufanya sisi Waislamu tupingane nawe. Iwapo makala yako inakuja kutokana na kauli ya Mufti wa BAKWATA basi tutabidi tukuulize wewe Tangu lini Waislamu wa BAKWATA Ilikuwa Adui Wa CCM? BAKWATA ni zao la CCM (TANU) sasa ulitegemea iko siku itakwenda kinyume na CCM?
Unaposema CCM imekuwa rafiki wa Waislamu sijui unaweza kutowa ushahidi gani kuonyesha kuwa CCM ni rafiki wa Waislamu (sio BAKWATA) hivi sasa? Waislamu walikuwa na sababu ya kuwa na urafiki na CCM mwaka 2005 wakati walipodanganywa lakini matokeo yakura ya kipindi hicho yalionyesha kuwa Waislamu wengi hawakukipigia kura CCM na badala yake Wakristo ndio waliompigia kura nyingi Rais na CCM kutokana na mafundisho ya viongozi wao kuwa Kikwete ni Chaguo la Mungu. Nafikiri kama unaleta swali la kuuliza nini kimetokea nafikiri ungeuliza nini kimetokea hata waliosema kuwa ni chaguo la Mungu waliamua kutompigia kura mgombea wa CCM?
Ama kwa upande wa Waislamu jibu lako ni rahisi sana. Kilichowapelekea Waislamu wakipigie kura CCM ni mfumo uliojitokeza wa kila mmoja na ndugu yake kwani ilikuwa jambo la logic kabisa kwa Waislamu kufata yaliofanya na Wakristo. Uchaguzi wa 2010 Tanzania kwa mara ya kwanza tulishuhudia Waraka za kidini zikihamasisha waumini na sio wananchi kwa ujumla. Pengine hii ilikuwa solidarity kwa kiongozi wa dini (kwani kiongozi wa dini utabaki hivyohivyo hata ukijitia kwenye siasa) Hapo ndipo uchama ulipoondoka na kuja udini huo unaojaribu kuwapaka nao Waislamu. Nafikiri utafiti wako umesahau factor hiyo niliyokueleza. Kwa elimu yetu ya uraia Tanzania hili la kuwa ignorant mbele ya dini inapply kwa pande zote. Sijuwi una maana gani ya kuuliza Waislamu na mshikamano na CCM huku usiulize solidarity ya Ukiristo na CHADEMA.
Hili la kuuliza iwapo Waislamu wawe wanakubali bila kutafakari ya serikali ya CCM nafikiri nawe umepatwa na jinamizi lilelile la kujiegemeza na upande mmoja. Swali lako halikuwa swali bali ni kejeli kwa Waislamu kuwa hawafikiri (infact kichwa cha habari kinalenga kuwadharau Waislamu). Hivyo kwa maoni yako kila kinachofanywa na CHADEMA ni kizuri na kila kilichosemwa na Mufti na kupotoka? Iwapo chama kina sera yake si haki ya mwengine kuipinga sera hiyo iwapo msimamo ni tofauti? Iwapo CHADEMA kwa vitendo na maneno wameshaleta machafuko kwa hayo mazuri wanayoyafanya huoni busara kwa mwengine kupinga machafuko hayo? Kwani kwa mtazamo wako CHADEMA hawawezi kuhamasisha watu kwa mikutano ya Hadhara isipokuwa kufanya maandamano ambayo yanaleta mtafaruku? Kwani mtu unapoandamana unakuwa unawaelimisha watu zaidi pale unapokaa kwenye kiriri na kutowa hutuba?
Waislamu wana haki na uwezo wa kupambanua kipi na yupi na wakati gani ktowa sapoti kwa kikundi fulani cha kijamii mradi jambo muhimu ni kuwa jumuia hiyo inaweza kuleta manufaa kwa Waislamu kama kundi katika jamii na wananchi kwa ujumla. CCM ilishawadanganya Waislmu lakini bora anaekudanganya kuliko yule anaejenga uhasama nawe. Namalizia kwa kukuliza Mwanakijiji CHADEMA inatambua kero za Waislamu ndani ya jamii jee inashirikisha hayo matatizo yao kwenye maandamano au upo uhusiano gani kati ya Waislamu na CHADEMA?.

Nategemea makala yako utaiandika hapo utakapokuwa umeondokana na dhana ya kuona upande mmoja tu ndio uko sahihi na upande mmoja tu uko kwenye makosa.
 
Ila wana bahati mbaya kwa Sababu ukiangalia Alama zote mbinguni na duniani, zinaonyesha kuwa Mgombea ajaye wa CCM, LAZIMA atakuwa Mkristo. Ila sijui tu atatoka kanisa gani na la muhimu zaidi ni Je, Ni Mkristo wa ukweli au kama huyu alisemwa na Nyerere yaani George Kahama kuwa ni Mkristo ila nyumbani ana wake wawili?

Kama Kikwete ni Muislaam wa kweli, basi kweli kuna siku Papa atatoka JAMAICA.

kibanga hapa nimekufa kabisa haha
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom