Ni lini CCM ilibadilika na kuanza kuwa rafiki wa Waislamu Tanzania?

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
the truth is that the CCM government has acted arbitrarily and is not alive to the grave situation into which it has plunged the country. By being biased and allowing itself to be duped by the Catholic clergy that Muslim preaching was insulting to Christianity, the CCM government has embarked on a course of action which violates the constitutional rights of Muslims to propagate religion, is arbitrary and without any regard to the due process of law - http://www.islamtz.org/mwembechai/index.html(Barua ya Abu Aziz kwa Mwanasheria Mkuu; Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania)

Nipo katika kuandika makala fupi yenye kuhusiana na kichwa hicho cha habari. Swali hili limekuja baada ya kusoma hoja alizotoa Mufti Shehe Shaaban Bin Simba akiitetea serikali ya CCM na uongozi wake.

Nilichukua muda kidogo na kurudi kusoma vitabu viwili ambavyo ni maarufu miongoni mwa Waislamu wa Tanzania ambavyo vinaelezea kwa kirefu jinsi CCM na serikali yake ilivyowakandamiza Waislamu. Kitabu cha Prof. Hamza. M. Njozi - ambaye kwa wanaokumbuka nilifanya naye mahojiano ya kina mwaka 2006 - cha "Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania" na kupitia maandishi ya Bw. Mohammed Said kuhusu historia ya Waislamu katika harakati za uhuru - ikiwemo kile kitabu kinachomhusu Abdulwahid Sykes.


Vitabu hivyo viwili na maelezo mengi ya ziada kabla ya 2010 yalijaribu kutuaminisha kuwa CCM ndio ilikuwa kikwazo cha maendeleo ya maslahi ya Waislamu:

a. Kuanzia kufutwa kwa EAMWS hadi mauaji ya Mwembechai na mambo mengine yote kati yake.

b. Kwamba pamoja na jitihada mbalimbali CCM iligeuka na kuwa sehemu ya Kanisa au kutumiwa na Kanisa - Dr. Njozi na barua ya Abu Aziz vinathibitisha mashtaka hayo makubwa.

Sasa, bila ya kwenda mbali sana kuna kitu kimebadilika hivi karibuni ambacho kinawafanya Waislamu kuiunga mkono CCM na uongozi wake. Utetezi mkubwa uliofanywa na vyombo mbalimbali vya habari vya Kiislamu na watu mbalimbali wakati wa kampeni kuitetea CCM kwa wapiga kura vinanifanya niamini kabisa kuwa kuna kitu cha msingi sana ambacho kimebadilika kiasi cha kuifanya CCM - chama ambacho kilikuwa kinaonekana na kiini cha tatizo ya Waislamu kuanza kupendwa, kukumbatiwa na hata kufikia serikali yake kutetewa kwa kiasi ambacho hatujawahi kuona.

Ndio swali liko mbele yetu; CCM imebadilika kitu gani hadi kuwa rafiki wa Waislamu leo hii? Ni sera na mfumo gani wa CCM ambao unawafanya baadhi ya Waislamu kuona kuwa maisha na maslahi yao yatalindwa vizuri na CCM kuanzia sasa? Je, endapo uongozi ujao wa CCM utakuwa ni wa tofauti na huu uliopo bado CCM itapata support hii kubwa? Je, makosa yote ya CCM na serikali yake ya huko nyuma yamesamehewa na sasa "tugange yajayo" au yamewekwa kiporo tu ili ukija uongozi tofauti na huu wa sasa yakumbushiwe tena?

Je, Waislamu wote wanatakiwa kuanzia sasa kuiunga mkono CCM, kutoikosoa, kutoilalamikia, kutoonesha makosa yake wala kutokubaliana hata kidogo na wale wenye kuikosoa? Kwa maneno mengine, Muislamu anaweza kuwa Muumini mzuri huku bado anaendelea kuipinga CCM kinyume na maelekezo ya viongozi wake wa kidini? Au bado wapo baadhi ya Waislamu ambao msimamo wao haujatetereka dhidi ya CCM na serikali yake?

Ni maswali ya uchokozi wa kifikra tu. Natumaini mawazo yenu juu ya somo husika yatanisaidia kuandika makala ambayo itajaribu kushughulikia suala hili kwa kiasi cha kutosha.

MAKALA ILIYOTOKANA NA MJADALA HUU:

UTETEZI mkali wa Mufti Sheikh Shaaban Bin Simba kuitetea serikali ya CCM na hasa Rais Kikwete wiki iliyopita, umenifanya nibakie na swali moja ambalo bado sijapata jawabu lake la uhakika; ni lini Chama Cha Mapinduzi kimebadilika na kuwa rafiki ya Waislamu?
Ni swali la muhimu kwa sababu utetezi wake (na hata wa watu wengine) ulijikita katika suala la "sisi" dhidi ya "wao". Ulikuwa ni utetezi unaosema kuwa "sisi" – Waislamu dhidi ya "wao" – wasio Wakristu. Kwa vile hoja hii ya udini inazidi kusukumizwa katika akili zetu hatuna budi kulizungumzia kwa sababu kuendelea kuikwepa ni kutoa kibali kuwa pande zenye mirengo ya kidini kuendelea kutulazimisha kukubaliana na hali iliyopo bila ya kuipinga.
Nina bahati ya kwamba nimekisoma kitabu kizima cha Profesa Hamza M. Njozi ambacho kilituelezea kwa kiasi historia ya mahusiano ya CCM na Waislamu nchini. Kitabu hicho ambacho kilipigwa marufuku nchini kinaitwa "Mauaji ya Mwembechai na Hatma ya Kisiasa ya Tanzania".
Vile vile nimepata kusoma maandishi mengi ya mmoja wa wanaharakati wa Kiislamu nchini. Mohammed Said ambaye naye ameandika vitabu na insha kadha wa kadha ambazo ndani yame ametudokeza (wakati mwingine kwa kirefu) jinsi gani utawala wa CCM ulivyokuwa ukiwakandamiza Waislamu.
Dk. Njozi ambaye nilipata nafasi ya kufanya naye mahojiano ya kina miaka kama mitano iliyopita kuhusiana na kitabu chake hicho alinielewesha kwa kirefu sana jinsi gani utawala wa CCM haukuwa rafiki mzuri wa Waislamu.
Japo watu wengi wanafikiria kitabu cha Njozi kilipigwa marufuku kwa sababu ya madai yake juu ya mauaji ya Mwembechai binafsi baada ya kukisoma na kukielewa (hasa ambatisho la barua ya Abu Aziz kwenda kwa Mwanasheria Mkuu) nimegundua kuwa tatizo kubwa la kitabu hicho ilikuwa ni madai yake makali dhidi ya viongozi wa CCM na Chama Cha Mapinduzi.
Katika mjadala wa hivi karibuni na Said kwenye mtandao wa JamiiForums.com na baada ya kusoma maandishi yake mbalimbali ya huko nyuma niliweza kuelewa kwamba tatizo la Waislamu muda mrefu halikuwa dhidi ya Nyerere tu (hili la Nyerere ni la siku za karibuni zaidi) bali ulikuwa ni dhidi ya utawala wa CCM.
Kwa muda mrefu viongozi mbalimbali wa Kiislamu wamekuwa na matatizo na utawala wa CCM, sera zake, uongozi wake, ahadi zake na mipango yake. Kabla ya miaka hii miwili iliyopita viongozi wengi wa Waislamu walichukulia CCM kama ni sehemu ya tatizo linalotishia maslahi ya Waislamu.
Hata hivyo, inaonekana matatizo yote ambayo jamii ya Waislamu ilikuwa nayo katika miongo karibu mitano ya Uhuru wa Tanzania bara sasa yamekwisha. Madhambi na mambo yote ambayo tuliaminishwa kuwa ni matatizo ya Chama Cha Mapinduzi dhidi ya Waislamu yamesamehewa na kama maneno ya Mufti hivi karibuni ni ya kuaminiwa (na sioni sababu ya kutoyaamini) uhusiano mpya wa mapatano kati ya Chama cha Mapinduzi na Waislamu umeanza. Kuanzia sasa Jamii ya Waislamu imepoteza haki ya kuilalamikia CCM na serikali yake.
Jamii yetu hii imepoteza haki ya kulalamikia suala la Mahakama ya Kadhi kama ilivyopoteza haki ya kulalamikia suala la OIC. Mambo yote mawili yameliliwa na Waislamu kwa muda mrefu na baada ya kurushwa rushwa na kutokupewa majibu kamili yamebakia kama maneno matamu ya kuvutia. Sasa hivi wale wanaosimamia mambo hayo hawawezi tena kuyadai kwa nguvu bila kuonekana wako kinyume na serikali. Kilichobakia ni kutegemea wema na huruma ya CCM kuweza kupatiwa mambo haya.
Lakini haya yanavutia baadhi tu ya Waislamu na wala si Waislamu wote. Kitu ambacho kinanishangaza sana ni kujaribu kuangalia Waislamu kama watu wanaoongozwa na hitaji moja tu linalofanana. Sote tunafahamu kuwa hata kwenye nchi ambazo zina Waislamu wengi kama Saudia, Yemen, Oman, Libya, Misri, Syria, Iran, na hata Iraq Waislamu huunganishwa na maslahi mbalimbali zaidi ya yale ya imani.
Mtu yeyote ambaye alichukua muda kufuatilia au anayeendelea kufuatilia mwamko wa mabadiliko kwenye nchi hizo atagundua kuwa wananchi wa nchi hizo hawaandamani kwa sababu wanakandamizwa na tawala zenye kuongozwa na makanisa au ambazo tunaweza kusema kuwa zisizo za Kiislamu; la hasha viongozi wa nchi hizo zote ni Waislamu na baadhi ya nchi hizo zina mifumo ya Kiislamu ambayo inatawala.
Tungetarajia kwa mfano nchi kama Iran wananchi wake wote wangekuwa hawana malalamiko yoyote dhidi ya serikali ya Mapinduzi ya Kiislamu. Kwamba, kwa vile wanaongozwa kwa kiasi kikubwa na mifumo inayoendana na imani yao basi kusingekuwa na malalamiko ya kudai uhuru zaidi au demokrasia zaidi.
Hili ni kweli hata kwenye nchi kama Saudia ambako tungelazimika kuamini kuwa maslahi ya kila Muislamu yanalindwa. Lakini haikuwa hivyo; tunakumbuka kuwa baada ya wimbi la mabadiliko la Tunisia kupamba moto na pale mlipuko wa Uwanja wa Tahrir ulipozidi watawala wa Saudia kwa haraka wakatangaza kuongeza posho mbalimbali kwa wananchi wao!
Jawabu ambalo linaweza kutolewa mara moja ni kuwa nchi hizo zote ambazo ziko katika msuko suko wa kisiasa ziko karibu na Marekani na Israeli na hivyo wananchi wake ndio maana wameinuka dhidi yake. Hata hivyo, hilo halina ushahidi kwani yeyote ambaye amefuatilia matangazo ya Al-Jazeera ataona kuwa wananchi wa hizo wanachodai ni utu wao. Huwezi kuishi kwenye taifa ambalo kuna hali ya hatari kwa miaka thelathini na ukajiona kuwa uko huru! Huwezi kuishi kwa furaha katika nchi ambayo watawala wake wanashikilia nafasi zote za utajiri nawe ukajiona ni sehemu ya jamii hiyo?
Waislamu wa nchi hizo kumbe walitambua kile ambacho naamini ndugu zetu wa Tanzania walikitambua miaka michache iliyopita kwamba matatizo yao yanahusiana kabisa na utawala ulioko madarakani. Yeyote ambaye amewasoma vizuri kina Njozi na Said, Abu Aziz na waandishi wengine wa Kiislamu nchini ataona kuwa walielewa kile ambacho Wamisri na Wayemen wamechelewa kukielewa. Kile ambacho napendekeza kuwa Mufti Simba anataka Waislamu wakisahau mara kuwa matatizo yao yanahusiana na utawala ulioko madarakani - yaani utawala wa CCM.
Barua ya Abu Aziz iliyoko mwishoni mwa kitabu cha Njozi (Nyongeza ya 1) ina haya ya kusema juu ya CCM na Waislamu "the truth is that the CCM government has acted arbitrarily and is not alive to the grave situation into which it has plunged the country. By being biased and allowing itself to be duped by the Catholic clergy that Muslim preaching was insulting to Christianity, the CCM government has embarked on a course of action which violates the constitutional rights of Muslims to propagate religion, is arbitrary and without any regard to the due process of law."
Yaani, "ukweli ni kwamba Serikali ya CCM imefanya kiholela na haionyeshi kujali dimbwi la hatari ambalo imeiingiza nchi. Kwa kuonesha upendeleo na kukubali kudanganywa na mapadri wa Kikatoliki kwamba mahubiri ya Waislamu yana kashfu Ukristu, Serikali ya CCM imejielekeza kuchukua hatua ambazo zinavunja haki za Kikatiba za Waislamu kutangaza dini, ni za kiholela na ambazo hazijali kabisa kufuata sheria" (Italiki na tafsiri zote toka Kiingereza zangu).
Hiyo ni sehemu ya hukumu kali ya Abu Zaid ambaye sehemu nyingine katika Waraka mrefu kwa Mwanasheria Mkuu akamka pasipo utata kuwa "The CCM government has used the criminal justice system to silence Muslims simply because they are exercising their constitutional right of propagating religion.
The response by the CCM government has been characterised by abuse of power." Yaani, "Serikali ya CCM imetumia mfumo wetu wa sheria kunyamazisha Waislamu kwa sababu tu wanatumia haki yao ya Kikatiba kutangaza dini. Mwitikio huo wa CCM umeendana na matumizi mabaya ya madaraka".
Naye Mohammed Said akiandika katika makala aliyoita "Islam and Politics in Tanzania" anapitisha hukumu hii dhidi ya CCM na Bakwata "The Party is weak, it no longer commands respect, dignity and enthusiasm it did in the days of yore. The Party has alienated itself from its founders. The de-Islamisation of the Party has gone full circle and its Muslim history has been erased. Bakwata has sided with the government thus failing to uphold Muslim values and principles."
Kwamba, "Chama (CCM) ni dhaifu na hakina tena heshima, hadhi, na mvuto kilichokuwa nayo miaka ya nyuma. Chama kimejitenga na waasisi wake. Kuondolewa kwa kumbukumbu za Uislamu toka ndani ya chama kumekamilika na historia yake ya Waislamu imefutwa. BAKWATA imechukua upande wa serikali na hivyo kushindwa kusimamia tunu na kanuni za Kiislamu".
Sasa haya yote ni ya kweli na ni madai mazito na kama nilivyodokeza hapo juu ndio sababu kubwa ya kitabu cha Njozi kupigwa marufuku nchini. Watu wengi wanafikiri kilipigwa marufuku kwa sababu ya kutuelezea na kutuwekea ushahidi wa yaliyotokea Mwembechai; la hasha. Nina uhakika hata Njozi akiulizwa leo atakubaliana nami kuwa sababu kubwa ni kuwa kitabu chake kiliweka bayana ile siri ambayo ilikuwa inajulikana pembeni kuwa CCM inahusika na matatizo ya Waislamu.
Sasa kama hili ni kweli - na bado sijapata sababu ya kuona kuwa siyo. Huu urafiki mpya ambao tumeuona hivi karibuni kati ya viongozi wa Kiislamu, makundi kadhaa ya Waislamu na Chama Cha Mapinduzi umetokana na nini? Ninajiuliza kuwa kauli ya Sheikh Mkuu Bin Simba kwamba "Misikiti iungurume na wala isikae kimya, ukimya ufe na yalaani mabaya yote hayo pamoja na dini ya Kiislamu kufanywa tabaka la chini, tuamke na tushikamane kwa pamoja." Imetoka wapi?
Au kauli yake hii kwamba "Wanasiasa wanataka kuivuruga nchi kwa visingizio kuwa wanataka kulinda amani, hivyo Waislamu tumeamua kuvunja ukimya uliodumu kwa muda mrefu na kuamua kukemea vitendo hivyo" tunaweza kuipa uzito gani hasa ikizingatiwa kuwa amani ilipovunjwa mwaka 1998 na 2001 Bakwata hawakuwa wakali kwa serikali kiasi hiki?
Ni wazi kwamba BAKWATA nayo imeamua kujivika taji la kuitetea serikali ya CCM. Kwa Waislamu wengine hili si jambo geni (kama nilivyoonyesha hapo juu) kwani mara zote BAKWATA imekuwa ikisimama na serikali ya CCM.
Lakini pia kitu kipya ambacho kimetokea sasa hivi na hasa wakati wa kampeni ni kuwa hata wale viongozi wa dini ya Kiislamu ambao walikuwa kinyume na serikali ya CCM walijitokeza na wengi wanaendelea kujitokeza kuitetea CCM mbele ya umma. Sisi wengine tunajiuliza CCM ilibadilika lini na kuwa rafiki wa Waislamu?
Ninabakia na majibu kadha wa kadha kubwa ambalo laweza kuonekana ni kuwa hatimaye matatizo ya Waislamu yamepatiwa tiba ndani ya serikali ya CCM.
Kwamba sera na ahadi za CCM kuelekea 2015 ni bora zaidi kuliko wakati mwingine wowote na kuliko za chama kingine chochote. Kwamba uongozi wa CCM umeonyesha kuelewa matatizo ya Waislamu kuliko uongozi wa chama kingine chochote. Kama hii ni kweli; ina maana ya kwamba.
Ÿ Makosa yote ya CCM ambayo imeyafanya huko nyuma yamefutwa na kusamehewa rasmi na sasa Waislamu wote waiunge mkono CCM kwa sababu moja tu kuwa hatimaye maslahi yao kama Waislamu yamepata mtetezi;
Ÿ Madai yote ambayo yamekuwa yakitolewa dhidi ya Kanisa ambalo tuliaminishwa kuwa ndilo liko nyuma ya CCM - wengine walifikia kuiita CCM - Catholic Church Movement hayana ukweli tena - kwa sababu kama CCM bado ni Catholic Church Movement ina maana Waislamu wanaoiunga mkono CCM wanaunga mkono Kanisa Katoliki;
Ÿ Madai kuwa upo Mfumo Kristo hayana msingi wowote kwa sababu kwa miaka karibu hamsini Tanzania imekuwa chini ya Chama Cha Mapinduzi ambacho ndicho kilitengeneza mfumo wa utawala ambao leo unatetewa na kutafutiwa udhuru.
Hii ni kinyume na sisi wengine ambao tunaamini upo "MFUMO FISADI a.k.a MFUMO CCM" ambao umetunyang'anya haki zetu, kutudhulumu utu wetu na kutufanya tuwe kama wageni katika nchi yetu.
Ni mfumo ambao umeendeleza umaskini wa Waislamu, Wakristu na Wenye Imani za Jadi! Mfumo Kristo ni kisingizio, mfumo fisadi ni sababu!
Mfumo huu ambao leo unatetewa kwa nguvu zote unahitaji ujasiri mkubwa sana kutetewa.
Pamoja na hayo ni wazi tuamini kuwa yumkini kuna sababu nyingine kwani kwa kipimo chochote kile hakuna mabadiliko yoyote ambayo yametokea ndani ya CCM hata kuweza kudai kuwa CCM ni bora kwa Waislamu nchini; siyo tu kwa Waislamu lakini kwa Watanzania wote kwani maslahi ya Watanzania yote yanabeba ndani yake maslahi ya Waislamu, Wakristu, Wapagani na wasioamini kabisa!
Pendekezo ambalo limetolewa na Shehe Mkuu ambalo yumkini ndio msingi wa utetezi unaoendelea ni kuwa Rais Kikwete anatetewa kama Muislamu na si kwa sababu ya CCM. Kwamba, Waislamu wameamua kujitokeza kumtetea Muislamu mwenzao kwa sababu inaonekana Wakristu na Makanisa yanamshambulia na kushambulia utawala wake kwa sababu ya Uislamu wake. Kwa maoni ya watetezi wa misingi hiyo wanaona kuwa akija kiongozi Mkristu basi Wakristu watakuwa na haki ya kumtetea kwa misingi ya dini yake.
Kuhusu hili la "uenzetu huu" niliwahi kuandika Oktoba 12, 2009 katika makala yangu niliyoiita "Na Huu ‘Uenzetu huu' tutashindwa kuwajibishana" nilisema hivi "Tutaanza kupiga hatua kubwa ya kuwakataa mafisadi pale tutakapoanza kukataa umoja nao na ushirika nao. Ukisikia fisadi ni Mkristu mwenzako, Muislamu mwenzako, Mnyakyusa mwenzako, Mhaya mwenzako; vuka hisia zako za "uenzetu" na umpime kwa matendo yake tu na umpinge vilivyo.
Ni lazima katika fikra zetu tuwe tayari kukataa dhulma, uonevu, wizi wa utajiri wetu, ubadhirifu, matumizi mabaya ya madaraka, ukandamizaji, unyanyasaji, unyonyaji wa aina yoyote ile na kwa mahali popote bila ya kujali unafanywa na nani au kama anayefanya tunafanana naye kwa namna yoyote. Vinginevyo, mafisadi hawa ambao ni wenzetu ndio kweli mafisadi wenzetu!"
Kwa sababu kama kuna Waislamu wanaomtetea Kikwete kwa sababu tu ya Uislamu wake (kama ambavyo Mufti anataka tuamini) basi ni wao ambao wanajiweka mahali pabaya sana;
Sera za CCM zinaweza kusababisha madhara mengi kwa watoto na familia za Waislamu lakini kwa sababu ni "mwenzetu" basi Waislamu wasilalamike;
Mipango ya maendeleo yaweza isisimamiwe vizuri lakini kwa vile ni "mwenzetu" Waislamu wasilalamike;
Shule za Kata ambazo zina changamoto nyingi zinaweza kuendelea kufanya vibaya na kuathiri watoto wengi wa Kiislamu lakini Waislamu wasipaze sauti kubwa kwa sababu ni "mwenzetu";
Vitendo vya kifisadi kwenye taasisi za fedha na mikataba mibovu iliyogharimu mabilioni ya shilingi isilalamikiwe kwa nguvu zote hata kama fedha hizo zingeweza kutumika kuboresha mahospitali, mashule, kliniki, barabara, usafiri n.k visipigiwe kelele na Waislamu kwa sababu ya huu "uenzetu."
Yote haya na mengine mengi yakikubaliwa ni tatizo zaidi. Kwa sababu, itakuwaje kama kiongozi ajaye wa Tanzania atakuwa ni Mkristu? Na itakuwaje kama atakuwa ni kiongozi toka nje ya CCM? Itakuwaje kama kuna chama nje ya CCM ambacho sera na mipango yake ni ya manufaa kwa Watanzania wote na si kikundi kimoja tu? Je, wale Waislamu wenye kuunga mkono CCM leo hii watakuwa tayari kukaa na CCM katika upinzani wakisubiri nafasi nyingine?
Hata hivyo hata baada ya kusema hayo yote bado kuna mambo mengi ya kutua moyo. Viongozi wa Waislamu hawawazungumzii Waislamu wote kwani Waislamu siyo kundi moja linalofanana kwa kila kitu (homogenous).
Waislamu wa Tanzania kama walivyo Watanzania wengine wana maslahi zaidi ya kukubaliana kidini. Wakiumwa wanaenda kwenye mahospitali yale yale wanayoenda Wakristu na Wenye imani za jadi; wakisafiri wanapita barabara zile zile; shule wanazosoma za umma ni zile zile wanazosoma watu wengine; polisi wanaowalinda ni wale wale wanaowalinda Watanzania wengine n.k
Kumbe kuna kundi la Waislamu ambalo halijanunuliwa na "huu uenzetu huu". Kundi hili ni la vijana na wazee ambao wanatambua kuwa maslahi yao hayana tofauti na maslahi ya Watanzania wengine. Kundi hili linataka elimu bora kama wanavyotaka Watanzania wengine; wanataka mafao bora ya uzeeni kama wanavyotaka Watanzania wengine; wanataka mishahara mizuri kama wanavyotaka Watanzania wengine na wanataka maisha bora yenye hadhi na utu wa mwanadamu kama wanavyotaka Watanzania wengine. Kundi hili la Waislamu halikubali ghilba ya kidini kwani linajua wazi kuwa kufanikiwa kwa Tanzania nzima ni kufanikiwa kwa kila Mtanzania.
Hili kundi limesoma, halishawishiwi kwa maneno ya kidini tu au ya kiimani lakini linajuliza maswali ya msingi na linatafuta majibu ya kweli. Kundi hili linauwezo wa kuchambua mambo kwa kusababisha maswali ya msingi yajibiwe kwanza kabla halijarukia kwingine.
Linajiuliza kwa mfano kwanini leo tuambiewe tuiunge mkono CCM wakati miezi michache tu CCM ilikuwa ndio adui yetu? Kwanini tumtetee Kikwete kwa sababu ya dini yake tu lakini tusihoji uongozi wake? Je ni kweli mfumo Kristo upo au upo Mfumo Fisadi ambao unaathiri Waislamu kama unavyoathiri Wakritu na Wapagani? Je, tunaweza kufanikiwa kama Waislamu tu bila kuhakikisha tunafanikiwa kama Watanzania?
Kundi hili ndilo ambalo unaliona likijitenga na siasa za kidini na kuunga mkono upinzani wa kweli na haliogopi kujitokeza kufanya hivyo. Kundi hili halijalishi wachungaji au mapadre wanasema nini kwani linajua kinachotaka.
Kundi hili haliogopi kushirikiana na Watanzania wengine katika kuupinga mfumo dhalimu wa kifisadi kwa sababu ni katika kufanya hivyo linajitengenezea lenyewe, na Watanzania wengine mazingira ambapo kila Mtanzania atapata nafasi nzuri ya kufanikiwa na kuishi kwa uhuru, amani na utu bila kujali rangi, dini, kabila, mahali, hadhi au nafasi.
Ninaamini kabisa kuwa kundi hili ni kubwa lakini lililo kimya (the silent majority) na ambalo linatambua bila ya shaka kuwa tatizo la Tanzania linahusiana kabisa na CCM.
Hili ni kundi ambalo linahofiwa sana na watawala kwa sababu likijitokeza wazi na kuunga mkono harakati za mabadiliko ya kweli (na nina uhakika litafanya hivyo siku si nyingi) ambayo yatamnufaisha kila Mtanzania - CCM itakuwa imepoteza karata ya mwisho ya kuishikilia Tanzania kama paka anavyobeba kitoto chake shingoni, yaani Udini.
 
Kabla sijachangia au kujibu swali lako, wewe kwa uchambuzi na ufahamu wako unakubaliana na lalamiko la Waislamu kuwa wamefanywa daraja la pili au kudhulumiwa na Serikali zote tangu Mkoloni, Nyerere na mpaka sasa? maoni yako wewe ni yapi? ikiwa utajibu swali hili basi nami nitakujibu kuhusu Waislamu na CCM ya sasa!!!!
 
Nipo katika kuandika makala fupi yenye kuhusiana na kichwa hicho cha habari. Swali hili limekuja baada ya kusoma hoja alizotoa Mufti Shehe Shaaban Bin Simba akiitetea serikali ya CCM na uongozi wake.

Nilichukua muda kidogo na kurudi kusoma vitabu viwili ambavyo ni maarufu miongoni mwa Waislamu wa Tanzania ambavyo vinaelezea kwa kirefu jinsi CCM na serikali yake ilivyowakandamiza Waislamu. Kitabu cha Prof. Hamza. M. Njozi - ambaye kwa wanaokumbuka nilifanya naye mahojiano ya kina mwaka 2006 - cha "Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania" na kupitia maandishi ya Bw. Mohammed Said kuhusu historia ya Waislamu katika harakati za uhuru - ikiwemo kile kitabu kinachomhusu Abdulwahid Sykes.


Vitabu hivyo viwili na maelezo mengi ya ziada kabla ya 2010 yalijaribu kutuaminisha kuwa CCM ndio ilikuwa kikwazo cha maendeleo ya maslahi ya Waislamu:

a. Kuanzia kufutwa kwa EAMWS hadi mauaji ya Mwembechai na mambo mengine yote kati yake.

b. Kwamba pamoja na jitihada mbalimbali CCM iligeuka na kuwa sehemu ya Kanisa au kutumiwa na Kanisa - Dr. Njozi na barua ya Abu Aziz vinathibitisha mashtaka hayo makubwa.

Sasa, bila ya kwenda mbali sana kuna kitu kimebadilika hivi karibuni ambacho kinawafanya Waislamu kuiunga mkono CCM na uongozi wake. Utetezi mkubwa uliofanywa na vyombo mbalimbali vya habari vya Kiislamu na watu mbalimbali wakati wa kampeni kuitetea CCM kwa wapiga kura vinanifanya niamini kabisa kuwa kuna kitu cha msingi sana ambacho kimebadilika kiasi cha kuifanya CCM - chama ambacho kilikuwa kinaonekana na kiini cha tatizo ya Waislamu kuanza kupendwa, kukumbatiwa na hata kufikia serikali yake kutetewa kwa kiasi ambacho hatujawahi kuona.

Ndio swali liko mbele yetu; CCM imebadilika kitu gani hadi kuwa rafiki wa Waislamu leo hii? Ni sera na mfumo gani wa CCM ambao unawafanya baadhi ya Waislamu kuona kuwa maisha na maslahi yao yatalindwa vizuri na CCM kuanzia sasa? Je, endapo uongozi ujao wa CCM utakuwa ni wa tofauti na huu uliopo bado CCM itapata support hii kubwa? Je, makosa yote ya CCM na serikali yake ya huko nyuma yamesamehewa na sasa "tugange yajayo" au yamewekwa kiporo tu ili ukija uongozi tofauti na huu wa sasa yakumbushiwe tena?

Je, Waislamu wote wanatakiwa kuanzia sasa kuiunga mkono CCM, kutoikosoa, kutoilalamikia, kutoonesha makosa yake wala kutokubaliana hata kidogo na wale wenye kuikosoa? Kwa maneno mengine, Muislamu anaweza kuwa Muumini mzuri huku bado anaendelea kuipinga CCM kinyume na maelekezo ya viongozi wake wa kidini? Au bado wapo baadhi ya Waislamu ambao msimamo wao haujatetereka dhidi ya CCM na serikali yake?
Ni maswali ya uchokozi wa kifikra tu. Natumaini mawazo yenu juu ya somo husika yatanisaidia kuandika makala ambayo itajaribu kushughulikia suala hili kwa kiasi cha kutosha.
Hivi ujui usemi wa wahenga ya kwama zimwi likujualo halikuli ukaisha; na hivyo kwa mujibu wa hivyo vitabu ulivyovinukuu Bakwata ilifinyangwa na kpewa uhai wake na TANU ambayo ndiyo chimbuko la CCM. Kwahiyo Mufti kama kiongozi mkuu wa Bakwata yuko sahihi kabisa anapoitetea CCM. Jambo linaloshangaza ni kwa haya makundi mengine ambayo yamekuwa yakilalama ya kuwa dini yao kwa kupitia Bakwata imekuwa ikiendeshwa kama asasi ya serikali, kuona hivi sasa yamegeuka na kuwa mtetezi mkubwa wa serikali hiyo hiyo!

 
Kabla sijachangia au kujibu swali lako, wewe kwa uchambuzi na ufahamu wako unakubaliana na lalamiko la Waislamu kuwa wamefanywa daraja la pili au kudhulumiwa na Serikali zote tangu Mkoloni, Nyerere na mpaka sasa? maoni yako wewe ni yapi? ikiwa utajibu swali hili basi nami nitakujibu kuhusu Waislamu na CCM ya sasa!!!!

NIKIYAAMINI maneno ya kina Njozi na Said na wengine juu ya udhalimu wa CCM najikuta sina uchaguzi isipokuwa kukubali kuwa matatizo ya Waislamu yamesababishwa na kuchangiwa na CCM.

Haya nijibu.
 
Mzee Mwanakijiji ... kwanza heshima mbele

hapa umemaliza kabisa ..... uadui iliyonayo CCM kwa wananchi wakiwemo waislamu muda wote wa utawala wake kwa kuwanyima maendeleo na maisha bora ndicho kitu tunachotakiwa kujiuliza .... na sasa uadui huu CCM inataka kuupeleka/kuhamishia kwenye chama fulani ambacho imeona ndicho tishio ili basi waendelee kuvimbiwa na rasilimali za nchi yetu nzuri tanzania ..... sasa basi sisiem itujuze je ni lini waliwahi kuwasifia waislam au hata kuwapatia ushauri kwa ajili ya maendeleo ya taifa kwa ujumla na si kuwatumia kwa maslahi tu ya kujikita madarakani .... hivyo basi kuhamishia ugomvi wa watanzaniA wakiwemo waislamu na sisiem kwa CHADEMA ...... hakika sisiem inatenda dhambi ambazo hakuna dini inayoweza kusamehe
 
Mzee Mwanakijiji, waswahili wanasema; 'zimwi likujualo' au kwa kiiglishi, it's better to work with the devil you know than trying the unknown. Kumbuka hii move ya waisilamu ni counter-attack inayotokana na jinsi kampeni za uchaguzi wa 2010 zilivyoendeshwa na hadi sasa majeraha hayajakauka!
 
Mzee Mwanakijiji, waswahili wanasema; 'zimwi likujualo' au kwa kiiglishi, it's better to work with the devil you know than trying the unknown. Kumbuka hii move ya waisilamu ni counter-attack inayotokana na jinsi kampeni za uchaguzi wa 2010 zilivyoendeshwa na hadi sasa majeraha hayajakauka!

lakini yote wanayoyajua juu ya CCM ni mabaya at least kama wasomi na wanazuoni walivyojaribu kutushawishi. Sasa kama kuna kitu kimebadilika kwenye sera, mfumo, muundo au hat aahadi za CCM kwa WAislamu ndio nataka kujua maana inawezekana hiyo memo haijawahi wazi bado.
 
Mzee Mwanakijiji,
Unakumbuka nadhani ilikuwa katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2000 au 2005 baadhi ya Waislamu walitoa mwito CCM isipigiwe kura. Nadhani wakati huo matumaini yalikuwa ni kwamba CUF ndio chama chenye matumaini kwa malengo/maslahi ya waislamu. CCM ikawaahidi mahakama ya kadhi, malalamiko yakaisha. Akachaguliwa Kikwete. Akaanza kupanga safu za kuwapromote Waislamu serikalini, kwenye nafasi za juu na nafasi nyeti. Ndugu zetu wakanyamaza. Wakaona, aah, kumbe huyu Muislamu mwenzetu anajali maslahi yetu. Sasa tugeukie 2010.
Chadema walipomsimamisha Slaa, nadhani kuna watu ndani ya CCM walishtuka. Akaanza kushambuliwa na magazeti ya Rostum. Suala la udini likawa injected kwenye kampeni. Na aliyeanzisha suala hilo, kwa kutumia marionette wake, alikuwa Jakaya Kikwete. Sasa baada ya uchaguzi,Chadema kikaibuka chama kikuu cha upinzani nchini. Wale wenye udini wakashtuka, kukiwa pamoja na huyo puppeteer wao. Akawafadhili mashehe kwenye kikao chao pale Diamond Jubilee, eti wanakemea udini. Sasa ni kama wametangaza vita kamili dhidi ya Chadema kana kwamba Chadema ndicho kimeleta matatizo yanayoikumba Tanzania ya leo. Hawazungumzii tatizo la ufisadi, hawazungumzii tatizo la kushuka kwa kiwango cha elimu Tanzania, hawazungumzii tatizo la kupanda kwa gharama za maisha, hawazungumzii jinsi Tanzania inavyotafunwa na wachache wakishirkiana na mabwana zao kutoka nje. Kikwete is the puppeteer behind the religious marionettes, and you can quote me on that any time.
 
Dini ni SIASA Mwanakijiji.....

Kuna hii sentesi inasema "Nations have no permanent friends and no permanent enemies. Only permanent interests." Kwa maana hiyo, hata Waislaam wanaangalia tu wapi wataweza kuganga njaa kwa urahisi.

Sasa hapa ukiangalia, wanajua kabisa kuwa wakija Chadema kutawala, wengi wao watakufa njaa maana mirija mingi inaweza kukatwa. Hapo ndiyo inakuja ile statement ya Mkuu hapo juu kuwa kwa Waislaam wa Tanzania, pamoja na mabaya yoote ya CCM, wanaona kweli wachague ZIMWI LIKUJUALO.

Kibaya zaidi kwao ni kuwa CUF imejitia kitanzi yenyewe na umekuwa mwisho wao baada ya kuchezea IMANI za Watanzania. CCM badala ya kuiacha walau iwe inapumua kidogo, waliishambulia na kuiacha hoi.

Wakija Chadema, itabidi kucheza RAFU kwa WAVIVU na wezi wote Tanzania bila kujali dini. Itakuwa vizuri kuwaanzia kwanza Wakristo kuwapandisha kizimbani na mwisho wanamalizia kwa Waislaam na wasio na dini.
 
Labda wanayasema hayo wanayoyasema ili kuandaa platform kwa chadema kutafuta njia za kushiyokiana nao maana wakati mwingine inabidi mtu atoe malalamiko ili mlengwa amuondolee wasiwasi! Sijajua ni vipi chadema wanapanga au kama kuwatoa Waislam wasiwasi pindi wakishika dola ! Hata hivyo Madai ya Waislam huwa hayako wazi sana ni kama vile wanaendana current issues mfano ni maandanano ya kupinga Libya kushambuliwa
 
Kwa utamaduni wa CCM mwaka 2015 kwa namna yoyote ile mgombea lazima atakuwa mkristo, mwenye notebook aandike maneno haya, na hapo ndipo unafki wa wale baadhi ya waislamu walioamuwa kwa makusudi kuzifungia akili zao stoo utakapowajuwa. CCM wameshajichimbia kaburi wenyewe, kinachosubiliwa ni kuwazika rasmi mwaka 2015. hii dhambi ya Udini aliyoileta Kikwete haitawaacha salama.
 
Nafikiri hapa ni udini tu kwa sababu raisi ni muislam wanadhani itakuwa ni vema kutetea ccm na selikari yake ili kwa vile raisi ni muislamu awapendelee waislamu zaidi mi sioni kama kuna urafiki hapo.
 
Ila wana bahati mbaya kwa Sababu ukiangalia Alama zote mbinguni na duniani, zinaonyesha kuwa Mgombea ajaye wa CCM, LAZIMA atakuwa Mkristo. Ila sijui tu atatoka kanisa gani na la muhimu zaidi ni Je, Ni Mkristo wa ukweli au kama huyu alisemwa na Nyerere yaani George Kahama kuwa ni Mkristo ila nyumbani ana wake wawili?

Kama Kikwete ni Muislaam wa kweli, basi kweli kuna siku Papa atatoka JAMAICA.
Huko kitambo nyumaTANU na CCM viliigeuza BAKWATA kuwa taasisi yao...Sasa BAKWATA inaigeuza CCM taasisi yao
 
ndugu yangu rangi2, kwa hakika nakwambia aliyeleta/anaye inject dhana ya udini ni mh j. kikwete. na maskini ya mungu waislamu(no niseme masheikh na viongozi baadhi) maana naamini kuna waislamu wengi tu hawaafikiani na matamko/movements za viongozi wao/masheikh. hatari yake ni kubwa sana mbeleni na bahati mbaya mr president anaangalia kusolve tu problem ya wakati huu wa maandamano, mikutano,kuhamasishana. ni kikwete ndugu yangu ndo anapandikiza dhana hii ya udini
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom