Ni lazima tugawanyike; Lazima tusiwe na umoja! -Yes I said it

Unacho-advocate mgawanyiko ni dhana potofu kupita zote

Kinachotakiwa si kuwanyika bali ni kukubaliana katika kutofautiana

kwamba mbuzi na chui wakubaliane kutofautiana kuwa nani kati yao amle mwenzake; halafu wanatakiwa kuheshimu "tofauti hiyo".!
 
Kuna tofauti kati ya kugawanyika na kutofautiana. Tunatofautiana. Hatujagawanyika. Wala hatutagawanyika kamwe. Umoja na mshikamano ni urithi wa Chama kilichotukomboa.Tuuenzi na kuulinda umoja na utulivu. Kwa pamoja, Mwanakijiji, Mwanajiji, Mkulima, Mfanyakazi, Mfanyabiashara na Mwekezaji, tujenge Taifa letu changa.

Umoja ni Nguvu!

kamwe haiwezekani kuwa na umoja mwituni...!
 
kuna kila dalli kuwa hapa jamvini kuna watu wana kazi ya kumpigia makofi mwanakijiji hata kama hawajaelewa ametoa mawazo gani!!!!!!!!!!!

jamani jaribuni kuthink critically, kama ni kutofautiana kimtazamo, matakwa, itikadi nk. mbona tayari tunatofautiana? tutofautiane mara mbili? au mara ngapi???

ishu ni "kugawanyika" nipeni mfano wa nchi kama yetu hususani ya kiafrika "iliyogawanyika" halafu hapakutokea mapigano/umwagaji damu na badala yake waka[pata maendeleo..............

nakubaliana na hoja ya tumaini..............

Usishangae ndio wala 70% ya JK kila kitu anachosema mwanakijiji kwao "ndiyo mzee" pathetic

Hakuna watu walioendelea huku wamegawanyika Iran mfano mzuri walipokuwa wamoja wamliweza kumuondoa Shah (dhalimu)

Kugawanyika ni mtazamo mwingereza kuwaganya watu ili watawale, ni vurugu katika kugawanyika ndio matagemeo yetu
 
kwamba mbuzi na chui wakubaliane kutofautiana kuwa nani kati yao amle mwenzake; halafu wanatakiwa kuheshimu "tofauti hiyo".!

Kwamba mbuzi na chui waishi kila mtu ale urefu wa kamba yake na uwezo wake bila kuharibu na kupigana japo wanatofautiana kwa namna na viwango vya ulaji kwakuwa wako tofauti kimaumbile, elimu, uwezo nk.
 
hayo ndiyo mawazo ya kusikitisha; sasa chui ale kwa urefu wa kamba yake; ale majani?
 
i come in peace.

what this guy is talking about is POLITICAL AWARENESS. tanzanians are alittle bit timid when it comes to politics. i do not not wish tanaziania to have the tribal politics of kenya BUT you cannot deny that kenyans are very politically active and sensitive which makes it a vibrant democracy. imagine the corrupt and greedy kenyan leaders never had an active kenyan population and media to keep the kenyan politicians in check? kenya would be worse than somalia.

the little democracy kenya has is purely because the common mwananchi stood up and fought for it.
on the other hand tanzanian leaders know that tanzania is democratic but a DORMANT democracy becuz tanzanians are not politically active or sensitive. the political class of tanzania know that tanzanians WILL NOT hold them accountable.

on the other hand i guess it is a good thing that tanzania is politically "dormant" that is why tanzania is so peaceful. something that other EAC countries do not have.
i guess you cant have both ways.

just my opinion.
 
jamani tumechoka na amani?

tumekerwa na utulivu?

tunaomba mapambano?

tutnatamani vita?

huko zanzibar damu ilimwagika, wanofaidi sasa bado ni wanasiasa wachache sana matunda ya ile damu, nao ni mfano, hamadi rashid mohamedi maalim seif, sasa jusa ladhu nk

kenya damu ilimwagika, wanaofaidi matunda ya ile damu ni wachache kama raila, nk.

tunawezaje kuwatamani hawa? wanasiasa wanawatamani lakini watu wa kawaida hata huko walikogawanyika wanawatamani watanzania!!!!!!!!!! pamoja na umbumbumbu wetu.

mwanakijiji wewe unaishi marekani, nami pia kwa sasa naishi nje, kumbuka kuna wenzetu wengi sana huko nyumbani ambao kama tukigawanyika na baada ya kitambo kidogo tukaanza kutwangana basi watakufa hadi waishe!!!!!!!!!

katika lolote linalohusi amani, sitakubali tugawanyike

heri tuwe masikini na kuonekana nwajinga, kuliko kuwa matajiri wajanja wanaouana kwa kuchochewa na wanasiasa.............

Mungu ibariki tanzania

you must be kidding...nani afe?mtakufa nyie mliokimbilia nje ya Tanzania.tunataka kugawanyika.
 
Kugawanyika kimtazomo, kimaslahi, liuchumi na hata kisiasa ni muhimu katika jamii yoyote ile iliyostaraabika na kuelemika vya KUTOSHA.Hapa Tanzania ni kipi cha kutufanya tushikamane ili tusiweze kugawanyika? Viongozi wanarithishina madaraka, watoto wao wanasoma shule za kimatifa yenye walimu wa kutosha, matokeo yawe ya form fou au six wana division one, wakati watoto wa wakulima wainaishia kwenye shule zam kata mwalimu mmoja au wawili mbaya zaidi hata wenyewe hajui pa kulala wala kucharge simu zao, Umoja unatatoka wapi katika mazingira kama haya kama siyo unafiki? Imefikia wakati tusema sasa tunahitaji maendeleo na ili kupata maendeleo lazima tuwe na siasa safi, rasilimali na uongozi bora.
Mimi sina sababu za mtu kuja kunihubiri kuwa tushikame, kwa lipi hasa? shame up on you shameless leaders failed to fulfil their responsibility na kutufanya tuishi maisha ya dhiki.
 
kuna kila dalli kuwa hapa jamvini kuna watu wana kazi ya kumpigia makofi mwanakijiji hata kama hawajaelewa ametoa mawazo gani!!!!!!!!!!!

jamani jaribuni kuthink critically, kama ni kutofautiana kimtazamo, matakwa, itikadi nk. mbona tayari tunatofautiana? tutofautiane mara mbili? au mara ngapi???

ishu ni "kugawanyika" nipeni mfano wa nchi kama yetu hususani ya kiafrika "iliyogawanyika" halafu hapakutokea mapigano/umwagaji damu na badala yake waka[pata maendeleo..............

nakubaliana na hoja za tumaini na companero..............

Kaka tangu ulipoanza hoja zako ni nzuri zina nguvu na kinachotakiwa hapa jamvini ni kutofautiana kwa hoja, na kuelekea sehemu moja, our mission is the same, we want to reach where we are dreaming

Lakini ukishaanza hoja za kutuhumu wengine kwa kufikirika sio vizuri, kuna wengine humu huwa tunapinga na kukubali hoja regardless nani katoa.

Dont feel inferior, usitafute mawe, twende kwa hoja. Mimi nimeanza kusoma taratiiibu thread hii na nikafurahi nilipoona mawazo yako , lakini ulichosema hapo juu sijakifurahia, kuwa watu wanakubali tu anachosema MKJJ!!

Mimi naona lugha fulani ya kitu kimefichwa hapa!

Kwamba mbuzi na chui waishi kila mtu ale urefu wa kamba yake na uwezo wake bila kuharibu na kupigana japo wanatofautiana kwa namna na viwango vya ulaji kwakuwa wako tofauti kimaumbile, elimu, uwezo nk.

Lakin in reality nature haiwaruhusu wafungwe kamba!!! Chui lazima atafute mawindo! Mbuzi ndio anaweza kufungwa kama akiwa chini ya binadamu tu. mbuzi lazima wawe na mchungaji pia kama hutaki kumfunga kamba

Then mawazo yako kuwa kuna chui na mbuzi ni ya kusikitisha zaidi from very beginning! wrong prima faci!

what if Chui ni fisadi na mbuzi ni clean person like Tumaini?
 
Web,
Kama chui ni fisadi (kumbe hana makucha anakula majani kama tumain) then wako sawa kimaumbile tunaweza kuendelea na hoja

Tutafoutiana na huyo fisadi na tutamnyaganya anachokula ambacho si chake sisi kina tumain bila kugawanyika
 
kuna kila dalli kuwa hapa jamvini kuna watu wana kazi ya kumpigia makofi mwanakijiji hata kama hawajaelewa ametoa mawazo gani!!!!!!!!!!!

jamani jaribuni kuthink critically, kama ni kutofautiana kimtazamo, matakwa, itikadi nk. mbona tayari tunatofautiana? tutofautiane mara mbili? au mara ngapi???

ishu ni "kugawanyika" nipeni mfano wa nchi kama yetu hususani ya kiafrika "iliyogawanyika" halafu hapakutokea mapigano/umwagaji damu na badala yake waka[pata maendeleo..............

nakubaliana na hoja za tumaini na companero..............

Ndio maana nikasema hapo awali kuwa inategemeana na maamuzi,hivi wewe unaweza kuishi tu bila kufanya maamuzi yoyote yale?Mkitofautiana kimawazo,kimaamuzi mtagawanyika,sasa kigumu kuelewa hapo ni kipi?
Hatuwezi kupata maendeleo kama hatutafanya maamuzi flani flani,kutokufanya maamuzi ni kubaya sana,kumetufikisha hapa tulipo,na hivyo sikushangai.
 
Sasa naanza kuelewa.
Kuna kuna chui wanaokamata mabango kuwa chui wengine wasiwale swala
Wakati inajulikana wazi kuwa watawala tu hata mesia aje.
Kwa nn swala wasitofautiane na chui kwa kutowaamini na kuamua kutafuta
Mkakati wa kuendelea kuishi bila kuwaua chui wote asituni?
 
Inawezekana kuwakusanya chui wote na kuwapa semina ya mahusiano bora mwituni na swala? Kwamba tuwaastarabishe na kuwaeleza ubaya wa kitendo chao cha kukimbiza swala na kuwa ni uvunjaji mkubwa wa haki za swala? Baada ya semina ya kila siku nzima huku chui wakiwa wamemaliza mkutano na kukubaliana kuwa siyo vizuri na haki kwa wao kula swala halafu akajipitisha swala wakati chui wanatoka Ngurdoto unafikiri chui wataangalia notes zao...
 
Si lazima tuganyike ili kufikia malengo,tunaweza kutofautiana kimawazo,tena kwa muda tu,lakini inapofika kwenye maslahi ya taifa ni lazima tuache tofauti zetu,nani kawaambia Warekani huwa wanagawanyika,ninachojua hutofautiana kwa hoja tu lakini inapofika kwenye swala lenye maslahi ya wamerekani hakuna cha democrats au republican they all join hands,mfano mzuri ni vita ya Iraq aliyoianzisha Bush,alipowaambia Wamerekani sababu ya vita ni kupigania maslahi ya marekani wengi waliamua kumuunga mkono hata kama mioyo yao ilikuwa dhaifu,..kwa hiyo tupingane kwa hoja lakini tusigawanyike hasa linapokuja kwenye swala la uchagua amani au vita,ufisadi au uadilifu,..ni lazima sote tuungane kutetea amani na uadilifu na tusigawanyike kwa hili,eti liwepo kundi la watetea ufisadi halafu pia liwepo kundi la wapinga ufisadi...
 
Hli nalo neno.
Yupo chui aliye tayari kufanya plastic surgery na kuondoa makucha yake, awekewe meno yasiyo na ncha ili aweze kula majani?
Ni nani basi chui aliye tayari kuyafanya haya kwa uwazi ili swala amuamini?
Sisi mbuzi tuliobahatika kupata protection japo si ya kudumu dhidi ya chui, hatuna budi I kuwasaidia
Swala ili tuwe na mpango dhabiti wa kuhakikisha majani yanapatikana kwa wingi na chui hapati nafasi ykuamya
Na chui hawapati nafasi ya kututafuna kila wasikiapo njaa. Plan ambayo itawafanya chui wajifunze kula nyasi na
Kunywa maji ya mtoni au korongoni.
 
Si lazima tuganyike ili kufikia malengo,tunaweza kutofautiana kimawazo,tena kwa muda tu,lakini inapofika kwenye maslahi ya taifa ni lazima tuache tofauti zetu,nani kawaambia Warekani huwa wanagawanyika,ninachojua hutofautiana kwa hoja tu lakini inapofika kwenye swala lenye maslahi ya wamerekani hakuna cha democrats au republican they all join hands,mfano mzuri ni vita ya Iraq aliyoianzisha Bush,alipowaambia Wamerekani sababu ya vita ni kupigania maslahi ya marekani wengi waliamua kumuunga mkono hata kama mioyo yao ilikuwa dhaifu,..kwa hiyo tupingane kwa hoja lakini tusigawanyike hasa linapokuja kwenye swala la uchagua amani au vita,ufisadi au uadilifu,..ni lazima sote tuungane kutetea amani na uadilifu na tusigawanyike kwa hili,eti liwepo kundi la watetea ufisadi halafu pia liwepo kundi la wapinga ufisadi...

Uungane na nani dhidi ya ufisadi?Utaungana na mafisadi dhidi yao?Kama Richmond et al ndo maslahi ya Taifa, then kuna haja gani ya kugawanyika?
Siyo kila kitu ni maslahi ya Taifa,na ndio maana umoja unaweza usiwepo,usikariri,na ndio maana kuna kutofautiana na migawanyiko,mfano wako ni sawa na kufananisha machungwa na ndizi....Umeshaambiwa chui ni chui na mbuzi ni mbuzi tuuu! ha ha!
 
jamani tumechoka na amani?

tumekerwa na utulivu?

tunaomba mapambano?

tutnatamani vita?

huko zanzibar damu ilimwagika, wanofaidi sasa bado ni wanasiasa wachache sana matunda ya ile damu, nao ni mfano, hamadi rashid mohamedi maalim seif, sasa jusa ladhu nk

kenya damu ilimwagika, wanaofaidi matunda ya ile damu ni wachache kama raila, nk.

tunawezaje kuwatamani hawa? wanasiasa wanawatamani lakini watu wa kawaida hata huko walikogawanyika wanawatamani watanzania!!!!!!!!!! pamoja na umbumbumbu wetu.

mwanakijiji wewe unaishi marekani, nami pia kwa sasa naishi nje, kumbuka kuna wenzetu wengi sana huko nyumbani ambao kama tukigawanyika na baada ya kitambo kidogo tukaanza kutwangana basi watakufa hadi waishe!!!!!!!!!

katika lolote linalohusi amani, sitakubali tugawanyike

heri tuwe masikini na kuonekana nwajinga, kuliko kuwa matajiri wajanja wanaouana kwa kuchochewa na wanasiasa.............

Mungu ibariki tanzania

KUPINGANA HUKO NI KWA HOJA NA KAMA KIKUNDI FULANI KITASHINDWA KWA HOJA HAKIWEZI KULETA VURUGU BALI KITAKAA KANDO NA KUANGALIA WALIO SHINDWA WANAFANYA NINI.KAMA MSHINDWA ATALETA VURUGU BASI HAKUNA DEMOKRASIA.
Anachotaka na kusisitiza mkjj ni demokrasia inayoruhusu uhuru wa mawazo,kama kiongozi kakosea aambiwe na kama hataki kubadilika apingwe kwa hoja.
 
Mara kwa mara watawala wamekuwa wakituasa kuwa tofauti zetu zisisababishe mgawanyiko katika jamii na kuwa ni muhimu kuendeleza "umoja, utulivu na mshikamano".

Mimi nimeamua kukataa kuwa na umoja wa namna hii! Demokrasia ya kweli inatulazimisha kutofautiana kwa hoja, sera, na hata mitazamo; tofauti hizi zinatusababisha kushindwa kukaa pamoja na kukubaliana. Hivyo, kuna wakati ambapo mgawanyiko siyo tu ni muhimu lakini ni lazima vile vile.

Mgawanyiko tunaouona kula Iran
Mgawanyiko tuliouna kati ya mashabiki wa Bush na Obama
Mgawanyiko kati ya KANU na kina Mwai

Kama tunataka tupige kura inavyopaswa mwaka huu, ni lazima tugawanyike! CCM wanaelewa lugha ya mgawanyiko tu.. ndio maana leo wamekubali kukaa meza moja na CUF kwa sababu Wazanzibari wamegawanyika!!

Bara tunaogopa siasa za "kugawanyika" na hivyo tunalazimishwa kuwa katika umoja wa ulaghai na mshikamano wa uongo; haiwezekani kuwafunga ng'ombe na punda walime pamoja!

Wao wenyewe wanatugawanya sana karibu kila siku; tatizo kuwa tukianza kugawanyika wanashangaa mbona tunagawanyika! Ni kama mambo yale ya "Ukipanda nshale, ukishuka nshale, ukitingishika nshale, usiseme wala usimumunye!! "

Kwanini tunaogopa kugawanyika?

Mwanakijiji, ingekuwa vema kama ungeelezea kidogo 'kugawanyika' ulikokukusudia na kwa nini hutoi suggestion bali unarule kwamba ni lazima tugawanyike.

Ama baada ya hapo, ueleze jinsi tutagavyogawanyika. Sio sahihi kusema tugawanyike bila kutoa muongozo wa huko kugawanyika, at least hata kwenye hitimisho.

Kwa independent thinker, inakuwa vigumu kuunga mkono au kuyakataa mawazo yako ya kulazimisha watu wagawanyike.
 
Back
Top Bottom