Ni lazima nafasi nyeti zichukuliwe na "wastaafu"?

kweli nchi inaendeshwa kishkaji...umenikumbusha kitu...!!

waziri masha ameshamlalamikia huyu jamaa kwa rais kuwa hawaheshimu yeye waala naibu wake.....na katika siku za karibuni habari za uhakika walikuwa kama paka na panya.....nadhani jk amechukia kwa nini jamaa hamuheshimu rafiki yake....kaamua kumpeleka dampo ya mahasimu wake wizara ya ardhi akakae pale na waziri magufuli!!!!

Kwani JK alishampeleka Magufuli Wizara ya Ardhi kutoka Mifugo?.......hee basi nimepitwa na mengi


pia natoa pongezi kwa salome sijaona ...kwani ni kati ya makatibu wakuu waadilifu.., ardhi kuna kashfa sana lakini sijapata kumsikia na tatizo pale......na amekaa miaka mingi sana pale.............
kudos salome!!

Kwa kweli Mama ni mchapa kazi muadilifu......nafikri Mrema wa TANROADS atakuwa amepata relief sana kusikia hizi habari..........

BTW.....Phil.....huyu Mama hizi siku zake za mwisho pale Wizarani amekuwa na pilika pilika nyingi sana kwenye mambo ya ardhi na hasa kule kwao........nahisi ndio alikuwa anajijengea channel ya ubunge..........ngoja tusubiri time will tell.............
 
Mkandara,

..Rutabanzibwa alipinga IPTL wakati akiwa Kamishna wa Nishati. tena aliipinga wakati wa utawala wa Mzee Mwinyi.

..alipoingia Mkapa, Rutabanzibwa akateuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Madini na Nishati.

..madudu mengi sana yametokea Wizara ya Madini ktk kipindi ambacho Rutabanzibwa alikuwa katibu mkuu.

..hata MOU kati ya serikali na Richmond kujenga bomba la mafuta ilisainiwa na Rutabanzibwa.

..sijui ni kwanini tunafikiri Rutabanzibwa atafanya maajabu huko Wizara ya Ardhi, wakati alishindwa kuzuia madudu yaliyofanyika Wizara ya Nishati na Madini.

Jasusi,

..sasa kama Rutabanzibwa alimshindwa Mkapa mnategemea atamuweza Kikwete?

..kwa nchi kama yetu Raisi ni mtu muhimu sana, kwa hiyo tunapaswa kuwa makini tunapopiga kura.
 
Mtu B,

..hebu tueleze Maywether na Cheka ndiyo nani manaake umeniacha solemba.
 
Mkandara,

..Rutabanzibwa alipinga IPTL wakati akiwa Kamishna wa Nishati. tena aliipinga wakati wa utawala wa Mzee Mwinyi.

..alipoingia Mkapa, Rutabanzibwa akateuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Madini na Nishati.

..madudu mengi sana yametokea Wizara ya Madini ktk kipindi ambacho Rutabanzibwa alikuwa katibu mkuu.

..hata MOU kati ya serikali na Richmond kujenga bomba la mafuta ilisainiwa na Rutabanzibwa.

..sijui ni kwanini tunafikiri Rutabanzibwa atafanya maajabu huko Wizara ya Ardhi, wakati alishindwa kuzuia madudu yaliyofanyika Wizara ya Nishati na Madini.

Jasusi,

..sasa kama Rutabanzibwa alimshindwa Mkapa mnategemea atamuweza Kikwete?

..kwa nchi kama yetu Raisi ni mtu muhimu sana, kwa hiyo tunapaswa kuwa makini tunapopiga kura.

Joka,

Kwa kweli inashangaza sana kuona watu wanampa credit Patrick pamoja na madudu mengi aliyoyafanya...........hata lile dili la IPTL inawezakana alikuwa bado hajaingizwa kwenye "Network".......maana inashangaza kuona mtu alipinga dili la IPTL huku mara ghafla kaanza kutuingiza mikenge........
 
Mtu B,

..hebu tueleze Maywether na Cheka ndiyo nani manaake umeniacha solemba.

Hao jamaa ni mabondia professional, huwajui? Mayweather hajawahi kupigwa tangu aanze za kulipwa, na mara ya mwisho alimtwanga muingereza Hatton ambaye naye pia alikuwa hajapigwa. Wa kimataifa huyu Mayweather, mmarekani mweusi.

Cheka ni wa hapa bongo, kawatwanga wote wenye longolongo kuanzia kina Marwa, Matumla, na juzi kamdondosha kwa TKO bishoo flani anaitwa Kaseba, ngumi moja hadi nje ya ulingo.

Nawe nikuulize: Unadhani yule Hatton aliyepigwa TKO na Mayweather ati atamshindwa Cheka?
 
Mtu B,

..nimekuelewa.

..lakini si unaona jinsi Rutabanzibwa anavyopigwa danadana kwa kuhamishwa toka sehemu moja kwenda nyingine?

..kwa ujumla uongozi wa CCM hauna nia ya dhati kubadilisha ufumo wa utawala na uwajibikaji ktk nchi yetu.

..well inawezekana Mkapa alikuwa anaiba huku amekunja sura, lakini Kikwete naye anaiba huku anatabasamu. at the end of the day wote wawili wameiba.


..
 
Joka,

Kwa kweli inashangaza sana kuona watu wanampa credit Patrick pamoja na madudu mengi aliyoyafanya...........hata lile dili la IPTL inawezakana alikuwa bado hajaingizwa kwenye "Network".......maana inashangaza kuona mtu alipinga dili la IPTL huku mara ghafla kaanza kutuingiza mikenge........
Ogah,
I think the problem is not Patrick. It is the system. Wenzako wakiwa wanafanya madudu na wewe hushiriki au unawapinga you become the enemy.
 
OOppssss! i keep telling people we don't need to rotate the current leaders from one ministry to the other or from one post to the other,we need to change the whole system...yaani kama ni engine then kuifanyia overhauling......."to change a system it needs a more strong system"hii ndio naona challenge sio tu kwa vyama vya upinzani bali wale wote wapendao maendeleo ya kweli
 
Jokakuu,
Ebu tujikumbushe vizuri kwa sababu Patrick kawa sehemu mbili tofauti kwa nyakati mbili tofauti..Nachokumbuka mimi Ruta alikuwa wizara ya nishati wakati wa Mwinyi (Ok kamishna) na ndiye aliyesimamisha mkataba wa IPTL.. hilo halina ubishi au sio?.. Ni Ruta tene huyu huyu alikuwa tena PS wizara hiyo wakati Mkapa hadi Kikwete anaingia madarakani na ndiye aliyepinga ununuzi wa Richmond (rejea report ya Mwakyembe). Hii pia kuna report yake ambayo tuliitumia hapa JF siku za nyuma..Kisha mkuu wangu habari ya ujenzi wa bomba ilikuwepo toka wakati wa Mkapa, hivyo kusema kwamba Ruta ndiye aliweka sahihi mkataba wa Richmond nadhani hapa mkuu nitahitaji ushahidi hata mdogo tu kwani Ruta ndiye alikuwa kizuizi kikubwa cha Richmond/ kina Lowassa ndio maana madudu mengi yalifichuka..

Huko nyuma sikumbuki vizuri isipokuwa najua Ruta aliwahi kuwa PS Wizara ya mambo ya ndani wakati wa scandal ya TanGold (Meremeta), kesi inayomkabili Mgonja. Kwa hiyo kuwepo kwake Wizara ya ndani ni mara ya pili sielewi ni wakati gani alihama toka wizara ya nishati kwenda mambo ya ndani kisha akarudi tena Nishati na kurudishwa tena mambo ya ndani... kifupi inachanganya sana Ruta alikuwa wapi wakati kitu fulani kinatokea na nini nafasi yake..Amekuwa akizunguka wizara hizo kwa kipindi.

Hata hivyo nimechimba JF na kupata habari hii ndefu sana aloiweka Mzalendo -POWER and The VAINGLORY
 
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ameteua makatibu wakuu wapya wanne wa Wizara, na amewahamisha wawili.

Rais Kikwete pia amemteua Katibu wa Rais, mabadiliko hayo yanaanza leo Oktoba 19.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, imeeleza kwamba, Rais Kikwete amefanya mabadiliko hayo kwa kuwa baadhi ya makatibu wakuu wa Wizara wamestaafu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ikulu, Rais Kikwete amemteua, David Kitundu Jairo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.

Kabla ya uteuzi huo, Jairo alikuwa Katibu wa Rais. Jairo anachukua nafasi ya Arthur Mwakapungi, amestaafu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Rais Kikwete pia amemteua, Sethi Kamuhanda, kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.

Kabla ya uteuzi huo, Kamuhanda alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kamuhanda anachukua nafasi Dkt. Florence Turuka.

Turuka anahamishiwa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kuwa Katibu Mkuu.

Turuka anachukua nafasi ya Dkt. Naomi Katunzi, kwa kuwa Novemba mwaka huu anamaliza mkataba wake wa utumishi wa Serikali.

Luhanjo amesema, Rais Kikwete pia amemteua, Sazi Salula, kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kabla ya uteuzi huo, Salula alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Taarifa hiyo pia imebainisha kwamba,Rais amemteua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais,Mbarak M. Abdulwakil, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Abdulwakil anachukua nafasi ya Patrick Rutabanzibwa. Rutabanzibwa amehamishiwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa Katibu Mkuu.

Rutabanzibwa anachukua nafasi iliyoachwa na Salome Sijaona, amestaafu.

Taarifa ya Luhanjo imee;eza kwamba,Rais Kikwete pia amemteua,Christopher N. Sayi kuwa Katibu Mkuu wa Wizata ya Maji na Umwagiliaji.

Kabla ya uteuzi huo,Sayi alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo hiyo, anachukua nafasi ya Wilson Mukama. Mukama ameanza likizo ya kustaafu kwa mujibu wa sheria.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,Rais Kikwete amemteua, Prosper Mbena, kuwa Katibu wa Rais.

Kabla ya uteuzi huo, Mbena alikuwa Msaidizi wa Katibu wa Baraza la Mawaziri, anachukua nafasi ya Jairo.

http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3929
 
Huwa nashuhudia kila mara Mheshimiwa President anateua makatibu wakuu katika wizara mbalimbali. Kwa ninavyofikiria mimi hawa wanatakiwa wawe professionals kwenye wizara wanazoteuliwa sababu wao ndio watendaji wakuu katika wizara hizo. lakini kila kukicha tunashuhudia uozo wa kila namna kwenye mawizara yetu na mara nyingi sana tunatupia lawama kwa mawaziri ambao ni political figures.
Huwa najiuliza mara nyingi hawa makatibu wakuu wanakuwa wapi wakati mawaziri wao wakifanya uozo wanaoufanya? Ina maana wao huwa hawashirikishwi kwenye maamuzi ya hizo wizara?
 
Nimeinakili habari ifuatayo kutoka http://drfaustine.blogspot.com/

Kikwete appoints ambassadors

President Jakaya Kikwete has appointed new ambassadors to Japan, Saudi Arabia and Burundi to fill vacant posts with immediate effect.

Kikwete has appointed the retired Permanent Secretary in the Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development, Ms Salome Sijaona as a new has Ambassador to Japan to replace Ambassador Elly Mtango who has retired.

The president has appointed Prof Abdillah Omari, Director of Centre of International Relations in Dar es Salaam as the new Tanzania ambassador to Saudi Arabia, replacing retired Judge Khamis Msumi who has retired.

President Kikwete has also appointed Dr James Nzagi, a director in the President’s Office to be Tanzania’s Ambassador to Burundi, replacing retired Brigadier General Francis Mndolwa who has retired.

My Take: Do you see the pattern here? How many retirements is a civil servant in Tanzania allowed to have?

KUMEKUWA NA TABIA YA NAFASI NYINGI NYETI KUPEWA WASTAAFU...HIVI HAWA WATAWALA WETU WANATAKA KUTUAMBIA WAMEKOSA WATANZANIA WENGINE WENYE SIFA
MPAKA KUTEUA WASTAAFU? JE TUTAFIKA KWA MTINDO HUU? AU NDO KULIPANA FADHILA? NADHANI MTU AKIFIKIA UMRI WA KUSTAAFU KATIKA UTUMISHI WA UMMA APEWE STAHILI ZAKE NA AACHWE APUMZIKE - NDO MAANA YA KUSTAAFU. TUNAWEZA KUWAPA AJIRA LABDA WALE MAOFISA WA JESHI WANAOLAZIMIKA KUSTAAFU WAKIWA WANGALI VIJANA LAKINI SI MTU AMBAYE AMESHAVUKA MIAKA 60.
 
Haraka haraka utaona kama ni kulipana fadhila kweli. Lakini mbona wakongwe hawa walikuwa watu wazito sana kabla hawajastaafu mwanzoni ????.

Halafu tunaambiwa watawekwa madarakani vijana zaidi siku za usoni!!!. Watatoka wapi, wakati hawana nafasi ya kupata uzoefu ???.

Hapa tunadanganyana!!!!.

Unaisikia kabisa kauli ya kuomba kura 2010 !!!!.

Watu hatuna mpango kabisa na Tz ya baadaye. Kila mtu na lwake. Wajao nao watatengeneza Tz yao. Watuache na hii yetu tuifaidi kadri tutakavyo!!!.

Jujawamajuja
 
Jk hana uwezo wa kuangamiza ukristo" you can play with the whole world but you will name play with Rome" karibu nusu ya bajet ya dunia inayakiniwa na Roman-Jewish Federation.Let us live in p-eace
 
Back
Top Bottom