Ni lazima mwanangu akikua ajue coz ninajuta kumpenda baba yake

dah pole mdada mzuri Mungu yupo atakusaidia nimeona umejoin jf soon tarehe 29 mwezi jana sijui ndo ulikuwa unataka ushauri au. Naomba nichukue fursa hii kukukaribisha humu ndani
 
mwaya pole sana kwa hayo yalio kutokea lakini kwanza itabidi uwe mwangalifu sana kwa wamuzi utakao uchukua . manake usije ukajiingiza mwenyewe kwenye makosa
 
mtoto ana mwezi tu

...haya sasa, bibie, nilionalo mimi unahitaji ushauri nasaha tu kukabiliana na post traumatic stress
baada ya kujifungua. wewe sio mwanamke wa mwanzo kukumbwa na hali hiyo ya wasiwasi...

mshukuru mwenyezi mungu kwa kujaaliwa mtoto mzuri mwenye afya, nawe ukiwa mzima wa afya..
hakikisha kwa kipindi hiki unatulia, unakula vizuri, na mwanao anapata +ve vibes toka kwako...
unajipa presha bure tu bidada,...ukiiendekeza itakuletea depression...

piga moyo konde, na uyapokee yote yanayokujia sasa kama challenges na blessings...
sitaki na wala sitopenda kusikia ati nawe ni miongoni wa wale kina dada wanaowachukia watoto wao kwa
kisingizio wamewaletea matatizo duniani...

focus kwenye malezi ya mtoto kwanza miezi hii ya mwanzo nawe ule vizuri mtoto apate lishe bora,
mengineyo yatakaa sawa tu,...
usiwe na wasiwasi...huibiwi na acha kumlaumu mzazi mwenzio, ...huenda nae anakushangaa ulivyombadilikia
ghafla na hizi lawama....

kila la kheri.
 
mwaya pole sana kwa hayo yalio kutokea lakini kwanza itabidi uwe mwangalifu sana kwa wamuzi utakao uchukua . manake usije ukajiingiza mwenyewe kwenye makosa
na ndo kinachonichanganya akili coz ctaki kumshirikisha mtoto kwenye matatizo yetu mm na baba yake.na vilevile ctaki kuacha kumweleza ukweli wa kilichotokea.
 
...haya sasa, bibie, nilionalo mimi unahitaji ushauri nasaha tu kukabiliana na post traumatic stress
baada ya kujifungua. wewe sio mwanamke wa mwanzo kukumbwa na hali hiyo ya wasiwasi...

mshukuru mwenyezi mungu kwa kujaaliwa mtoto mzuri mwenye afya, nawe ukiwa mzima wa afya..
hakikisha kwa kipindi hiki unatulia, unakula vizuri, na mwanao anapata +ve vibes toka kwako...
unajipa presha bure tu bidada,...ukiiendekeza itakuletea depression...

piga moyo konde, na uyapokee yote yanayokujia sasa kama challenges na blessings...
sitaki na wala sitopenda kusikia ati nawe ni miongoni wa wale kina dada wanaowachukia watoto wao kwa
kisingizio wamewaletea matatizo duniani...

focus kwenye malezi ya mtoto kwanza miezi hii ya mwanzo nawe ule vizuri mtoto apate lishe bora,
mengineyo yatakaa sawa tu,...
usiwe na wasiwasi...huibiwi na acha kumlaumu mzazi mwenzio, ...huenda nae anakushangaa ulivyombadilikia
ghafla na hizi lawama....

kila la kheri.

mkuu nashukuru umefunguka maana umetoa kitu kizito
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
na ndo kinachonichanganya akili coz ctaki kumshirikisha mtoto kwenye matatizo yetu mm na baba yake.na vilevile ctaki kuacha kumweleza ukweli wa kilichotokea.

ni mapema sana kufikiria kumweleza ukweli maana heri hata mtoto angekuwa na miaka 7 lakini mtoto hata maternity hujamaliza unawaza ya miaka 15 ijayo???
 
habari wana jf.
kwa muda wa takriban miaka 6 sasa.na nilikuwa naishi naye na.tuliishi kwa upendo na amani.nikapata ujauzito nikalea mimba nikiwa nae mpaka ikafika muda wa kwenda kujifungua nikasafiri kuja kwetu kaskazini kujifungua.

ckupendezwa nikamwambia basi aendelee na ustaarabu wake na mm nitalea mtoto peke yangu coz hata nikimtegemea ni kazi bure coz hakuna alichowahi kunisaidia.
KINACHONIUMA.
~nilimpenda kupita kiasi
~nilipoteza vitu vingi ikiwa ni pamoja na kuacha chuo ajili yake.
~niligombana na ndugu zangu coz of him.
~nw nimeishia njiani sijui nimtambulishe mwanangu kwa baba yake au niache.na sijui moyo wangu utawezaje hata kuniruhusu kuongea nae coz ninamchukia vibaya sana.
AND THATS Y NASEMA MTOTO WANGU AKIKUA LAZIMA NIMPE KISA CHA BABA YAKE.COZ AMENITENDA HASWA.
NAWASHAURI MABINTI KAMA NI KUPENDA IWE NI KWA KIASI ISIWE TOO MUCH THEN MUWE NA MIOYO YA UJASIRI.

Nasita kuamini usemacho, mwenyewe unakiri mmeishi pamoja takribani miaka 6 tena kwa UPENDO na AMANI. na mimba mmelea wote hadi ulipokaribia kujifungua. Si rahisi mwanaume akabadilishwa kiasi cha kuacha mzazi mwenzie na mtoto! twambie ukweli unless lipo tatizo lingine ambalo huenda unahusika kama 'msababishi'.

Na humu unalalamika nini kama mwenyewe umemwambia aendelee na ustaarabu wake nawe utalea mtoto peke yako? Ndo tatizo lenu kinadada, mkiwa na vihela kidogo basi kidogo tu unatoka povu eti unaweza, 'subiri utaona'!

Halafu uwe na soni dada,
iweje miaka 6 mtu hakuna alichowahi kukusaidia! Acha hasira, tulia kisha andika tena maoni yako ili usaidiwe na sio kufura kwa hasira, utaharibu badala ya kujenga.

Kumpenda kupita kiasi hapo nahisi unatudanyanga, kwa kipimo gani? Kupoteza vitu hizo ndo gharama za upendo hapo hakuna jipya.

Huyo mtoto umtambulishe ama la, umwambie au usimwambie alichofanya babaye, ujue kuna siku atamtaka baba yake. Na huo ujinga wenu na mzazi mwenzio msiupandikize kwa mtoto. Mfundishe tabia njema, mlee vizuri ujipatie kibali kwake, ukimdekeza ili akupende na amchukie baba yake utakuwa mjinga maana utampotosha na kumpoteza kimaadili.

Na huo ushauri wako potofu kwa mabinti acha kabisa, kukukuta wewe si maana yake kuwa wote yatawakuta.

By the way piga moyo konde, maisha hayasimami. Punguza hasira ujipange vizuri u can win back ur man.
Mungu akusaidie dada!
 
kuna mtu naplan kumfanyia kama ulivyofanyiwa wewe,make nishamwambia home hawamtaki yeye hatk kuamini,wait...
Sometimes matatizo mengine mnajitakia wenyewe!
 
Jamani mbona visa vya namna hii vipo vingi sana. Kwa nini wanawake hamjifunzi au ndiyo yaleyaleee kwamba mapenzi hayana macho. Pole sana dada yangu na endelea kulea mtoto bila wasiwasi kwani huyo baba mtoto wako ndiyo kakata kamba hivyo. Anaweza kukurudia baadaye mtoto atakapokua.
 
Alikuwa ni mumeo au mlikuwa mnazini tuu?

Kama hajakuoa ni astahili yako na iwe fundisho kukaa na mwanamme bila kuolewa. Huo ni uzinifu na hayo ndio baadhi tu ya malipo yake, ngoja upate bwana mwingine aanze kmyanyasa huyo kwa kuwa si wake, hiyo ni part 2 ya adhabu. Halafu bado unajisifu eti kaniachisha Chuo. Chuo uliacha mwenyewe kwa uzinzi wako na tamaa zako.

Hivi huwa mnategemea wanaume ndio wawape fedha za kulelea watoto wenu na ilhali mmewazaa nje ya ndoa? unanshangaza sana. Au ndio bado ni magolikipa mnaotegemea wanaume kwa kila kitu? Mnafanya uzinzi halafu hamjui hata kujikimu. Ungekuwa unataka mwanamme wa kukutimizia mahaitaji yako ya kila siku basi ungetafuta mume na si kuwa na hawara. Kama kaweza kuwa na wewe ki hawara tu, kwa nini asiwe na wengine?

Huwa mnajitakia wenyewe kwa tamaa zenu za kijinga. Hata umwambie huyo mwanao, hivi huna haya kumwambia mwanao kuwa "wewe ni mtoto wa nje ya ndoa na baba yako alinitia mimba yako halafu akakataa kukutunza". Hilo ndio taifa jema mnalolijenga?

Tutolee huu uchafu hapa.
 
Ni laana hiyo, wazazi walidisturb bajeti yao wakusomeshe chuo ww ukaona uache chuo uishe na mume, zaidi kinyume na taratibu za dini na mila zetu,wala bila baraka za wazazi.Mungu amekunyoshea kidole rudi kwake bado anakuhitaji ww mwanampotevu.
 
ooh my god habari yako imeniumiza kichwa mpendwa ,pole sana haya ni majaribu ya maisha huna budi kupigana nayo,sasa mama fanya namna mtoto akikua urudi shuleni sahau mambo ya visasi,angalia maisha yako kwanza ,mwenyezi mungu atakupigania
 
Maneno ya Faiza machungu lakini yana kaukweli ndani yake!

Ila Faiza; wewe umekuwa na huenda umepitia mikasa mingi ndio maana waweza toa ushauri! Hufikiri kuwa na wengine wana haki ya kukosea ili wajifunze kama wewe? Najua wenye busara wanajifunza kutokana na makosa ya wengine lkn pia experience ni better teacher mradi tu waweza simama na kuanza upya!
 
Pole sana mpendwa, vitu kama hivo huwa vinawapata wanaume wanawake wao wakiwa wajawazito mpaka kujifungua, unaweza rudi mjini ukajikuta mikononi mwake tena na kusahau yote hayo uliyosema juu yake, kuhusu kumwambia mtoto juu ya baba yake wala usije jaribu, coz usije hata siku moja kuleta magomvi yenu kwa mtoto,mwache ae aone mwenye we kama baba yake ni mtu wa aina gani
 
Back
Top Bottom