Ni lazima kizazi hiki kipite kwanza ndipo CCM ing'oke madarakani!

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,241
92,234
Wakuu leo sina maneno mengi nimekuja kwa style ya habari picha, CCM ilishachokwa siku nyingi tu lakini hata hizo kula chache wanazopigiwaga wanapigiwa na watu frustrated kama huyu mama hapa. Hii picha nimeipata kwenye wall ya Nape Nnauye bila aibu haoni kama hii ni dhiaka kwa huyu mama fukara.

562644_376773555677397_100000342668655_1270263_1866941268_n.jpg


========
DEC 2013:
CCM kufa ni lazima ila inaweza kuchelewa kufa lakini kifo, kiko pale pale. Nyerere mwaka 1995 aliwaambia kamati kuu ya C.C.M kwamba watanzania wanahitaji mabadiliko na wasipo yapata C.C.M watayatafuta sehemu nyingine.Mabadiliko yameanza Tanzania na huwezi kuyazuia.

Watanzania watayatafuta mabadiliko popote hata kama itakuwa kwa shari. Ni kwa nini nasema C.C.M haiwezi kupona kwanza kabisa kizazi hiki cha miaka ya 1990 ni kizazi ambacho kinafuatilia taarifa na wanajua kuhoji sio kama wale waliokuwa wanafundishwa zidumu fikra za Mwenyekiti.

Pia hiki kizazi huwezi ukawaambia C.C.M imekulea maana wamekuwa wauona mfumo wa vyama vingi kwa hiyo wabunge wa C.C.M wanavyosinzia,wanavyozomea,wanavyo shabikia ujinga vijana wanaona kwa hiyo C.CM kufa ni lazima.

Pili katika kizazi hiki ambacho wanaona mafisadi,wauaji wabakaji na wauza unga wanatamba serikalini na C.C.M imewaacha watambe C.C.M haiwezi kupona.

Mtu kama Kamuhanda ameshuhudia polisi wakimuua Mwangosi halafu kesho yake akapandishwa cheo C.C.M haiwezi kupona.Cha muhimu muandae majeneza yenu.

Tatu katika kizazi ambacho babu zao walioitumkia nchi kwa uaminifu wanapigwa mabomu na maji ya pilipili kisa wazee walidai haki zao. Wazee wanalalamika mpaka wanavua nguo barabarani hakika C.C.M haiwezi kuikwepa hiyo laana fuatilia sakata la wazee wa Afrika Mashariki Tatizo la ajira haliwezi likawaacha salama.

Mtwambie hawa watu wanaomaliza vyuo mnawapeleka wapi?.Mmewasaidia namna gani?.Ofisini mnaweka vigezo eti mtu awe na uzoefu wa miaka mitano.

Huo uzoefu wanaupata wapi?Na sasa hivi mmeanzisha propaganda eti wajiajiri Je mmewapatia mtaji wa kujiajiri?.Hawa siku moja watajitoa mhanga ili kumuondoa mkoloni C.C.M. Katika kizazi ambacho kinaona C.C.M mumeua reli yetu ambayo ilikuwa msaada kwa wananchi wa chini mmeiua ili mabasi na malori yenu yafanye kazi.

Hakika yake ipo siku mtalia na kusaga meno. Katika kizazi ambacho mnasema mmeboresha elimu mwanafunzi anasoma masomo ya Sayansi na anamaliza kidato cha nne hajawahi kuiona ''Test tube''.

Huyu hatawaacha lazima C.C.M mtambe. Mnadai mmeboresha huduma za Afya mbona nyie kucheki afya mnaenda Afrika ya Kusini, India, Uingereza na Marekani.Piteni hospitalini muone mgonjwa mmoja anamlalia mwingine. Mara unaambiwa hospitali hazina dawa .

Ila nawapongeza maana wakati wa msiba mnaonyesha huruma lakini hiyo haitawasaidia. Mama Ntilie mnawakimbiza usiku na mchana machinga hawana raha na maisha yao wakati wa uchaguzi mtawaambia nini? Hakika yake kifo cha C.C.M ni lazima Hivi hii kilimo kwanza mmemsaidiaje mkulima?mbona wakulima wa pamba,korosho,kahawa, kila siku wanalia mbona kuna sehemu nyingine Tanzania bado kuna tatizo la chakula tukiuliza mnatuambia tulime kilimo cha kisasa.

Je hicho kilimo mmetufundisha? Hakika siku ikifika mtawaambia nini wakulima? Zamani walimu walikuwa wapiga kampeni wenu siku hizi mmewageuka . Mishahara yao midogo madai yao hawalipwi nasikia wanapigwa hadi viboko .

Je mna uhakika kama mmegeukwa na walimu ambao wamesambaa nchi nzima mtapona? Jiandae kwa ajili ya kifo cha ukweli.

Haiwezekani ndani ya nchi ya Kidemokrasia kama Tanzania watu wanapigwa mabomu,watu wanang'olewa kucha,watu wanamwagiwa tindikali, halafu Waziri Mkuu mwenye akili timamu anasema watu wapigwe tu kisa yeye kachoka.Na tumesikia juzi Mawaziri wamejiudhuru yeye kaendelea kuwa Waziri Mkuu. Hakika yake kwa sababu mliruhusu watu kupiga na kuua.

Siku moja mtapigwa nyie maana apandacho mtu ndicho avunacho. Wanafunzi hawa wote wanaopata daraja 0 hawa wote ni zao lenu na lazima siku moja ndio watasimama na kuwapiga chini.

Hakika yake siku hiyo hamtaamini lakini ndio itakuwa imetokea. Wakati wa Mwalimu Nyerere tulikuwa na viwanda vya nguo,viatu hadi redio siku hizi mmeua vyote.Ajira ndio hivyo zimeondoka kazi yenu ni kubinafsisha kila kitu mwisho mtabinafsisha hata wake zetu hakika yake C.C.M haitapona.

Suluhisho ni C.C.M kuwaomba msamaha watanzania na kuamua kugeuka. Msipofanya hivyo jiandae kuondoka kwa kilio na kusaga meno.

Imeandikwa na MCHUNGUZI .J. NAMALA 0776655066
 
mkuu usiogope kwa hizo propaganda!mwambie nape atuwekee picha ya kina mama wa soko la tengeru kama anaweza.
Huyo mama kavuta elfu kumi yake na jumamosi anawaelekeza kibla ccm.
KULA KWA CCM KURA KWA CDM
 
huwezi kuuza kibanda halafu ukakaa nyumba nzuri hivyo!
Yaani huyu mama hauzi karoti,matango,karoti,machungwa,maparachichi,vitunguu au chumvi?nape acha kujidanganya wewe!
 
sio lazima wafe, wafia chama wataendelea kuwepo hata kama chama chao kinanuka harufu ya uvundo wa ufisadi.
 
Ufukara wake ni nini huyo mama? anauza nyanya na viazi huku ana mzinga wa nyumba inameremeta.

Sasa hapo ni ufukara huo? Amma kweli huna maana hata kidogo.
 
wanajua jinsi wanavodanganya watanzania
inafaa wakifa wazikiwe wakiangalia chini na sio juu
 
hakuna anachouza hapo,hata kudanganya neshindwa,shame on u migamba
 
Mama mjasiria mali nimemkubali sana pia hicho sio kibanda, we kibanda kina geti la nondo na chuma?
Kawaue wazazi wako kwanza tuone kama CCM itaondoka madarakani.
Hii contradiction!!! Mara vijana bado kwanza mara wazee wafe!
 
Ukiangalia kwa makini huyu mama kapose kwaajili ya picha halafu hata genge dogo haliwezi kuwa na nyanya chache namna hiyo halafu hadhi ya genge na nyumba haviendani nape hizi ni propaganda za miaka ya 1925
 
Nilipokuwa mdogo nakumbuka tukikamatwa mwizi tulikuwa tunampeleka kwenye ofisi ya CCM, tulikuwa na imani kubwa na jinsi walivyokuwa wanwashughulikia wahalifu. Shule za chekechekea zilikuwa katika matawi ya CCM. Ikitokea shughuli kubwa tunatakutana katika ofisi za CCM bila kujali kama tunaipenda CCM au haitupendi, yenyewe ilitupenda.

Siku hizi ukienda kwenye ofisi ya CCM, inawezekana ukamkuta mtu ambaye wakati ule ndiye tuliyemkata na kumpeleka kwenye ofisi ya CCM, sitaki kusema yanayofanyika ndani ya CCM.

Siku hizi unasikia mafisadi kutoka ngazi ya taifa hadi ngazi ya nyumba 10, CCM ya Bridegia Moses Nnauye na CCM ya Nnauje Jr hazifanani hata kidogo.

Ukiona muuza genge, kizee au mkulkima kijijini anaisifu CCM, anakiukumba CCM ile akidhani bado inampenda. Ukiona msomi na kijana mwenye akili timamu anaiunga mkono CCM, 1. anatafuta maslahi ya kisiasa au ananufaika na status quo. 2 Ana matatizo ya akili au hajui CCM inafanya nini kwa Tanzania.
 
huwezi kuuza kibanda halafu ukakaa nyumba nzuri hivyo!
Yaani huyu mama hauzi karoti,matango,karoti,machungwa,maparachichi,vitunguu au chumvi?nape acha kujidanganya wewe!

Na ww kuwa muelewa sio kuwa huyo mama io nyumba ni yake io nyumba inavyoonekana ni vibanda vya vibiashara ambavyo zitakuwa zinamilikwa na ccm lakini kwa vile wanataka kura kwasasa wako rangi upange biashara yako hata pale getini ikulu ilimradi uwape kula baada ya hapo unafukuzwa kama mbwa.
 
Wakuu leo sina maneno mengi nimekuja kwa style ya habari picha, CCM ilishachokwa siku nyingi tu lakini hata hizo kula chache wanazopigiwaga wanapigiwa na watu frustrated kama huyu mama hapa. Hii picha nimeipata kwenye wall ya Nape Nnauye bila aibu haoni kama hii ni dhiaka kwa huyu mama fukara.

562644_376773555677397_100000342668655_1270263_1866941268_n.jpg

Kila siku nasisitiza kuwa Tanzania hatajatambua maskini ni wapi?
 
Jf ni nouma! Had vigogo na vipisi wanachungulia!?.Na tunawaomba wataarifiane huko wajisajiri humu wapate dawa yao maana hakuna wanachokifanya.Nnauye jr zamani ndo ilikuwa danganya toto bin changa la macho!,cku hizi ni pipoz pawa!Kizazi hki hakidanganyiki kwa ccm maana ugumu wa maisha wanaushuhudia live ambao the root cause ni wewe na ccm yako.Kizaz hki kinahitaji changes via movement for change yaan m4c.Ccm mtaji wenu umeshafilisika na watu wameamka na 2015 ni bye bye Nnauye.
 
Kuna siku nilijiliza hivi leo ikatokea tunaingia vitani.... tuseme na jirani yetu uganga.... kuna watu watajitolekwa hari na mali kuikomboa nchii kama 1978? nape usijibu maana wakati wa vita hukuwepo!
 
Back
Top Bottom