Ni kweli wanataka kuwajua hawa?Donge nono hiloo

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
2008-03-10 18:22:02
Na Mwandishi Wetu, Jijini

Wakati timu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kuchunguza upotevu wa mabilioni ya pesa za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje, EPA, ikiendelea kupigana kiume kuchunguza zali hilo zito, taasisi moja nyeti nchini, imetangaza donge nono kwa mwananchi yeyote atakayetoa taarifa zitakazoiwezesha kunyaka mafisadi.

Tangazo hilo limekuja huku kukiwa na mwamko wa hali ya juu wa wananchi kuwasakama watu wanaoendesha vitendo vya kifisadi na kujinufaisha kwa kutumia raslimali za umma.

Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA, ndiyo taasisi iliyojitoa kimasomaso kuutangazia umma kuwa iko tayari kutoa kitita cha fedha kwa mtu yeyote atakayefanikisha kufichua fisadi ndani ya mamlaka hiyo.
Uamuzi huo wa kumzawadia mtu atakayefichua ufisadi, imetangazwa na Kamishna wa Forodha nchini, Bw. George Lauwo.

Bw. Lauwo amekaririwa akisema kuwa TRA itamlinda mtoa taarifa na kumpatia zawadi ya pesa kwa kujitolea kwake kufichua ufisadi ndani ya mamlaka hiyo nyeti kwa uchumi wa nchi.

``Tunawaomba wananchi waendelee kutupatia taarifa za ufisadi ndani ya TRA kwa kutumia mameneja wetu au hata makao makuu, watoa siri watalindwa na pia watalipwa fedha,`` Bw. Lauwo amekaririwa akisema.
Bw. Lauwo ametoa kauli hiyo wakati akizungumzia maofisa watatu wa TRA ambao wamesimamishwa kazi mkoani Kilimanjaro, wakituhumiwa kufanya vitendo hivyo vya kifisadi.

Maofisa hao wamesimamishwa sanjari na kufutwa kwa kampuni moja ya uhakiki, uingizaji na utoaji wa bidhaa ndani na nje ya nchi kwa tuhuma za kuingiza mzigo wenye thamani ya shilingi milioni 80, lakini wakaonyesha kwenye vitabu vyao kuwa ulikuwa na thamani ya shilingi milioni 19.

Mzigo huo ambao unadaiwa ulitokea nchi jirani ya Kenya, uliingizwa nchini kupitia mpaka Tarakea Desemba 4, mwaka jana.

Bw. Lauwo amewaomba wananchi kutoa taarifa zozote walizonazo ambazo zitasaidia kutokomeza kabisa vitendo hivyo vya ufisadi ndani ya mamlaka hiyo nyeti, yenye jukumu la kukusanya kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Sakata la ufisadi liliibuliwa mwaka jana na kambi ya upinzani ambayo ilidai kuwa kulikuwa na ubadhirifu mkubwa ndani ya Benki Kuu ya Tanzania, BoT.

SOURCE: Alasiri
 
Lauwo naye keshaanza kuwatania watz!!

Ndiyo maana nimeuliza kwamba wana nia njema ama watu wanataka kutuo ondoa kwenye hoja ? Ina maana mimi mtu wa Kijichi sijawahi kuingia hata Long room naweza kuwa na clue ya nini kinafanyika kwenye ma file ya TRA ?
 
Back
Top Bottom