Ni kweli... Uwekezaji wa namna hii, hautatusaidia.

Mwanakili90

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,568
245
Jaribio la januari 5, 2012, la kutaka
kuiteka dhahabu iliyokuwa
inasindikizwa kutoka kwenye mgodi wa dhahabu wa Geita
ikipelekwa kwenye uwanja
mdogo wa ndege kwa ajili ya
kusafirishwa nje ya nchi.

Mwanzoni ilielezwa kwamba
dhahabu iliyokumbwa na
msukosuko huo ilikuwa na
uzito wa tani moja (kilo elfu
moja), kabla ya Wakala wa
Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) kuingilia kati na kutoa
ufafanuzi kwamba dhahabu
hiyo ilikuwa na uzito wa nusu
tani, yaani kilo 569.672.

Wakala hao wakazidi kueleza
kwamba dhahabu hiyo
ilikuwa na thamani ya dola za
Marekani milioni 26.16 sawa
na shilingi za Kitanzania bilioni
43.5.

Wakala hao wakaongeza kwamba kati ya hizo shilingi
bilioni 43.5, Tanzania
inaambulia shilingi bilioni 1.18
tu kama mrabaha (loyalty).

Baada ya ufafanuzi huo wa
TMAA ndipo maswali
yanapojitokeza. Swali la
kwanza ni kwamba jaribio
hilo la kutaka kuteka dhahabu
lilikuwa limelenga kupora au kuzuia uporaji?

Source:TANZANIA DAIMA.
 
Back
Top Bottom