Ni kweli upo nje unabeba maboksi?

mbongopopo

JF-Expert Member
Jan 24, 2008
1,611
759
Unafanya kazi gani? Kweli unabeba maboxi?

Ningependa kuona unaniambia kazi gani unafanya huko nje ya nchi.mfano kama wewe ni chef. Utaandika MIE CHEF

Basi tu maaana wabeba maboxi bado kichwani nafikiria mnabeba kweli wengine na elimu zenu

Natanguliza ili wanaoogopa ulaya wasidhani ni hali ngumu maisha wakitaka amia huko.

Najiwahi - mie nilisoma na kurudi tz.
 
Hii inaonyesha uwezo wako wa kufikiri ulivyo mdogo..hii ndiyo inawafanya watanzania hasa vijana kuwategemezi na kuomba omba(kupiga mizinga)nchi za watu hawachagui kazi na wala kazi ya mwenzio haikusaidii chochote..unafikiri mtu akiwa CEO inakusaidia nini wewe?muhimu nikuwa angalia maisha yako binafsi na farmilia yako.Imagine mtanzania yuko nchi fulani anabeba mabox anatangeneza dollar4,500 kwa mwezi..akirudi bongo ataipata hiyo pesa compuni gani..

Napenda kuwatia moyo watanzania wenzangu walioko nje akitafuta cash kwa nguvu zao zote wasikate tamaa mradi unapata chochote cha kuwakumbuka Ndugu zako bongo basi fanya kazi kwa bidii hajarishi hiko katika mazingira gani ya kazi,siku ukisikia kuchoka basi unaweza kurudi nyumbani na tutakupokea na mikono miwili..
 
Endeleeni kubeba maboksi, kuwa mayaya wa watoto, kusafisha mazingira na kufanya usafi na kupanga bidhaa katika super market, na wale mlioko south africa (maana nako ni ulaya) endeleeni na ile biashara yenu, hii yote ni kujipatia kijungu jiko na hata kutukumbuka siye dugu wa bongo 2naoishi chini ya dola.
Nyumbani ni nyumbani lakini hali inatisha sana, endeleeni kukomaa.
 
Unafanya kazi gani? Kweli unabeba maboxi?Ningependa kuona unaniambia kazi gani unafanya huko nje ya nchi.mfano kama wewe ni chef. Utaandika MIE CHEFBasi tu maaana wabeba maboxi bado kichwani nafikiria mnabeba kweli wengine na elimu zenuNatanguliza ili wanaoogopa ulaya wasidhani ni hali ngumu maisha wakitaka amia huko. Najiwahi - mie nilisoma na kurudi tz.
kazi ni kazi mkuu...
 
Jamani bongo hari ngumu usipime wala usiambiwe na mtu..kama huamini uliza mabalozi wangapi au unawajua wewe wakitanzania wanapomaliza mda wako wakiwa mabalozi au kustaff wanarudi bongo?
 
Jamani bongo hari ngumu usipime wala usiambiwe na mtu..kama huamini uliza mabalozi wangapi au unawajua wewe wakitanzania wanapomaliza mda wako wakiwa mabalozi au kustaff wanarudi bongo?
maboksi yapi hayo wanayoyabeba ya mizigo au ni modern swahili
 
akili za watu na maisha ya kila mtu binafsi ni ya ajabu sana umesoma,umejielewa na unajua lengo lako kwanini unganganiye kuishi ulaya kwa kubeba mabox tena hadi jina lako unachange kisa ulaya,wanao sema bongo hamna siyo kweli 25 percentage,kuna new opportunity kibao kwa mtafutaji wa kweli wa maisha,rudini nyumbani au ufe na stress ulaya.
 
Hii inaonyesha uwezo wako wa kufikiri ulivyo mdogo..hii ndiyo inawafanya watanzania hasa vijana kuwategemezi na kuomba omba(kupiga mizinga)nchi za watu hawachagui kazi na wala kazi ya mwenzio haikusaidii chochote..unafikiri mtu akiwa CEO inakusaidia nini wewe?muhimu nikuwa angalia maisha yako binafsi na farmilia yako.Imagine mtanzania yuko nchi fulani anabeba mabox anatangeneza dollar4,500 kwa mwezi..akirudi bongo ataipata hiyo pesa compuni gani..Napenda kuwatia moyo watanzania wenzangu walioko nje akitafuta cash kwa nguvu zao zote wasikate tamaa mradi unapata chochote cha kuwakumbuka Ndugu zako bongo basi fanya kazi kwa bidii hajarishi hiko katika mazingira gani ya kazi,siku ukisikia kuchoka basi unaweza kurudi nyumbani na tutakupokea na mikono miwili..
wewe unaishi karne gani? Bado unachagua kazi? Mh umenishangaza sana mkuu!
 
Halafu hawa watu wengi walioko ughaibuni kama hawakwenda kwa pesa za ufisadi wa baba zao basi ni wazamiaji! Kwa maana hakuna mtoto wa mkulima kule Tanganyika Masagati anayewaza ku-afford kwenda ulaya! Halafu wanajifanya wana uchungu na nchi hii! Hawa nao ni sehemu ya kansa ya TZ!
 
Halafu hawa watu wengi walioko ughaibuni kama hawakwenda kwa pesa za ufisadi wa baba zao basi ni wazamiaji! Kwa maana hakuna mtoto wa mkulima kule Tanganyika Masagati anayewaza ku-afford kwenda ulaya! Halafu wanajifanya wana uchungu na nchi hii! Hawa nao ni sehemu ya kansa ya TZ!
Kwahiyo hao wazamiaji nao ni kina mambo safi!?
 
Kwanini mtu anafanya kazi? Ukishajua hilo basi hutajihangaisha kuulizia kazi za watu.

Ukishajua mtu anabeba au kushusha box, kuendesha taxi, kusafisha barabara au hata kutunza wazee so what? Utawapa ajira mbadala unazodhania zinafaa?
 
afu mkiona mtu katoka nje mnamganda kama ruba, huku unadharau kazi zake. kazi yako haimsaidii mtu ndugu,acha kila mtu akomae kivyake.hapa bongo kuna siku nili-serv-iwa juice na dr wa wanyama kwenye aeroplane!tukafurahi kuonana na kufurahia maendeleo!
 
Kwanini mtu anafanya kazi? Ukishajua hilo basi hutajihangaisha kuulizia kazi za watu.

Ukishajua mtu anabeba au kushusha box, kuendesha taxi, kusafisha barabara au hata kutunza wazee so what? Utawapa ajira mbadala unazodhania zinafaa?


bora kubeba mabox kuliko maisha yenu bongo
mimi sio proffesional lakini naondoka na dollar 2000 kwa mwezi
napata hela nyingi kwa mwezi kuliko mbunge wako
 
Back
Top Bottom