Ni kweli SURUPWETE la MKAPA limempwaya KIKWETE?

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Wapo watu, katika kada mbalimbali enzi za mwalimu Nyerere waliwahi kusema kwa ujasiri kabisa bila woga kuwa. Maisha katika awamu hiyo yalikuwa mabaya afadhali yale ya enzi za ukoloni. Maneno yaliyomtia sana uchungu hayati Babu yule. Leo hii wapo wanaotumia usemi huohuo kwa kusema kuwa, maisha katika awamu hii ni afadhali enzi ya utawala wa MKAPA..

Kigezo kikubwa ikiwa ni kupanda kwa gharama za maisha kutokana na mfumuko wa bei usiokoma. Hii inaashiria nini? Je, Suti aliyoiacha Mkapa imeku oversize kwa JK Kiasi cha kushindwa kuivaa?

Amakweli ikulu si mchezo wa kitoto manaake hata vibibi kizee navyo vimezidiwa kiasi cha kupaza sauti kudai kuwa vimechoka! Watoto nao siku hizi wapo kwenye maandamano nao hawaogopi mabomu ya machozi. Kila mtu anasema kachoka, kila kikundi cha watu story ni tumechoka, kweli hali ni tata.
 
Back
Top Bottom