Ni Kweli Simu Za Kichina 'Zinazimwa'?

Elisha Ray

JF-Expert Member
Mar 19, 2012
323
94
Habari zenu wakuu? Kuna taarifa nimepata kuwa simu zile (za bei rahisi) toka China zimeanza kuzimwa (kupoteza network) hivi ni kweli taarifa hizi? Maana kuna baadhi ya watu walio na hizo simu leo hii hazifanyi kazi. Najua serikali ilisema haina mpango wa 'kuzizima' kama Kenya walivyofanya au ndo inafanya kimya kimya? Wenye info watujuze maana hii itakuwa 'crisis.'
 
Bado kwanza mafisadi hawajapewa 10% zao kusaini huo mkataba, wakipewa mtajulishwa na mtapangiwa tarehe ya mwisho kuzitumia hizo mchina zenu
 
Natamani siku wakizipiga marufuku jamani tuungane wote tuzirudishe pale ubalozi wa china au tuunde jumuia ili tuzitoe msaada ata congo wandugu!
 
mi nataka zizimwe,ili atakayemiliki kweli awe na uwezo kweli.Cyo kila mtu,mtoto,vijana,wazeze,wajinga,wapumbavu,wanaf.ngendere,mbwa,sungura.n.k.wanamiliki CMU.WHAT IS THAT?imekuwa familia ya Kambale kila mtu ana ndevu.TCRA zima haraka na orijino ianzie laki 2 na kupanda.Hatutaki cmu za buku ten.
 
sio cm za kichina isipolkua ni cm feki...watu wamekariri mchina ni mtu wa magumashi bt anauza mpka ulaya'''so cm feki sio za kichina
 
Bado! japo kuna jamaa wanadai sim zao hazifanyi kazi.
Zikizima serikali iwajibike kulipa fidia maana kazi ya TBS ni nin?
 
Nchi hii hatuwezi kufanya maamuzi magumu yenye manufaa kwa taifa na raia wake,kwa hiyo bidhaa feki itaendelea kutawala soko la bibi
 
mi nataka zizimwe,ili atakayemiliki kweli awe na uwezo kweli.Cyo kila mtu,mtoto,vijana,wazeze,wajinga,wapumbavu,wanaf.ngendere,mbwa,sungura.n.k.wanamiliki CMU.WHAT IS THAT?imekuwa familia ya Kambale kila mtu ana ndevu.TCRA zima haraka na orijino ianzie laki 2 na kupanda.Hatutaki cmu za buku ten.

haswa!
 
Hata zikizimwa Tanzania hatuna hasara kabisa, kwanza kabisa nataka wazizime leo kwani nani aliwaambia wanunue simu feki, tena tanzania kwa ujumla hakuna haja ya kuwatangazia kuzima kwa kuwa anakuna anayewaambia wanunue simu na vitu feki. Rahisi gharama. Wewe unanua simu imeandikwa sumusungu, nokilia, sono eliksong unanunua tu kama sio ujinga ni ujima.
 
mi nataka zizimwe,ili atakayemiliki kweli awe na uwezo kweli.Cyo kila mtu,mtoto,vijana,wazeze,wajinga,wapumbavu,wanaf.ngendere,mbwa,sungura.n.k.wanamiliki CMU.WHAT IS THAT?imekuwa familia ya Kambale kila mtu ana ndevu.TCRA zima haraka na orijino ianzie laki 2 na kupanda.Hatutaki cmu za buku ten.
Kaka kuku anakula kulingana na mdomo wake! Sisi wengine vipato vyetu ni vidogo. Ndiyo maana vyakula tunanunua vya mafungu, sukari robo au kijiko, mkaa wa mafungu na kadhalika. Kama unataka anayemiliki simu awe na uwezo, wengine watakuambia tupige marufuku magari yaliyotumika kutoka Dhubai au Japan, yaletwe ma Hammer au VX 9! Au usafiri uwe wa ndege tu hapa nchini, je, itawezekana?
 
Back
Top Bottom