Ni kweli, regia e. Mtema hatunaye kimwili tena! Sasa tufanye nini?

Mpui Lyazumbi

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
1,856
371
Wana JF wenzangu na watanzania wote kwa ujumla, Regia amefariki! Mwanga huu umepotea haraka sana. Kwangu mimi tangu nilipopata habari hizi kupitia mtandao huu nimejitahidi kulazimisha kuwa ni uongo. Hapana. Mbunge wetu mahili katangulia mbele za haki. Nasoma mabandiko mengi sana humu jamvini, mengi ya maoni nashindwa kuendelea kuyasoma - inaniuma. Kijana hodari na mwenye uthubutu kaitika mbele ya Muumba. Nimefuatilia habari zake tangu ajali iliporipotiwa, tabata, karimjee na leo ifakara, kwa ujumla ni huzuni, simanzi, masikitiko na sura za ukweli kwamba Regia E. Mtema lilikuwa ni tumaini la watanzania wanyonge walioweka matumaini yao kwake na kwa moyo wa dhati kabisa.
Sasa leo, na hata kama hatuamini, hatutaki, tunamuombea, tunasikitika... Mapenzi ya Mungu yametimizwa! Ametumia utu wake na maisha yake kwa wapenda haki wote nchini. Na alipokwisha kuyafanya hayo kaitwa rasmi.

Sasa tufanye nini?????????

Naikumbuka misiba mbalimbali iliyopata kutukumba: - Edward Moringe, Julius Nyerere, Amina Chifupa, Bibi Titi Mohamed, Mtwa Mkwawa, Chifu Milambo ongeza na wengine wa kariba hiyo. Hivi tunafanya nini kwa mawazo, matendo, maneno, tabia... katika kuwaenzi mashujaa wetu? Kutaja majina yao kwenye mabweni? Viwanja? Mashule? n.k? Hebu wana jamvi nisaidieni...

Tufanye nini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom