Ni kweli Rais anapotoshwa?

Na wewe huna point, umekoroga maneno tu. Kajipange upya. Hii ni rubbish.
Nimehitimu shule ya kata, ambayo haikuwa na walimu na vitabu no madawati hiyo nilichoandika ni kwa uelewa dogo nilionao. Naamini kama shule yangu ingepewa uwekezaji mzuri ktk walimu, vitabu n.k badala ya kujitajirisha nyie wachache Kwa jasho wetu sote leo ningeandika point na si kukoroga.
 
Rais anapotoshwa na propaganda za tbc na habari leo, jana na leo wameripoti kuwa huduma Mhimbili zimerudi ktk hali ya kawaida lakin ukweli ni kuwa hata madaktari bingwa wameamua kugoma.
rais hapotoshwi ndivyo anavyotaka na anajua fika...tunaopotoshwa ni cc hasa raia wajinga tuliompigia kura kwani wanasema wajinga ndio waliwao
 
Rais anapotoshwa na propaganda za tbc na habari leo, jana na leo wameripoti kuwa huduma Mhimbili zimerudi ktk hali ya kawaida lakin ukweli ni kuwa hata madaktari bingwa wameamua kugoma.

Sasa afuatiie mwenyewe aende kutembea wodini peke yake, maana ikiwe ni presidential entourage kamwe hatakuwa na nafasi ya kudadisi/kufany uchunguzi at all costs!!!
 
Nimehitimu shule ya kata, ambayo haikuwa na walimu na vitabu no madawati hiyo nilichoandika ni kwa uelewa dogo nilionao. Naamini kama shule yangu ingepewa uwekezaji mzuri ktk walimu, vitabu n.k badala ya kujitajirisha nyie wachache Kwa jasho wetu sote leo ningeandika point na si kukoroga.

Usilaumu shule, na akili pia inachangia
 
raisi hapotmshwi udhaifu wake mwenyewe.mbana awamu zilizopita kulikuwa hakuna matukio ya kupotoshwa au kudanganywa kama yalikuwepo ni macheche sana.naamini ni udhaifu wake na uwezo wake mdogo
 
Rais hapotoshwi maana sakata la madaktari alikaa nao na anajua wanataka nini, sasa wa kumpotosha yuko wapi?
 
rais hapotoshwi ndivyo anavyotaka na anajua fika...tunaopotoshwa ni cc hasa raia wajinga tuliompigia kura kwani wanasema wajinga ndio waliwao
Exactly..anajua ukweli wote, tatizo hawezi kufanya maamuzi magumu.
Njia pekee iliyobaki ni propaganda za kudanganya wananchi kupitia media uchwara, wapambe na wanasiasa waongo.
Hatudanganyiki!!
 
hivi kulikuwa na madai mangapi na alijibu mangapi kabla hatujasema kapotoshwa?
afadhali maana nahisi kuna watu hata ile hotuba hawakuisikiliza wala mgomo hawaufuatilii wanachangia tuu, madaktari wapo kisiasa na kimaslahi zaidi na hawana uzalendo wa kweli kulipa fadhila za kodi za watanzania walio wasomesha
 
Kazi yake ni kudhurura na kupiga picha na wakina beckham na warembo tofauti duniani.

Kwa hilo na msifu sana,
 
Rais hapotoshwi maana sakata la madaktari alikaa nao na anajua wanataka nini, sasa wa kumpotosha yuko wapi?

sasa hata mimi hapa ndio napatwa na mashaka hapo. Ndio maana nikasema kwa nini hao wanaolalamikia kero zilizopo wanamtetea Rais? Madaktari hao hao walioongea na rais na kumweleza kinagaubaga matatizo yao leo hii tena wanasema kuwa rais anapotoshwa. I wonder!
 
Rais anapotoshwa sana,kwa mfano ukiangalia taarifa ya serikali kuhusu mgomo huu na kile rais alichokieleza kwenye hotuba yake ni vitu viwili kabisa visivyoshabiaana .Tatizo lake kubwa ni uvivu wa kutopenda kuhoji na kuchunguza.

nimependa comment yako lakini in summary ni kuwa HANA AKILI
 
Wenye akili walishajua tangu 2005 kuwa kikwete ni -at best- ni mswahili.

"They knew they were lying, and we knew they were lying"
Tundu Lissu (2012).

Yes we knew, but what did we do? Gaping! And of course we know they will lie again. Tujichunguze sana watanzania. Ni kwamba tunafananishwa na mbwa/paka ambaye anachezewa manyoya ya mgongoni na kutulia tuli.
 
Tukiangalia mara nyingi yale yanayoendelea hapa nchini na mwishowe kuleta mitafaruku, wanaolalamika wanasema 'Rais alishauriwa vibaya, Rais kada nganywa...' Ni kweli? Hivi suala la hali duni kwenye sekta ya afya mathalani, bado Rais anapotoshwa kwenye hilo? Kwani Rais huwa anasoma nini, anaongea na nani, anatembelea wapi hadi asikutane na uhalisia wa maisha ya mtanzania? Rais akipotoshwa kaamua mwenyewe. Aidha kaamua au hajui uhalisio, huo ni udhaifu.
Hakuna mtu anayepotoshwa. Rais hawezi kupotoshwa wakati yeye ndiye anayetoa maagizo ya mwisho isipokuwa sisi wenyewe ndio tunapotoshana kwa kutegemea tofauti..

Imenisikitisha sana kuwasoma madaktari wakisema Rais anapotoshwa wakati kasema wazi kilichotokea na kinachoendelea. Wao wajibu wamekubaliana na mapendekezo ya serikali au laa haya na kutumia jukwaa la siasa kujisafisha wakati wanadai haki zao haitasaidia kitu.

Tumekuwepo hapa tukifuatilia toka mgogo wa kwanza, mara hawataki kuonana na huyu ama yule isipokuwa waziri mkuu Pinda, haya wakaenda kunywa juice Ikulu na kuonana na rais, haya tukasikia majuzi rais kawaita tena wakagoma kwenda kuonana naye hadi wafanye mgomo wao, leo tena wanaomba wakutane na rais yaani usanii mtupu. Sasa iweje tena rais anapotoshwa ilihali ni wao ndio wana make calls ktk mgogoro mzima. Sisi wananchi ndio tunapotoshwa!
 
Hivi wewe Majebere I wish nikuone kwa macho.Hivi huko kwenye shule za kata kuna walimu wangapi? Kama hakuna hata library unategemea anaenda kujifunza wapi?Hakuna umeme,mtandano hakuna.
Ukiangalia kuna shule moja ambayo mwanafunzi wa kata amepata Div.2,hapo hana mwalimu angekuwa na mwalimu ingekuwaje?Usiangalie uwezo ulionao ukalinganisha na mzazi maskini kijijini ambaye hajui atakula nini lakini anahakikisha mtoto wake afike japo hiyo shule ya kata.
Jifunze kuheshimu point ya mtu.Kama kweli amesoma shule ya kata kwa point alizotoa tehn amekuzidi hata wewe uliyesoma mpaka hapo ulipofika.
 
Mkandara kama serikari inafikiri ma-Dr hawana utashi/akili ya kufanya maamuzi yao wenyewe hadi kuwapo na kundi/chama nyuma yao kinachowalazimisha kugoma kwa nini na wao wasifikiri kuwa ****** amepotoshwa?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom