Donyongijape
JF-Expert Member
- May 28, 2010
- 1,497
- 811
Nimesoma katika gazeti la Tanzania Daima na kukutana na hii kali ya mwaka, Eti Nape Hawajui Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Katibu wake, Dk. Willbrod Slaa katika duru za siasa nchini. Alikuwa akijubu tuhuma dhidi ya chama chake juu ya kile kilichodaiwa kuwepo kwa mipango ya kuwabambikizia kesi baadhi ya viongozi wakuu wa CHADEMA kwa lengo la kuwadhoofisha wao binafsi na chama kwa ujumla.Nape alisema hawezi kujibu madai yasiyokuwa na maana na pia hawajui hao wanaoitwa Mbowe na Slaa.
"Nimesahau kama wapo Dk. Slaa na Mbowe ndiyo unanikumbusha wewe," alisema na kuongeza kuwa viongozi wa CCM hawajakutana mahali popote kuzungumzia suala hilo na kueleza kuwa huo ni upuuzi usiokuwa na mashiko.
Nape alidai kuwa viongozi wa CCM hawana muda wa kuwafikiria CHADEMA, kwani si chama chenye maana kinachoweza kuwasumbua wala kuwapotezea muda.
"Uchaguzi umekwisha, hatuna muda wa kuwafikiria viongozi wa CHADEMA, kwanza si chama, sasa tunafikiria kutekeleza ilani ya chama chetu,'" alisema.
Alisema kuwa viongozi wa CHADEMA ndio wenye muda wa kuwafikiria viongozi wa CCM na kusema, "Wao ndiyo wanafikiria, ‘tumfanyeje Nape na JK'."
Majibu ya Nape yamekuja siku mbili tu baada ya kutoa matusi mazito katika mkutano wa hadhara uliofanyika jijini Mwanza.