Ni kweli Lema kawakimbia polisi Arusha?

Kwa haraka haraka wanaoanzisha thread mbovu mbovu na zisizo na mwelekeo hapa JF ni wachache sana, wakati mwingine inawabidi kujiandikisha na ID zingine ili waonekane wapo wengi lakini sivyo. Kwa kuwa nao ni watanzania, huwa nafurahi sana ninapowaona wakati mwingine wakizidiwa kiasi cha kuunga mkono hoja za msingi ama wakati mwingine kunyamaza kimya kiasi kwamba wanaona aibu kukosoa hoja fulani fulani za msingi. Nadhani hawa jamaa wapo kama sehemu ya changamoto pamoja na kutuelewesha kimsingi na hali halisi kwamba CCM hawajalala wanapambana, tusiwatukane maana wao ni sehemu yetu. Tuwape nafasi ya kutoa hoja zao za hovyo hovyo kwa mtindo huu ili na sisi tupate kujua wanafikiri nini. Tusiwe na hasira wanapotoa hoja za hovyo maana ukweli ni kwamba kuna mahala wanashindwa kutetea ikiwa jambo lenyewe ni uovu wa wazi kwahiyo wao hupinga kwa hoja za kuwatia hasira. Tukiwajibu kwa hasira tunakuwa tumeshindwa kwa kuanzia tu kwenye majibu yetu.Nyumbu wapo kwenye mzunguko kama sehemu ya chakula, huwezi kukasirika na kujiuliza ati kwanini nyumbu ni wajinga kiasi hicho. Ni swala la kuelewa kwamba nyumbu waliumbwa hivyo na wataendelea kuwa hivyo, nyumbu wasipokuwa wajinga... Mamba na wanyama wengine wanaokula nyama hawatopata mlo wao wa kila siku.Sisemi wenzetu ni nyumbu, ila najaribu kusema kuna walioumbwa hivyo. Wanaona kila kitu kinachotendeka nchi hii na wanaelewa lakini wao kazi yao ni kutetea wale wasioweza kuja hapa. Tukae tukijua kwamba Msekwa, JK, Kinana, Nape na wengine wengi hawawezi kuja JF wakati wote. Hili jukwaa sasa linaelekea kushika kasi, ni lazima waweke watu humu kufanya kazi ambayo wao walipaswa kuifanya ya kukitetea Chama.
 
Si Lema wala Mwanachadema yeyote aliyekimbia polisi,hatuna utamaduni wa uoga wala wa kukimbia kimbia
Kilichotokea baada ya kutoka mahakamani wananchi walikokuwa wamefurika mahakamani waliondoka kurudi makwao,na Lema akiongozana na makamanda watembea kurudi ofisini kwake,ambapo walitawanyika,lakini katika hali isiyo ya kawaida zilikuja gari tatu za polisi zikiongozwa na OCD wa Arusha mjini na kuingia ofisini kwa Lema na kuanza kukamata vijana na wananchi waliokuja kumwona mbunge wao,katika kamata kamata hiyo polisi walikuwa na picha za makamanda wa CHADEMA ambao walikamatwa na kupigwa kabla ya kufikishwa kituoni ambapo walifunguliwa mashtaka ya kuandamana na kufanya mkutano bila kibali,wakati hayo yanatokea Mh Lema hakuwepo ofisini kwake
Baadae viongozi wa chama waliwawekea dhamana wote waliokamatwa na kutakiwa kufika kituoni hapo kesho jumatatu
 
Back
Top Bottom