Ni kweli? Kabwe afurahia sitofahamu CCM

Selous

JF-Expert Member
Jan 13, 2008
1,325
144
Na Said Mwishehe, Majira

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Bw. Zitto Kabwe amesema anafurahishwa na hali ya mvurugano inayoendelea ndani ya Chama chaMapinduzi (CCM) na hasa kauli zinazotolewa NA Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Yusuph Makamba.

Kauli ya Bw. Kabwe imekuja siku moja tu baada ya Bw. Makamba kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema haogopi mtu yeyote ndani ya chama chake zaidi ya Mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Bw. Pius Msekewa.

Makamba alitoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa za baadhi ya wabunge wa CCM kutaka kujenga hoja ya kumng'oa kwenye wadhifa wake wa Katibu Mkuu wa chama hicho kwa madai kuwa amekuwa akikumbatia watu wasio na uwezo wa kukisaidia chama hicho.

Akizungumza na Majira jana Dar es Salaam, Bw. Kabwe alisema kwa hali halisi CCM ipo katika wakati mgumu na hata kauli za Bw. Makamba zinaashirisha wazi kuwa hali ni mbaya ndani lakini yeye anapenda kuona hali hiyo ikiendelea.

"Kitu ambacho kinaonekana hapa ni kwamba CCM sasa mambo ni magumu ndio maana hata viongozi wameanza kutupiana vijembe. Binafsi na CHADEMA kwa ujumla tunaomba hali hiyo iendelee na ikiwezekana mpasuko na mgawanyiko wa wanachama uwepo," alisema.

Alisema kwa bahati mbaya hata siku moja hawezi kuiombea mema CCM na hali inayojitokeza sasa ni dalili kwamba hali yake itafanikiwa na CCM kusambarika.

"Nilishatangaza hadharani kwamba CCM siipendi na nitafurahia kila aina ya jambo ambalo linaweza kusababisha mpasuko. Ndio maana ninasema kauli za Bw. Makamba ni bora zikaendelea kwani ndio mafanikio kwetu," alisema Bw. Kabwe na kuongeza kwamba ili demokrasia iweze kukua nchini lazima CCM isambaratike.

Wakati Bw. Kabwe akiomba hali hiyo iendelee ndani ya chama hicho, baadhi ya wabunge wa CCM waliozungumza na Majira kuhusu kauli za Bw. Makamba walisema inasikitisha kusikia kiongozi wao akitoa kauli za aina hiyo.

Walisema kwa hali ilivyo sasa wao wanaogopa kutoa maoni yao kuhusu kauli za Bw. Makamba na kusisitiza kuwa wanaamini chama chao kina maadili hivyo vipo vikao ambavyo vinaweza kutumika kumjadili.

Zitto,

Nakubaliana na wewe kuwa hata CCM wanapenda JF wakiwalaumu CHADEMA? Kimsingi mtanzania yeyote mwana upinzani anasubiri chama hiki kife ili watu wangine wenye dira tofauti waingie.

Mimi ni mshabiki wa CHADEMA, Operations Sangara inaendeleaje? i am serious sipo Tanzania.

Naamini hivi CCM ina wasomi wengi na incident hii kama wanabusara wanaifanyia investigation to correct the direct cause and indirect causes. Sasa kauli hii kama umeitoa means umewasaidia. Hope mmejidhatiti badala ya kuonekana kama mnawasaidia kugrade tatizo from insignificant to significant.
 
Back
Top Bottom