Ni kweli Hazina hakuna Pesa?

Mkulu PM,

Heshima mbele, serikali yetu ina matatizo mengi sana, na mazuri mengi pia, lakini hili la kukopa ni la kawaida hata US sasa hivi wanakopa ku-facilitate vita vya Iraq, deficit kwa kwenye hazina ya nchi yetu sio kitu cha ajabu,

so far ni rais mmoja tu duniani aliyeweza kulishinda hilo naye ni Clinton, ambaye akiwa rais wa US, alii-balance kwanza budget, na wakati anaondoka aliacha surplus, hakuna rais mwingine tena aliyeliweza hilo,

Hii topic inapaswa kuwa about deficit kwenye budget yetu, na kama tunavyoelewa kikao cha bajeti, nia na madhumuni yake huwa ni ku-project, yaani kukadiria meaning kwamba huwa wanatabiri, wote tunajua maana ya neno utabiri wa makisio ya matumizi ya pesa kwa serikali,

sasa check this out, utabiri wa hali ya hewa tu unatushinda je tutaweza wa bajeti?
 
FM-ES
mkubwa heshima yako kaka
unajua hii hali inachangiwa na ujuha wa baadhi ya viongozi kuiingiza serikali ktk ukata kutokana na tabia zao za kutojali. mfano niliuliza zile safari za mawaziri mikoani zilikuwa covered na bajet ipi?

Ok nakubali kwamba hazina kukauka sio kwamba kuna zero moni, lakini naomba nieleweshwe katika hili... serikali imeoverspend ktk shughuli zipi? na ulazima au udharura wa shughuli hizo ni upi? kama imeoverspend kwa normal activities basi nashauri walioplan bajeti na kuipeleka bungeni wafutwe kazi kwani wameidanganya serikali kiasi kwamba makisio yalikuwa madogo kuliko uhalisia.

Kama ni matumizi hasi, hatuna budi kuisuta serikali na kuiwajibisha ikibidi
 
mfano niliuliza zile safari za mawaziri mikoani zilikuwa covered na bajet ipi?


Mkulu Msanii,

Heshima mbele, this is very strong point ambayo wabunge wa upinzani wanapaswa kuwajia juu serikali, hasa waziri kivuli wa Finance, that was a waste of our taxes,

This one niko na wewe, mkulu!
 
Today is sunday and i must go holiday ili nirudi jijini kesho.
lakini hili suala la overspend linalete uchuro sana hapa
watu wanaitetea serikali ikifanya madudu mpaka inakinaisha. nawashauri JF tuwe wawazi maana bila kuiambia serikali ukweli itajiendea hovyo mwisho itasambaratika.

Wabunge wa upinzani natumaini wataisoma hoja ya FM-ES ili kujenga hoja....
wikned njema wakulu
 
Hapa patamu sana na naungana na pande zote mbili bila kujua shilingi inayozungumzwa ni ipi hapa. Hakika mtoa mada kidogo kaacha uwanja wazi hivyo tunalonga kama vile tunavyofahamu.
Hazina haina hela inaweza kuwa kweli matumizi ya serikali yamezidi (budget) kiwango kilichokusudiwa kutumiwa. Na hii haina maana kwamba mfuko wetu wa kuingiza tumeulamba wote isipokuwa kinachozungumziwa hapa ni zile zilizotengwa kutumiwa ktk kipindi hicho.
Sasa ikiwa hapa Mkulu ana maana tunatumia fedha zaidi ya pato la serikali kiasi kwamba tunalamba kila kinachoingia mfukoni mbali na fedha zilizotengwa kwa matumizi na taarifa iliyopo leo hii hatuna reserve kabisa... well hapa tunazungumza kitu kingine kabisa.

Mfano mdogo wa kuiweka mada hii ktk sura inayoridhisha nitatumia mfano wetu wenyewe...
1. Mimi katika matumizi yangu ya mwezi hupanga dollar 2000 kwa mwezi lakini kutokana na kupanda kwa bei za vitu ikiwa ni pamoja na vyakula ama kupata wageni nyumbani imefikia natumia 3000 kwa mwezi. Hii haina maana sina kitu benki kwani hizo ziada ya 1000 imetoka wapi? pamoja na kwamba nimesema mfuko wangu wa matumizi umekauka.

2. Pia kuna uwezekano kuwa ktk kutumia hizo 3000 yaliyotokana na ongezeko la matumizi ktk idara zangu binafsi muhimu na za starehe, nimefilsi akiba yote benki na sasa kila pato langu linaloingia benki nalinyapua kulipia madeni (visa) na matumizi ya kila siku..Yaani maisha yangu yamekuwa yakienda cheque by cheque!..Hapa mjomba nongwa!

kwa hiyo, tunaomba zaidi tufahamishwe lipi ni lipi?
 
Mkulu PM,

Heshima mbele, serikali yetu ina matatizo mengi sana, na mazuri mengi pia, lakini hili la kukopa ni la kawaida hata US sasa hivi wanakopa ku-facilitate vita vya Iraq, deficit kwa kwenye hazina ya nchi yetu sio kitu cha ajabu,

so far ni rais mmoja tu duniani aliyeweza kulishinda hilo naye ni Clinton, ambaye akiwa rais wa US, alii-balance kwanza budget, na wakati anaondoka aliacha surplus,


JAMBO MKUU!!!

heshima mbele...lakini mkuu huyu CHINGA BOY WETU [NZEE NKAPA]..si alipokea nchi ikiwa na national reserve ya kutosha imports za mwezi mmoja Tu!!..na ameondoka ametuachia national reserve nzuri kuliko wakati wote nafikiri tangu 1974!! ameacha national reserve ya kutosha miezi kumi [almost 2trillon usd]...hilo hata kaka yetu muungwana kakiri !!..na utawala wake
kukopa mabenki kuligeuka historia!
sasa mpiganaji labda tu nisaidie hapa ..kwa nini kwa safari hii tuina burst budget!! ina maana kama ameanza kukopa mabenki ile pesa aliyoiacha mkapa geneva[2trillion$] kwenye akauti ya taifa imekauka!!?? tuna haki ya kujua...
mambo ya uendeshaji nchi nakiri ni magumu ailikuwa namsikiliza alhaji mzee mwinyi akielezea namna alivyoipokea nchi from mwalimu anasema hakukuta pesa baada ya kukaushwa na vita,njaa.na vikwazo....anasema pesas pekee aliyoitumia kuanzia madaraka yake waliitafuta kwa ushirikiano na mwalimu baada ya kumuachia nchi nazo ni dola milioni 100$ kutoka kwa rajiv ghandi india na mugabe dola milioni 100$ ...wote hao ndio walioingiza pesa za kwanza za kuanzia awamu ya 2...baada ya kupigiwa simu binafsi na mwalimu ..hali ilkuwa mbaya....
nasema haya ili muone haja ya rais kutoichezea national reserve zaidi apigane kuongeza ..hadi ifike siku tuwe na reseve ya hata miaka kumi..
nchi isiyo na national reserve ni sawa na nchi bila jeshi..kwani adui akijua huna nafaka[reserve] anaweza kukuvamia muda wowote akijua akikuendesha mchaka mchaka hata kwa mwezi mmoja utakuwa unabanwa na njaa..na utasalimui amri tu..ukiwa huna akiba usishangae hata vinchi vidogo vitaaza kukuletea kiburi..nafikiri mnajua na mnaona namna congo inavyoletewa ubabe na vinchi vidogo..Hata enzi ya mfalme daudi waliweka nafaka kama akiba ili kujilinda na siku mbaya na maadui..
NATIONAL RESERVE IS OUR SECURITY
 
..naona kuna watu wamekuja kukemea wenzao!

..cha muhimu ni kuwa hoja inajadiliwa na kama mtu atatoa data ambazo sizo na ataambiwa!

..wote tunafahamu matumizi yamekuwa juu,wakati kanchi kenyewe masikini,ila nini kimesababisha ndio tunakijadili!sasa watu ni vyema wakawa huru kuchangia na sio wakichangia warushiwe madongo bila hoja!

..hoja hujibiwa kwa hoja!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom