Ni kweli CCM kuitawala CHADEMA ni akili ndogo kutawala akili kubwa!

Kaguta

JF-Expert Member
Jan 31, 2013
414
504
Jana nimemwanagalia muda wote Mh Pinda akifunga mjadala wa hotuba yake bungeni, alichukua zaidi ya saa moja kujibu kwa ubabaishaji na uongo hoja za Mbowe! Alikuwa hajiamini na mara nyingi alikiri kuwa hotuba ya Mbowe imempa shida sana. Muda mwingi alpotaka kwa mfano kutetea Tume ya mabadiliko ya katiba, alijisahau na kusema "tuliamua" badala ya kusema waliamua.

Alishindwa kwa mfano kutetea serikali yake kuhusu hoja ya Filikunjombe kuwa mawaziri kumi tu ndo wanafanya kazi, badala yake akasema amesikitishwa na kauli ya Filikunjombe. Hakujibu hoja ya Mh Selasini kuhusu UDOM kuijihusisha na udini! Na mengine mengi sana........

Lakini hebu angalia TISS wanavyohenyeshwa na wanausalama wachache lakini wenye ueledi wa Chadema wakati wao wana mtandao nchi nzima! Kauli ya Dr Slaa kuwa wao ni makini na imara kuliko serikali uanaweza kuipinga kwa hoja gani? Agalia walivyokuja na kauli za jumla kuhusu kuingilia mawasiliano ya mtu na kuacha kujadili suala la msingi " NJAMA ZA KUTEKA NA KUTESA"

Inatukumbusha walivyofungia Mwanahalisi kwa kumfichua mwarifu lakini mwarifu hawakushughulika naye! Unaweza kumlinganisha Mkurugenzi wa TISS na Mabere Marando? akili ndogo haitawali akili kubwa hapo? Unaweza kumlinganisha Mwanasheria mkuu na Tundu Lissu? Akili ndogo haitawali kubwa hapo? Unaweza kumlinganisha Dr Slaa na mkuu wa Magogoni? Akili ndogo haitawali kubwa hapo?

Asante Mh Msigwa kweli akili ndogo intawala akili kubwa Tanzania!
 
quote_icon.png
By Haki sawa
Taarifa ni kuwa hilo gari lililokamatwa sio la chama ila ni la mwanachama wetu ambaye wakati linakamatwa hakuwepo alikuwa amemuazima rafiki yake gari,

Pili, mwenye gari jana alienda polisi akiomba kutoa maelezo juu ya umiliki wa gari hilo ,polisi wakamkatalia , akaomba kuona hizo dola akakataliwa, waliokuwa wako kwenye gari waliachiwa ila usiku wakakamatwa tena .

So tupate majibu ya kina polisi , na kumbuka habari iko uhuru front page.
 
Back
Top Bottom