Ni kweli bila Nyimbo kusini CHADEMA imekufa?

Benazir Buto

Member
Sep 30, 2012
65
8
Watu wanazungumza sana kuhusu huyu mzee..kabla ya yeye kuwepo CHADEMA Njombe ilikuwaje? Mbowe amehangaika na CDM miaka 20 sasa yeye mwaka tu anaona hakuna mafao? Kweli tunapokea watu wa ajabu
 
Japo hujaeleweka vizuri ila tambua tu ya kwamba CHADEMA ni taasisi. Haimtegemei mtu mmoja. CDM ni mimi, wewe na yule. Ni muungano wa wanachama. Leo hii hata akiondoka Dr Slaa chama kitabaki tu kwa sababu chama si mtu mmoja. Chama ni wananchi waliokubaliana kufuata ideology fulani ili kutafuta kutawala. Kwa hiyo kujitoa kwa Nyimbo si chochote wala lolote ndani ya CDM kusini. Mtu ataondoka chama kitabaki. Pamoja tuijenge CHADEMA.
 
Ndugu zangu watanzania hatukuumbwa kusemewa na viongozi maarufu na kuwategemea katika kila mwelekeo na mwongozo hawa nao tunaowategemea wanapata vikwazo ,vishawishi, vitisho, ukatishwaji tamaa, kibinadamu wanaweza kuyumba ama hata kusita je kila wanaposita na sisi wote tusite?

Katika vita hii ya kuiondoa tuta CCM kuwa na misuko suko mingi saana sasa hivi wanajeruhi watu wanaua wanafunga watu jela wanatumia dola vibaya hii yote ni mbinu ya kuturudisha nyuma tusipoamua kusonga mbele na kuangalia nyuma eti nyimbo kazama nani kapotea ndugu zangu tutashindwa TUSONGE MBELE NYIMBO ALIYOYAFANYA YAMETOSHA TUFANYE SISI PIA SASA NI ZAMU YETU
 
Wapo wanaofikiri Nyimbo ataondoka na CDM huko Njombe. Ni haohao waliofikiri CDM ingeondoka Mbeya na Sambwee shitambala.
 
Kimsingi siasa za tanzania kwa sasa hazitegemei haiba ya mtu...ufuasi wanaopata CDM ni kwa vile tu wanatoa jibu lenye matumaini kwa wananchi siku wakibadili mahubiri yao na ufuasi wa umma nao utakoma..

Huyo mzee ashukuriwe kwa mema aliyofanya na ikiwezekana uongozi wa CDM watoe taarifa rasmi ya kumshukuru bila kutaja madhaifu yake wala kumnanga kwa namna yoyote ile.

Parting ways kistaarabu....tanzania KWANZA.
 
Watu wanazungumza sana kuhusu huyu mzee..kabla ya yeye kuwepo CHADEMA Njombe ilikuwaje? Mbowe amehangaika na CDM miaka 20 sasa yeye mwaka tu anaona hakuna mafao? Kweli tunapokea watu wa ajabu

Msaliti hakosi sababu...let him go
 
Watu wanazungumza sana kuhusu huyu mzee..kabla ya yeye kuwepo CHADEMA Njombe ilikuwaje? Mbowe amehangaika na CDM miaka 20 sasa yeye mwaka tu anaona hakuna mafao? Kweli tunapokea watu wa ajabu

Kwanza ipo haja ya vyama vya upinzani kwa ujumla kuwaangalia hawa wahamiaji toka chama tawala. uzoefu unaonesha kuwa mwanasiasa yeyote anayegundua kuwa amechokwa au amepoteza ushawishi ndani ya CCm hukimbilia vyama pinzani kwa mbwembwe sana na matusi makali, anapopewa nafasi na jina lake kuanza kung'ara hukimbia na kurudi kwenye chama chake kwa madai rukuki lakuonekana kama mpiganaji aliyekuwa amepotea njia! Kwa maana nyingine wanakuja huku kuja kusafisha nyota tu ili wakirudi kwao warudi kama mashujaa. (FUATILIA WOTE WALIOFANYA HIVYO)
My TAKE: ni heri vyama kukomaa na wapiganaji wake ambao wameanzanao katika hali ya shida lakini wamevumilia hadi kuvifikisha vyama vyao hapa vilipo kuliko kuhangaika na hizo pumba ambazohazina vituo. NI USHAURI TU.
 
Watu wanazungumza sana kuhusu huyu mzee..kabla ya yeye kuwepo CHADEMA Njombe ilikuwaje? Mbowe amehangaika na CDM miaka 20 sasa yeye mwaka tu anaona hakuna mafao? Kweli tunapokea watu wa ajabu
CDM bado ingekwenda Huko na kusimika bendera yake fasta.Kwani mikoa mingapi walikuwa hawapo na walikwenda na sasa CCM wanahemea drip huko?
 
Huyo mzee Thomas Nyimbo hakuja CHADEMA kuwa mwanachama, alikuwa anataka kuendelea kuwa Mbunge, huyu mzee ni kama jamaa wetu wa Maswa Maghale Shibuda. kadi anayo moja hivyo hakuna haja kuhangaika naye. Amekosa alichohitaji na kesho mtasikia karejea CCM akisema ndicho chama pekee kilicho safi, au kasikia Injinia Mahenge hatagombea tena?
 
Back
Top Bottom