Ni kweli balozi zetu nje ya nchi zimeishiwa fedha?

Hii ya serikali kuishiwa mbona siyo habari mpya wakuu. Zito kabwe alilisema hili mwaka jana sijui mwaka juzi lakini mkuu wa pesa akakanusha na kumwita siyo mzalendo. Mimi hadi leo 14/2/2012 mshahara wa december 2011 sijauona. Serikali nyeupe hii!!!!
 
hii ni laana ya kuichukia Israel na kuwapenda maadui zake. Tanzania ina ofisi za ubalozi katika nchi cuatro(nne) maadui wa Israel, saudi arabia, Qatar, UAE na Iran lakini haina ofisi ya ubalozi Israel, kwa nini tusilaaniwe? atakaye kupenda nami nitampenda na atakaye kulaani nami nitamlaani, kifungu hiki ndicho kinachoifanya wizara mama iliyoimport laana hapa nchi kukosa mishahara ya kulipa wafanya kazi wake.

na laana bado inapiga hodi katika migomo ya madaktari, walimu na mengi yatajitokeza! pesa zitaibwa na wanasiasa, uchumi haukui na kila kukicha tunajikuta ni watu wa kuhuzunika tuu.

Naiomba serikali yetu iachane na utumwa wa kuwaogopa waarabu eti tukifungua ubalozi pale tel aviv, basi jamaa watatuchukia. tukafungue ubalozi tel aviv na kuonesha dunia kuwa sisi ni watu huru na Israel ni kipenzi chetu. nakuambia wiki moja tuu utasikia Kyela, mbamba-bay na sehemu nyingi mafuta yamegundulika.
 
Hakuna azimio la Arusha, kwanini wanateseka. Balozi zetu sio lazima wafanye kazi za kidplomasia wangefanya vitovu vya biashara kukwepa kodi.
Mfano una emport viazi vingi harafu unasema ni matangazo ya utalii wakati mna duka lenu mjini. Kwi kwi kwi, ama kila balozi inakuwa na kampuni la kitalii Tz.

Mbona ofsi nyingi za ubalozi za nchi za magharibi si ofsi za kidplomasi bali ni ofsi za kitelenjisia kwa mgongo wa diplomasia.
 
huyo ndiyo kikwete...ametutoa kuleee na kutufikisha hapa... bado miaka mitatu ya kulia na kusaga meno...!
 
Acha ushamba wewee! Hivyo ndivyo inavyoandikwa...jitahidi uwe unasoma hotuba za bajeti..uandishi wa kiasi cha fedha za bajeti ni tofauti na jinsi ulivyofundishwa darasa la nne.

Katika bajeti tukisema kuwa kiasi kilichotengwa ni shilingi milioni kumi na tatu laki nne elfu mbili na themanini na moja na senti ishirini (13,402,081.20); basi kwenye uandishi wa kibajeti huandikwa "kiasi kilichotengwa ni shilingi milioni 13,402,081.20" na hii husomeka sh 13,402,081.20.

Neno milioni halimaanishi kuwa hizo pesa ni 1,000,000 x 13,402,081.20 bali hutangulia kumuelekeza msomaji atambue kuwa hiyo pesa iko katika kiwango cha milioni bila kuhesabu idadi ya sifuri au commas.

Jaribuni kufuatilia habari za bajeti za serikali kujua jinsi gani taarifa za bajeti zinavyoandikwa badala ya kuwaita waandishi ni VILAZA wakati WEWE ndiye kilaza usiyejitambua.
Mtumeee!

Yani wewe ndio typical mwandishi wa Kitanzania, yani ni watupu mpaka mnatisha! Mimi ndio mshamba?

Bajeti ya serikali hii hapa, nionyeshe sehemu ilipoandikwa kitu kama "shilingi milioni 13,402,081" wakimaanisha 13,402,081 /=.

Neno "milioni" za shilingi limetumika kwenye bajeti katika sentensi tano tu, kama ifuatavyo:

Hatua hizi katika Ushuru wa Bidhaa kwa pamoja
zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi
milioni 99,521.5

Hatua hizi kwa pamoja zitapunguza mapato ya Serikali kwa
shilingi milioni 2,007.6

Hatua hizi kwa pamoja zinatarajiwa kupunguza mapato ya
Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 4,669.7

Hatua hizi katika Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa
pamoja zitaongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha
shilingi milioni 71,518.9

Hatua hizi za Kodi ya Mapato zitapunguza mapato ya
Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 20,287.5
Mbona hawakuongeza masifuri mbele ya hizo "milioni 20,287.5" kwa mfano, isomeke "shilingi milioni 20,287,500"? Unataka kutuongopea hapa wakati bajeti ni document ya wazi? Unaandika taarifa za kifedha na bajeti halafu hujui hata the most basic of arithmetic principles? Mmesoma wapi nyinyi vilaza wa magazetini kazi kuandika uhoro mtupu kila uchwao? Eti natumia hesabu za darasa la nne, kwani misingi ya fundamental arithmetics inabadilika? Ulitaka bajeti ya Tanzania ya kujumlisha na kutoa itumie hesabu gani, third order differential equations na eigen function expansions? You are out of your pitiful mind!

Ukiandika shilingi milioni 13,402,081.20 hizo ni bilioni 13,402 namba nzima, au shilingi trilioni 13.4! Sasa utasemaje Balozi Nyang'anyi kapoteza shilingi trilioni 13 za ubalozi wakati bajeti nzima ya foreign affairs haifiki trilioni hata moja? Kilaza mkubwa we!
 
Ni ukata mkali hadi mishahara hakuna
headline_bullet.jpg
Katibu Mkuu asema hali ni tete mno

Cheyo(16).jpg

Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo.

Wakati Serikali ikikabwa koo na madaktari juu ya madai ya nyongeza ya posho na mishahara yao, hali kadhalika walimu wakiwa wamekwisha kutoa ilani juu ya nyongeza ya mishahara yao, imethibitika kwamba Ofisi za Tanzania nje ziko hoi kutokana na kukosa fedha za matumizi ya kawaida.

Kama haitoshi, baadhi ya balozi zinadaiwa kuendeshwa bila mishahara kwa kipindi kirefu sasa, hali inayovunja heshima na hadhi za ofisi hizo ughaibuni.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule, alibainisha hali hiyo jana jijini Dar es Salaam mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Haule alisema kwa mwaka 2011/2012, serikali ilitenga Sh. bilioni 150 kwa ajili ya matumizi ya kawaida, lakini Hazina iliwapa Sh. bilioni 80 na kwamba hatua hiyo imeifanya wizara yake kuwa na wakati mgumu katika kulipa mishahara pamoja na kugharamia uendeshaji wa ofisi za balozi.

Alithibitisha kuwa, kushuka kwa sarafu ya Tanzania kunachangia hali hiyo na kwamba serikali inashindwa kumudu kulipa mishahara kwa kuwa watumishi wa balozi za Tanzania wanaolipwa kwa Dola ya Marekani kutokana na bajeti kutengwa kwa kutumia shilingi.

“Nikiri kwamba hali katika balozi zetu ni mbaya kutokana na ukata unaoikabili wizara yangu ambayo inaziangalia balozi hizi,” Haule aliwambia wajumbe wa kamati hiyo ambayo Mwenyekiti wake ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo.

Haule aliongeza kuwa, bajeti ya kuzihudumia balozi za Tanzania inazidi kupungua mwaka hadi mwaka. Ingawa hakutoa takwimu, lakini alisema hali hiyo imekuwepo kwa kipindi cha miaka saba hadi sasa.

Katika kudhibiti matumizi ya fedha kidogo ambazo wizara yake inatengewa na serikali, Haule aliambia kamati hiyo kuwa serikali imezuia mafao ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania, Abu Dhabi, Falme za Kiarabu, Mustafa Nyang’anyi, baada ya kubainika kwamba alitumia fedha za huko Dirham 31,000 (Sh. milioni 13, 402,081.20) bila kuzitolea maelezo.

Haule alisema kuwa, zaidi ya shilingi milioni tano alizostahili kulipwa kama mafao zimezuiliwa na kwamba serikali itaendelea kumdai fedha zingine kwani hizo hazitoshi kulipia kiasi anachodaiwa.

Kuhusu mahusiano ya kimataifa, Haule, alisema Tanzania imefunga ubalozi wake nchini Uholanzi kutokana na matatizo mbalimbali yakiwemo ya kupishana mtazamo wa masuala mbalimbali.

Kwa upande wake, Cheyo, alisema anasikitishwa na kitendo cha serikali kushindwa kuwalipa mishahara watumishi wake katika balozi zake.

Cheyo alisema mtumishi akiwa hapa nchini akikosa mshahara angalau anaweza kwenda kukopa kwa ndugu yake, lakini anapokuwa nje ya nchi anapata shida na kuishia kukopa benki.

Alisema ni aibu kwa Tanzania kuendesha ofisi zake za nje kwa kuhaingaika na kwamba lazima serikali ihakikishe inachukua hatua na kumaliza tatizo hilo.

“Kwa miaka 50 ya uhuru wa Tanzania sikutegemea kama balozi za Tanzania zitaendeshwa nama hii kwa kukosa fedha na watumishi wake kuendelea kuhangaika,” alisema Cheyo, ambaye aliongozana na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zainabu Vulu na wajumbe wengine.

Kamati hiyo ilipitia hesabu za Wizara hiyo na kubaini kwamba katika Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda matumizi yake yalizidi na kumuagiza Haule kufuatilia suala hilo na kuwapatia taarifa.

Katika kikao hicho kilichofanyika katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam, Haule, alifuatana na maofisa kadhaa wa wizara na taasisi zilizoko chini ya wizara hiyo.

Hivi karibuni madaktari waligoma nchini wakidai nyongeza ya posho na mishara yao, mgomo ambao ulisababisha kukosekana kwa huduma za kitabibu katika hospitali kuu nchini kwa takribani mwezi mmoja.

Mgomo huo ulisitishwa baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kukutana nao na kutangaza nyongeza ya posho hizo, huku ikiundwa kamati ya kupitia madai ya nyongeza ya mishahara ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha kazi, na kuwachunguza Katibu Mkuu wa Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu, Dei Mutasiwa, kwa tuhuma mbalimbali za ufisadi.

Walimu nao wametaka nyongeza ya mishahara kwa zaidi ya asilimia 100 kuanzia Julai mwaka huu, vinginevyo wataanza mgomo.

CHANZO: NIPASHE
 
Ahsante Mizizi kwa kutuamsha....
Tunakila sababu kama nchi kuingia kwenye kitabu cha record cha dunia!
Kama this time katibu wa wizara amekiri wazi hivyo basi ni kituko.
Mwanzoni Zitto alipotoa tathimini ile ilionekana kama anakijiba na ililazimishwa kujenga picha ya propaganda....
Tusubiri majibu saiv.
 
Hata wizara ya ulinzi hakuna fedha kabisa. Huu ni mwezi wa 3 other charges maafsa wa jeshi hawajapokea. Chakusikitisha Makao Makuu ya jeshi la maji jana limewaaga makamanda kwenda kyela kufungua kambi mpya ya jeshi la maji ziwa Nyasa bila fedha. Hali ni mbaya jamani, msidhani ni huko tu.
 
Niwape mawazo ya nini cha kufanya wakati hauna fedha ya kutosha serikalini? Maana inaonekana hakuna watu wanaweza kufikiria nini cha kufanya au wanajua cha kufanya lakini hawataki kukifanya!
 
Father Mkulo chapisha chapaa baba.

Achapishe mara ngapi??? hiyo plan alishatekeleza na ndipo alituletea noti za ajabu tulizo nazo- low value wachumi wanasema kuchapisha noti daima iwe plan ya mwisho baada ya ku-maliza zingine, sasa baada ya hapo mkulo hana jinsi ni kutangazwa TANZANIA MUFILISI
 
CUFtifu.jpg

Maoni ya Katuni

Miongoni mwa habari zilizopewa uzito katika vyombo vya habari nchini jana ni kilio kwamba Balozi za Tanzania nje zinakabiliwa na ukata mkali kiasi cha watumishi wa umma kukosa hata mishahara yao.

Hali hiyo imeelezwa kuwa imekuwa ikiendelea kwa muda sasa, kiasi cha kufanya uendeshaji wa ofisi hizo kuwa mgumu mno.
Habari za kukosekana kwa fedha za kuendesha ofisi hizo ziliwekwa wazi na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Ofisi za balozi za nchi yoyote Tanzania ikiwamo, ndiyo mwakilishi wa nchi hiyo ugenini. Ni kioo cha taifa moja ndani ya taifa lingine, ndiyo maana sheria za kimataifa kwa mfano zinatambua pale zilipo ofisi za balozi fulani eneo hilo huchukuliwa kama ardhi ya nchi husika. Ni

dhahiri ofisi za balozi ndizo zinatangaza nchi, iwe kwa jema au kwa baya kulingana na ilivyokaa na inavyoendesha mambo yake.
Tunatambua kwamba serikali kwa ujumla wake imekuwa ikilalamika kuwa inakabiliwa na ukata, hali hii ndiyo imeleta malalamiko ya

makundi mbalimbali ya watumishi wa umma kama ilivyoonekana hivi karibuni kwa madaktari na kama ambavyo imekuwa inaonekana kwa walimu. Kilio cha makundi haya ni malipo duni.

Wakati serikali ikikiri kukabiliwa na ukata, Mamlaka ya Mapato (TRA) imekuwa ikitoa taarifa ya jinsi ilivyofanikiwa kukusanya mapato ya serikali aghalab kwa kuvuka malengo; hata hivi karibuni taarifa yake ilisema kuwa kwa Desemba mwaka jana ilikuwa imevunja rekodi kwa kukusanya zaidi Sh. bilioni 600 kwa mwezi.

Hicho ni kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa na mamlaka hiyo. Mbali na makusanyo hayo kuwa juu, TRA kwa muda mrefu sasa imekuwa inakusanya mapato mengi mwezi baada ya mwezi, hali ambayo ingeliiongezea serikali uwezo wake kutekeleza majukumu yake

kama fedha husika zingelitumika vizuri na kwa kuzingatia vipaumbele vya maana kwa ustawi wa taifa na watu wake.
Ni bahati mbaya kusikia kwamba wakati ukusanyaji wa mapato ukiongezeka, hali ya watumishi wa umma inazidi kuwa mbaya kama hawa

wa balozi ambao sasa wanadaiwa kuishi maisha ya kubangaiza kwa kiwango kikukubwa sana. Kukosa mshahara kwa mtumishi wa umma ni kashfa kubwa kwa serikali, lakini pia ni aibu kwa taifa mbele ya mataifa mengine ambako tunawakilishwa.

Hali hii ikijumuishwa na vilio vya ujira kijungu jiko kwa watumishi wa umma, picha inayojengeka ni kwamba hali si nzuri serikalini; na kwa maana hiyo serikali kwa ujumla wake ilipaswa kuonekana ikiendesha mambo kama serikali inayokabiliwa na ukata. Lakini mambo si hivyo, ni kinyume chake.

Bado serikali yetu imefungwa katika ugonjwa wa posho, mabilioni ya shilingi kila mwaka yanateketea kwenye posho, na hata hivi karibuni tu taifa lilitikisika kwa madai ya posho za wabunge.

Kumekuwa na tatizo kubwa sana ndani ya ofisi za serikali juu ya matumizi bora ya kodi za wananchi, matokeo yake fedha nyingi hazipelekwi sehemu ambazo zingelileta mabadiliko ya kweli kwa taifa na ustawi wa watu wake.

Ukichukulia suala la watumishi wa umma walioko nje ya nchi kuishi bila mishahara inakuwa ni vigumu mno kuelewa wenye dhamana ya kuhakikisha watumishi hao wanalipwa ujira wao wanafikiria nini, hasa kwa sababu ukiwa ughaibuni hakuna cha mjomba wala rafiki wa

kukopa, kibaya zaidi hakuna duka la Mpemba au la Mangi la kwenda kukopa ili kulipa mwisho wa mwezi, au ukijaliwa.
Kwa kweli kuwaacha watumishi wa umma katika madhila kama haya si jambo linalokubalika wala kuvumilika, ndiyo maana sisi tunasema

kuwa wakati umefika sasa kwa serikali kuwa makini walau kwa kiwango kidogo tu ili kutekeleza hata yale majukumu yake ya lazima bila mikwaruzo kama inavyotokea sasa.

Tunajua, serikali ina majukumu mengi, pia tunaelewa pamoja na ongezeko la makusanyo ya mapato mahitaji ya fedha nayo ni mengi mno, lakini bado tunaamini kwamba kama serikali ikijipanga vizuri na kujielekeza kwenye mambo ya muhimu katika vipaumbele, hakika

itafanikiwa kuondokana na malalamiko mengi sana ya watumishi wake, pia kuanza kupata fedha za kugharimia hata miradi ya maendeleo kwa fedha za ndani.

Hizi si porojo, huko tulikotoka wakati wa utwala wa awamu ya tatu tulipata kujenga barabara zetu kiwango cha lami kwa fedha za ndani kwa asilimia 100, inawezekana, TRA ni ile ile, watumishi ni wale wale na serikali ni ile ile ya Chama Cha Mapinduzi; kama iliwezekana huko

nyuma ni kwa nini leo isiwezekane? Inawezekana tu kama serikali itajiendesha kwa nidhamu ya hali ya juu katika matumizi, lakini la muhimu zaidi kuachana na anasa.

Anasa ni nyingi serikalini, zinaonekana katika matumizi ya vitu vingi vya kifahari, posho nyingi, na kila aina ya mbwembwe ambazo hakika hazina ulazima wowote si kwa watumishi wa umma wenyewe wala wananchi kwa ujumla wao. Tubadilike.

Dr. Slaa aliwaambia watanzania kuwa mkimchagua JK ni janga la taifa, hamkumsikia mkadhani anataka urais. Sasa yametimia, ngoja tuchomeke tu, kila mtu afe lwake!!!!
 
Hata wizara ya ulinzi hakuna fedha kabisa. Huu ni mwezi wa 3 other charges maafsa wa jeshi hawajapokea. Chakusikitisha Makao Makuu ya jeshi la maji jana limewaaga makamanda kwenda kyela kufungua kambi mpya ya jeshi la maji ziwa Nyasa bila fedha. Hali ni mbaya jamani, msidhani ni huko tu.

unanutisha au ni kweli?
 
Back
Top Bottom