Ni kwanini Mauaji ya Rwanda yanaitwa ya Kimbari Genocide

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Hii ndiyo maana (wikipedia) ya mauaji ya kimbari ni maangamizi ya mpango ya kundi zima la watu au ya sehemu yake kwa msingi wa taifa, kabila, rangi au dini!

Sasa nijuavyo mimi Rwanda kuna watu wa aina moja tu, yaani Wanyarwanda, kuna kabila moja tu yaani la Kinyarwanda na kuna Lugha Moja tu yaani Kinyarwanda, sasa kwa nini mauaji yaliyofanyika huko kutokana na hiyo vita yaitwe ya Kimbari??

Kwa kukumbushia Mauaji ya kimbari kulingana na Umoja wa Mataifa wanavyosema ni pale kundi moja linapoamua kilimaliza kabisa kundi lingine, sasa Rwanda kuna kundi moja tu la watu yaani Wanyarwanda, hapo ndipo ninaposhindwa kuelewa!
 
Hapo kwenye kabila kuna kitu kinaitwa ethnicity. Ndipo hapo tunapopata watutsi na wahutu ndani ya kabila moja la wanyarwanda.

Hakuna kitu kama hicho Rwanda kuna one ethnic group!
 
Kuna wahutu na watusi

Lakini Watusi/Wahutu siyo Kabila bali ni matabaka tu na hakuna tofauti baina yao isipokuwa madaraja ya kimaisha tu, na hivyo nashindwa kuelewa inaangukia vipi kwenye mauaji ya Kimbari!
 
Nlkuaga na historia yake kwny kjarida...ngoj nkipata ntakutumia...utaelewa fresh
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Hakuna kitu kama hicho Rwanda kuna one ethnic group!

Ati nini unasema?

slide_10.jpg
 
Umeuliza ili upate kufahamu au umeuliza ili ubishane?

Sijauliza ili nibishane bali nimeuliza ili nipate ufahamu zaidi ya ule ninaoufahamu hivyo kama hauna zaidi ya ninavyo fahamu unaweza kukaa pembeni, sijakuita wala kukulazimisha!
 
Wana tofauti kubwa sana na hata wakati wa mkoloni (mbeligiji) walikuwa wanapiwa kwa kutumia vernier callipers pua zao kuwatofautisha. Ya mtutsi ikiwa ndefu zaidi........

384782989.jpg

Lakini kwa nini wanaongea Lugha moja kama ni watu wawili tofauti???
 
Wewe mbona unaongea lugha moja na mimi wakati hatuko sawa?

Hapana kuna tofauti kati ya Lugha ya nchi ya kuwasiliana na lugha ya asili ya mtu! Mimi na wewe kinachotuuganisha ni Lugha ya Taifa letu ambalo ni jipya yaani kabla ya Wazungu/Mwarabu halikuwepo au tuseme kama Mwarabu/Mzungu asingekuja mimi na wewe tusingeongea lugha moja lkn Unyarwanda wanaongea Lugha Moja ya asili kabla hata ya Wakoloni kuja wote ni sehemu ya Banyarwanda, na hiyo ndiyo tofauti, yaani Wakoloni waliwakuta hawa Wanyarwanda wa leo kama walivyo na Lugha yao Moja ya Asili, sasa ni kwanini wawe na Lugha Moja kama ni watu wawili tofauti?
 
Sasa Kinyarwanda si ndio lugha ya taifa la Rwanda? Hata Somalia wanaongea Kisomali na wanatandikana toka 1991. Umeambiwa kuna tofauti ya tribe na ethnicity na mdau hapo juu. Jaribu kuelewa tu.....Lugha ni kitu kioja na kuna vingine vingine pia
 
Hapana hakuna tofauti kati ya tribe na ethnicity ni kitu kile kile tu, isipokuwa tribe ni neno negative la kumtusi Mwafrika na ethnicity ndiyo linalotumika Dunia nzima lkn wakimaanisha kitu kile kile!
Ningeweza pia kusema kwamba Rwanda ina one ethnic group na ili uwe ethnic group ni lazima uwe na lugha Moja hiyo ndiyo hasa inayotofautisha ethnic group moja na nyingine!

Umetoa mfano mzuri wa Somalia, sasa ni kwa nini mauaji ya Somalia hayaitwi ya Kimbari lkn ya Rwanda yanaitwa hivyo wakati wote Wasomali na Wanyarwanda wana ethnic group moja???
 
Mleta mada una asili ya ubishi japo wote tunaongea lugha moja. Mabishano yasiyoisha huweza kupelekea mauaji ya kimbari katika jamii.
 
Hakuna kitu kama hicho Rwanda kuna one ethnic group!
Kwa kiasi fulani naweza kukubaliana na wewe. Hapo mwanzo tutsis and hutus were merely "vyeo". Kwa hiyo kimsingi hakutakiwi kuwa na ethnic groups in Rwanda. Ila baada ya wakoloni kuja na sera zao sasa kuna 3 ethnic groups in Rwanda. Regardless of how stupid kwa wanyarwanda kuwa na ethnicity lakini zipo na zina nguvu sana.
 
Lakini kwa nini wanaongea Lugha moja kama ni watu wawili tofauti???
Sasa Kinyarwanda si ndio lugha ya taifa la Rwanda? Hata Somalia wanaongea Kisomali na wanatandikana toka 1991. Umeambiwa kuna tofauti ya tribe na ethnicity na mdau hapo juu. Jaribu kuelewa tu.....Lugha ni kitu kioja na kuna vingine vingine pia
Hata hao wasomali pia wana tatizo hilo hilo la Rwanda la kuwa kabila moja lakini kuna ethnicity humo ndani, ndio maana wanapigana kila siku. Ndani ya wasomali kuna makundi ya wasomali wana damu ya kiarabu, wengine wana damu za kishirazi, wengine wana damu za kibantu ila wote ni wasomali.
 
Kwa kiasi fulani naweza kukubaliana na wewe. Hapo mwanzo tutsis and hutus were merely "vyeo". Kwa hiyo kimsingi hakutakiwi kuwa na ethnic groups in Rwanda. Ila baada ya wakoloni kuja na sera zao sasa kuna 3 ethnic groups in Rwanda. Regardless of how stupid kwa wanyarwanda kuwa na ethnicity lakini zipo na zina nguvu sana.

Ndiyo maana nashindwa kuelewa ni kwanini mauaji yaliyofanyika yanaitwa ya kimbari, kwa maana kuita mauaji ya kmbari ina maana ni kundi moja linaamua kuwaua kwa makusudi kundi jingine kwa laengo la kuwaangamiza kabisa, sasa kwa Rwanda kuna watu wa aina moja tu yaani Wanyarwanda na hao wanaoitwa Watusi/Wahutu ni matabaka tu ya watu wa jamii moja, ambayo kama ulivyosema wazungu waliyatumia kuwaganya lkn wote wana same genetic pool!
 
Back
Top Bottom