Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,412
4,558
Broiler.jpg

Hey JF Members.

Ee bwana kuna mtu anaweza kunipa msaada wa mchanganuo wa kufuga kuku. Naona soko la kuku ni kubwa sana. Hii ni biashara ambayo soko lake liko tayari. hotels, functions, vibanda vya chipss. Yeyote mwenye idea naomba msaada please!

BAADHI YA MASWALI NA MAHITAJI YA WADAU
Habari wakuu:

Bila shaka kuna watu ambao wanafuga kuku au walishawahi kufuga kuku. Naomba watu wenye uzoefu na maarifa kuhusu kufuga kuku, wanipe mawazo maana nataka kuanza kufuga kuku na sijawahi kufanya hivyo, hivyo nahitaji mawazo yenu wakuu.

Natanguliza shukrani zangu wakuu:
Habari wadau,

Naomba mnisaidie, nataka kuanza ufugaji mdogo wa kuku na nitaendelea kukua siku zinavyokwenda.
Nahitaji kuanza kufuga kuku waliochanganyika breed, wa kisasa na wa kienyeji.

1. Wanaotaga wa kisasa ni vizuri kuchukua kuku wa umri gani kwa mbegu nzuri?
2. Jogoo mmoja anatosha kuku wangapi?
3. Kuna mahali wanauza vifaranga ambao tayari ni breed ya kisasa na kienyeji?
4. Soko la kuku waliochanganywa breed lipo au ni kama soko la kuku wengine?
5. Kama kuna mashamba ya mfano maeneo ya Dar au Yanayozunguka naomba mnifahamishe niweze kwenda kuona practically inavyokuwa.
Habari ndugu zangu,

Naomba mnisaidiye nataka kuanza kufuga kuku wa kisasa ila sina elimu nao.

Naombeni mwenye ujuzi anisaidie

Sent using Jamii Forums mobile app


MICHANGO YA WADAU MBALIMBALI
WALISHE VIZURI, KUWA NA MTAALAMU WA KUHAKIKI AFYA NA USTAWI WAO
Mlachake, una experience kwenye ufugaji kuku? kama huna basi,
kuanza na kuku 1000 utakuja kulia!!! Na kama ni lazima uanze na kuku wengi,basi usiwe na mkono wa birika, kwamba usiwe bahiri!!

Lazima utafute part time animal scientist ambae atakuwa mara kwa mara anakushauri suala zima la poutry management!!! aidha,usiwe bahiri, hususani kwenye feeding!!! poultry keeper wengi wana-collapse kv wanataka kubana matumizi kwenye chakula---manake wale jamaa wanafukia ile mbaya!

in order to have productive layers or broilers, lazima kwenye masuala ya misosi wajiachie!!! and even more important, especially kama ni kuku wa mayai, tenga bajeti ya chakula pembeni na usiichezee kwa kitu kingine chochote kile, iwe pale ready for feeding!! Kama utapata mtaalamu, akakupa techinques za kutengeneza chakula itakuwa more wise kwako, kwavile feed cost ipo juu sana!!!

BUT be careful, usi-opt tu kutengeneza chakula chao wakati feed chemistry haunayo!!! kama ni wa mayai, badala ya kuanza kutaga after 5 ro 6 months, wataanza after 8 months!!!Kama unazani hutaweza kufanya mixing vizuri, u better ukajilipue kwenye vyakula vya madukani ambavyo ni very expensive- but don' worry, bei hiyo haitakufanya upate hasara, but itapunguza faida!! na kitu kingine muhimu, don buy day old chicks mitaani, utakuja kulia!!!hizo ni few hints, but the project, inalipa wangu!!!

Mengine yote, unaweza kushauriwa na animal scientist, but the first good strategy--- tafuta kijana ambae tayari ameajiriwa kwenye suala zima la utunzaji kuku--- mchomoe anakofanya kazi na mpe mshahara mkubwa zaidi, na mpangie room very close na yalipo mabanda yako!!! uki-opt kujenga annex ya kukaa poultry keeper, itakuwa ni more productive idea! wish u all the best
UFUGAJI BORA WA KUKU WA NYAMA NA MAYAI

Wiki ya Kwanza: Siku ya 1 – 6, Wape: glucose broiler boost au aminovit au super vitvigo start kwenye chakula (kilo 1 kwa mfuko 1 wa kg 50) kuanzia wiki ya kwanza hadi ya 4.

Siku ya 7: Chanjo ya newcastle - masaa 2 tu, weka maji na vitamin mara baada ya kutoa maji ya chanjo.

Wiki ya pili: Chanjo ya gumboro - masaa 2 tu, halafu endelea na maji ya vitamin.

Wiki ya tatu: Doxicol au ctc20% na amprolium, vitamin na molasses kwa siku 5 - 7.

Wiki ya nne: Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dose kubwa ya vitamin.

Wiki ya sita: Wape kuku wa nyama maji ya vitamin asubuhi na matupu jioni.

Wiki ya nane: Wape kuku wa mayai chanjo ya ndui, dawa za minyoo (piperazine au lekiworm) vitamin au supervit layers walishe growers mash au farmers concentrate hadi miezi 3 na 1/2 tumia layers mash wakifika miezi 4 kamili au wape majani

Wiki ya kumi na mbili: Wape chanjo ya newcastle (rudia kila baada ya miezi 3) masaa 2 kisha wape maji ya vitamin

Wiki ya kumi na sita: Kata midomo kisha wape neoxyvital kwa siku 3-5 andaa viota.

Wiki ya 54: Wape virutubisho vyenye kuongeza wingi wa mayai mfano glp (kilo 1 kwa kila kilo 50 za chakula, wiki ya kwanza na nusu kwa wiki zinazofuata na vitamin.

Wiki ya 72: Tumia v rid kusafisha mabanda ili kuua vijidudu pia weka maji ya dawa hii kwenye dish ya kusafishia miguu (footbath) ili kuhakikisha udhibiti wa vijidudu (biosecurity) na kwamba vifaranga wanaowekwa hawaathiriwi na vijidudu hivyo.

Wiki ya 96: Ondoa kuku wote waliozeeka.

All the Best
ZINGATIA HAYA KWA USTAWI WA BIASHARA HII
Mradi wa kuku ni mzuri haswa pale ambapo unakuwa na uzoefu wa jinsi ya kuwatunza na kufuatilia soko lake. Kwa mtizamo wangu naona kama unapendelea zaidi kuku wa nyama ambao kiasi fulani ni wagumu kuliko kuku wa mayai.

Ni muhimu ukiangalia yafuatayo kwa ustawi wa kuku wa nyama.

1. Kuwa na banda zuri lenye hewa ya kutosha pamoja na joto la kutosha (unaweza kupata vitabu kutoka kenye veterinary mbali mbali). Banda ni wastani wa mita 4 kwa 4 kwa kuku 200 wa nyama au 100 wa mayai. Hakikisha banda ni safi na umelipulizia dawa kabla ya kuingiza kuku (unaweza kutumia detto).

2a. Kwa mtu unaeanza ni vizuri kutumia chakula cha kiwandani kwa ubora kwani mara nyingi vyakula vya kujitengenezea vinaweza kuwa ma upungufu au kutengeezwa katika mazingira yasiyo mazuri na hatimaye kuwa na matokeo duni. Kumbuka wanahitaji vakula veyenye virutubisho tofauti kulingana na umri (mfano starter & finisher kwa broiler)

2b. Hakikisha wanapata chanjo ya newcastle wiki ya pili kwa kukuwapya utakaowaleta. Ni muhimu sana. Pia viatamini na madini kama utakavyoshauriwa na watalamu wa mifugo

3a. Kama una uwezo mzuri ni vizuri kufuga kwa awamu. Mathalani wapishane kwa wiki 2, (yaani unaingiza kukuwapya kila baada ya wiki mbili). Hii inakupa nafasi nzuri haswa kupunguza gharama za malisho na nafasi, kwani kadri wanapokuwa ndivyo unavyoongeza nafasi ya banda. Kumbuka broiler.

3b. Hakikisha kuna vyombo vya chakula na maji vya kutosha. Kuku wa nyama hawahitaji kwenda umbali mrefu kutafuta maji, na viwe na maji pamoja na chakula wakati wote.

3c. Hudumia kuku wadogo kwanza, ndipo umalizie kwa wakubwa. Usafi ni muhimu sana. Kuwe na masodasti na hakikisha hakuna unyevu unyevu ili wasipate maambukizo ya magonjwa ya baridi.vifo vingi sana huweza kutokea. Ni vizuri ukahakikisha kuwa hakuna kuku wa kienyeji, kwani mara nyingi huwa chanzo cha magonjwa.

4. Soko ndio kichaa kikubwa katika biashara ya kuku wa nyama, na faida yote hupotea baada ya kukomaa endapo soko linakosekana. Jiandae vyema kama ikiwezekana baada ya kufikisha uzito stahili (baada ya wiki 5-6) unawachinja wote na kuwauza au kuwahifandhi ndani ya jokofu na kuwauuza taratibu.

Baada ya hapa unaweza kuangalia nafasi yako ya kukuwa na kuwa uzoefu kupanua biashara. Ushauri wa wataalamu ni muhimu sana kufanikisha malengo, ila pia kumbuka ubabaishaji ni mwingi Afrika!
MWONGOZO WA UFUGAJI WA KUKU BORA WA MAYAI

SIKU YA 1-5
Wape Glucose na mchanganyiko mmojawapo kati yah ii ifuatayo;

· Neoxyvital au otc plus na typhorium au trimazin
· Fluban na vitamin kama vile aninovit au supervit au vitalyte


CHAKULA

Weka vigostart ambayo ina ridocox kwenye chakula, kilo moja kwa mfuko kuanzia wiki ya kwanza hadi nne ili kuzuia coccidiosis. Baada ya kuacha endelea kutumia ridocox 200g/tani kwa kuzuia coccidiosis hadi wanapoanza kutaga mayai.

SIKU YA 6

Wape vitamin ambayo ni vitastress

SIKU YA 7

Chanjo ya Newcastle masaa mawili tu. Weka maji ya vitamin(vitastress) mara baada ya kutoa maji ya chanjo

WIKI YA PILI

Chanjo ya gumboro masaa mawili tu. Halafu endelea na maji ya vitamini (vitastress)

WIKI YA TATU

Wape doxycol au otc 20% au anflox gold au fluban na amprolium,vitalyte au vitastress,molasses kwa siku 5-7

WIKI YA NNE

Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dozi kubwa ya vitamin (vitastress)

WIKI YA TANO

Hakikisha kuku wanakuwa katika dozi ndogo ya vitamin (vitastress)

WIKI YA SITA

Wape kuku maji ya vitamin asubuhi na matupu jioni

WIKI YA NANE
· Wape kuku chanjo ya ndui
· Dawa ya minyoo (piperazine au levamisole)
· Vitamin (supervit layers)
· Walishe grower mash hadi miezi 3 na nusu na tumia layer mash wakifika miezi 4 kamili
· Pia hakikisha wanapata chakula chenye ridocox hadi wanapoanza kutaga, pia kumbuka kuwapa majani

WIKI YA KUMI NA MBILI

Chanjo dhidi ya Newcastle (rudia kila baada ya miezi mitatu) kwa masaa mawili kasha wape maji ya vitamin

WIKI YA KUMI NA SITA

Kata midomo kisha wape neoxyvital kwa siku 3-5 na pia anza kuandaa viota kwa ajili ya kutagia mayai

WIKI YA AROBAINI NA NANE

Wape virutubisho vyenye kuongeza wingi wa mayai kama vile G.L.P (kilo moja kwa kila 50 za chakula wiki ya kwanza na nusu kilo kwa wiki zinazofuata) na vitamin

WIKI YA HAMSINI NA MBILI

Chagua kuku wasio na dalili za kutaga kabisa, wenye magonjwa sugu na wenye tabia zisizofaa wauze ili kupunguza gharama

WIKI YA SABINI NA MBILI

Tumia V-RID kusafisha mabanda ili kuua vijidudu. Pia weka maji ya dawa hii kwenye kusafisha miguu (footbath) ili kuhakikisha udhibiti wa vijidudu (biosecurity) na kwamba vifaranga wanowekwa hawaathiriwi na vijidudu hivyo kwa lengo la kuepuka magonjwa

WIKI YA TISINI NA SITA

Ondoa kuku wote waliozeeka kwa ajili ya batch mpya ya vifaranga

HITIMISHO

Kwa maswali na maelekezo zaidi usisite kuwasiliana name kwa maelezo zaidi

Imeandaliwa na Doctor of veterinary medicine

Phone: 0712784472

theriogenology
KILA HATUA NITAKAYOPITIA KAMA MFUGAJI

UPDATE 20TH FEB 2015

Habari za masiku wadau na heri ya mwaka mpya.
Napenda kuwaletea mrejesho kama nilivyoahidi.

Kwakweli changamoto nimekumbana nazo nyingi sana. Kama sio roho ngumu ningeacha kufuga.

Kuku wangu wana week 40 sasa na walianza kutaga at 18 weeks exactly.

Changamoto ya 1 ni magonjwa. Kuku wangu wameugua sana typhoid na mafua. So far wameshakufa over 100 layers.
Kitu nilichokosea ni kutowachanja typhoid na mafua. Sababu nilishauriwa kuwa typhoid is not common na kama wakipata inatibika. Kumbe wapi typhoid inatibika lakini inatabia ya kujirudia.

2. Joto pia liliua sana kuku. Kutokana kwamba niliwaweka juu sana karibu na bati. Sasa ivi nimewashusha na mambo yanaenda vizuri.

3. Soko la mayai lilisumbua sana. Wakati kuku walianza kutaga mwezi wa 10 bei ya mayai ilishuka sana na hata kuuza ilikuwa shida. Hapa watu waliuza sana kuku. Kwakweli nilipambana kufa na kupona nikafaulu kupata walau chakula cha kuku. At this point walikuwa wanakula 80, 000 per day. Iyo ni chakula tu. Mwezi wa kwanza soko lika improve ndio kidogo kafaida nikakaona.

So far napata tray 22 -25 per day. Faida kwa mwezi napata angalau 1.5m. Na hapa kuku wamekufa sana.

Nilichojifunza ni kwamba next time ntachukua mbegu tofauti. Maana inaelekea hawa nilionao either parent stock yao ilikuwa na matyphoid au ni mbegu tu ndio dhaifu kwa magonjwa.
Always hakikisha kuku wako wanapata chanjo zote. Utaserve hela nyingi sana kwenye madawa.

Nakaribisha maswali

Mimi ni mdau mpya katika fani ya ufugaji. Baada ya kufanya utafiti kwa mda mrefu kupitia hapa JF na kwa wafugaji wazoefu nimeamua kuanza na kuku wa mayai yaani layers.

Kwanza kabisa nilianza kujenga banda kwa kufuata maelekezo ya wataalamu. yaani layers wanahitaji ventilation ya kutosha. banda la layers linashauriwa kujengwa kwa kupandisha tofali 2 then chicken wire mpaka juu. inashauriwa squire metre 1 kwa layers 5.

sasa basi mi nimeanza na layers 1000. ivi ninavyoandika wamefikisha siku ya nne. kwakweli nashukuru Mungu so far wanaendelea vizuri na wamechangamka fresh tu.

Siku ya kwanza walipofika, niliwafikishia kwenye banda ambalo nililiandaa kwa kuweka chokaa kwenye sakafu, then maranda ambayo yamekauka vizuri na kuchujwa vumbi, juu ya maranda nilitandika magazeti. juu ya magazeti nilimwaga glucose ambayo walikuwa wakiidonoa wakati nawaandalia maji.

pia niliweka majiko special ya mkaa kwa ajili ya kuwapatia joto la kutosha, kwa kiasi fulani na banda nimelizibaziba mpaka watakapofikisha week mbili ndio niwafungulie.

pili nikawakorogea glucose gm 100 kwa lt 10 za maji ya uvuguvugu (hii unawapa bila chakula). maji ya uvuguvugu yanasaidia kulainisha utumbo wao kabla ya kuwapatia chakula kwa mara ya kwanza. baada ya masaa mawili niliwabadilishia maji na kuwawekea maji yenye vitamin na dawa kukausha vitovu, hapa niliwapa na chakula.

Dawa ya vitovu(Aliseril) watakunywa for 5 to7 days.

hapo ndio nilipofikia tutaendelea kujulishana kadiri wanavyoendelea.

03/06/14 - Leo ni siku ya tano na vimeshakufa 3. Nimemconsult dr. Akaniambia ni tatizo la vitovu. Amenitoa hofu kwa kusema vifo kwa vifanga kwa idadi mpaka 10 kwa week ya kwanza ni vitu vya kawaida mradi isiwe rate ya kutisha. Despite all that vifaranga wanaendelea vizuri.

Jana tarehe 6/06/14 ambayo ilikuwa siku ya saba, nimewapa chanjo ya new castle ambayo procedure zake, niliwanyima maji for 2 hrs kabla ya kuwapa chanjo. lazima maji yachemshwe alafu yapoe. Then ktk lt 20 nilishauriwa kuweka vijiko 14 vya chakula vya maziwa ya unga baada ya nusu saa ndio unachanganya maji hayo na chanjo. Nikawapa kwa mda Wa masaa2.

vifaranga vyangu vimetimiziza week 3 sasa. samahani siku update kwa mda kidogo, nilibanwa kidogo.
nilichojifunza kwenye chanjo ya kwanza kuku walidonoana sana. niliita mtaalamu akanieleza ni sababu ya stress ya kuwanyima maji for 2 hrs. alishauri next time niwanyime for 1 hr inatosha. nilifanya ivyo kwenye chanjo ya Gomboro na tatizo la kudonoana likatoweka. procedure za kuchanja Gomboro ni kama nilivyofanya kwenye New castle.

siku ya 18 nilishauriwa niwachanje MAREX. huu ni ugonjwa unawapataga layers pale wanapoanza kutaga na ivyo kushindwa kutaga.. kwa kawaida wanatakiwa kupata hii chanjo na anayekuuzia. lakini kutokana na uaminifu mdogo wa baadhi ya makampuni inabidi kutake pre caution. hii wanachanjwa na Dr. kwa kuchomwa sindano ya shingoni.

Nimerudia chanjo ya new castle siku ya 21, procedure ni zilezile.. vifaranga vinakua vizuri. tuendelee kuelimishana.
FAIDA NA HASARA ZA KUKU WA KISASA

Faida
  • Wanaweza kufugwa hata kwenye eneo dogo la uani, mradi uwe msafi mfano kuku 200 kwa banda la mita 3 kwa 5 /6
  • Wakitunzwa vizuri kwa kufuata masharti ya chakula chao hadi kufikia kuuzwa au kutaga wanakufa wachache sana (<5 kwa banda la kuku 200)
  • Wanachukua muda mfupi hadi kuuzwa mfano wa mayai utawalisha miezi 6 wanaanza kutaga na kuku wa nyama ni mwezi na nusu (wiki 6 au 7) kutegemea na uzito utakaotaka. Hivyo ukipishanisha kuku wa nyama kwa wiki mbili kila mwisho wa mwezi una kuku wa kuuza. Na kuku wa mayai kila siku una mayai unauza hadi miezi 18 unawauza kuku wenyewe pia. Hii ni faida kubwa na inaweza kukuwezesha usihitaji mshahara wako. Soko la kuku wa nyama na mayai ni kubwa na linatabirika (bei mara nyingi inajulikana toka unachukua vifaranga)
  • Very tamed... labda ukosee masharti ya dawa na chakula, lakini wa mayai wakianza kutaga ni moja kwa moja, pia ukiwakata midomo mayai yapo salama. Kama nyumba zao ni salama na hakuna wezi wanaoingia sio rahisi kutoka nje na kuibiwa au kutaga mayai nje.
Hasara
  • Inahitaji mtaji: hela ya chakula na dawa bila kukosa, ukiwakosesha chakula au dawa kwa wakati wao utapata hasara kubwa (wanaweza kufa, wakawa viwete, kudumaa wasikue au kutotaga mayai), chakula chao pia ni bei kubwa kama huchanganyi mwenyewe, maji lazima uweke waterguard au chemsha hasa wiki za mwanzo.
  • Wanahitaji umeme au taa ili waweze kula masaa 24 (hata mkaa wakiwa wadogo kama kuna baridi)
  • Nyumba zao ziwe za bati au tofali ili kuzuia unyevu wa ardhini pia sakafu ipigwe plasta, wanahitaji hewa safi hivyo madirisha makubwa hewa itembee. Ziba mianya yote ya mwewe, kunguru, vicheche kuingia kwa kuweka wavu madirishani
  • Kama hufuati masharti ya chanjo na dawa unaweza hatarisha afya za walaji kwakuwa utahitajika kuwatibu wakiugua wiki za mwisho ambapo unawauza. Vitamini pia zinatakiwa zipunguzwe wiki za kuuza kuku wa nyama.
  • Wanahitaji usafi kwenye banda: randa za mbao (saw dusts) zinahitajika ili kuzuia vinyesi visilete ubichi na ubaridi wa floor wanapolala. Kubadilisha hizi randa kila zikilowa ili kuzuia ugonjwa wa mafua.

Kuku wa kienyeji
Faida

  • Ni gharama ndogo kuwatunza: chakula chao ni rahisi, pia wanaweza kujitafutia wenyewe, maji yao pia sio lazima yawe maji salama.
  • Hawahitaji umeme au taa usiku au wakati wa baridi kwa vifaranga, labda uwe umenunua vifaranga na hawakuzalishwa na majike wa kuwafunika usiku
  • Nyumba zao ni rahisi zinaweza kuwa za mabanzi/ mbao au mabati / tofali kutegemeana na uwezo wa mtu
  • wanastahimili magonjwa, hivyo hawahitaji kuwatibia mara kwa mara au kuwapa vitamin (Newcastle tu au chanjo ya mdondo ndio inahitajika)
  • Ni chakula bora ambacho mlaji anaweza kula kila siku bila kuhofia madhara ya madawa au vitamin
  • Ni kama pets katika familia kwasababu wanakua taratibu
Hasara
  • Wanahitaji nafasi kubwa, kwa ajili ya kujitafutia chakula pia kukuwezesha kuhamisha nyumba zao kuzuia vinyesi vyao visiwaletee magonjwa
  • Vifo vingi wakiwa vifaranga (ajali, mwewe, vicheche) magonjwa na ukubwani wezi pia (maana hawafungwi sana pia wanaweza toka nje bila wewe kujua wakaibiwa)
  • Wanachukua muda mrefu hadi kuwatayari kuuzwa, hivyo sio biashara ya haraka haraka. Soko lao linategemea na eneo na bei yake haitabiriki (unaweza kufuga kuchi/jogoo na majike kwa gharama sawa ila kuuza bei tofauti kwani uzito wao hautabiriki hivyo unapokuwa na vifaranga hujui utavuna kiasi gani)
  • Hawatabiriki kuhusu kuongezeka au kuzaliana mfano anaweza atage mayai mengi ukamwacha alalie, kisha siku chache kabla ya kutotoa akayaacha, pia wanakunywa mayai maana hawakatwi midomo.
FAHAMU NAMNA YA KUTENGENEZA CHAKULA, WAANDALIE MAZINGIRA YA JOTO
Kwa jinsi nnavyo ielewa biashara ya kuku, lazma uwe na uwezo wa kutengeneza chakula, uje vizuri yale madawa ya chanjo, uwe umejipanga kuhusu umeme/mkaa kwa ajili ya joto, aina ya vifaranga wakuanza nao coz kunavifaranga kuanzia 750/= mpaka 1250/= kwa jinsi bei inavyokwenda juu ndo ubora unaongeza!

Fanya utafiti wa soko, bei ya kuuzia against matumizi, kwa kuku 1000 watakuwa wanakula mifuko 2 mpaka mi5 kwa siku, na mfuko mmoja ni 27,000/= nadhani. Kama ni kuku wa nyama, hawa huwa wanakua kwa wiki 4 mpaka 5, ila hapa inategemea na jinsi unavyowapa msosi!

Ukiwanyima msosi wanadumaa, ukiwapa msosi vizuri wananenepa kinoma! Ila mchanganyiko wa kwenye vyakula uwe sahihi(dagaa, damu, chokaa, pumba kavu za mahindi, etc) Usimamizi nao unahitajika sana, coz hawa kuku wa nyama huwa wanakula usiku na mchana! Na kabla ya kuwaweka lazma upige dawa(fumigate) banda lote, na vyombo vyao vya maji unatakiwa kuvifanyia usafi kila siku.

Siku wakifika hao vifaranga unatakiwa uwapige glucose kama watakuwa wamechoka ili wapate nguvu, tofauti na hapo utaanza kuingia hasara ya mapema kabisa. Ila wanalipa sana kama utawafuga inavyotakiwa! Soko la kuku haliishi, kila siku demand inaongezeka!

Mshindwe wenyewe!
UFUGAJI WA KUKU NI BIASHARA NZURI, IMENIWEZESHA MENGI

Mimi nilishawahi kufuga kuku na kwa kiasi fulani zimechangia kuniendeleza ki eleimu na kuwasaidia baadhi ya wategemezi - kuku nawakubali.

Ufugaji wa kuku inategemeana unataka wa aina gani (kisasa au Kienyeji) kwa kuku wa kisasa kidogo wanahitaji nguvu ya ziada na umakini wa hali ya juu wakati wakiwa wadogo na wanapokuwa kwa mazao bora. Vile vile kwa kuku wa kienyeji.

Kwa hapa nitatoa ushauri wa ju juu tu kwa kuwa taratibu zote za ufugaji ni nyingi kiasi kwamba kuandika hapa haitatosha, pia inategemeana unaishi wapi yaani maeneo ya baridi sana au joto.

Kwa kifupi, Ukitaka kufuga hasa wa kisasa wa mayai, chukua vifaranga vilivyozaliwa siku hiyo hiyo uanze kuvifuga wewe na si vile vilivyokaa juani kama pale buguruni kwa zaidi ya wiki1 au zaidi. Pia hakikisha unachukua vifaranga kwa mzalishaji ambaye anajali na si mchakachuaji kwa kuwa kama mazlishaji hakuwapa dawa fulani wakati wanataga mayai kuku wa kuzalisha vifaranga, vifaranga vinapozaliwa vinakuwa na ugonjwa wa kuzaliwa nao na vikifikisha miezi 3 vinakufa vyote kwa hiyo ni kuwa makini na utakaponunua vifaranga hivyo.

Ukifikisha vifaranga kutoka kwa aliyekuuzia unatakiwa uvipatie glucose ya kuku (Ya mifugo) na maji ya uvuguvugu kama unaishi mikoa ya baridi kama iringa au mbeya lakini kama dar hayahitajiki ya uvuguvugu. baada ya saa 2 unavipatia vitamini, vitamini hizo zipo za aina nyingi sana madukani kutokana na wazalishaji wengi na zingine inasemekana huwa ni feki inapaswa kuwa makini unaponunua, ila mimi napendelea Bidhaa za kutoka UFARANSA huwa ni nzuri zaidi.

Kwa maelezo zaidi ya ufugaji waweza kumtembelea mfugaji aliye karibu na wewe au hata daktari wa mifugo. Au MTAFUTE mwakilishi wa madawa ya kuku kutoka kampuni inayosambaza dawa za mifugo za LAPROVET, just I google tu, utamjua mwakilishi wa tanzania, ukimpigia simu hana kinyongo atakupa maelekezo ya kutosha.

Hata hivyo ufugaji wa kuku una tesa sana, kama hutafanya mwenyewe ukaajili msimamizi ambaye hayuko makin banda lote litateketea, halafu ukizembea kuwalisha watakonda na mazao hayakuwa mazuri na ndo mwanzo wa kuugua. Ukweli ni kwamba kuku wa kisasa wanakula balaa, yaani kama huna source nzuri ya pesa ya kununulia chakula cha kuku, bora usifuge, watakufilisi na mradi hautakuwa na matunda mazuri, kuku wanakula massaa 24, ila kuna rafiki yangu aliniambia wao kuku wao waliwazoesha kula mchana tu, na usiku walikuwa wakiwazimia taa. ukifanya hivyo utapata afueni, wanakula balaa.

Kwa kuku wa kienyeji ni rahisi zaidi, ukiwapa chakula cha kutosha na chanjo za kueleweka hawatakufa, kamwe na utapata faida nzuri zaidi.

Cha msingi katika ufugaji usizembee kuhakikisha unafuta taratibu zote za kutunza viumbe hawa, usikubali kumwachia mtu usiyemuamini kuwa atafanya unavyotaka na hata kama ni wa kisasa kienyeji jaribu kuwa na utaratibu wa kuwapa chakuala kwa muda fulani fulani na usipitilize hadi wazoee.

Pia usichelewe mpaka waanze kupiga makelele. La kuzongatia kabisa katika ufugaji wa kuku na mazao bora ni CHAKULA CHA KUTOSHA< UKIWEZA HILO HATA MAGONJWA HAYATAKUWA MENGI NA UTAFAIDI UFUGAJI WAKO.

Nawasilisha kama kuna sehemu nimekosea, hayo ni wawazo yangu naomba sahihisho tafadhali.
UGONJWA WA MAFUA YA KUKU NA NAMNA YA KUZUIA
Leo niuzungumzie ugonjwa wa mafua (Infectious coryza)

Mafua ni ugonjwa mojawapo unaoshambulia mfumo wa upumuaji wenye tabia ya kumfanya kuku kutoa kamasi puani,kupiga chafya,kichwa kujaa maji na kuvimba.Ugonjwa huu huwaathiri kuku,bata mzinga na kanga.
Mafua ni ugonjwa unaowapata jamii ya ndege wa umri wote lakini zaidi ni kwa wakubwa.Ueneaji wake ni kwa njia ya hewa na chanzo chake ni ndege wanaougua au waliougua.

KISABABISHI
Mafua ya kuku husabibwa na Kimelea (Bacteria) kiitwacho Haemophilus paragallinum

DALILI ZA MAFUA
Dalili za mafua huanza kuonekana kuanzia siku ya 3-10 toka kuambukizwa.Sehemu zinazodhihirika zaidi ni pua,macho,mapafu,koo na koromeo.
  1. Kuku kuzubaa na kuto makamasi wakati mwingine yenye damu.
  2. Kubadilika rangi ya mapanga(Comb and wattle) na kuwa ya rangi ya bluu
  3. Huvimba macho,hali inayosabababisha kuku kuziba jicho moja na wakati mwingine yote mawili
  4. Kuvimba mapanga na uso
  5. kukosa hamu ya kula na kupunguza utagaji
  6. Kuku kukoroma wakati wa kupumua
  7. Kuhara uharo wenye harufu mbaya hasa kama kuna maambukizi mengine ya vimelea
  8. Vifo ni vichache na kuku hupona baada ya wiki

NAMNA YA KUZUIA
  • Usafi wa mazingira na kuhakikisha hakuna vimelea wanaosababisha ugonjwa huu
  • Kuku wagonjwa watengwe mbali na kuku wazima
  • Hakikisha vifaranga wanaagizwa kutoka kwenye makampuni yanayofuata kanuni bora za ufugaji
TIBA
Mafua ni ugonjwa unaotibika mfugaji unaweza kumwona afisa mifugo aliye karibu nawe ili akuandikie dawa sahihi ya kutumia.
CHANJO NA KINGA DHIDI YA MAGONJWA MBALIMBALI YA KUKU WA MAYAI, NYAMA (BROILERS) AU CHOTARA (CROSSED BREED)


UMRI



KATIKA



SIKU/WIKI


AINA



YA



UGONJWA


CHANJO/KINGA


NJIA YA UTOAJI



WA



DAWA


Mara baada ya kutotolewa


Marek's


HVT


SINDANO(Kiwandani)


1


Kuondoa uchovu


Glucose


Maji


2-6


Pullorum


Trisulmycine,Trimazine 30%au Cotrim+Vitalyte,Amin'total au Broiler booster


Maji


7


Mndondo


Newcastle vaccine(Lasota)


Maji


14


Gumboro


Gumboro (Bursine vaccine-IBD)


Maji


16-20


Coccidiosis


Trisulmycine/Trimazine/Esb3 30%+Dawa yoyote ya Vitamin


Maji


21


Mdondo


Newcastle vaccine(Lasota)


Maji


23-27


Kinga dhidi ya magonjwa mengi


OTC 20%+Dawa ya vitamin yoyote


Maji


28


Ndui


Fowl pox vaccine


Sindano kwy mabawa


35-39


Mafua
Coridix,Tylosine75%+dawa yoyote ya vitamin

Maji


56-60


Kinga dhidi ya magonjwa mengi


OTC 20%+Dawa yoyote ya vitamin


Maji


WIKI YA 12


Taifodi(Fowl typhoid)


Gentamyzine sulphate


Sindano


Wiki ya 13


Minyoo


Pipperazine cirtrate+Dawa yoyote ya vitamin


Maji


WIKI YA 15


Ukataji midomo


Dawa ya vitamin itumike baada ya zoezi


Maji


WIKI YA 16


Kipindupimdu (fowl cholera)


OTC 20% Injection


Sindano


WIKI YA 17


Mafua (Infectious coryza)


Tylosine Injection


Sindano


WIKI YA 18


Taifodi(Fowl typoid)


Gentamizine sulpate


Sindano





MUHIMU

· Dawa ya minyoo irudiwa kila baada ya miezi 3 toka ilipotolewa awamu ya kwanza .
· Dawa ya mdondo irudiwa kila baada ya miezi 3 toka ilipotolewa siku ya siku ya 21.

KIASI CHA CHAKULA ANACHOHITAJI KUKU KUANZIA WIKI YA 1 HADI
MWISHO WA UTAGAJI WIKI YA 80



AINA
YA
CHAKULA
CHICKS'
STARTER
GROWERS'
MASH


LAYERS'



MASH
UMRI/
WIKI
0-8 9-20

21-80
CHAKULA/
KUKU
2kg 6kg 52kg
CHAKULA/
KUKU 500
1000kg 3000kg 52kg
MIFUKO@
50Kg/KUKU 500
20 60 520

MUHIMU
· Kuanzia wiki ya 18-20, kuku wanapaswa kupewa chakula cha Growers kilichochanganywa na Layers.
HATUA KWA HATUA UFUGAJI WA KUKU BORA WA NYAMA (BROILER)

Lengo la makala hii ni kukuwezesha wewe mkulima kupata kuku wa nyama wenye uzito sahihi kukuwezesha wewe kupata faida. Hivyo basi wewe kama mfugaji ni vyema ukajua ya kwamba wiki mbili za mwanzo katika uleaji wa kuku wa nyama ni muhimu sana na hivyo yakupasa kuwa mwangalifu.

★ Mambo ya kuzingatia kabla vifaranga wako hawajafika kwenye shamba

Banda la kuku, mazingira yanayolizunguka na vyombo vyote vilivyotumiwa kwa batch iliyopita yapaswa kusafishwa vyema kwa maji safi na dawa ili kuua vimelea ambavyo vinaweza sababisha magonjwa.

Hakikisha sehemu ya kuwekea vifaranga (brooding area) linapashwa na joto saa limoja kabla ya vifaranga kuingia ndani ya brooding area.

Kwa matokeo chanya na yenye faida vifaranga vyapaswa kufikishwa kwenye banda haraka iwezekanavyo na kama inawezekana wapewe chakula muda huo huo.

Kamwe usisafirishe vifaranga kwa kutumia buti la gari mara nyingi vifaranga husafirishwa wakiwa wamewekwa kwenye seat ya gari ambapo watapata hewa ya kutosha na kuepuka stress.

Nafasi ya vifaranga inatakiwa kuwa vifaranga kumi kwa mita square moja (10bird/1m2) epuka kuwajaza kuku wengi katika eneo dogo.

Mambo ya kuzingatia baada ya vifaranga kufika eneo la shamba

Mara wafikapo tu vifaranga wanatakiwa kuondolewa kwenye box mara moja. Unapowachelewesha ndani ya box utawafanya kuku kuwa na stress na hivyo kupelekea vifo au kuku kutokua vizuri.

Kwa siku saba za mwanzo wape mwanga kwa masaa23 ili kuwawezesha vifaranga kuzoea mazingira mapya na kuwafanya wao kula chakula.

Wape maji na chakula baada ya vifaranga kuingia bandani na hakikisha unaongeza vitamin kwenye maji au glucose kabla ya kuwapa hao vifaranga.

Hakikisha unapanga vyema vyombo vya kulia (feeders) na vyombo vya maji (drinkers) katika mpangalio ambao utawawezesha vifaranga kula na kunywa maji bila kuapata shida.

★ JOTO

Nunua thermometer (kipima joto) na kiweke katika urefu unaozidi vifaranga kidogo lakini iwe mbali na heater or chanzo chochote cha joto.

Rekodi joto la kila siku kwa kawaida joto sahihi la vifaranga linapaswa kuwa kati ya 40-41 degree centrigrade. (na njia sahihi ya kupima joto la vifaranga chukua miguu ya vifaranga na uweke katika shavu au shingo lako ukisikia miguu inajoto jua vifaranga wapo kwa joto sahihi lakni ukisikia miguu ni ya baridi basi jua ya kwamba vifaranga wanahitaji joto zaidi na hivyo unashauliwa kuongeza joto).

Joto ni muhimu sana katika ukuaji wa vifaranga kwa wiki ya kwanza na hivyo ni vyema kulifuatilia kila siku kuepuka vifo visivyotarajiwa.

★ RATIBA MWANGA

Angalia jedwali katika picha hapo chini

Unashauriwa kuwapima uzito vifaranga/kuku wako kila wafikishapo siku ya 7,14,21,28 na 35kwa kutumia digital balance

★ MAJI

Mabadiliko yoyote katika unywaji wa maji ni njia sahihi au kihairishi moja wapo ya kwamba maji huvuja, kuna tatizo katika chakula au magonjwa. (Kuku kutokunywa kielezo tosha ya kwamba kuku wako wana shida).

Kwa kawaida inatakiwa drinkers 4 kwa kuku 100 na hakikisha maji ni masafi na salama na yanapatikana katika banda kwa masaa yote 24 na jua ya kwamba upungufu wa maji hupelekea kuku kudumaa.

★ CHAKULA

Chakula kinapaswa kuwekwa katika tray za mayai zilizo safi na salama, gunia or magazeti kwa siku saba za mwanzo kuwawezesha vifaranga kula chakula na baada ya siku saba taratibu anza kuwawekea chakula feeders.

Kwa kawaida inashauriwa kuweka tray 4 za chakula kwa vifaranga mia moja. (na hii inafaa kufiti eneo la 50% tu la brooding area).

Kwa feeder za kawaida inashauriwa inapaswa kuwa feeders 3 kwa kuku 100, na hakikisha chakula kinahifadhiwa sehemu salama mbali na mwanga, majimaji na panya. Epuka kuwalisha vifaranga chakula ambacho kina unyevu unyevu au fangasi wa chakula.

Ili kufahamu kama vifaranga wako wanakula chukua vifaranga 5 kama sampuli waangalie baada ya masaa8 then masaa 24 kama wamekula nah ii hufanya kwa kugusa mfuko wa chakula taratibu ukikuta mfuko wa chakula uko umetuna na unagusika jua ya kwamba wamekula na kinyume ya hapo ni kweli pia.

★ AINA YA CHAKULA KWA VIFARANGA

a) Chick starter

Wape 0.5kg kwa kifaranga kimoja kikiwa katika mfumo wa pellet kwa muda wa wiki 2

b) Grower

Wape 1.5kg chakula cha ukuaji kwa vifaranga kikiwa katika mfumo wa pellet kwa muda wa wiki 2

c) Finisher

Wape 1.5kg chakula cha umaliziaji kwa muda wa wiki mbili kabla ya kuwachinja au kuwauza.

★ CHATI YA ULISHAJI WA KUKU BROILER

Angalia katika jedwali hapo chini

ZINGATIO: Jedwali hili lipo applicable kwa broiler waliokuzwa kwa wiki 6 pekee kwa wale wanaowatoa ndani ya wiki tano gharama za uendeshaji pia zinapungua.

★ BROILER TIPS

a) SIKU 1-5

Wape glucose na mchanganyo mmoja wapo kati yah ii ifuatayo;
Neoxyvital au otc plus na typhorium au trimazin
Fluban na vitamin kama vile broiler boost au aminovit au supervit broiler au vitalyte

CHAKULA

Weka vigostart ambayo ina ridocox kwenye chakula, kilo moja kwa mfuko kuanzia wiki ya kwanza hadi nne ili kuzuia coccidiosis, baada ya kuacha endelea kutumia ridocox 200g/tani kwa kuzuia coccidiosis hadi wiki 1 kabla kuwauza kwa nyama.

★ SIKU YA 6

Vitamini (vitastress)

★ SIKU YA 7

Chanjo ya newcastle masaa mawili tu, halafu endelea na maji ya vitamin (vitastress)

★ WIKI YA PILI

Chanjo ya gumboro masaa wawili tu, halafu endelea na vitamin (vitastress)

★ WIKI YA TATU

Wape doxycol au ctc 20% au anflox gpld au fluban na amprolium,vitalyte au vitastress,molasses kwa siku 5-7

★ WIKI YA NNE

Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dozi kubwa ya vitamin (vitastress/vitalyte/broiler boost/supervit broiler)

★ WIKI YA TANO

Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dozi ndogo ya vitamin (vitastress/vitalyte/broiler boost/supervit broiler)

★ WIKI YA SITA

Wape kuku maji ya vitamin asubuhi na matupu jioni

Na baada ya hapo kuku wako watakuwa wako tayari kuingia sokoni kwa ajili ya mauzo

★ HITIMISHO

Na imani kwa muongozo huo hapo juu utakuwa msaada mkubwa kwa wale ambao wangependa kuanzisha project ya kuku wa nyama na pia kwa wale wenye project hiyo.

Kama upo na uhitaji wa muongozo bora wa kuku wa mayai na pia formular za kutengeneza chakula cha Kuku ili kuepeuka gharama zaidi basi usisite kuwasiliana nasi nasi tutaitikia wito wako

Kwa maswali na msaada zaidi usisite kuwasiliana nami
C.E.O ( JMVC)
464bd28e64ec39af880e0018369f467d.jpg
0ade42736bc1cdb649c97aa62c435d78.jpg

Dr : Theriogenology
Phone : +255686236365 (whatsaap)

 
Coaster mzee mfuko mdogo! hapo parefu kidogo mzee. 40m kwa mwajiriwa ni parefu kidogo.
 
Mkuu ulishawai kufuga kuku, japo 50?

Maana kama ni wale broilers wakipata ugonjwa unaweza kupata presha, tena kama pesa ndo za FINCA, itakula kwako. Bora kuku wa mayai, ila ndio hivyo uwe na mtaji mnene coz wanakula kwa miezi 5-6 ndo waanze kutaga mayai!
 
Hapo sawa ila idea ya kusubili mpaka upate 40m hapana ilikuwa haivutii (there waz no growth orientation), swahiba karibu katika kada hii ya ujasiliamali hata hivyo si lazima uache kazi ndoo uingie kwani jambo zuri na la busara katika ujasiliamali ni kuhakikisha unamiliki mtandao ambao utakuwa unakuingizia fedha hata kama upo kwenye machela, mathalani wewe umeliona hilo na kutaka kujikita ktk kuku. Good idea, and for further info just ni PM.
 
Kuku ni biashara nzuri sana lakini inabidi uwe mjanja, kwanza jifunze kutengeneza chakula cha kuku mwenyewe
usiwe unanunua. Pili usiwe mbahili, hakikisha wanakula vizuri na madawa ya kupulizia kwenye mabanda unatumia
anza na kuku 2000.

Good luck.
 
Kuku ni biashara nzuri sana lakini inabidi uwe mjanja, kwanza jifunze kutengeneza chakula cha kuku mwenyewe usiwe unanunua. pili usiwe mbahili. Hakikisha wanakula vizuri na madawa ya
kupulizia kwenye mabanda unatumia anza na kuku 2000.

Good luck.

Well said, ni sawa kabisa, kujifunzia unaweza anza na cha kununua, ila faida hamna, tengeneza chakula mwenyewe, hakikisha usafi wa vyombo na banda, zuia ubichi bandani, hakikisha wakiumwa tu, watenge ukianza kusitasita ndo anavyosema huyo banda zima linakwisha.

Unaweza fuga kiasi chochote ila as a precaution nakushauri weka 200 banda moja kwa kuanzia ila pata ushauri wa vipimo per sq mita.
 
Biashara ya kuku poa. Ila kwa wafanyakazi, nawapa ushauri wa bureeeeeeeee, msifuge kuku. Endeleeni tu na kazi zenu, jioni na weekend mkapumzika? Ila muwe na bajeti. Siyo mtu unapata laki 3, unataka kukimbizana na watu kama sisi-kwenye pombe upo, gari unataka, wanawake wewe.Headache za nini!?
Yaani umenichekesha kweli. Unajua umenigusa na hapo kwenye Red! Huo ndo ukweli, lakini sisi wafanyakazi ndo tunajazaga Bar mida ya jioni.
 
Mlachake, una experience kwenye ufugaji kuku? kama huna basi, kuanza na kuku 1000 utakuja kulia. Na kama ni lazima uanze na kuku wengi,basi usiwe na mkono wa birika, kwamba usiwe bahili.

Lazima utafute part time animal scientist ambae atakuwa mara kwa mara anakushauri suala zima la poutry management!!! aidha,usiwe bahiri, hususani kwenye feeding!!! poultry keeper wengi wana-collapse kv wanataka kubana matumizi kwenye chakula---manake wale jamaa wanafukia ile mbaya.

In order to have productive layers or broilers, lazima kwenye masuala ya misosi wajiachie!!! and even more important, especially kama ni kuku wa mayai, tenga bajeti ya chakula pembeni na usiichezee kwa kitu kingine chochote kile, iwe pale ready for feeding!! Kama utapata mtaalamu, akakupa techinques za kutengeneza chakula itakuwa more wise kwako, kwavile feed cost ipo juu sana.

BUT be careful, usi-opt tu kutengeneza chakula chao wakati feed chemistry haunayo!!! kama ni wa mayai, badala ya kuanza kutaga after 5 ro 6 months, wataanza after 8 months!!!Kama unazani hutaweza kufanya mixing vizuri, u better ukajilipue kwenye vyakula vya madukani ambavyo ni very expensive- but don' worry, bei hiyo haitakufanya upate hasara, but itapunguza faida!! na kitu kingine muhimu, don buy day old chicks mitaani, utakuja kulia!!!hizo ni few hints, but the project, inalipa wangu!!!

Mengine yote, unaweza kushauriwa na animal scientist, but the first good strategy --- tafuta kijana ambae tayari ameajiriwa kwenye suala zima la utunzaji kuku -- mchomoe anakofanya kazi na mpe mshahara mkubwa zaidi, na mpangie room very close na yalipo mabanda yako!!! uki-opt kujenga annex ya kukaa poultry keeper, itakuwa ni more productive idea! wish u all the best
 
Mradi wa kuku ni mzuri haswa pale ambapo unakuwa na uzoefu wa jinsi ya kuwatunza na kufuatilia soko lake. Kwa mtizamo wangu naona kama unapendelea zaidi kuku wa nyama ambao kiasi fulani ni wagumu kuliko kuku wa mayai.

Ni muhimu ukiangalia yafuatayo kwa ustawi wa kuku wa nyama.

1. Kuwa na banda zuri lenye hewa ya kutosha pamoja na joto la kutosha (unaweza kupata vitabu kutoka kenye veterinary mbali mbali). Banda ni wastani wa mita 4 kwa 4 kwa kuku 200 wa nyama au 100 wa mayai. Hakikisha banda ni safi na umelipulizia dawa kabla ya kuingiza kuku (unaweza kutumia detto).

2a. Kwa mtu unaeanza ni vizuri kutumia chakula cha kiwandani kwa ubora kwani mara nyingi vyakula vya kujitengenezea vinaweza kuwa ma upungufu au kutengeezwa katika mazingira yasiyo mazuri na hatimaye kuwa na matokeo duni. Kumbuka wanahitaji vakula veyenye virutubisho tofauti kulingana na umri (mfano starter & finisher kwa broiler)

2b. Hakikisha wanapata chanjo ya newcastle wiki ya pili kwa kukuwapya utakaowaleta. Ni muhimu sana. Pia viatamini na madini kama utakavyoshauriwa na watalamu wa mifugo

3a. Kama una uwezo mzuri ni vizuri kufuga kwa awamu. Mathalani wapishane kwa wiki 2, (yaani unaingiza kukuwapya kila baada ya wiki mbili). Hii inakupa nafasi nzuri haswa kupunguza gharama za malisho na nafasi, kwani kadri wanapokuwa ndivyo unavyoongeza nafasi ya banda. Kumbuka broiler.

3b. Hakikisha kuna vyombo vya chakula na maji vya kutosha. Kuku wa nyama hawahitaji kwenda umbali mrefu kutafuta maji, na viwe na maji pamoja na chakula wakati wote.

3c. Hudumia kuku wadogo kwanza, ndipo umalizie kwa wakubwa. Usafi ni muhimu sana. Kuwe na masodasti na hakikisha hakuna unyevu unyevu ili wasipate maambukizo ya magonjwa ya baridi.vifo vingi sana huweza kutokea. Ni vizuri ukahakikisha kuwa hakuna kuku wa kienyeji, kwani mara nyingi huwa chanzo cha magonjwa.

4. Soko ndio kichaa kikubwa katika biashara ya kuku wa nyama, na faida yote hupotea baada ya kukomaa endapo soko linakosekana. Jiandae vyema kama ikiwezekana baada ya kufikisha uzito stahili (baada ya wiki 5-6) unawachinja wote na kuwauza au kuwahifandhi ndani ya jokofu na kuwauuza taratibu.

Baada ya hapa unaweza kuangalia nafasi yako ya kukuwa na kuwa uzoefu kupanua biashara. Ushauri wa wataalamu ni muhimu sana kufanikisha malengo, ila pia kumbuka ubabaishaji ni mwingi Afrika!
 
Mkuu tazama hizo picha hapo chini;

Nilikuwa mmikoa ya kusini just three weeks ago, tutatembelea banda la mkulima mmoja na kuona jinsi alivyojikwamua kwa ufugaji kuku wa kienyeji. Alianza kufugia kwenye banda la kupikia, then sasa amejenga banda jipya, anafuga kwa kutumia njia bora zaidi kuku wale wale wa kienyeji. Kwa hivyo haihitaji kuanza na maelfu ya kuku, bali kidogo kadri unavyoweza, kikubwa ni kuhakikisha unawapatia huduma bora zikiwamo chakula na madawa.

Cheers..!

DSC04282.JPG
DSC04286.JPG
 
Mradi wa kuku ni mzuri haswa pale ambapo unakuwa na uzoefu wa jinsi ya kuwatunza na kufuatilia soko lake. Kwa mtizamo wangu naona kama unapendelea zaidi kuku wa nyama ambao kiasi fulani ni wagumu kuliko kuku wa mayai.

Ni muhimu ukiangalia yafuatayo kwa ustawi wa kuku wa nyama.

1. Kuwa na banda zuri lenye hewa ya kutosha pamoja na joto la kutosha (unaweza kupata vitabu kutoka kenye veterinary mbali mbali). Banda ni wastani wa mita 4 kwa 4 kwa kuku 200 wa nyama au 100 wa mayai. Hakikisha banda ni safi na umelipulizia dawa kabla ya kuingiza kuku (unaweza kutumia detto).

2a. Kwa mtu unaeanza ni vizuri kutumia chakula cha kiwandani kwa ubora kwani mara nyingi vyakula vya kujitengenezea vinaweza kuwa ma upungufu au kutengeezwa katika mazingira yasiyo mazuri na hatimaye kuwa na matokeo duni. Kumbuka wanahitaji vakula veyenye virutubisho tofauti kulingana na umri (mfano starter & finisher kwa broiler)

2b. Hakikisha wanapata chanjo ya newcastle wiki ya pili kwa kukuwapya utakaowaleta. Ni muhimu sana. Pia viatamini na madini kama utakavyoshauriwa na watalamu wa mifugo

3a. Kama una uwezo mzuri ni vizuri kufuga kwa awamu. Mathalani wapishane kwa wiki 2, (yaani unaingiza kukuwapya kila baada ya wiki mbili). Hii inakupa nafasi nzuri haswa kupunguza gharama za malisho na nafasi, kwani kadri wanapokuwa ndivyo unavyoongeza nafasi ya banda. Kumbuka broiler.

3b. Hakikisha kuna vyombo vya chakula na maji vya kutosha. Kuku wa nyama hawahitaji kwenda umbali mrefu kutafuta maji, na viwe na maji pamoja na chakula wakati wote.

3c. Hudumia kuku wadogo kwanza, ndipo umalizie kwa wakubwa. Usafi ni muhimu sana. Kuwe na masodasti na hakikisha hakuna unyevu unyevu ili wasipate maambukizo ya magonjwa ya baridi.vifo vingi sana huweza kutokea. Ni vizuri ukahakikisha kuwa hakuna kuku wa kienyeji, kwani mara nyingi huwa chanzo cha magonjwa.

4. Soko ndio kichaa kikubwa katika biashara ya kuku wa nyama, na faida yote hupotea baada ya kukomaa endapo soko linakosekana. Jiandae vyema kama ikiwezekana baada ya kufikisha uzito stahili (baada ya wiki 5-6) unawachinja wote na kuwauza au kuwahifandhi ndani ya jokofu na kuwauuza taratibu.

Baada ya hapa unaweza kuangalia nafasi yako ya kukuwa na kuwa uzoefu kupanua biashara. Ushauri wa wataalamu ni muhimu sana kufanikisha malengo, ila pia kumbuka ubabaishaji ni mwingi Afrika!

Mkuu naona shule hapo imetulia!

Lakini mbona mnazungumzia haya makuku ya kisasa tu? Je, ufuguja wa kitaalam wa kuku wa KIENYEJI unakuwaje? Kumbuka hawa nao wana soko zuri sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom