Obi
JF-Expert Member
- Jul 6, 2009
- 374
- 79
Mara nyingi sana tumeshuhudia vurugu na machafuko yaliyopoteza maisha ya watu wakiwepo watoto wagodo wasio na hatia katika nchi zetu hizi za Africa. Machafuko na vurugu hizo yanaambatana na mambo mengi mabaya yakiiwemo ya ubakaji na mauaji ya kutisha sana. Sio hayo tu ni mengi sana yakiwepo ya wananchi wa nchi husika kuwa wakimbizi na wengine kuwa ombaomba na kukosa mwelekeo katika maisha yao.
Vurugu na machafuko hayo yanasababishwa na baadhi ya viongoozi wa nchi husika kung'ang'ania madaraka hata kama chaguzi huru na za haki zikiwa zimefanyika na wananchi kuwachagua viongozi wao wanaowapenda. Mifano ni dhahiri sana. Kwa mfano tumeshuhudia vurugu na machafuko yaliyotokea katika nchi ya jirani Kenya. Uchaguzi umefanyika lakini watu hawataki kukubaliana na matokeo ya uchaguzi huo. Zimbabwe nako mambo ni yaleyale viongozi hawataki kukubaliana na matokeo.
Najiuliza kukataa huko matokeo ni kwa maslahi ya nani hasa? Je ni kwa ajili ya nchi na wananchi wake au ni kwa nini hasa?
Katika utawala wa Dk. Salmin Amour Juma, aliyekuwa Rais wa Zanzibar wa awamu ya tano, walitokea watu na wapambe waliomshawishi kutaka kubadilisha Katiba ya Zanzibar , ili imwezeshe kuendelea kuongoza visiwa hivyo, kwa muhula wa tatu. Hilo lilishindikana. Nakumbuka Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kusema Muogopeni kama ukoma mtu anayetaka kuingia Ikulu, kwa gharama yoyote hata kwa kutoa rushwa, kwani Ikulu ni mzigo mkubwa kwa jamii". Alisema kuwa Ikulu ni tatizo kubwa kwa sababu ukiwaona watu wana njaa, wana shida, wana maradhi na hata matatizo mengine yote, hayo yanakuhusu wewe, kwani hao ni watu wako waliomo katika nchi yako, hivyo kila kinachowasumbua kinakuhusu.
Katiba ni kitu cha kuheshimiwa sana kwa sababu ndio muongozo wa Nchi yeyote katka Dunia hii.
Huku kungangania madaraka kwa baadhi ya viongozi wetu wa kiafrika ni kwa maslahi ya nani? Kuna nini ikulu? Kuna biashara gani zaidi ya kuwasaidia watu?
Mungu Ibariki Taifa letu la Tanzania.
Naomba kuwasilisha