Ni kwa nini TFF wanamuogopa Michael Richard Wambura?.......Mizengwe yote hii ya nini?...

Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,476
4,752
Salama wakuu wangu wapenda michezo....

Kwa muda mrefu nimegundua kwamba TFF ya Leodgar Chilla Tenga imekuwa ikifanya jitihada kuhakikisha kwamba Michael Richard Wambura kwa namna au njia yoyote ile hashiriki shughuli za TFF.......Je tatizo ni nini hasa?.......Wanamuogopa?.......Ni kwa nini mara zote wamekuwa wakimuwekea mizengwe kiasi cha kukataa hata Rufaa zake mara anapoenguliwa katika kugombea uongozi,mfano juzi jina lake lilienguliwa katika kugombea nafasi ya Uenyekiti wa chama cha soka cha mkoa wa Mara na jana alipojaribu kupeleka rufaa yake kupinga uamuzi huo watendaji wa TFF pale Ilala walikataa katakata kuipokea Rufaa hiyo.............Kunani?

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limekataa kupokea rufani ya mgombea nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara (FAM), Michael Wambura kwa maelezo kuwa hakuna mamlaka yenye uwezo kusikiliza shauri lake nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Wambura alisema anashangazwa na hatua ya TFF kwani alifika kwenye ofisi za shirikisho hilo Uwanja wa Karume, Ilala jana mchana kuwasilisha rufani
yake kwa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF lakini alikataliwa.

“Nimekaa kwa zaidi ya saa mbili, najaribu kuwaeleza wapokee rufani yangu lakini hawataki,
inaelekea kuna maelezo kutoka juu wamepewa hawa watu wa mapokezi wasipokee rufani ya
Wambura, inasikitisha sana,” alidai.

Wambura alieleza kuwa baada ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF kumuengua alitaka kukata rufani Kamati ya Nidhamu inayoongozwa na aliyepata kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana.

Juzi Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliondoa jina la Wambura kwa madai kuwa aliwahi kupeleka masuala ya soka mahakamani kinyume na Katiba ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), TFF na FAM.

Akizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alikiri jambo hilo kutokea na
kwamba waliamua wasipokee sababu kulingana na kanuni za TFF, Kamati ya Uchaguzi ndiyo
yenye mamlaka ya mwisho kwa hapa nchini.

Alisema Wambura anaweza kukata rufani kwenye Mahakama ya Rufaa ya Michezo (CAS) iliyopo Lausanne, Uswisi.

Alisema TFF ilizifanyia marekebisho kanuni zake na kuwa chombo ambacho kinaweza kutengua maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ni CAS na si Kamati ya Nidhamu ya TFF.

Hata hivyo, Osiah alisema pamoja na Wambura kuelezwa hivyo aling’ang’ania fomu zake
zipokelewe, lakini si rufani ila iwe kama barua, hivyo akawaagiza wafanyakazi wake kuipokea kama barua ya kawaida na kuwataka wasipokee ada ya rufani.

Lakini Wambura akizungumzia maelezo hayo ya Osiah, alisema ni ya kushangaza na
hayapaswi kutolewa na kiongozi kama yeye kwani sio msemaji wa Kamati ya Nidhamu.

“Mimi nawashitaki TFF, sasa yeye anawasemea Kamati ya Nidhamu, TFF wao wanachopaswa ni kupokea rufani yangu, kisha Kamati ya Nidhamu ndiyo itasema haina uwezo wa kusikiliza.

“Hata mahakamani, kesi inafika kwanza huko hata iwe ya mauaji, inaweza kuanzia mahakama
ya kawaida, baadaye shauri linapelekwa Mahakama Kuu, ila huwezi ukasimama pembeni
ukasema usilete kesi hiyo.
 
Wote wanabaniana tu ulaji. Siiependi TFF (zamani FAT) imekaa kifisadi sana hakuna mianya ya uwajibikaji. Watendaji karibu wooote wako after their own bellies
 
Hawamuogopi bali hawamtaki........namjua Michael vizuri sana toka tukiwa watoto.......a very hard man to please and work with....na system in mkono katika kumbania pia
 
Michael anatakiwa kupeleka malalamiko yake kwenye vyombo vya sheria bila kujali upuuzi wa FIFA wa kuzuia masuala ya michezo kupelekwa kwenye mahakama za kawaida.

Vinginevyo hawatoheshimiana na TFF kamwe.
 
Ni yeye tu na kimbelembele chake alikuja kujikuta ametengeneza maadui wengi.Binafsi namshauri aishi maisha engine nje ya soka.Yeye si ni fundi cherehani bana.
 
He is a criminal, FULL STOP!!! Mbona hujauliza kwa nini kafukuzwa uanachama Simba???
Acha kumpakazia ,mbona RAGE alifungwa jela lakini still amerudi kwenye uongozi wa soka.Hakuna sababu ya msingi kumkataa Wambura halafu matapeli kama Rage,Hasanoo wameruhusiwa kugombea uongozi wa soka.Kwa kifupi Leodgar Tenga ameshindwa kazi TFF alianza vizuri lakini sasa amekuwa hana tofauti na kina Ndolanga.Hata wachezaji wenzake aliocheza nao wanasema jamaa ni mbishi
 
He is a criminal, FULL STOP!!! Mbona hujauliza kwa nini kafukuzwa uanachama Simba???
Ni nani mhalifu kati ya mwizi ISMAIL ADEN RAGE aliyefungwa jela na baada ya kutoka akpewa uongozi wa Moro Utd na baadae Simba?......Ni kwa nini mwizi kama RAGE alipewa fursa ya kugombea uongozi na kupewa lakini WAMBURA ananyimwa?......
 
Ni yeye tu na kimbelembele chake alikuja kujikuta ametengeneza maadui wengi.Binafsi namshauri aishi maisha engine nje ya soka.Yeye si ni fundi cherehani bana.
Kiukweli TFF ya Tenga ni bora hata ya FAT ya Ndolanga......Wanamuogopa WAMBURA kwa sababu wanajua atawabania kwenye masuala ya pesa

TFF ya Tenga ni wezi wa kutupwa,wao wanachoangalia ni pesa tu na si maendeleo ya soka.....Mikataba ya udhamini ni mibovu, ratiba ya ligi inabadilishwa kila uchao......

TFF wao ni PESA mbele maendeleo ya soka NYUMA......

Wanakera kweli
 
Hawa TFF wana nini na Wambura?......Je Leodgar Tenga na Angetile Osiah wanamuogopa Wambura?.....Zengwe lilianzia kwenye uchaguzi wa TFF mwaka 2004,likaja kwenye uchaguzi wa Simba 2010, baadae likahamia kwenye uchaguzi wa FA ya Mara mwaka 2011 na sasa limehamia DRFA........Lazima kuna kitu hapa.....Si bure

TFF yaanza ‘fitna' tena kwa Wambura


na Juma Kasesa

SAA chache baada ya Chama Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kuanika tarehe ya uchaguzi wa chama hicho, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeibuka na kudai kuwa, Katibu Mkuu wa zamani wa Chama Soka Tanzania (FAT), sasa TFF, Michael Wambura, hana sifa za kugombea.
Tayari Wambura, alishaonyesha nia ya kuwania nafasi ya uenyekiti wa DRFA, baada ya kupewa baraka na Kamati ya Rufaa chini ya Profesa Mgongo Fimbo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alisema uamuzi uliotolewa na Kamati ya Rufaa ya Shirikisho hilo, kumrejesha Wambura katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa Mkoa wa Mara (FAM), alikokuwa akiwania nafasi ya uenyekiti, haumhalalishi kuwania uongozi, kwa kuwa mzimu wa tuhuma za kukosa uadilifu na kupeleka masuala ya soka mahakamani bado unamuandama.
Wambura alikatiwa rufaa na mmoja ya wagombea wa uchaguzi wa FAM, Titus Osoro, kwa kile alichodai hakuwa na sifa za kuwania uongozi, ambapo Kamati ya Uchaguzi ya TFF, ilimuengua kabla ya mgombea huyo kukata rufaa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi, ambayo iliitupilia mbali kwa kuwa haikuwa na mamlaka kusikiliza rufaa za masuala ya uchaguzi.
Alisema uamuzi wa Kamati ya Rufaa, kumrejesha Wambura katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa FAM baada ya mgombea huyo kupinga uamuzi wa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi, haujamuondolea tuhuma zilizokuwa zikimkabili awali, ambapo mara mbili ameishazuiliwa kuwania uongozi wa nafasi mbalimbali za michezo ikiwamo ndani ya shirikisho hilo.
Osiah alisema kilichoamuliwa na Kamati ya Rufaa ni kutupilia mbali rufaa ya Osoro dhidi ya Wambura, kwa kuwa haikufuata taratibu za kisheria ambapo mkata rufaa alipaswa kuanzia ngazi mkoa, lakini badala yake alianzia ya taifa, jambo ambalo ni kinyume na taratibu.
Alifafanua kuwa kilichoamuliwa na kamati hiyo ni kumrejesha Wambura katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa FAM, japo kuwa uchaguzi wake ulikuwa umeshafanyika ambapo ilieleza Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilifanya makosa kumuengua mgombea huyo kwa kutumia rufaa ya Osoro ambayo haikuwa halali, lakini siyo kumsafisha tuhuma zilizokuwa zikimkabili mgombea huyo.
Alibainisha kuwa kwa mujibu wa katiba ya TFF, maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ni ya mwisho, hasa kwa uchaguzi unaohusu ngazi ya mkoa na wilaya, isipokuwa kwa uchaguzi wa ngazi ya kitaifa, ambapo Kamati ya Rufaa ndiyo inaweza kuingilia maamuzi ya kamati hiyo.
Katibu huyo alisema katiba inafafanua kuwa Kamati ya Rufaa inasikiliza shauri lisilo la uchaguzi, hivyo uamuzi wake wa kuingilia maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi umeleta mkanganyiko ambapo sekretarieti ya shirikisho hilo imelazimika kuiandikia barua Kamati ya Sheria, Haki na Hadhi za Wachezaji, kuomba ufafanuzi wa kisheria kuhusu muingiliano wa maamuzi wa kamati za TFF.
Kabla ya DRFA kuanika tarehe ya uchaguzi huo ambayo imepangwa kuwa Machi 18, tayari Wambura ameonyesha nia ya kuwania uongozi wa chama hicho, ambacho mwenyekiti wake ni Amin Bakhresa huku katibu akiwa ni makamu wa kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani, hivyo kuonyesha kuanza kupanda kwa homa ya uchaguzi huo.



 
hawa tff wana nini na wambura?......je leodgar tenga na angetile osiah wanamuogopa wambura?.....zengwe lilianzia kwenye uchaguzi wa tff mwaka 2004,likaja kwenye uchaguzi wa simba 2010, baadae likahamia kwenye uchaguzi wa fa ya mara mwaka 2011 na sasa limehamia drfa........lazima kuna kitu hapa.....si bure

tff yaanza ‘fitna' tena kwa wambura


na juma kasesa

saa chache baada ya chama soka mkoa wa dar es salaam (drfa), kuanika tarehe ya uchaguzi wa chama hicho, shirikisho la soka tanzania (tff), limeibuka na kudai kuwa, katibu mkuu wa zamani wa chama soka tanzania (fat), sasa tff, michael wambura, hana sifa za kugombea.
Tayari wambura, alishaonyesha nia ya kuwania nafasi ya uenyekiti wa drfa, baada ya kupewa baraka na kamati ya rufaa chini ya profesa mgongo fimbo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam jana, katibu mkuu wa tff, angetile osiah, alisema uamuzi uliotolewa na kamati ya rufaa ya shirikisho hilo, kumrejesha wambura katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa mkoa wa mara (fam), alikokuwa akiwania nafasi ya uenyekiti, haumhalalishi kuwania uongozi, kwa kuwa mzimu wa tuhuma za kukosa uadilifu na kupeleka masuala ya soka mahakamani bado unamuandama.
Wambura alikatiwa rufaa na mmoja ya wagombea wa uchaguzi wa fam, titus osoro, kwa kile alichodai hakuwa na sifa za kuwania uongozi, ambapo kamati ya uchaguzi ya tff, ilimuengua kabla ya mgombea huyo kukata rufaa kamati ya nidhamu na usuluhishi, ambayo iliitupilia mbali kwa kuwa haikuwa na mamlaka kusikiliza rufaa za masuala ya uchaguzi.
Alisema uamuzi wa kamati ya rufaa, kumrejesha wambura katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa fam baada ya mgombea huyo kupinga uamuzi wa kamati ya nidhamu na usuluhishi, haujamuondolea tuhuma zilizokuwa zikimkabili awali, ambapo mara mbili ameishazuiliwa kuwania uongozi wa nafasi mbalimbali za michezo ikiwamo ndani ya shirikisho hilo.
Osiah alisema kilichoamuliwa na kamati ya rufaa ni kutupilia mbali rufaa ya osoro dhidi ya wambura, kwa kuwa haikufuata taratibu za kisheria ambapo mkata rufaa alipaswa kuanzia ngazi mkoa, lakini badala yake alianzia ya taifa, jambo ambalo ni kinyume na taratibu.
Alifafanua kuwa kilichoamuliwa na kamati hiyo ni kumrejesha wambura katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa fam, japo kuwa uchaguzi wake ulikuwa umeshafanyika ambapo ilieleza kamati ya uchaguzi ya tff ilifanya makosa kumuengua mgombea huyo kwa kutumia rufaa ya osoro ambayo haikuwa halali, lakini siyo kumsafisha tuhuma zilizokuwa zikimkabili mgombea huyo.
Alibainisha kuwa kwa mujibu wa katiba ya tff, maamuzi ya kamati ya uchaguzi ni ya mwisho, hasa kwa uchaguzi unaohusu ngazi ya mkoa na wilaya, isipokuwa kwa uchaguzi wa ngazi ya kitaifa, ambapo kamati ya rufaa ndiyo inaweza kuingilia maamuzi ya kamati hiyo.
Katibu huyo alisema katiba inafafanua kuwa kamati ya rufaa inasikiliza shauri lisilo la uchaguzi, hivyo uamuzi wake wa kuingilia maamuzi ya kamati ya uchaguzi umeleta mkanganyiko ambapo sekretarieti ya shirikisho hilo imelazimika kuiandikia barua kamati ya sheria, haki na hadhi za wachezaji, kuomba ufafanuzi wa kisheria kuhusu muingiliano wa maamuzi wa kamati za tff.
Kabla ya drfa kuanika tarehe ya uchaguzi huo ambayo imepangwa kuwa machi 18, tayari wambura ameonyesha nia ya kuwania uongozi wa chama hicho, ambacho mwenyekiti wake ni amin bakhresa huku katibu akiwa ni makamu wa kwanza wa rais wa tff, athuman nyamlani, hivyo kuonyesha kuanza kupanda kwa homa ya uchaguzi huo.




ndugu yangu;
yote hiyo ni njama tu za tff za kutaka kumzibia wambura. Kwani hata barua ya kumsafisha iliandikwa katibu mkuu wa tff bwana osia. Lkn jana tena huyo isia anajichanganya tena ktk hili suala la wambura. Nafikiri ni mizengwe tu za tff, kwani nchi hii kila kitu kiko hovyo.
 
Back
Top Bottom