Ni kwa nini rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar hapewi nafasi ya kukagua gwaride la muungano?

Rais wa Zanzibar yupo na tunamuona, Jee Rais wa Tanganyika yuko wapi nae japo ahudhurie tu sherehe?

Swali zuri sana kwa magamba wenzako wanaoung'ang'ania muungano. Je siku muungano ukifa Tanganyika rais atakuwa nani?
 
Pindi waznz wanafiki watakapo Jua kuwa CCM wanayoipenda ndio kero number 1 wa muungano na kamwe muungano hauwezi vunjika au kujadiliwa CCM ikiwa Madarakani hapo ndipo watakapogundua kuwa Chadema ndio chama makini kinachowatakia heri ya nchi yao kuliko CUF
 
Ni suala la itifaki tu kwa mujibu wa katiba iliyopo sasa.
Msaidizi wa rais wa JMT ni Makamo wa Raisi, kikatiba anapokuwa hawezi ama kwa ugonjwa au safarini (zisizokwisha kwa huyu wa sasa), Makamo wa Rais ndiye anayefanya kazi zake. Kwa hivyo, kama kuna mtu mbadala wa kukagua gwaride la Muungano, huyu anakuwa makamo wake, sio raisi wa ZNZ wala Waziri Mkuu.

Zamani, wakati nafasi ya makamo wa kwanza wa raisi alipokuwa raisi wa Zanzibar, hilo liliwezekana; lakini kwa katiba ya sasa, raisi wa ZNZ hana uwezo huo.
 
Mkuu Jumakidogo,

Huu mchango wa MAMMAMIA unaeleza vizuri kwa nini Rais wa Zanzibar hakagui Gwaride la Muungano.

Mbali na hilo yale mabadiliko ya kumuondoa Rais wa Zanzibar katika Umakamo wa Rais mimi nayachukulia kuwa ni utapeli, au ndio baba na mama wa kero za Muungano.

Unapoondoa kiungo kikuu cha Muungano(nusu) wa nchi mbili na kumfanya kuwa waziri asiye na wizara maalum inakuwa sio utapeli tu bali ni upimbi pia.

Muungano nusu kwa sababu Muungano ni wa baadhi ya mambo tu ambayo yanaitwa mambo ya muungano.

We wacha tu...magamba wamelikoroga sasa itawabidi walinywe tu. Tunaposikia wazenj wanataka kura ya maoni kuhusu Muungano kabla ya uandikaji wa Katiba mpya ili kuamua kama wanataka muungano na aina ya muungano wanaoutaka. Magamba wanajifanya kuziba masikio.

Magamba bana...ujanja mingi, mbele ............. Interesting scenerio!
 
Mchango wa MAMAMIA nimeupenda sana, lakini tungetaka muungano wa kweli ni pamoja na rais wa Zanzibar kupewa nafasi ya pili ya madaraka. Awe makamu wa rais wa jamhuri ya muungano pia. Unajua hawa jamaa wanapolalamika kuna watu huku wanachukia na kuwashangaa. Lakini wamebanwa kiasi muungano haueleweki na kuonekana wa kisanii zaidi. Huu ni muungano wa ajabu, wana rais. Wana bendera na wimbo wa taifa. Lakini rais puto tu.
 
Ni suala la itifaki tu kwa mujibu wa katiba iliyopo sasa.
Msaidizi wa rais wa JMT ni Makamo wa Raisi, kikatiba anapokuwa hawezi ama kwa ugonjwa au safarini (zisizokwisha kwa huyu wa sasa), Makamo wa Rais ndiye anayefanya kazi zake. Kwa hivyo, kama kuna mtu mbadala wa kukagua gwaride la Muungano, huyu anakuwa makamo wake, sio raisi wa ZNZ wala Waziri Mkuu.

Zamani, wakati nafasi ya makamo wa kwanza wa raisi alipokuwa raisi wa Zanzibar, hilo liliwezekana; lakini kwa katiba ya sasa, raisi wa ZNZ hana uwezo huo.

Maneno yako ni mazuri sana. Unadhani ni kwa nini rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar alipokwa umakamu wa kwanza wa rais.
 
Huwa nashuhudia gwaride la sherehe za kumbukumbu ya muungano likikaguliwa na rais wa jamhuri ya muungano pekee wakati muungano una serikali mbili? Kwa nini rais wa Zanzibar naye asiwe anapewa kanafasi japo ka kukagua gwaride la mgambo tu?

Yeye ni rais akiwa visiwani, akishavuka maji ni waziri kama Nahodha na wengine. Kwani hilo gwaride ni la muungano au smz? Aliapa kama raisi wa smz na pia kama waziri ndani ya muungano. Akija bara yuko chini ya mizengo kayanza, hivyo hawezi kukagua gwaride wakati hata pinda hakagui.
 
Huwa nashuhudia gwaride la sherehe za kumbukumbu ya muungano likikaguliwa na rais wa jamhuri ya muungano pekee wakati muungano una serikali mbili? Kwa nini rais wa Zanzibar naye asiwe anapewa kanafasi japo ka kukagua gwaride la mgambo tu?

acheni kuleta mada za kitoto na kijinga. sababu muungano niw atanganyika ndio wanaoufagilia Zanzibar hawana haja na muungano na ndio maana miaka yooote shehere zinafanyika tanganyika zikienda kufanyika kule kwa kuwa watu wana akili na hawataki muungano wakutotokea watu wengi kusherekea upuuzi huo.
 
Mbona Rais wa Kenya hapewi nafasi ya kukagua gwaride la Muungano wa Tanzania? Zanzibar ni nchi sawa na Comoro tu so hawana haki huku Bara hata kama Wabunge wao wanapewa kuongoza wizara ambazo sio za muungano. Si walifanya marekebisho ya katiba?
 
Back
Top Bottom