Ni kwa nini nguruwe anaitwa kiti moto?

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
740
Nijuze wenye miito, ukweli nami nijuwe,
Nahaha kama mtoto, ninaranda kama mwewe,
Kichwa kinawaka moto, nimejawa na kiwewe,
Nijuze kwani nguruwe, anaitwa kiti moto?

Ewe malenga Mpoto, kihabarishe kijiwe,
Hivi ni neno mpito, mjuzi nani mwanzowe?
Nguruwe hata mtoto, kitimoto tambuliwe,
Nijuze kwani ngurue, anaitwa kiti moto?
 
Hapa mie nakujuza, kitimoto maana yake,
Ulapo nakueleza, lazima na moto wake,
Utamu wake wakaza, kikiwa na moto wake,
Hili ndilo jibu lake, kwa swali lako sikia.

Asili yake ni bongo,likaenda nako Kenya
Uganda wao si bongo, kitimoto kutopenya,
Jina hili si uongo, ni la mpito kupenya,
Hili ndilo jibu lake, kwa swali lako sikia.

Jina limejizolea, umarufu Tanzania,
Umakini elezea, wahitajika sikia,
Yasiwe ni mazoea, unene kuwaingia
Hili ndilo jibu lake, kwa swali lako sikia.
 
nimekusoma nshairi, nao wako udadisi,
utata umeukiri, mzito na si mwepesi,
kujibu bila kiburi, jibu linaloakisi,
si sawa kuita kiti, sahihi ni kitumoto

kiti kikiwa moto nani atakalia,
iwe mrisho mpoto, mie na wewe sawia,
ikiwa ni kitumoto, na joto lote twabwia,

Miss Judith na wewe kumbe ni malenga mahiri...hongera
 
nimekusoma nshairi, nao wako udadisi,
utata umeukiri, mzito na si mwepesi,
kujibu bila kiburi, jibu linaloakisi,
si sawa kuita kiti, sahihi ni kitumoto

kiti kikiwa moto nani atakalia,
iwe mrisho mpoto, mie na wewe sawia,
ikiwa ni kitumoto, na joto lote twabwia,
si sawa kuita kiti, sahihi ni kitumoto

Judi wanipa fukuto, kwa huo wako weledi,
Kumbe ni 'kitumoto', ndiyo yake fuadi,
Tukisema kitimoto, lugha tunaihasidi?
Ninakushukuru Judi, u malenga motomoto.
 
Hapa mie nakujuza, kitimoto maana yake,
Ulapo nakueleza, lazima na moto wake,
Utamu wake wakaza, kikiwa na moto wake,
Hili ndilo jibu lake, kwa swali lako sikia.

Asili yake ni bongo,likaenda nako Kenya
Uganda wao si bongo, kitimoto kutopenya,
Jina hili si uongo, ni la mpito kupenya,
Hili ndilo jibu lake, kwa swali lako sikia.

Jina limejizolea, umarufu Tanzania,
Umakini elezea, wahitajika sikia,
Yasiwe ni mazoea, unene kuwaingia
Hili ndilo jibu lake, kwa swali lako sikia.

Achengula mdadisi, ahsante kwa lako jibu,
Ni moto sio yabisi, umepekua vitabu,
Akujalie mkwasi, utende zako wajibu,
Misi Judi katujibu, 'kitimoto' si halisi?
 
Salam kwako Kashaija, Judi nawe Achengula
Nami ulingoni naja, kitimoto nami nala,

Nauvutiwa lake paja, maini nayo salala,
'Kitumoto' masihala, 'Kitimoto' muhamala.

Achengula amenena, asili yake ni bongo
Kitimoto hata China ,utaikuta si uongo
Sinza Afrika Sana, watu wala kwa usongo,
'Kitumoto' ni uongo, 'kitimoto' ndilo jina.

Juzi nilikula kona, na bibie nyumba ndogo
Starehe niloona, nisingeipa kisogo,
Ikaletwa iliyonona, na kachumbari ya tango,
'Kitumoto' ni uongo, 'kitimoto' ndilo jina.

Judi hapa nakupinga, ''kitumoto' si nguruwe,
Hili lako umetunga, kutoka kwenu Msewe,
Karibu kwetu Ukonga, kilo moja ufungiwe,
'Kitimoto' ndo nguruwe, 'kitumoto' nakupinga.
 
Kiti moto asili yake ni kipindi cha tv,cha dtv kilikuwa kinaendeshwa na pascal mayala...kilikuwa kinaitwa kiti moto....
 
Kiti moto asili yake ni kipindi cha tv,cha dtv kilikuwa kinaendeshwa na pascal mayala...kilikuwa kinaitwa kiti moto....

Na jina hili lilianzia pale mwenge, kama sikosei kulikuwa kunaitwa kwa Ticha (Around 1996 - 1998). Ndiyo sehemu ambayo ilianza kuuza kitimoto commercially in the fashion you see it today.
 
Enyi walaji wa kitumoto ama kitimoto sijuwi naomba msome kitabu cha biblia injili ya marco mtakuta yesu alimlaani nguruwe!!
 
Enyi walaji wa kitumoto ama kitimoto sijuwi naomba msome kitabu cha biblia injili ya marco mtakuta yesu alimlaani nguruwe!!
Soma mwenyewe! Hajawalaana aliwatumia kumponya mgonjwa. Kwa bahati mbaya au nzuri walikuwa karibu na uponyaji huo.

Hakuna dalili Yesu alijali habari za nguruwe; hii ni habari ya kumsaidia na kumponya mtu.
 
na mshindwe na mlegee ninyi mnaonikumbusha kitimoto....mnanifanya niache shughuli a kujenga taifa letu tukufu nikamtafute alipo......mshindwe tena mshindwe....huyo huwa hatajwi mida ya kazi jamani...nasema mshindwe...hata JF nita-SIGN OUT....kwa sababu ya mwanzisha mada....nimesema mshindwe katika ujenzi na uendelezaji wa taifa hili asitajwe popote pale kwani atarudisha nyuma maendeleo....!
ANGALIZO; WAISLAMU,WASABATO & CO.......MSIJE MKALOGWA MKAJARIBU HIYO KITU IACHANE KABISA ILI WALAJI TUZIDI KUWA WACHACHE
OMBI; MNISAMEHE KWA KUTOKUJIBU SWALI....ILA MAELEZO YANAJITOSHELEZA
 
Nyama tamu kupita zote duniani.
 
Salam kwako Kashaija, Judi nawe Achengula
Nami ulingoni naja, kitimoto nami nala,

Nauvutiwa lake paja, maini nayo salala,
'Kitumoto' masihala, 'Kitimoto' muhamala.

Achengula amenena, asili yake ni bongo
Kitimoto hata China ,utaikuta si uongo
Sinza Afrika Sana, watu wala kwa usongo,
'Kitumoto' ni uongo, 'kitimoto' ndilo jina.

Juzi nilikula kona, na bibie nyumba ndogo
Starehe niloona, nisingeipa kisogo,
Ikaletwa iliyonona, na kachumbari ya tango,
'Kitumoto' ni uongo, 'kitimoto' ndilo jina.

Judi hapa nakupinga, ''kitumoto' si nguruwe,
Hili lako umetunga, kutoka kwenu Msewe,
Karibu kwetu Ukonga, kilo moja ufungiwe,
'Kitimoto' ndo nguruwe, 'kitumoto' nakupinga.

mwenzetu msome bosi, hakika yeye kalonga,
katoa yote mikosi, ya kwenu huko ukonga,
kasema siyo halisi, lako ndilo la kutunga,
kitimoto cha ditivi, ulacho ni kitumoto.

nenda kawajuze sinza, ukonga afrika sana,
kuwa wapaswajifunza, kama wataka kunona,
jina lisijewaponza, wapishi oda kukana,
kitimoto cha ditivi, ulacho ni kitumoto.

kitu kikiwa baridi, na kiti kikiwa moto,
kukitema huna budi, shuruti kipashwe joto,
na kiti hutofaidi, heri kalia kokoto,
kitimoto cha ditivi, ulacho ni kitumoto.
 
Enyi walaji wa kitumoto ama kitimoto sijuwi naomba msome kitabu cha biblia injili ya marco mtakuta yesu alimlaani nguruwe!!

Hatukatai wala kubisha kwa Yesu kumlaani Nguruwe na marco kuandika injili na sisi tusome bibilia na tumesoma, ila sisi tunaokula kiti moto kosa letu lipi,kilicho laaniwa ni nguruwe, elewa tofauti ya (mchanganyiko wa mahindi na maharage) na kuwa (makande)........(nguruwe) na (Kiti moto) ni vitu tofauti, KITIMOTO hoyeeeeeeee
 
Ni vile kinavyowekwa kwenye sahani kubwa halafu watu wanaanza kukishambulia, utakuta kikifika mezani watu story zote zinaisha wanaanza kushambulia utafikiri hawajala wiki au wametokea ethiopia. sasa watu wakatafasiri kama huyo mdudu anavyoshambuliwa ni kama anawekwa kiti moto vile
 
Enyi walaji wa kitumoto ama kitimoto sijuwi naomba msome kitabu cha biblia injili ya marco mtakuta yesu alimlaani nguruwe!!

Marko sura ya saba, Yesu kafuta tetesi,
Ukila lishe washiba, haitii unajisi,
Kula nguruwe kibaba, hata bakuli la ngisi,
Kimtokacho mtu ndani, ndicho kilicho najisi.

Yesu akafafanua, mabaya yatoka ndani,
Wivu chuki na umbea, vyote vyatoka rohoni,
Kuiba uzinzi kuua, haviingii tumboni,
Kimtokacho mtu ndani, ndicho kilicho najisi.

Vyakula vyote halali, mwisho vyaenda chooni,
Kupiga mtu kabali, hiyo yatoka moyoni,
Kitimoto na ugali, iweje unilaani?
Kimtokacho mtu ndani, ndicho kilicho najisi.
 
Nijuze wenye miito, ukweli nami nijuwe,
Nahaha kama mtoto, ninaranda kama mwewe,
Kichwa kinawaka moto, nimejawa na kiwewe,
Nijuze kwani nguruwe, anaitwa kiti moto?

Ewe malenga Mpoto, kihabarishe kijiwe,
Hivi ni neno mpito, mjuzi nani mwanzowe?
Nguruwe hata mtoto, kitimoto tambuliwe,
Nijuze kwani ngurue, anaitwa kiti moto?

Yaliwa ikiwa na moto, kwenye kiti huwezi tulia
kwa kuwa lake joto, ni utamuwe asilia
si mkubwa wala mtoto, ya moto hupendelea
kikipikwa kitimoto, kula hutachelea
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom