Ni kwa nini miss judy?

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
740
Judi nijibu swali, kwa nini unaitwa 'Misi'?
Ni mwembamba yako hali, au mrembo tausi?
Ulimi wako asali, wa tamaa kama fisi?
Ni kweli wewe ni 'Misi', nijuze mie rijali.

Pichani sio kigoli, iweje uitwe 'Misi"?
Hulandani nao wali, kuna vitu vinamisi,
Hauna ndoa halali, ni kwanini 'Misi' basi?
Ni kweli wewe ni 'Misi', nijuze mie rijali.

Judi nakiri mkali, usotishwa naye pusi,
Ingawa nakwona mbali, nimekuchunguza nyusi,
Wewe ni mama halali, sioni wako 'umisi',
Ni kweli wewe ni 'Misi', nijuze mie rijali.
 
Kwa mimi ninavyohisi...Bibie Judy afaa kuitwa miss
Jinale hajabadili...bado aweza kuitwa mwali
Ikiwa hajaolewa ....na nyumbani hajatolewa
Usianze kumdiss ...kwa yeye kukunyima kiss!

:)
 
Kwa mimi ninavyohisi...Bibie Judy afaa kuitwa miss
Jinale hajabadili...bado aweza kuitwa mwali
Ikiwa hajaolewa ....na nyumbani hajatolewa
Usianze kumdiss ...kwa yeye kukunyima kiss!

:)

Ee Lizi,
Njoo nikupe ndizi,
Nikuzamishe na mbizi,
Nivute yako shimizi,
Ninyonye kama mbuzi,
Nikutekenye kama sisimizi,
Mwisho niseme 'Ahsante Lizi'.
 
Ee Lizi,
Njoo nikupe ndizi,
Nikuzamishe na mbizi,
Nivute yako shimizi,
Ninyonye kama mbuzi,
Nikutekenye kama sisimizi,
Mwisho niseme 'Ahsante Lizi'.

Kakubugudhi Cheusi,
Punguza zako kasi,
Miss Judy si rahisi,
wala hana wasiwasi,
Lizzy wamtaka kiss,
Upunguze ukakasi?
Hahahahahaha...............
 
Hapa tumeingia kwa mama mkwe,

Sie tusio na tunzi wala vina tutatumia lugha gani wajameni?

Naona MMU imefikia TBS!!!

Babu DC
 
Ee Lizi,
Njoo nikupe ndizi,
Nikuzamishe na mbizi,
Nivute yako shimizi,
Ninyonye kama mbuzi,
Nikutekenye kama sisimizi,
Mwisho niseme 'Ahsante Lizi'.

Ehhhh tafadhali unikome na sio unikomalie...
Nna wangu mpenzi hilo ulitambue...
Usije nizulia zogo nyumbani anitimue..
Au utolewe ngeu polisi ukimbilie...
Utuletee balaa familia kutuvunjia...
Kwa chako kimbelembele vya wenzio kuvizia..

Kwa hisani ya baba mchungaji a.k.a Rev Masa!:)
 
Ehhhh tafadhali unikome na sio unikomalie...
Nna wangu mpenzi hilo ulitambue...
Usije nizulia zogo nyumbani anitimue..
Au utolewe ngeu polisi ukimbie...
Utuletee balaa familia kutuvunjia...
Kwa chako kimbelembele vya wenzio kuvizia..

Kwa hisani ya baba mchungaji a.k.a Rev Masa!:)

Malenga watisha lol!
 
Kwa mimi ninavyohisi...Bibie Judy afaa kuitwa miss
Jinale hajabadili...bado aweza kuitwa mwali
Ikiwa hajaolewa ....na nyumbani hajatolewa
Usianze kumdiss ...kwa yeye kukunyima kiss!

:)
liz mwali kavishwa pete
Rijali tayari kukata utepe
Mwali uzuri wake kama kachori
umbo lake la kati, Mtamu kama jodari
 
liz mwali kavishwa pete
Rijali tayari kukata utepe
Mwali uzuri wake kama kachori
umbo lake la kati, Mtamu kama jodari

Pete gani isooekana hata asitambulike..
Rijali mwenye tamaa haifai aaminike..
Sifa atajimwagia mradi asifike...
Mwenzie atamharibia ili asipendeke...
 
Pete gani isooekana hata asitambulike..
Rijali mwenye tamaa haifai aaminike..
Sifa atajimwagia mradi asifike...
Mwenzie atamharibia ili asipendeke...

Wanachana mashairi,
Hata babu anakiri,
Lizzy nawe una habari,
Mebobea kisharishari.
 
Judi nijibu swali, kwa nini unaitwa 'Misi'?
Ni mwembamba yako hali, au mrembo tausi?
Ulimi wako asali, wa tamaa kama fisi?
Ni kweli wewe ni 'Misi', nijuze mie rijali.

Pichani sio kigoli, iweje uitwe 'Misi"?
Hulandani nao wali, kuna vitu vinamisi,
Hauna ndoa halali, ni kwanini 'Misi' basi?
Ni kweli wewe ni 'Misi', nijuze mie rijali.

Judi nakiri mkali, usotishwa naye pusi,
Ingawa nakwona mbali, nimekuchunguza nyusi,
Wewe ni mama halali, sioni wako 'umisi',
Ni kweli wewe ni 'Misi', nijuze mie rijali.

Jina limeleta zogo, butege umeisha wema,
Mbona hilo bado dogo, kubwa u bado kusema,
Nahisi wewe kigogo, wameza bila kutema,
hata usiwe rijali, sikufichi miye misi

misi ni lao wazungu, sie kwetu mlimbwende,
adimu kama uvungu, hupati hata upinde,
japo uwinde kwa rungu, miye napiga umande,
hata usiwe rijali, sikufichi miye misi

vipi usome picha, watesa yako akili,
wakodoa hadi kucha, eti Judi mkali,
heri kutafuna kucha, ukwepe yangu makali,
hata usiwe rijali, sikufichi miye misi

bado kufikwa umama, hilo nalo naringia,
bikira yangu ni njema, wengi wanaizingia,
heri wajua mapema, japo huwezi sogea
hata usiwe rijali, sikufichi miye misi
 
bUtege kama wewe samaki basi ni ngisi
kila nikikusoma unatema risasi
umemshindwa cheusi
sasa uko kwa misi
uwe mwangalifu lina miba hilo nanasi

kwa nini wajita wasiwasi
na mambo ya kuhisi
utaonekana kama kamasi
mbele ya kadamnasi
uwe mwangalifu lina miba hilo nanasi

hizi wala sio tetesi
ni ukweli usio na kesi
butege huyo kweli ni miss
kwa vipimo vya TBS
uwe mwangalifu lina miba hilo nanasi
 
Jina limeleta zogo, butege umeisha wema,
Mbona hilo bado dogo, kubwa u bado kusema,
Nahisi wewe kigogo, wameza bila kutema,
hata usiwe rijali, sikufichi miye misi

misi ni lao wazungu, sie kwetu mlimbwende,
adimu kama uvungu, hupati hata upinde,
japo uwinde kwa rungu, miye napiga umande,
hata usiwe rijali, sikufichi miye misi

vipi usome picha, watesa yako akili,
wakodoa hadi kucha, eti Judi mkali,
heri kutafuna kucha, ukwepe yangu makali,
hata usiwe rijali, sikufichi miye misi

bado kufikwa umama, hilo nalo naringia,
bikira yangu ni njema, wengi wanaizingia,
heri wajua mapema, japo huwezi sogea
hata usiwe rijali, sikufichi miye misi

Kawadanganye watoto, sio mie kijogoo,
Bikira kwako ni ndoto, ilishafichwa stoo,
Palishafanywa mapito, kabomoa komandoo,
Milioni naitoa, kama hiyo bado njema.
 
Wanachana mashairi,
Hata babu anakiri,
Lizzy nawe una habari,
Mebobea kisharishari.

Babu wakiri lizzy si odinaree
Biggie nae anaona blaki and wairee
Yeye amwaga vesi hana kwere
Hakuna anyeleta kihere here
Lizzy kateleza kwenye list ya wajukuu
Mamb yake yako level yani yapo juu
 
Wanachana mashairi,
Hata babu anakiri,
Lizzy nawe una habari,
Mebobea kisharishari.
Jamani babu jamani mbona wanijaza sifa...
Nisije jaa kiburi kujiona nimefika..
Kwa maneno yako mazuri nikapotoka kabisa..
Kujiona nimewini jitihada kusitisha..
...................................................
Sisahau kushukuru kwakuniona mahiri..
Maneno yako dhahiri yataniongezea mori...
 
Jina limeleta zogo, butege umeisha wema,
Mbona hilo bado dogo, kubwa u bado kusema,
Nahisi wewe kigogo, wameza bila kutema,
hata usiwe rijali, sikufichi miye misi

misi ni lao wazungu, sie kwetu mlimbwende,
adimu kama uvungu, hupati hata upinde,
japo uwinde kwa rungu, miye napiga umande,
hata usiwe rijali, sikufichi miye misi

vipi usome picha, watesa yako akili,
wakodoa hadi kucha, eti Judi mkali,
heri kutafuna kucha, ukwepe yangu makali,
hata usiwe rijali, sikufichi miye misi

bado kufikwa umama, hilo nalo naringia,
bikira yangu ni njema, wengi wanaizingia,
heri wajua mapema, japo huwezi sogea
hata usiwe rijali, sikufichi miye misi

Una kipaji, Let me be your manager.
 
Kawadanganye watoto, sio mie kijogoo,
Bikira kwako ni ndoto, ilishafichwa stoo,
Palishafanywa mapito, kabomoa komandoo,
Milioni naitoa, kama hiyo bado njema.

mbona warusha mazito, maneno yaso hekima,
hata ungetoa bito, bikira huwezichuma,
sitamani hata vito, nalinda yangu heshima,
ubikira wangu wito, kwa ndoa yenye heshima,

tunza zako milioni, au zitoe hisani,
sio kwake sokoni, bidhaa huna yakini,
wawezatupa shimoni, bila wapa masikini
ubikira wangu wito, kwa ndoa yenye heshima,
 
Back
Top Bottom