Ni kwa nini IFM inatunuku shahada (Degree) wakati siyo Chuo Kikuu?

Kwaio wewe chuo kikuu unataka cha namna gani? IAA, TIA, DIT wanatoa degree je unasemaje kuhusu hilo? Acha ukocho.
 
ifm na taasisi nyingine kama tia,ija,iaa zinaruhusiwa kutoa bachelor mbona ,ila hazina uwezo wa kutoa phd tu na mengine mengi ningekueleza lakn jua hivyo kwanza ...sawa?
AU ULIKUWA UNATAKA KUPIGA MAJUNGU MAANA TAASISI NYINGINE UMEZIACHA UMEITAJA IFM TU.
 
ifm na taasisi nyingine kama tia,ija,iaa zinaruhusiwa kutoa bachelor mbona ,ila hazina uwezo wa kutoa phd tu na mengine mengi ningekueleza lakn jua hivyo kwanza ...sawa?
AU ULIKUWA UNATAKA KUPIGA MAJUNGU MAANA TAASISI NYINGINE UMEZIACHA UMEITAJA IFM TU.

IJA hawatoi degree
 
Pia kuna hii ITA wataalam nayo mnaisemaje?

Yap, ni kweli kabisa! Unajua hamna binadamu ambae siyo mbinafsi. Kwa hiyo mtu anachukizwa kuona IFM kwa mfano wanatoa bachelor degree wakati yeye ni faraja kwake kuona ni (UDSM pekee kwa mfano) ndo inatoa degree. Kiukweli miaka kabla ya TCU, kulikuwa na Higher Education Accreditation Council, ambayo iliratibu elimu ya juu. Hii ilikuwa ni watchdog wa Vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu. Baadae ikabadilishwa na kua TCU kwa upande wa Universities na NACTE(National Accreditation Council for Technical Education) kwa taasisi za elimu ya juu. Kimantiki University ni Institute lakini siyo kila Institute ni University. Kwa maana nyepesi ni kwamba University ni mkusanyiko wa taasisi nyingi zenye taaluma mbalimbali kama utakavyoona DIT ni taasisi sawa na CoET zote hutoa wahandisi, lakini School of Journalism ni taasisi pia hutoa taaluma ya wanahabari, sawa na School of Law hutoa wanasheria. Sasa hizo taasisi tatu tu kwa mfano yaani CoET, SMJ, SL na taasisi nyingine zilizotoholewa kutoka kwenye zile zamani zikiitwa Faculty/ vitivo na sasa School, basi zote kwa pamoja ndo unapata University. Kwa hiyo yule aliyesema Institute ni maalum kwa tasnia fulani yuko sahihi.
 
nimekuelewa ndugu hata mimi nilikuwa sifahamu kwasababu ya kutokufuatilia, ila umesema kitu ambacho ni kweli hata mimi ninaingia bachelor ya account tia na sina shaka na chuo maana najua ni chuo kikongwe na account hapo ndio nyumbani kwao
Narubongo na Nyota Yao wamemaliza kila kitu, hizi zinazoitwa institute zinakuwa zipo more specific kwenye fani flani flani ambazo ni chache kama ilivyo CDTI (community development, gender , project planning), IFM (finance and insurance), TIA (finance), Ushirika/MUCCOB (cooperatives) etc ambavyo those days vilikuwa vinatoa Advanced Diploma kabla ya kuvipa hadhi ya kutoa degree baada ya kufanya marekebisho kwenye mambo flani flani hasa kwenye issue ya kuongeza idadi ya wahadhiri waliobobea na katika vyuo vyote IDM mzumbe yenyewe ndio ilifanikiwa kuwa University moja kwa moja kwa kuwa hata kabla ya kuwa university ilikuwa ina course nyingi inatoa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom