Ni kutetea Israel au ni Ubaguzi kama tuujuavyo?

Mwanjelwa

JF-Expert Member
Jul 29, 2007
956
145
US boycotting, Iran starring, at UN racism meeting (Source:UN global conference on racism set to open)

GENEVA – The United Nations' global conference on racism opens Monday without the U.S. or at least seven other countries who have boycotted the event out of concern that Islamic countries will demand that it denounce Israel and ban criticism of Islam.

The administration of President Barack Obama, America's first black head of state, announced Saturday that it would boycott "with regret" the weeklong meeting in Geneva, which already is experiencing much of the bickering and political infighting that marred the 2001 conference in Durban, South Africa.

The Netherlands, Germany and New Zealand announced their boycotts Sunday, while Australia, Canada, Israel and Italy already had said they would not attend.

The French foreign minister said his country's ambassador to Geneva would attend, but would walk out "immediately" if the conference turned into a platform for racist comments against Israel. Britain had earlier said it would attend.

Obama, speaking in Trinidad on Sunday after attending the Summit of the Americas, said: "I would love to be involved in a useful conference that addressed continuing issues of racism and discrimination around the globe."

But he said the language of the U.N.'s draft declaration risked a reprise of Durban, during which "folks expressed antagonism toward Israel in ways that were often times completely hypocritical and counterproductive."

"We expressed in the run-up to this conference our concerns that if you adopted all of the language from 2001, that's not something we can sign up for," Obama said.

"Hopefully some concrete steps come out of the conference that we can partner with other countries on to actually reduce discrimination around the globe, but this wasn't an opportunity to do it," he said.

At the Vatican, Pope Benedict XVI said the conference is needed to eliminate racial intolerance around the world. Asia News, a Catholic news agency that is part of the missionary arm of the Vatican, said of the pope's comment: "The Holy See is distancing itself from the criticisms of some Western countries."

U.N. human rights chief Navi Pillay, who is hosting the conference, said she was "shocked and deeply disappointed" by the U.S. decision not to attend.

She conceded some countries were focusing solely on one or two issues to the detriment of the fight against intolerance, but said it is essential that the issue of racism be tackled globally.

The major sticking points regarding the proposed final U.N. declaration are its implied criticism of Israel and an attempt by Muslim governments to ban all criticism of Islam, Sharia law, the prophet Muhammad and other tenets of their faith.

Iranian President Mahmoud Ahmadinejad — who repeatedly has called for the destruction of Israel and denied the Holocaust — is slated to speak on the first day.

He arrived in Geneva on Sunday evening and met privately with President Hans-Rudolf Merz of Switzerland, the country that represents the diplomatic interests of the United States in the Islamic republic.

The pullout of Germany is significant since it has played a leading role in U.N. anti-racism efforts as a result of its troubled historical legacy. In recent meetings, it has expressed dismay about some governments' attempts to downplay the significance of the Holocaust.

Germany said Sunday that it made its boycott decision after consulting with other European Union nations.

"This decision was not easy," said German Foreign Minister Frank-Walter Steinmeier. "As in Durban in 2001, this conference could be abused by others as a platform for their interests. We cannot accept that," he said.

The bland U.N. draft statement does not mention Israel by name, but it reaffirms the Durban statement and its reference to the plight of Palestinians. That document was agreed after the United States and Israel walked out over attempts to liken Zionism — the movement to establish a Jewish state in the Holy Land — to racism.

Israel and Jewish groups have lobbied hard against Western participation in the meeting, arguing that the presence alone of American and European negotiators would give legitimacy to what they fear could become an anti-Semitic gathering.

On Sunday, Israel's Foreign Ministry thanked the boycotters and predicted the conference would "once again serve as a platform to denigrate Israel and single it out for criticism."

Still, after years of preparations there appears little evidence to validate these fears. The statement of 2001 that is so contentious now was cheered in Israel at the time, as it recognized the Jewish state's right to security.

Regarding its boycott, the Obama administration said it could not endorse any statement that singled out Israel or included passages demanding a ban on language considered an "incitement" of religious hatred. Such calls "run counter to the U.S. commitment to unfettered free speech," said State Department spokesman Robert Wood.

Many Muslim nations want curbs to free speech to prevent insults to Islam they claim have proliferated since the terrorist attacks in the United States on Sept. 11, 2001. They cite the 2005 cartoons of Muhammad published by a Danish newspaper that sparked riots in the Muslim world.

European countries also have criticized the meeting for focusing heavily on the West and ignoring problems of racism and intolerance in the developing world.

___

Associated Press writer Frank Jordans contributed to this report from Geneva.
 
Kwa kuwa wameshiba damu za ubaguzi na dhulma MABEPARI na " wauwaji" hawatakubali kusemwa na kuambiwa "mfanyavyo hivi sivyo" au "kama hamuwezi kuacha khiyana basi walau punguzeni" siku zote, kupitia ubaguzi na udhalimu ndo maendeleo ya MABEPARI hawa yanapatikana, hatawacha kuifanya dunia chungu kwa wanyonge kwani kwa kufanya hivyo kutawakosesha "maslaha" ya mali na fakhari za ulimwengu. Siku zote watakuwa pamoja katka khiyana na hawatakaa pamoja na wale watakaosema "ubaguzi na dhulma kwa wanyonge haufai"
 
Lakini speech ya Ahemedijan umeiona/kuisikia? Nadhani yuko nje kabisa ya mstari. Si sishangai jamaa kususia
 
"Lakini speech ya Ahemedijan umeiona/kuisikia? Nadhani yuko nje kabisa ya mstari. Si sishangai jamaa kususia..."

***********************
Mwanjelwa:
Nimeiona na hakuwa nje ya mstari. Aliishambulia Israel kwa ubaguzi na sera za kibaguzi na za kikatili dhidi ya watu wa Palestina, watu ambao kama hawako ktk makambi ya wakimbizi, basi wako katika magereza ya Israel -- watu ambao ardhi yao imeporwa na waporaji wamejenga ukuta (mithili ule uliokuwapo wa Berlin uliokuwa unalalamikiwa sana na nchi za Magharibi) na kuwalazimisha kupita kwenye crossibng points kwa tabu nyingi na vitambulisho, kama vile ilivyokuwa kwa watu weusi wa Afrika ya Kusini wakati wa utawala wa wabaguzi wa rangi.

Wayahudi wanamlalmikia Ahmedinajad kwa kutaka kulifuta taifa la Israel kutoka ktk ramani ya dunia. Lakini wengi tunasahau kwamba taifa la Palestina lililokuwapo lilifutwa, jee kwa nini hoja hii huwa haitolewi? Badala yake hoja iko ktk kutaka kuifuta Isael tu, na siyo kwa taifa ambalo tayari lilikwisha futwa!
 
Anachemka tu. Na ideology zake za hovyo. Ule Ukuta (Wall of Shame) haukujengwa Palestina. Umejengwa mpakani na lengo ni kudhibiti watu ambao hawathamini utu wao (suicide bombers). Ni kichaa kabisa mtu kuamini kuwa ukijiua na wakati huo huo kuua wenzako ati utapata thawabu mbinguni. Lunatic! Sasa angalia, baada ya ukuta hakuna tena Suicide bombers, na kama ziko basi ni very localised.

Huyu Ahamedjani alichotakiwa yeye kwanza ni kuruhu Demoscracy nchini kwake na si kuangalia mateso ya Palestine au Afghanistan au popote Duniani. "Charity Begins at home". Kule Iran watu wakitongoza na kukamatwa wanauwawa! Wanawake hawaruhusiwi ku-drive! Hakuna pombe! Hakuna madanguro hata sehemu moja! Nchi gani hii!!? Wapi kwenye vitabu vy aDini walipokataza Madanguro, wanawake wasiendeshe magari au kuzuia uhuru wa watu kujieleza? Ni nani, katika vitabu vya dini, aliyeruhusu watu wengine kutoa hukumu kwa wenzao humu Duniani? Ni watu wehu kama hawa tu wanaoweza kunyima uhuru wa wenzao.

Angalia Europe au hata America. Ukikutana na Iranians! Utashangaa sana. Kwa nini wajisikie huru na raha kuwa nje ya nchi yao na si kwao!
 
Ila basi wangemslikiliza tu huyu jamaa,

na ndo wachekeche pumba na ukweli!

sasa huyu raisi wa Iran je amesema uongo?? ameongea!

Ni aibu kuona US na mataifa wanaojiita Champions za freedom kumkimbia jammaa anayetoa mawazo yake!

Poa waliindoka walikuwa sii wengi ila waliobaki walimsikiliza hata kama hawakubaliani na maoni yake!
 
Anachemka tu. .....

... Huyu Ahamedjani alichotakiwa yeye kwanza ni kuruhu Demoscracy nchini kwake na si kuangalia mateso ya Palestine au Afghanistan au popote Duniani. "Charity Begins at home"...

ni kweli ustaarabu uanzie nyumbani na upuuzi wa kukatana vichwa ovyo noma.

lakin mwache jamaa awasemee ambao anaona na wengi tunaona wanavyotendwa sivyo. vipi kama unaona mwenzio anaonewa, usipige makelele kuwa anaonewa? hii haijalishi kama kwako watu wanonewa pia au la
 
Anachemka tu. Na ideology zake za hovyo. Ule Ukuta (Wall of Shame) haukujengwa Palestina. Umejengwa mpakani na lengo ni kudhibiti watu ambao hawathamini utu wao (suicide bombers). Ni kichaa kabisa mtu kuamini kuwa ukijiua na wakati huo huo kuua wenzako ati utapata thawabu mbinguni. Lunatic! Sasa angalia, baada ya ukuta hakuna tena Suicide bombers, na kama ziko basi ni very localised.

Huyu Ahamedjani alichotakiwa yeye kwanza ni kuruhu Demoscracy nchini kwake na si kuangalia mateso ya Palestine au Afghanistan au popote Duniani. "Charity Begins at home". Kule Iran watu wakitongoza na kukamatwa wanauwawa! Wanawake hawaruhusiwi ku-drive! Hakuna pombe! Hakuna madanguro hata sehemu moja! Nchi gani hii!!? Wapi kwenye vitabu vy aDini walipokataza Madanguro, wanawake wasiendeshe magari au kuzuia uhuru wa watu kujieleza? Ni nani, katika vitabu vya dini, aliyeruhusu watu wengine kutoa hukumu kwa wenzao humu Duniani? Ni watu wehu kama hawa tu wanaoweza kunyima uhuru wa wenzao.

Angalia Europe au hata America. Ukikutana na Iranians! Utashangaa sana. Kwa nini wajisikie huru na raha kuwa nje ya nchi yao na si kwao!

Kaka hayo maneno kweli upo serious!? Umeshafika Iran au just unanakili kile ambacho BBC na CNN wanacho kuonyesha!?

Hivi uhuru maana yake ni kuwa huru kufanya ngono zembe, uzinzi, kuwa na madanguro, wanawake kutumika kwenye matangazo ya biashara huku wakiwa uchi!?

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=zu2ZjuvURy4]YouTube - Iranian Women! This is Iran...![/ame]
 
Watu (hasa Watanzania) wanaopinga kwamba Israel hawana siasa za kibaguzi, aidha hawaelewi vizuri kuhusu maswala ya kimataifa, wana mwelekeo wa udini, au wanasikiliza habari za upande mmoja bila kuchunguza kinaganaga juu ya suala hilo. Nadhani baadhi yenu mtashangaa kwamba, aliyekuwa raisi wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter, alijitokeza kimahiri na kusema kuwa serikali ya Israel inaendeleza siasa za kikandamizaji na ubaguzi dhidi ya Wapalestina. Ameyasema hayo katika kitabu kinachoitwa Palestine: Peace Not Apartheid. Katika kitabu hicho anasema kuwa amani itapatikana Mashariki ya Kati, pale tu Israel itakapoacha siasa zake za kibaguzi na ukandamizaji na kurudi katika mipaka yake ya kabla ya mwaka 1967. Kwa maelezo zaidi kuhusu kitabu hicho bofya hapa.
 
"Anachemka tu. Na ideology zake za hovyo. Ule Ukuta (Wall of Shame) haukujengwa Palestina. Umejengwa mpakani na lengo ni kudhibiti watu ambao hawathamini utu wao (suicide bombers). Ni kichaa kabisa mtu kuamini kuwa ukijiua na wakati huo huo kuua wenzako ati utapata thawabu mbinguni. Lunatic! Sasa angalia, baada ya ukuta hakuna tena Suicide bombers, na kama ziko basi ni very localised.

Huyu Ahamedjani alichotakiwa yeye kwanza ni kuruhu Demoscracy nchini kwake na si kuangalia mateso ya Palestine au Afghanistan au popote Duniani. "Charity Begins at home". Kule Iran watu wakitongoza na kukamatwa wanauwawa! Wanawake hawaruhusiwi ku-drive! Hakuna pombe! Hakuna madanguro hata sehemu moja! Nchi gani hii!!? Wapi kwenye vitabu vy aDini walipokataza Madanguro, wanawake wasiendeshe magari au kuzuia uhuru wa watu kujieleza? Ni nani, katika vitabu vya dini, aliyeruhusu watu wengine kutoa hukumu kwa wenzao humu Duniani? Ni watu wehu kama hawa tu wanaoweza kunyima uhuru wa wenzao.

Angalia Europe au hata America. Ukikutana na Iranians! Utashangaa sana. Kwa nini wajisikie huru na raha kuwa nje ya nchi yao na si kwao!"

*******************

Mwanjelwa:

Hujui kabisa unachokisema, naona unasukumwa tu na chuki. Huo ukuta haukujengwa kufuata mpaka wa 1948 unaotambuliwa na Umoja wa mataifa (Armistice Boundary). Ukuta umechota maeneo mengi sana ya Wapalestina.

Madanguro siyo kitu cha kujivunia kwani hata hapa tunayapiga vita. Suicide bombers wamezuka kwa sababu Wapalestina wamefikia ukutani -- hawana ndege, hawana vifaru, hawana chochote isipokuwa roho zao. sasa watapiganaje na adui mwenye kila aina ya silaha?

Kwa ujumla hawana zile silaha "za kiistarabu" ambazo wanazo Israel, na hivyo wanatakiwa wasalimu tu amri? Hebu tuambie: Mauaji gani ni ya kistaarabu? Kwa tafsiri yoyote ile, kwa vile huleta mauaji, vita yoyote ni ugaidi tu -- kwa sababu pia watu wasio na hatia hufa.

Jee unataka kusema kuwa vita inayotumia silaha "za kiistarabu" (kama wanazotumia Israel) basi ni vita halali? Wanaokufa, wanakufa kwa raha tofauti na wale wanaotokana na vitendo vya kujilipua? Wanahistoria wanasema iwapo utawala wa kibaguzi wa Afrika ya Kusini ungeendelea kwa miaka 10 tu mingine, wazalendo wa kule wangeamua kujilipua kama namna ya kupigana.

Hata hivyo nakubaliana na wale wanaosema haikuwa sahihi kwa nchi za Magharibi kususia mkutano huo. Wamefanya hivyo kwa sababu historia inatueleza kuwa wao ndiyo wamewahi kufanya ukatili mkubwa hapa duniani dhidi ya watu wengine waliowatawala katika karne zilizopita. Wahindi wekundu waliwindwa kama wanyama porini. Wazalendo wa Rhodesia (sasa Zimbabwe) walikuwa wanatundikwa mitini. Kule India Waingereza walifanya ukatili usiosemeka, kama vile mauaji ya kule Amritsar ya mwaka 1919 -- nk.

Kama ni mabingwa wa ustaarabu na wa kutoa hoja, waliogopa nini kufika kwenye mkutano na kuzijibu hoja za akina Ahmedinajad? Yaani hoja kwa hoja. Waliogopa kwa sababu waliona hawatakuwa na majibu ya maana. Bora lawama kuliko fedheha, au siyo?
 
Hivi kweli huu mkutano kama sisi waafrika unatusaidia nini? Yaani watu wazima na akili zenu mnaamini kwamba watu wakikutana Geneva wakatoka na declaration..itasaidia kupunguza ubaguzi pale ulipokuwepo? Hizi ni ndoto za mchana tuu kuwaweka ma-diplomats wetu busy..sishangai kuona US na wenzake wamegomea mkutano kama huu ni wastage of time and resources.

Hivi mimi kama mwafrika honestly..ubaguzi haunisumbui..I have far far...pressing issues..kama njaa, magonjwa nk. Yote haya ya ubaguzi watu tunayapigia kelele kwa sababu ya njaa. Hata ukienda huko ughaibuni..wanaolialia na ubaguzi wa rangi ni wale walio chini kwenye pyramid. Na huyo hatapata nafuu simply because watu wamekutana Geneva na kutoa tamko..Harafu ubaguzi ni natural. Its inherently within. Kwamba tunadai equality? hatuko serious...Tufanye kazi..jamaa wanatubagua kwa sababu ya umasikini wetu. Ulishamuona mmarekani anambagua muingereza au mjerumani? wote wana hali nzuri..ila mjerumani au muingereza atambagua mpolish au mrussia..kwa sababu ana njaa..ingawa wote ni weupe..

Waarabu wawe serious waache siasa mfilisi. Swala la wapalestina wanalitumia kama politics tuu..lakini hawana sera madhubuti ya kulitatua. Kama wako serious kwa nini wasimfukuze US toka Uarabuni au wamnyime mafuta kama wana jeuri? Its sheer stupidity...hawa jamaa mimi I no longer take them serious..zaidi ya kuwaona wamevaa vitambaa vyao kichwani na makanzu..

Harafu mimi wananibore..wanajifanya wana solidarity na sisi waafrika kama wana shida zao..wakiwa wanataka support yetu..zaidi ya hapo ndo wabaguzi wa kutupwa. Mfano Sudan sasa hivi anajifanya ni Africa kwa sababu ya lile so lake la kupelekwa The Hague..zaidi ya hapo..yeye anajiona mwaarabu kuliko wale wa SAUDIA..What hyprocricy...

Mimi nasema WE Africans should not trust anybody. We have terrible history. Hao wote wanaojifanya marafiki zetu-at some point walishatutenda. Tusimwamini yeyote. Tuhangaike kivyetu. ANAYETAKA URAFIKI NA SISI NI KUPEWA TERMS...WIN WIN SITUATION. Lakini tatizo: Sikio la kufa halisikii dawa kabisa!
 
"
Wayahudi wanamlalmikia Ahmedinajad kwa kutaka kulifuta taifa la Israel kutoka ktk ramani ya dunia. Lakini wengi tunasahau kwamba taifa la Palestina lililokuwapo lilifutwa, jee kwa nini hoja hii huwa haitolewi? Badala yake hoja iko ktk kutaka kuifuta Isael tu, na siyo kwa taifa ambalo tayari lilikwisha futwa!

Halijafutwa ndio maana lipo linadai haki zake. Lingekuwa lilifutwa tusingekuwa na mijadala hii
 
wanajifanya wana solidarity na sisi waafrika kama wana shida zao..wakiwa wanataka support yetu..zaidi ya hapo ndo wabaguzi wa kutupwa. Mfano Sudan sasa hivi anajifanya ni Africa kwa sababu ya lile so lake la kupelekwa The Hague..zaidi ya hapo..yeye anajiona mwaarabu kuliko wale wa SAUDIA..What hyprocricy...

Mimi nasema WE Africans should not trust anybody. We have terrible history. Hao wote wanaojifanya marafiki zetu-at some point walishatutenda. Tusimwamini yeyote. Tuhangaike kivyetu.

Inanipa maumivu hata kufikiri kuwa watu wanaopigana kupambana na ubaguzi wao ni vinara wa kubagua wengine. Wanasikia uchungu wakiandamwa na wamagharibi lakini wao wanapotuandama weusi wanaona raha sana. Afadhali hata kule USA unaweza kuona trace na trail ya weusi waliopekwa huku kutumikishwa. Swali langu waafrika waliopelekwa Uarabuni kuwa watumwa decendants wao wako wapi? What happened to them?

Je Katika Arab league March 2001 kule Amman Jordan wakati Gadafi alipowakaribisha openly Waarabu kuja na kuimiliki Afrika aliposema
"The third of the Arab community living outside Africa should move in with the two thirds on the continent and join the African Union 'which is the only place we have'..." Arabanisation of Africa ni project ambayo imekuwa agenda katikati ya Waarabu na hiyo hawaiongelei. "You are aware that the end of all our effort and this expense is to procure Negroes. Please show zeal in carrying out our wishes in this capital matter" Muhammad Ali Pasha ruler of Egypt of arabic origin, 1825, in a letter to one of his generals in Sudan, quoted in {Nyaba, 2002:36}. "We want to Islamize America and Arabise Africa" Dr Hassan El-Turabi, chief ideologue of Jellaba-Arab minority rule in Sudan, 1999, quoted in {Nyaba, 2002: 27} Inakuwaje Waarabu ambao kwao ni Arabia wameiteka na kuitwaa sehemu kubwa ya supra-Sahara Africa toka Sinai peninsula kupita Morrocco hadi pwani ya Antlantic. Na je wale weusi waliokuwemo katika maeneo hayo wako wapi leo? Black Egyptians, Balck Berbers wameenda wapi maskini? Tangu Waarabu walipoiteka Misri miaka ya 642 kikawa kitovu chao. They have seized and lebensraumized Africa.

Katika baadhi ya maandiko yao wanakiri kuwa watu weusi halali yao ni utumwa kwa ajili ya ngozi yao iliyounguzwa na jua na bila shaka na ubongo wao umechemka kwa joto kali la jua anasema .al Dimashqi.Hata na Ibn al-Faqih al- Hamadhani ana matamshi kama hayo. Kama mambo yote haya yangekuwa tu historia ya kale, hayaendelzwi hadi leo ningewaelewa Waarabu wapinga ubaguzi. Lakini leo tunaya ona Darfur halafu waseme eti wanapinga ubaguzi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kaka hayo maneno kweli upo serious!? Umeshafika Iran au just unanakili kile ambacho BBC na CNN wanacho kuonyesha!?

Hivi uhuru maana yake ni kuwa huru kufanya ngono zembe, uzinzi, kuwa na madanguro, wanawake kutumika kwenye matangazo ya biashara huku wakiwa uchi!?

YouTube - Iranian Women! This is Iran...!

Yes. Huo ndiyo uhuru. Kufanya utakacho bila kuzuiwa na bila kuvunja sheria. Hiyo ya 'You Tube' jamaa ameivizia tu sehemu. Juzi juzi (sikumbuki lini) kuna jamaa 12 kule Iran wameuwawa kwa kosa la kufanya mapenzi nje ya ndoa. Wameuwawa hadharani.
 
Ila basi wangemslikiliza tu huyu jamaa,

na ndo wachekeche pumba na ukweli!

sasa huyu raisi wa Iran je amesema uongo?? ameongea!

Ni aibu kuona US na mataifa wanaojiita Champions za freedom kumkimbia jammaa anayetoa mawazo yake!

Poa waliindoka walikuwa sii wengi ila waliobaki walimsikiliza hata kama hawakubaliani na maoni yake!

Politicians wanasema 'YOu cannot discuss the obvious'. Huyu jamaa kabla hajaongea tayari anajulikana kilichomo kichwani.
 
Kwa kuwa wameshiba damu za ubaguzi na dhulma MABEPARI na " wauwaji" hawatakubali kusemwa na kuambiwa "mfanyavyo hivi sivyo" au "kama hamuwezi kuacha khiyana basi walau punguzeni" siku zote, kupitia ubaguzi na udhalimu ndo maendeleo ya MABEPARI hawa yanapatikana, hatawacha kuifanya dunia chungu kwa wanyonge kwani kwa kufanya hivyo kutawakosesha "maslaha" ya mali na fakhari za ulimwengu. Siku zote watakuwa pamoja katka khiyana na hawatakaa pamoja na wale watakaosema "ubaguzi na dhulma kwa wanyonge haufai"

Katika hii Dunia, nimepita sehemu kibao, lakini sijawahi ona wabaguzi kama WAARABU. Sina hakika kama ina uhusiano na dini, ila jamaa ni wabaguzi sana sana.
 
"Anachemka tu. Na ideology zake za hovyo. Ule Ukuta (Wall of Shame) haukujengwa Palestina. Umejengwa mpakani na lengo ni kudhibiti watu ambao hawathamini utu wao (suicide bombers). Ni kichaa kabisa mtu kuamini kuwa ukijiua na wakati huo huo kuua wenzako ati utapata thawabu mbinguni. Lunatic! Sasa angalia, baada ya ukuta hakuna tena Suicide bombers, na kama ziko basi ni very localised.

Huyu Ahamedjani alichotakiwa yeye kwanza ni kuruhu Demoscracy nchini kwake na si kuangalia mateso ya Palestine au Afghanistan au popote Duniani. "Charity Begins at home". Kule Iran watu wakitongoza na kukamatwa wanauwawa! Wanawake hawaruhusiwi ku-drive! Hakuna pombe! Hakuna madanguro hata sehemu moja! Nchi gani hii!!? Wapi kwenye vitabu vy aDini walipokataza Madanguro, wanawake wasiendeshe magari au kuzuia uhuru wa watu kujieleza? Ni nani, katika vitabu vya dini, aliyeruhusu watu wengine kutoa hukumu kwa wenzao humu Duniani? Ni watu wehu kama hawa tu wanaoweza kunyima uhuru wa wenzao.

Angalia Europe au hata America. Ukikutana na Iranians! Utashangaa sana. Kwa nini wajisikie huru na raha kuwa nje ya nchi yao na si kwao!"

*******************

Mwanjelwa:

Hujui kabisa unachokisema, naona unasukumwa tu na chuki. Huo ukuta haukujengwa kufuata mpaka wa 1948 unaotambuliwa na Umoja wa mataifa (Armistice Boundary). Ukuta umechota maeneo mengi sana ya Wapalestina.

Madanguro siyo kitu cha kujivunia kwani hata hapa tunayapiga vita. Suicide bombers wamezuka kwa sababu Wapalestina wamefikia ukutani -- hawana ndege, hawana vifaru, hawana chochote isipokuwa roho zao. sasa watapiganaje na adui mwenye kila aina ya silaha?

Kwa ujumla hawana zile silaha "za kiistarabu" ambazo wanazo Israel, na hivyo wanatakiwa wasalimu tu amri? Hebu tuambie: Mauaji gani ni ya kistaarabu? Kwa tafsiri yoyote ile, kwa vile huleta mauaji, vita yoyote ni ugaidi tu -- kwa sababu pia watu wasio na hatia hufa.

Jee unataka kusema kuwa vita inayotumia silaha "za kiistarabu" (kama wanazotumia Israel) basi ni vita halali? Wanaokufa, wanakufa kwa raha tofauti na wale wanaotokana na vitendo vya kujilipua? Wanahistoria wanasema iwapo utawala wa kibaguzi wa Afrika ya Kusini ungeendelea kwa miaka 10 tu mingine, wazalendo wa kule wangeamua kujilipua kama namna ya kupigana.

Hata hivyo nakubaliana na wale wanaosema haikuwa sahihi kwa nchi za Magharibi kususia mkutano huo. Wamefanya hivyo kwa sababu historia inatueleza kuwa wao ndiyo wamewahi kufanya ukatili mkubwa hapa duniani dhidi ya watu wengine waliowatawala katika karne zilizopita. Wahindi wekundu waliwindwa kama wanyama porini. Wazalendo wa Rhodesia (sasa Zimbabwe) walikuwa wanatundikwa mitini. Kule India Waingereza walifanya ukatili usiosemeka, kama vile mauaji ya kule Amritsar ya mwaka 1919 -- nk.

Kama ni mabingwa wa ustaarabu na wa kutoa hoja, waliogopa nini kufika kwenye mkutano na kuzijibu hoja za akina Ahmedinajad? Yaani hoja kwa hoja. Waliogopa kwa sababu waliona hawatakuwa na majibu ya maana. Bora lawama kuliko fedheha, au siyo?
Kimsingi hakukuwa na taifa la Israel kabla ya 1948,na ata mipaka inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa ya 1948 kimsingi mataifa ya kiarabu hayakuyakubali,ndio maana immediately wakaanzisha vita na taifa jipya la Israel,mpaka muda huo Israel ilikuwa inaomba mji wa Yereusalemu ugawanywe upande wa magharibu uwe Israel na Mashariki uwe Palestina,lakini waarabu walikataa,baada ya kuanzisha mapambano na Israel na kupata kipigo kikubwa kilichoipa fursa Israel kupanua mipaka yake 1967 ambapo pia mji wote wa Yerusalemu ulitwaliwa,Waarabu ndipo walipoanza kukubali reality ya kabla ya 1967 na hapa ndipo one time i agree with George Bush,haitawezekana kamwe kurudi kwenye mipaka ya 1948,lazima tukubaliane na new reality na complexity ya mgogoro wenyewe,ni lazima pande zote ziwe tayari kufanya painful compromise,wapalestine wapoteze baadhi ya madai yao na Waisrael pia wapoteze baadhi ila kurudi blindly kwenye mipaka ya 1948 ni ndoto,mwaka 2000 Yassen Arafat alipoteza nafasi nzuri sana Camp David ya kumaliza mgogoro huu kwa msimamo wake wa kushikilia masuala makubwa mawili
1.Mji wa Yerusalemu(Ni la msingi hili)
2.Wakimbizi wa kipalestina wanaoishi nchi za nje(zaidi ya watu Million 4) warudi kwenye maeneo waliyokuwa wanaishi mwanzo ata kama maeneo hayo yatakuwa ni maeneo ya Israel baasa ya makubaliano(Huu ni ujinga).

Kwenye suala la Yerusalemu wakati ule Ehud Barack alikuwa tayari kuipatia Palestina baadhi ya maeneo ya Mashariki mwa mji wa Yerusalem lakini bado Arafat akang'ang'ania pia suala la pili,hili lilikuwa ni kosa la kimkakati na kimsingi haitawezekana kamwe kwa Wapelistina kupata ambacho wangeweza kukipata kwenye mazungumzo yale.
 
Hawa wakimbizi walijipa ukimbizi wenyewe. Hakuna aliyewatimua na hawakuwa na sababu ya msingi kufanya hivyo. Wenzao bado wako kule Israel wanaishi maisha ya raha mustarehe.
 
AHMADINEJAD pia ni mbaguzi sana kama tukisimamia ukweli. Kama uliisikiliza speech yake jana na huna bias,utakubaliana na mimi. Waisrael ni kweli wanawaua wapalestina kama wapalestina wanavyowaua waisraeli. Kwa hiyo wanauana,cha muhimu mataifa mengine kama kweli tunataka kusaidia tusichague upande tunapotoa maoni. Tutoe maoni kwa kuziambi aukweli pande zote mbili. Unapoishambulia Israel peke yake au Palesina peke yake unawapa ignition watu kufanya mabaya wakijua ulimwengu unawaunga mkono.
Ahmadinejad napingana nae moja kwa moja kwa kupinga holocaust,kwani ushahidi kwamba ilitoke uko wazi. Unajua kuna watu wanaopinga kuwa hata mauaji ya Rwanda hayakutokea wakati ulimwengu umeshuhudia si muda mrefu sana(1994) na wakimbiz wamekuwepo kwetu Tanzania mapaka hivi karibuni.
Huu anaoufanya Ahmadinejad ni ubaguzi uliojengwa katika misisngi ya dini. Kwakuwa sehemu kibwa ya wapalestina anashare nao dini basi hata kama hawako right anawaunga mkono tu. Msimamo mzuri ni kupinga mabaya hata kama anayefanya ni baba au mama yako au ndugu wa kuzaliwa naye.
Speech anazotoa jamaa ni za kibaguzi kwani several times amesikika akisema Taifa la Israel na Uzayuni ataufutilia mbali,wazayuni nao wana haki ya kujilinda kama wapalestina pia.Muhimu ni kuwaweka watu wa palestina na Israel pamoja wakubaliane maisha watakayoishi bila external pressures like Iran and US.
Ni mtazamo tu,msijenge chuki.
 
Back
Top Bottom