Maiti za vitoto zaidi ya 10 zafukuliwa shimo moja

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,303
Katika hali ya kustaajabisha, maiti za watoto wanaokadiriwa kuwa na umri wa siku moja au zaidi, zinazofikia idadi ya 11, zimefukuliwa katika shimo moja, jirani na maeneo ya hospitali ya Mwananyamala mcha wa leo!!. Tukio hilo limevuta hisia za watu wengi eneo hilo na kustaajabisha watu wengi. Hadi sasa haijajulikana maiti hizo zilizikwa hapo na nani na wazazi ni akina nani. kwa habari ya kina, fuatailia gazeti la Uwazi kesho hapa mtandaoni.

Piacha ziko hapa: http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/maiti-za-vitoto-zaidi-ya-10
 
hii nimeiona kule kwa Shigongo pia. But inasikitisha sana jamani. where are we heading to?
 
Kama hizo ni mimba zimetolewa ndani ya siku moja; jee wiki, mwezi na mwaka? Bei ya condom nayo imepanda sana au; kwanini mimba zitungwe kama kondomu zinatumika?
 
Kama ni mimba mbona balaa. Halafu hiyo ni hosipitali moja tuu
 
Hii ni hatari sana... at least wangetafuta namna ya kuficha hii kitu. sasa itawaletea shida sana hao mwananyamala
 
Hii ni hatari sana... at least wangetafuta namna ya kuficha hii kitu. sasa itawaletea shida sana hao mwananyamala

Kwa staili ya Bongo yetu waliofanya au kusaidia kufanyika kwa hayo watapeta kiulani
 
Habari nilizozipata kupitia redio Clouds ni kwamba kuna shimo moja pale makaburini ambapo wamekutwa watoto 11 wakiwa wamekufa bila kuzikwa kistaarabu, haijulikani nani kafanya hivyo na kwa sababu gani, mwenye taarifa zaidi hatuhabarishe juu ya tukio hii la kushangaza
 
Inatisha
 
innalillah wainallah rajiun!Matokeo hayo ya vijana kuichukia ccm na serikali yake!hivyo vijana wanaanza kupungua polepole pabaki wazee
 
hakika ni hatari sana,kama ni kweli shimo moja basi ni tenda ya madaktari wa M'nyamala hosp.kutoa mabinti mimba,lakini mtujuze vizuri wanaelekea kuwa wa umri gani?.
Wahusika watapeta kiulaini kama alivyosema EMT
 
Habari nilizozipata kupitia redio Clouds ni kwamba kuna shimo moja pale makaburini ambapo wamekutwa watoto 11 wakiwa wamekufa bila kuzikwa kistaarabu, haijulikani nani kafanya hivyo na kwa sababu gani, mwenye taarifa zaidi hatuhabarishe juu ya tukio hii la kushangaza

Mkuu watoto wachanga au wa umri tofauti? Fafanua please? Kuna ndugu zetu wamepotelewa na watoto na hawajapatikana.
 
Pole kwa familia za wafiwa na jamaa wote. Mtoa taarifa, Kindly pprovide more details. Clouds wametuma reporter, wamesoma ktk gazeti au wamesource wapi? Je ni Mwananyamala makaburi yapi? Maana kuna makaburi mengi. Pia je, ni watoto waliokufa recently au wamekufa siku nyingi? Inamaana hakuna wazazi waliopata kuripoti kupotelewa na watoto wao? 11 kids ni wengi sana ku-go missing bila kuleta media attention kihivyo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom